Naomba msaada wenu kuhusu hili swali langu

uliza ujibiweCategory: Bible StudyNaomba msaada wenu kuhusu hili swali langu
James asked 2 years ago

Nimekuwa na maswali mengi kuhusu biblia pindi navyoisoma na kukosa majibu au mtu wa kumuuliza kwa wale ambao Mungu amewapa uwezo wa kutafsiri kitabu hiki kitakatifu ninaomba mtupe majibu yenu hapa.

Kwa kuanzia naomba niulize swali. Bible inasema Mungu alimuumba Adam na Hawa. Ila ukija kusoma katika bible unaona kama walikuwepo watu wengne duniani kwa mfano katika Mwanzo 4. Adamu na Hawa walikuwa na watoto wawili Kain na Habili baada ya Kain kumuua Habili mazungumzo kati ya Mungu ya Kaini yaliashilia kuna watu wengine zaidi ya Adam na Hawa.

Mwanzo 4: 1-15.

1 Adam akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, “nimepata mtoto mwanaume kwa bwana.”
2 Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi.
3 Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana.
4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;
5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.
6 Bwana akamwambia Kaini, “Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.”
8 Kaini akamwambia Habili nduguye, “Twende uwandani” Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua.
9 Bwana akamwambia Kaini, “Yuko wapi Habili ndugu yako?” Akasema, “Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?”
10 Akasema, “Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia katika ardhi!
11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;
12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao dunian.”
13 Kaini akamwambia Bwana, “Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.
14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.”
15 Bwana akamwambia, “Kwa sababu hiyo yeyote atakayemwua Kaini atalipiziwa kisasi mara saba.” Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.

Swali langu ni hili, hao watu ambao wangemzulu Kaini ni watu gani ni wazazi wake Kaini ambao ni Adamu na Hawa au kulikuwa na watu wengine ambao Kaini alikuwa anawaofia? Na kama ni wazazi wake kwanini biblia haijaweka wazi kuwa walikuwa wanawazungumzia Adam na Hawa? Naombeni msaada kwa watu ambao mmeelewa icho kifungu mnisaidie. Natunguliza shukrani.

Your Answer