Hivi kuangalia picha za ngono ni dhambi?

uliza ujibiweCategory: Vijana na MahusianoHivi kuangalia picha za ngono ni dhambi?
Cath asked 2 years ago

Bwana Yesu Asifiwe. Mimi ni msichana niliyeokoka na nimekuwa mwaminifu sana katika maisha yangu ya wokovu ila kuna jambo linanisumbua sana na ningependa kupata msaada wenu watu wa Mungu, Hivi kuangalia picha za ngono ni dhambi? kwa maana wakati mwingine nimejikuta nikiangalia japo mimi mwenyewe huwa sipendi. Sasa kama ni dhambi tutajifunzaje jinsi ya kuwahandle waume zetu pindi tutakapokuwa katika ndoa? Naomba msaada wenu.

7 Answers
HK answered 2 years ago

Mimi ninajibu kwa ufupi kwa sasa.
Ni vizuri kwamba umeokoka na kwamba umekuwa ‘mwaminifu’ sana katika wokovu ISIPOKUWA jambo hilo linalokusumbua.
Kwa ninavyoelewa mimi kuwa mwamininfu katika wokovu ni pamoja na kujilinda na kujiepusha na mambo ambayo yanaweza kukuingiza katika dhambi.

Kama si ya matendo iko dhambi ya mawazo pia. Kwa hiyo ili uamifu wako ukamilike ni HERI ukajiepusha na majaribu ya kutengeneza wewe mwenyewe! Picha hizo chafu ambazo huwa unaziangalia na wakati mwingine pasipokupenda hiyo ni ishara tosha kwamba unalazimisha kitu ambacho hatari katika maisha yako ya wokovu, huku dhamiri yako ikiwa inakusuta! Kama huwa hupendi lazima ujiulize kwa nini uangalie kitu usichokipenda? Ni lazima kuwe na nguvu inayokulazimisha kufanya hivyo.

Watengeneza picha za ngono ni watu wanaoendeshwa na roho chafu. Roho zilizosababisha Sodoma na Gomora ziangamizwe. Roho ya zinaa! Roho za tamaa mbaya. Roho ambazo zimesambaratisha na zinaendelea kusambaratisha ndoa nyingi duniani. Kinachoenezwa na picha hizo ni tabia ya zinaa. Kila mtu mwenye kuangalia na kufurahishwa na picha hizo yuko katika hatari kubwa ya kutekwa na roho ya zinaa! Kinachofundishwa na katika picha hizo ni zinaa na wala si namna ya ku-handle mume kama ulivyosema wewe.

Kama kuna mtu alikuambia kwamba humo wanafundisha namna ya ku-handle mume alikudanyanga. Anataka kukuingiza katika shimo ambalo ukiingia humo kutoka ni vigumu sana. Watu ambao hawana ndoa, wanaotengeneza mikanda hiyo, hawawezi kufundisha mtu namna ya ku-handle mume. Sana sana unachoweza kujifunza ni namna ya ku-handle buzi!

Lakini kwa kuwa wewe umeokoka hayo mambo yako mbali nawe. Hakuna maadili yoyote wala namna njema utakayopata kutoka katika picha hizo kwa sababu humo huwa hawafundishi namna ya kuishi na mume. Ili kuweza kujifunza namna ya kuhudumia waume/wake ni lazima kujifunza katika Neno la Mungu na kusikiliza mafundisho yanayotolewa kanisani kuhusu namna ya kuishi katika na nyumba. Yako mafundisho mengi kwa vijana ambao hawajawa na wenzi na kwa watu ambao wako kwenye ndoa tayari. Mafundisho haya yenye msingi wa Neno la Mungu huwa na material sahihi kwa ajili ya wana wa Mungu.

Hudhuria semina mbali mbali kanisani ambazo huwa zina mafundisho kwa ajili ya ndoa na unyumba! Kuendelea kuangalia picha hizo ni kujichimbia shimo ambalo ukijitumbukiza mwenyewe ni wewe mwenyewe utatakiwa kujitoa maana hukutambuwa yakupasayo USALAMA WA WOKOVU WAKO.
Kama kweli umeokoka kaa na ishi maisha ya mtu aliyeokoka ambayo yanaelekezwa katika BIBLIA.

Rebeca answered 2 years ago

Dada yangu mpenzi Cath
tunae mwalimu wetu ambaye ni mwalimu wa walimu yeye atatufundisha yote yafuatanayo na utakatifu wala hakuna elimu nyingine zaidi inayomzidi Yesu.usiangalie picha za ngono kabisa hazifundishi lolote ila zitakusababishia mawazo ya zinaa na pia ni dhambi kuangalia hizo picha kwa mwana wa mungu,yesu atakufundisha, ndie aliyekuita naye atahakikisha unaweza kuishi bila mapungufu kwenye ndoa.Ubarikiwe maana naamini kuwa utajitenga na picha za ngono.

Debora answered 2 years ago

Dada Cath  zingatia sana alichokufundisha kaka HK.
 
Pia kwa kuongezea, jua kwamba miili yetu ni hekalu la roho mtakatifu. Hivyo usimhuzunishe Roho wa Bwana. Hakuna ibada yoyote takatifu katika “ponography” Unapoangalia hizo picha, ziko roho chafu kama tamaa, uasherati nk zitakuingia na ndipo utashangaa utakapoingia katika ndoa,mapepo hayo yanaweza kujidhihirisha na kuharibu ndoa yako. Nimeona shuhuda nyingi sana za watu wanaosumbuliwa na “spirit husbands or spirit wives”. Matokeo yake utajikuta unafanya uasherati na hayo mapepo wakati ukiwa umelala na ni mpaka ufanyiwe deliverance ndipo yanatoka.
 
Hebu kubali kuacha huo uovu kwa USALAMA WA WOKOVU WAKO.

Mwana wa Mungu answered 2 years ago

Dada Cath,
Kifupi ni kuwa, ukiokoka picha hizo ni marufuku, kwa nini?
1. Wanaofanya hivyo huwa si mke na Mume – Hivyo kuangalia ni kinyume na Neno Efeso 5:11
2. Hata kama ni Mke na mume, lazima ukiangalia utawaka tamaa na kumtamani mke/mume wa mtu mwingine ni kuvunja Amri ya Mungu (Kut 20)
3. Si kuwa hupendi kuziangalia bure! Roho wa Mungu hukuonya kwa kuwa Yeye anajua hatari zote za kiroho kuliko sisi. Kumbuka, Roho anajua maandiko ambayo hata mengine hujawahi kusoma. Kwa hiyo kumtii bila swali ni njia njema ya kukwepa matatizo yanayoweza kukutokea baadae.
Ushauri wangu ni kuwa tubu na uache haraka. Ni hatari!

Emig answered 2 years ago

Ni mbaya na haitakiwi kama waliotangulia walivyosema,kuna Ushuhuda Mimi Luna watoto walikuwa wanaangalia picha za ngono,tena ni za jinsia moja.Wakaanza wao wenyewe kwanza mmoja alipoondoka kwenda shule yule aliyebaki nyumbani akaanza kumnajisi mjukuu Wa mjomba wake.Alipoulizwa kajifunzia wapi akasema huwa wanaenda kwenye vibanda wanakoonyesha video hizo za ngono.So watch out ni kinyume na mpango Wa Mungu.Wanaofanya hivyo ni Wa shetani.tubu na umuombe Mungu akkusamehe

Your Answer