Bibilia inasema nini kuhusu utumiaji mzuri wa pesa ?

uliza ujibiweBibilia inasema nini kuhusu utumiaji mzuri wa pesa ?
Jimmy asked 2 years ago

Naomba kujua au kufahamu kuhusu biblia inavyosema na kufundisha juu ya utumiaji mzuri wa pesa.

4 Answers
Debora answered 2 years ago

Bibilia iko na mengi ya kusema kuhusu usimamizi wa pesa. Kuhusu kukopa, Bibilia kwa jumla inashauri kinyume. Angalia Methali 6: 1-5; 20:16; 22: 7, 26-27 (“Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye…. Usiwe mmoja wao waeekao rahani; Au walio wadhamini kwa deni za watu; Kama huna ktiu cha kulipa; Kwani ukaondolee kitanda chao chini yako”). Mara na mara tena, Bibilia inatuonya kujiwekea utajiri na inatushauri kutafuta utajiri wa kiroho badala yake. Methali 28:20, “Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa.” Angalia pia Methali 10:15; 11:4; 18:11; 23:5.

Methali 6:6-11 yapeana maarifa kuhusu uzembe na utumiaji mpya wa fedha ambao utatokea. Tumeambiwa tuwatizame mchwa vile walivyo na bidii ambayo wafanya kazi kuweka hakiba chakula. Ufahamu huo pia watuonya kulala wakati tunastahili kufanya kazi kwa kitu ambacho ni cha faida. “Mtu goigoi” ni mvivu, mtu mzembe ambaye atapumzika badala ya kufanya kazi. Hatima yake imeakikishwa – umaskini na hitaji. Kwa upande mwingine mwisho wa spektra ni mtu aliyejawa na nia ya kujiwekea utajiri. Mtu kama huyo kulingana na Mhubiri 5:10 hatawai kuwa na utajiri wa kuthosha wa kumridhitisha na ataendelea kunyakua zaidi na zaidi. Timotheo wa Kwanza 6:6-11 pia yatuonya kuhusu mitego ya kudhamani utajiri.

Badala ya kuthamani kujiwekea utajiri, mfano wa bibilia ni ule wa kutoa, sio kupokea. “Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na atende kama alivokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu” (2 Wakorintho 9:6-7). Pia tumetiwa moyo tuwe watunzaji wema wa kile ambacho Mungu ametupa. Katika Luka 16:1-13 yesu alipeana mfano wa mtu mtunzaji asiye mwaminifu na kutuonya juu ya utunzaji mpaya. Maadili ya hadhiti ni “Basi kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe?”(aya ya 11). Pia tumewajibika kuwatafutia risiki wale wa nyumba yetu, vile 1 Timotheo 5:8 yatukumbusha: “Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.”

Kwa ufupi, nini Bibilia yasema kuhusu utunzaji bora wa fedha? Jibu linaweza wekwa kwa mukhtasari kwa neno moja-maarifa. Tunastahili kuwa wa maarifa na fedha zetu. Tunastahili kuweka akiba fedha, bali si kuzivuja. Tunastahili kutumia fedha, lakini kwa mwelekeo na kadirio. Tunastahili kumpatia Mungu, kwa ukarimu na thabihu. Tunastahili kutumia fedha kuwazaidia wengine, lakini kwa utambuzi na uongozi wa Roho wa Mungu. Si mokosa kuwa tajiri, lakini ni makosa kupenda pesa. Si makosa kuwa maskini, lakini ni makosa kuvuja fedha kwa vitu visivyo na maana. Ujumbe wa Bibilia ambao waendelea kila wakati kuhusu utunzaji bora wa fedha ni kuwa wa maarifa.

Reuben shadrack answered 1 year ago

Umeongea kweli mtumishi naomba uni add kwenye magroup Mengne uliyonayo napenda kujifunza Biblia na nna maono makubwa kufanya kazi ya Mungu +255758465064

bakenge answered 11 months ago

Mungu aku bariki mtumishi wa Mungu, somo zuri ambalo lina badili tena mwenendo wangu. Mungu akutiye nguvu

Setrika.info answered 7 months ago

Juventus and Manchester United will make some transfer deals in the summer of 2018. As reported by Calciomercato harga 2019 on Saturday (16/06/2018), to complete the transfer involving five players, Juventus and Man United will hold a meeting next week.

Currently, Juventus chasing two United players, Anthony Martial and Matteo Darmian. Meanwhile, the Red Devils-nickname Man United- eyeing three Juventus players. They are Alex Sandro, Sami Khedira and Mario Mandzukic.

Juventus require the presence of Darmian. For now, Juventus only has Mattia De Sciglio to serve as a fullback right. Meanwhile, the flexibility of the game from Martial so the main attraction for the Bianconeri-nickname Juventus.

In addition to functioning as a left winger in the pattern 4-2-3-1 concoction Massimiliano Allegri, Martial can also be played as an attacker. Skip to Man United camp. The Red Devil needs Alex Sandro to escort the left side of the defense. Because, Man United currently does not have a capable player to operate as a fullback left.

Meanwhile, Khedira’s high experience became something Man United needed. The Tunisian midfielder won numerous prestigious trophies in uniformed VfB Stuttgart, Real Madrid and now Juventus. Even in 2014, Khedira deliver the National Team (Timnas) Germany into champions 2014 World Cup.

Mandzukic? Croatian podium attacker will be plotted Jose Mourinho as a coating from Romelu Lukaku. Because last harga murah season’s upholstery, Zlatan Ibrahimovic, decided to leave LA Galaxy in March 2018.

Your Answer