Kuna aina ngapi za sadaka?

uliza ujibiweCategory: Bible StudyKuna aina ngapi za sadaka?
Peter asked 2 years ago

Naomba kujua aina za sadaka tunazopaswa kumtolea Mungu.

1558 Answers
Dr. Imma answered 2 years ago

AINA ZA SADAKA

  1. Sadaka ya kawaida: Hii ni sadaka ambayo mwanadamu anatoa kwa Mungu kushukuru kwaajili ya kumuongoza na kumlinda kwa wiki nzima.
  2. Sadaka ya FUNGU LA KUMI na ZAKA: Hizi ni sadaka ambazo ni lazima kutoa tena kwa ukamilifu. Malaki 3:7-10…” Pia soma Matendo 5:1-10 …utaona habari za ANANIA na SAFIRA mkewe ambao wote walikufa mbele ya mitume (petro) kwa kosa la kutokutoa walicho ahidi kwa ukamilifu na kujaribu kuficha sahemu ahadi yao kwa siri..
  3. Nadhiri na ahadi: kumbukumbu 23:21-23.”…Utakapoweka nadhiri kwa Bwana, Mungu wako, Usiwe mlegevu katika kuiondoa; kwa kuwa Bwana, Mungu wako,hataacha kuitaka kwako; nayo hivi itakuwa dhambi kwako…….23,…yaliyotoka mdomoni mwako yashike kuyafanya; kwa mfano uliyomwekea nadhiri Bwana,Mungu wako, ni sadaka ya hiari uliyoahidi kwa kinywa chako…..”
  4. Malimbuko: Hii ni sadaka ya mzaliwa wa kwanza. (a) Mshahara wako wa kwanza (kama mzaliwa wa kwanza) wote- sadaka kwa Mungu (b) Faida ya mapato ya kwanza-biashara, kilimo.. Mithali 3:9-10 .. .”…mheshimu Bwana kwa mali yako, na kwa malimbuko ya mazao yako yote. ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi….Pia soma Nehemia 12:44 , kumbukumbu 26:1-2 , 2nyakati 31:4-6
  5. Dhabihu : Hii ni sadaka ambayo roho mtakatifu husema na wewe moja kwa moja.. mwanzo 22:1-3… utaona habari za Ibrahimu

 
Tunapaswa kutoa sadaka wapi?
Mahali sahihi pa kutoa sadaka ni KANISANI yaani nyumba ya Mungu… Kumbukumbu 12:5-7….”…Lakini mahali atapochagua BWANA, Mungu wenu, …maana ni makao yake,elekezeni nyuso zenu huko,nawe wende huko;pelekeni huko sadaka zenu…na dhabihu zenu , na zaka zenu….nadhiri zenu na sadaka zenu za hiari, na wazaliwa wa kwanza….”
Kwanini tunatoa sadaka?
a) Kutoa sadaka ni agizo la Mungu- kumbukumbu 8:6 Kutoka 25:1-2..”..Mungu akanena na Musa, waambie wana wa israeli kwamba wanitwalie sadaka……:
b) Kutoa sadaka ni kuonyesha utii kwa Mungu.. Unapotii unapata…kumbukumbu 28:1-8…. na usipo tii unapata haya… kumbukumbu 28:15-22. Pia soma Matendo 4:34-36…utaona jinsi watu wakitoa kwa uaminifu Matendo 5:1-10…utapata habari za anania na safira..
Kwahiyo, kutoa sadaka ni muhimu na pia kusaidia wajane na yatima ni muhimu..Unapomsaidia mtu mwenye shida haimaanishi kwamba umetoa sadaka bali umemsaidia kwahiyo kutoa sadaka kuko palepale… ukisoma MALAKI 3:7-10… Mungu anamfananisha mtu asiyetoa sadaka na mwizi… tena anasema..”…mne niibia zaka na dhabihu,ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi….”

Richard answered 1 year ago

Naomba kufahamu nafasi ya sadaka za kishirikina katika maandiko biblia vine in gum I wake?

windhammer answered 4 months ago

Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.Waefeso 2:8,9

Kennethdrach answered 3 months ago

wh0cd177070 [url=http://atarax.icu/]buy atarax online[/url]

Kennethdrach answered 3 months ago

wh0cd177070 [url=http://cafergot.company/]cafergot[/url]

1 2 3 312 Next »
Your Answer