Nifanye nini katika hali kama hii?

uliza ujibiweCategory: UshauriNifanye nini katika hali kama hii?
Veronica asked 2 years ago

Bwana Yesu asifiwe sana,

naomba ushauri katika hili!
Mimi ni binti, nimeokoka nampenda Yesu, Nimetokea kuwa na mazoea na kijana mmoja tumekuwa marafiki wa kawaida tukiwasiliana kwa simu wakati mwingine akija kunitembelea ofisini kwangu! Huyo kaka nimemsoma baadhi ya vitu anaonyesha kuwa anataka kunichumbia ila anaogopa kunambia nilivyomuona, ila na mimi ninampenda kusema ukweli! tatizo yeye hajanitamkia kama ananipenda! Wapendwa naomba ushauri wenu nifanye nini katika hali kama hii!
Nni kwamba namuota sana ndotoni!
Naomba ushauri !

1 Answers
Benny answered 2 years ago

Ushauri wangu kwako,
Kama huyo amaeokoka na kama ana nia ya kukuchumbia kweli atakuambia ukweli. Watu waliookoka ni wajasiri. Atakueleza kusudi lake. Lakini kama hajaokoka jihadhari sana na mtego huo.
Kumuota sana ndotoni yaweza kuwa ni kwa sababu unamfikiria sana. Mara nyingi ndoto huja kwa sababu ya mawazo mengi. Hivyo kumuota sana ni uthibitisho kwamba unamuwazia sana.
Kitu cha kufanya endelea kumuomba Mungu ili jambo hilo lijidhihirishe wazi. Pia wakati huu angalia usije jirahisi sana kwake. Shikilia msimamo wako wa wokovu. Pia waweza kumueleza wazi pia kwamba kukutembelea ofisini kwako kunaweza kusababisha uambiwe kwamba wewe ni mzembe kwa sababu mara nyingi unakuwa unaongea na wageni na hufanyi kazi. Hata kama ni ofisi yako mwenyewe kuja kwake hapo kunaweza kukuharibia sifa na kuwafanya watu waanze kukusema vibaya. Utaharibu ushuhuda wako. Akija mtu ambaye anayetaka kukuchumbia kweli kweli anaweza ambiwa kwamba wewe hujatulia kwa sababu wanaume wanapishana hapo ofisini kwako. Si unajuwa tena watu wanavyotumika vibaya!
Kwa ufupi: Chukuwa tahadhari zote za kiroho kwa kuvaa silaha zote za Mungu. Efeso 6:11-12.
Yesu Kristo akutunze!

Your Answer