FAHAMU YAFUATAYO KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI UFANIKIWE KIMAISHA

FAHAMU YAFUATAYO KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI UFANIKIWE KIMAISHA.

*NA MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE*

*DODOMA UWANJA WA BARAFU*

*2 APRIL 2017*

*LENGO: KUIMARISHA UHUSIANO WAKO NA MUNGU KATIKA KRISTO YESU ILI UFANIKIWE KIMAISHA*.

Somo hili litatoa majibu ya Maswali ya watu wengi kadri Mungu atakavyotusaidia.

Hili somo halipatikani kirahisi rahisi na miaka ile tulivyooanza tulipata shida sana. Na hata vitabu havipo vingi sana vinavyoeleza mambo ya ndoto . Kwa hiyo twende pamoja.

*Jambo la 1.* *_Shetani anaweza kutumia ndoto kupandikiza vitu kwako ambavyo usipoving’oa vinaweza kwamisha maisha yako_*

_Ndipo huyo Elifazi, Mtemani, akajibu na kusema, Basi, nililetewa neno kwa siri, Sikio langu likasikia manong’ono yake. Katika mawazo yaliyotoka *katika maono ya usiku*, Hapo usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu. Hofu iliniangukia na kutetema, Iliyoitetemesha mifupa yangu yote. Ndipo pepo ilipita mbele ya uso wangu; Na nywele za mwili wangu zilisimama. Hiyo pepo ilisimama kimya, nisiweze kutambua sura zake, Mfano ulikuwa mbele ya macho yangu; Kulikuwa kimya, nami nilisikia sauti, ikinena,_ *AYUBU. 4:1, 12-16*

Maana ya maono ni ndoto na ndio maana maandiko yanasema

_Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. *Katika ndoto, katika maono ya usiku,* Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;_ *AYU. 33:14-15*

Hapa kuna vitu vinne yaani kuna

1 wazo liliingia ndani yake kwa ndoto

2 katika masikio iliingia sauti iliyoharibu usikivu wake

3 Hofu ilimwingia

4 Mifupa yake ikaanza kutetemeka

Na kuonesha kitu kilichokuja kwake na aliona pepo lililoingiza vitu ndani yake. Tangu siku hiyo hivyo vitu vilimsumbua sana kama hakupata msaada wa kuving’oa basi vilivuruga maisha yake.

Angalizo. Usiipuuzie ndoto unayo ota maana inaweza tumika

Kukuletea ujumbe wa Mungu
Kukuletea Maonyo
Au shetani anaweza pandikiza vitu.

*MFANO WA PILI*
_Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda BWANA, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. Tembeeni kwa kumfuata BWANA, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye._ *KUMBU KUMBU. 13:1-4*

Ndoto inaweza tumika na shetani
1.kupandikiza unabii wa uongo kwa kutumia ishara.

2.Wanapewa uwezo wa kushawishi watu wasimfuate Mungu katika Kristo Yesu.

Mara nyingi hatakuja na ndoto atakuja na ishara na utampokea kwa sababu ya ishara au muujiza. Na yeye ataleta na ujumbe na itakuwa ngumu sana kwako kukataa kwa sababu umeona ishara au muujiza . Na lengo kubwa ni kuwa uache kumfuata Mungu na kumpenda Mungu kutapoa na utapoteza hofu ya Mungu

Unapoteza kuambatana na Mungu.

Unatopeteza kusikia Mungu anachosema na utaanza kupotea na utaanza kusikia neno la mtumishi zaidi bila kufuata neno la Mungu. Na wengi wamekwama hapo.

Watumishi wameacha kumtumikia Mungu kwa sababu waliota ndoto na kuna vitu vilikuja na mbwembwe na wakidhani ni Mungu kumbe sio

*MFANO WA TATU.*
_Nimesikia waliyoyasema manabii wanaotabiri uongo kwa jina langu, wakisema, *Nimeota ndoto; nimeota ndoto.* Je! Mambo hayo yatakuwa katika mioyo ya manabii wanaotabiri uongo hata lini, manabii hao wenye udanganyifu katika mioyo yao wenyewe? Wanaodhania ya kuwa watawasahaulisha watu wangu jina langu kwa ndoto zao, wanazomhadithia kila mtu jirani yake, kama vile baba zao walivyolisahau jina langu, kwa ajili ya Baali._ YEREMIA. 23:25-27 SUV

*Hapa unaona ndoto ilipandikiza*
1.Unabii wa uongo

2.Udanganyifu moyoni mwake

3.Alipewa nguvu ya kushawishi watu wa Mungu walisahau jina la Mungu, jina linawakilisha heshima, uwepo au mamlaka aliyonayo mwenye jina kwako.

Mtu akikusahaulisha jina la Yesu.
Hujali tena neno la Mungu
Hutaona thamani wa uwepo wa Yesu.
Hutakuwa na heshima kwa Yesu

Na chanzo cha haya ni ndoto, na anahadhia watu ili kupandikiza kitu ndani ya mioyo ya watu ili wakae mbali na Mungu.

_Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema BWANA._
YEREMIA. 23:28

_Kisha akawaambia, Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, BWANA, nitajifunua kwake katika maono, Nitasema naye katika ndoto._
HESABU 12:6

Ndoto ni njia moja wapo Mungu anatumia kuwapa unabii watu. Na shetani nae anaiga na analeta manabii wa uongo, waalimu na mitume wa uongo.

Kuna manabii wa kweli Mungu anasema nao na kuna nabii wa uongo ambao shetani anaweka.

Pia hii itakusaidia kuchukua *tahadhari na kuweza kutofautisha*. Mambo haya yanahitaji ufutailiaji wa Karibu

Na nilipoanza kufundisha hili somo nimepata kuona ndoto nyingi sana na watu wengi sana wanauliza. Na bado naendelea kufuatilia

Mungu alianza kusema na mimi miaka ile ya 80 na ilinisukuma kufuatilia sana ndoto na wakati ule sijaokoka nilienda kwa waganga na walinipa tafsiri lakini sio kwa usahihi. Ndipo baada ya kuokoka Neema ya Mungu ilianza kunifundisha kwa hatua kwa hatua kwa muda mrefu kidogo ndipo sasa nilianza kufundisha..

*MFANO WA NNE.*
Kuna mtu aliniandikia kuwa kaota ndoto kuna mtu anakata kwa kisu kidole cha gumba cha mguu wa kulia na baada ya kuamka nilianza kusikia maumivu. miezi 3 baadae kidole kikaaza kuweka weusi pale alipokatwa na palikuwa peusi na kuanza kuwasha na hadi aliponisikia nikifundisha ndipo alianza kuchukua hatua

*MFANO WA TANO*
Naomba niombee niliota nang’atwa na mbwa mkono wa kushoto na sasa naanza kusikia maumivu hadi kwenye bega na nasikia ganzi.

*MFANO WA SITA*
Niliota nyoka kaingia mguu wangu wa kushoto na mguu wukaanza kupata shida alipata ganzi na akiingia kwenye maombi tumbo linajaa na kufura

*MFANO WA SABA*
Kuna mtu alianidika kuwa anaota mara kwa mara akiteleza kuangukia kwenye shimo au maji na mguu huo ndio anateleza kwanza .

Baada ya miezi kadhaa ule mguu ambao ndio unatanguliza ulipata shida na ndipo aligundua kuwa unakidonda..

Mwingine aliota kameza buibui na baada ya muda alianza kukohoa na kazunguka kila hospital ili kutafuta dawa kwa sababu kifua kinamsumbua na haponi. Baada ya kusikia somo hili ndipo alianza kuhusianisha na ndoto aliyoota na akatuandikia

ushuhuda wa mama aliyekuwa na binti yake alikuwa anachemea mguu na walikuja kunisalima nilipokuwa nje ya hospitali moja hapa nchini na nilisikia kumuuliza na alinieza na alisema kaota ndoto kuwa alikuwa anacheza mpira na alipopiga mpira kwenye ndoto aliumia na alipoamka akawa anachechemea. Na hospitali walipopima hawakuona kitu.
Na nilimuombea na baada ya maombi alipona..

*Kuna hatua za kijumla za namna ya kufanya au kuomba*

1.Lazima kuomba toba kwa ajili ya mlango uliofunguka na kuruhusu ndoto kuleta mashambulizi. Kwa hiyo usijihesabie haki ili umeota ndoto na ikaleta madhara ina maana kuna mlango hapo uko wazi

Kazi ya toba ni .
i)Kuondoa uhalali kwa kiroho wa shetani kukutesa.

 1. ii) Mungu kukusaidia/kupata uhalali wa kukusaidia.

Shetani ili kukushambulia huwa anashambulia kihalali/ kwa hiyo na wewe ili kupambana nae inabidi umuondolee uhalali.

2.Nyunyiza damu ya Yesu kwenye eneo uliloshambuliwa..
Mawazo ombea fikra zako
Sikio
Mguu
Fikra
Tumbo.

Inategemea ni eneo gani. Kazi ya damu ya Yesu ni nyingi.
Damu inaongea
Damu inaondoa
Damu inasafisha.

Kuna mtu alinitumia picha kwenye whatsapp na alikuwa na alama ya kung’atwa na nyoka na meno .lazima unyunyize damu ya Yesu hapo. Na sumu hiyo iondolowe hata kama sio ulimwengu wa mwili basi ulimwengu wa roho .

Damu inakomboa
Damu inazuia
Damu inafungua

3.Kemea roho za kipepo zilizoingia na mifupa ilivyotetemeka.

Limejifunua kwa picha ipi. Mfano yule wa nyoka kemea pepo la nyoka.
Buibui kemea bui bui au wanyama kemea kila picha ni roho.

Kama usipoona picha angalia kazi iliyofanyika kama unajiona umekufa kemea roho ya mauti.

4.Omba Mungu akuponye maeneo yote yaliyopata madhara kwa kupitia ndoto hiyo.

Mawazo Mungu aponye.
Hofu Mungu aondoe hofu na akupe amani.

Na Mungu atakupo6nya katika eneo ulilopata shida..

Mwingine aliona nyoka kaingia kwenye biashara na hakumtoa nyoka na baadaa yaa pale business ikafa.

Na mama mmoja aliota ndoto nyoka kapita tumboni kwake na ndoa yake ilipata shida

Na kuna mtu aliotaa mtu kachukua pochi ndogo ndani ya begi na alipoamkaa ile pochi haijarudi. Na alipoenda ofisini alibadikishiwa kazi na alishwa cheo. Yamkini alisema ntaomba kesho na usiku tu kufika asubuhi Tayari mambo yamebadilika

Watu wanota wanakula vitu na watu waliokufa.. na zoezi lilifanyika kuombea hali hiyo.

Si kila kula kwenye ndoto ni ishara mbaya.

Unakila na nani wapi saa ngapi na kwa ajili ya nini. Na kama wana israel walikula chakula baada ya kuabudu ndama. Kile kilikuwa ni sakramenti kwa miungu

Utakuta kama wenzio wanataka kukupeleka kwenye agano wanakupeleka kula chakula ambacho hakijakaa vizuri kwenye ndoto ..

Pia unaweza andika ndoto yako na kuituma ili iombewe na utampa mhudumu au andika kwa msg kwa namba za huduma.

Chukua namba hizo na andika ujumbe wa msg kwenda namba hizo kwenye link hii. http://www.mwakasege.org/kuchangia.htm

Au andika barua pepe angalia katika link hii. http://www.mwakasege.org/mawasiliano.htm

Pia nenda kwenye ukurasa wa Facebook na andika kwenye *inbox* https://web.facebook.com/Christopher-Diana-MwakasegeMana-M…/

Hakikisha unampata huyu Yesu hakiisha unaokoka na unakuwa na mahusiano mazuri na Mungu. Wokovu sio dini mpya bali unajenga uhusiano wako na Yesu.

Bonyeza maandishi haya kuungana na sala iliyofanyika uwanjani.

http://www.mwakasege.org/mafundisho/okoka.htm

Baada ya hapo soma kitabu cha Hongera kwa kuokoka.

http://www.mwakasege.org/mafundisho/hongera/utangulizi.htm

 

*SIKU YA PILI*

 

*SEMINA YA NENO LA MUNGU DODOMA UWANJA WA BARAFU*

*NA MWL MWAKASEGE*

*FAHAMU YAFUATAYO KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI UFANIKIWE KIMAISHA*

*TAR 3 APRIL 2017*

LENGO ni kuimarisha mahusiano yako na Mungu katika Kristo Yesu

Kuna mambo 2 ambayo yanaweza kutumika katika NDOTO

*JAMBO 1*
Shetani anaweza kutumia NDOTO kupandikiza mambo ambayo usipoyang’oa mapema yataharibu maisha yako

*JAMBO 2*
Kutazama ishara zitakazo kuonyesha kuwa NDOTO zinahitaji kufuatiliwa

*ISHARA*
1. Kujisikia kufadhaika moyoni kwa ajili ya NDOTO uliyoota

Kufadhaika maana yake ni mahangaiko unayoyapata ndani ya Moyo wako( kuutibua moyo)

_Mwanzoni 41:1-8″…… 8. Hata asubuhi roho yake IKAFAIDHAIKA akapeleka watu kuwaita waganga wote wa misri …_

Usifanye kosa kudharau NDOTO yoyote utakayoota Ukasema kumbe ni ndoto tu, inabidi kuifuatilia _Mwanzo 41. 7 b”Basi Farao akaamka , *kumbe ni NDOTO tu*._

_Mwanzo 40:5-6 “Wakaota ndoto wote wawili, kila mtu ndoto yake usiku mmoja, kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri waliofungwa gerezani. Yusufu akawajia asubuhi, akawaona *wamefadhaika*._

Yusufu aliwaona wote wawili mnyweshaji na mwokaji wote WAMEFADHAIKA

Mfadhaiko huja kama alarm,maana ukishaitega alarm ikilia lazima ushtuke.

 1. Kuota NDOTO hiyo zaidi ya Mara moja au inayofanana na hiyo
  Mwanzo 41:25-32
  Mst 32″… _*Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi*_.

Unapoota Mara 2 au zaidi ni kukutaarifu unatakiwa kuifuatilia hiyo NDOTO
*Ayubu 33:14-15*
_Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, *Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali*. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;_

Usipoifuatilia ndipo Mungu huirudisha Mara ya 2 au zaidi hadi utakapopata ufahamu wakulifanyia kazi

Jiulize kama Mungu katumia NDOTO kusema na wewe kwa nini iwe vigumu kuelewa maana yake

_Warumi10:17 Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa *neno la Kristo*._

Ukiwa na Neno LA Mungu lazima utaisikia sauti yake.

Mfano ukiwa na gari ni vema kujua baadhi ya vitu ili likipata shida uweze kulitengeneza sio lazima kila kitu unapeleka garage. Vivyo hivyo kwa watumishi, sio lazima kila tatizo lako unalipeleka kwa watumishi mengine yatatue mwenyewe Yale unayoona huyawezi ndio yapeleke huko, unapotaka kumweleza *Mtumishi jambo lako sikiliza Amani Ya moyo wako kwanza*

 1. Ndoto uliyoota kukutia hofu
  Daniel 4:5 na Ayubu 4:12-14

_Nikaota ndoto iliyonitia *hofu*; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa changu, zikanifadhaisha._
*DAN. 4:5*

_Basi, nililetewa neno kwa siri, Sikio langu likasikia manong’ono yake. Katika mawazo yaliyotoka katika maono ya usiku, Hapo usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu. *Hofu* iliniangukia na kutetema, Iliyoitetemesha mifupa yangu yote._
*AYU. 4:12-14*

 1. Ukiwa mambo uliyoota kwenye ndoto yanatokea katika mwili
  Ayubu 4:12-16??

Mfano
Ukiona umeota ndoto unakemea na ulivyoshtuka bado unakemea( fuatilia)

Au ulikuwa unalia kwenye ndoto na umeamka unakuta macho yana machozi pia fuatilia

 1. Ndoto kukunyima usingizi
  Daniel 2:1

_Hata katika mwaka wa pili wa kumiliki kwake Nebukadreza, Nebukadreza aliota ndoto; na roho yake ikafadhaika, *usingizi wake ukamwacha*_. *DAN. 2:1*

 1. Kwa na hamu ya kutaka kujua tafsiri ya hiyo ndoto
  Mwanzo 40:7-8,41:7-8

_Akawauliza hao maakida wa Farao, waliokuwa pamoja naye katika kifungo, nyumbani mwa bwana wake, akisema, Mbona nyuso zenu zimekunjamana leo? Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Kufasiri si kazi ya Mungu? Tafadhalini mniambie.MWA. 40:7-8 SUV_

_Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka, kumbe! Ni ndoto tu. Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo.MWA. 41:7-8_

Mstr 8 – alitaka kujua ndoto ile ilimaanisha nini

Ndoto ya Farao ilibeba maisha ya miaka 14 ya dunia nzima,kama angepuuzia sijui ingekuwaje kwa hiyo miaka 14. Kwa hiyo ule msukumo aliokuwa nao ndio ulisaidia utafsiriwa

 1. Ndoto uliyoota kukuletea mahangaiko moyoni mwako juu ya Imani na utumishi ulinao kwa Mungu

_Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda BWANA, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. Tembeeni kwa kumfuata BWANA, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.KUM. 13:1-4_

Usimwogope mtu Bali mwogope Mungu

Usikubali jina au huduma yako ivume kuliko jina la Yesu

*Mfano*: Punda aliembeba Yesu alitembea juu ya nguo kwa sababu tu alikuwa kambeba Yesu lakini baada ya kumshusha Yesu alitembea chini kama kawaida. Dhamani uliyonayo ni kwa sababu unae Yesu ndani yako

 1. Ukiona uliyoyaona kwenye ndoto yanapinga au ni tofauti ya mipango uliyonayo

Ayubu 33:14-17
_Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao, Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi;AYU. 33:14-17_

Unaweza kuota ili upangue kile kibaya ambacho kinaweza kutokea mbele,hivyo anapozungumza nawe anakusaidia usijeingia kwenye matatizo Fulani au kukuondoa katika mawazo uliyonayo

 1. Kusikia msukumo moyoni wa kusimulia ndoto uliyoota
  Mwanzo 37:5-11( Pale Yusuph alipowasimulia ndugu zake ndoto aliyoota)

Mathayo27:19 _Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, *Usiwe na neno na yule mwenye haki; kwa sababu nimeteswa mengi leo katika ndoto kwa ajili yake*._

Unaweza kuota ndoto kwa ajili ya mtu mwingine hivyo pale unapopata msukumo moyoni wa kumwambia we mweleze ila omba hekima, na kibali kutoka kwa ROho Mtakatifu

 1. Kusikia msukumo moyoni wa kuandika ndoto uliyoota

_Habakuki 2:2-3 BWANA akanijibu, akasema, *Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao*, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.HAB. 2:2-3_

Unaandika kwa sababu unaweza kuisahau asubuhi au kwa ajili ya kufuatilia huko mbeleni

Uwe unaandika ndoto zakusaidia baadae
Note:Kama huwa unasahau ndoto unazoota weka daftari na kalamu karibu ili unapoota tu uwe unaziandika na baadae iwe rahisi kuzifuatilia hatua kwa hatua.

 1. Ukiwa umesahau ndoto uliyoota ila moyoni unajisikia msukumo wa kutaka kujua

Daniel 2:1-5
Baada ya Nebkadreza kusahau ndoto Daniel alienda kumweleza hiyo ndoto tena

Ukiota ukasahau jitahidi kuifuatilia kwani ktk ulimwenngu wa roho imerekodiwa km ile ya Nebukadreza.

MAOMBI
Toba kama kuna mojawapo ya ishara hizi 11 hukuzifuatilia( kwa kujua au kutojua) Mungu arudishe hizo
Ndoto ili aseme nasi tena haijalishi muda gani umepita
Bwana Yesu Asifiwe. Tunawakaribisha kwenye semina inayoendelea Dodoma mjini katika uwanja wa barafu. Semina imeanza jana tarehe 2 April itaendelea hadi jumapili tarehe 9 April.

 

*SIKU YA TATU*

 

*SEMINA YA NENO LA MUNGU DODOMA UWANJA WA BARAFU*

*FAHAMU YAFUATAYO KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI UFANIKIWE KIMAISHA*

*NA MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE*

*4 APRIL 2017*

*LENGO: KUIMARISHA UHUSIANO WAKO NA MUNGU KATIKA KRISTO YESU ILI UFANIKIWE KIMAISHA*.

Jana tulipitia mambo mawili

*JAMBO 1*
Shetani anaweza kutumia NDOTO kupandikiza mambo ambayo usipoyang’oa mapema yataharibu maisha yako

*JAMBO 2*
Kutazama ishara zitakazo kuonyesha kuwa NDOTO zinahitaji kufuatiliwa

*Jambo 3*
Tumia viashiria vilivyokuja na ndoto ili kujua ikiwa umeiombea hiy Ndoto na kuifuatilia ipasavyo

VIASHIRIA- Imetoka katika Neno ishara

_Marko 16:17 *Na ishara hizi* zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;_

Ishara haziji peke yake huwa zina ambatanishwa na kitu Fulani
Kutoka 4:1-8
_Mstr 8… Basi itakuwa, wasipokusadiki, *wala kuisikiliza sauti ya ishara ya* kwanza, wataisikiliza sauti ya *ishara ya pili*._

Ishara zina sauti
Musa aliambiwa kwa ishara ya kijiti kilichokuwa kinaungua bila kuteketea

Ishara ilikuwa kama kibao ili kuelekeza kuwa hayo yaliyosemwa ni kweli

Ndoto lazima zije na viashiria ili uzifuatilie,ishara ndani yake imebeba msukumo wa kitu fulani

_Daniel 4:4-7 Mimi, Nebukadreza, nalikuwa nikistarehe katika nyumba yangu, nikisitawi katika nyumba yangu ya enzi. Nikaota *ndoto iliyonitia hofu;* mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa changu, zikanifadhaisha. *Basi nikatoa amri kwamba wenye hekima wote wa Babeli, waletwe mbele yangu, ili kunijulisha tafsiri ya ndoto ile.* Ndipo wakaingia waganga, na wachawi, na Wakaldayo, na wanajimu; nikawahadithia ile ndoto; wao wasiweze kunijulisha tafsiri yake._

Katika Ndoto ya Nebukadreza ilibeba mambo 4
1. Hofu
2.Mfadhaiko
3. Msukumo wa kupata tafsiri
4. Msukumo wa kuisumulia

Nia ya Nebukadreza ilikuwa ni kutafuta Tafsiri ya hiyo ndoto. Hizo Ishara 4 zilikuja kwa msisitizo ili kumfanya atafute maana yake ndio maana alitafuta watu mbalimbali kumtafsiria

Ukiona umeota ina ishara zaidi ya 1 ujue ina mzigo na inabidi uifuatilie
Daniel 4:6-7( hapa aliota ndoto) ??

thenDaniel 20-26( alipewa Tafsiri ya ndoto) _Ule mti uliouona, uliokua, ukawa na nguvu, urefu wake ukafika mpaka mbinguni, na kuonekana kwake mpaka dunia yote; ambao majani yake yalikuwa mazuri, na matunda yake mengi, na ndani yake chakula cha kuwatosha wote; ambao chini yake wanyama wa kondeni walikaa, na ndege wa angani walikuwa na makao yao katika matawi yake; ni wewe, Ee mfalme, uliyekua, na kupata nguvu; maana ukuu wako umekua na kufika mpaka mbinguni, na mamlaka yako yamefika mpaka mwisho wa dunia_.

_Tena, kwa kuwa mfalme alimwona mlinzi, naye ni mtakatifu, akishuka kutoka mbinguni, akisema, Ukateni mti huu, mkauangamize; ila kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya kondeni; kikatiwe maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na wanyama wa kondeni, hata nyakati saba zipite juu yake; tafsiri yake ni hii, Ee mfalme, nayo ni amri yake Aliye juu, iliyomjia bwana wangu, mfalme; ya kuwa utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni, nawe utalazimishwa kula majani kama ng’ombe, nawe utatiwa maji kwa umande wa mbinguni, na nyakati saba zitapita juu yako; hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa yeye amtakaye, awaye yote. Na kwa kuwa waliamuru kukiacha kisiki cha shina lake; ufalme wako utakuwa imara kwako, baada ya wewe kujua ya kuwa mbingu ndizo zinazotawala._

27- ( alipewa ushauri wa yapi ya kuyafanya)

_*Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha.*_

*NOTE*

⏩Watu wengi wanakuwa na hamu ya kutafsiriwa ndoto bila kutaka kusikiliza ushauri uliopo ktk hiyo ndoto

⏩Tafsiri ya ndoto ina vitu 2
*1. Ujumbe*
*2. Ushauri*

Ni vema uvipate vyote sio kimoja. Nebukadreza alichukua *Tafsiri akaacha ushauri*

*Jambo la 3* katika ndoto ya Nebukadreza. Daniel alipata kiashiria kama cha Nebukadreza ( mfadhaiko). Daniel alipopewa taarifa ya Ndoto ndani yake ilimtibua

⏩Daniel alitaka ajue
1. Yaliyokusudiwa ndani ya Ndoto yatatokea. Mfano kuna watu wanaoota mambo na baada ya muda yanatokea ,usifurahie hizi ndoto huwa ni taarifa ili kama ni mbaya uipangue mapema au kama nzuri uiombee. Una uwezo wa kuibadili Yale yaliyoonekana ktk mst 27

Mst 28″…. _*Hayo yote yakampata mfalme Nebukadreza*._

Kama Nebukadreza angefuata ushauri aliopewa na Daniel yasingemkuta hayo kwani alipewa allowance ya miezi 12 ya kutengeneza ila hakuyafuata na baada ya hiyo miezi 12 yakampata ya kukaa kondeni na wanyama miaka 7,
soma Daniel 4:31-33 _Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee mfalme Nebukadreza, maneno haya unaambiwa wewe; *Ufalme huu umeondoka kwako. Nawe utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni; utalishwa majani kama ng’ombe, na nyakati saba zitapita juu yako, hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yote. Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadreza; alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng’ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege.*_

⏩Kuna gharama za kupuuzia ushauri unaopewa ,ona yaliyomkuta Nebukadreza aliishia kutolewa ufahamu wake na kuishi porini na wanyama

?Ndoto aliyoota kwa muda mfupi aliipuuzia kwa miezi 12 na ilimtesa maisha yake kwa miaka 7

⏩Mungu alikiacha kiti cha Nebukadreza kwa miaka 7 bila kiongozi ili ajue kunae Mungu wa mbingu na nchi. Soma mstr 4: 34-37

_Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadreza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi; na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe? Basi wakati uo huo fahamu zangu zikanirudia, na kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu, enzi yangu na fahari yangu zikanirudia; na mawaziri wangu, na madiwani wangu, wakaja kunitafuta; nami nikathibitika katika ufalme wangu, nikaongezewa enzi kupita kiasi. Basi mimi, Nebukadreza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili._

 1. Unapo ikumbuka kuifuatilia ndoto mara kwa mara au unapoimbea na ukaona viashiria haviondoki ujue kuna jambo ndani ya ndoto inahitaji kuifuatilia

⏩Mfaidhaiko wa Nebukadreza sio wake ni ndoto aliyoota

⏩Unapopata mzigo wa kumuombea mtu kuombea *ombea saa hiyohiyo* usisubiri kumhadithia mtu hadi upate kibali,unaweza muhadithia ndio ukamvuruga zaidi.

⏩Unaweza kuta umeingizwa kwenye maagano ya ukoo ukawa unaomba bila mafanikio,inabidi ufanye maombi ya kujitoa kwenye hayo maagano kwa kulifuta jina lako kwa Damu ya Yesu ,usiwe kama wale wanaosema *”Ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya”* ni lazima ujitoe kwenye hayo maagano maana huwezi jua wanamtumia mungu gani unajikuta mambo yako hayafanikiwi kumbe umeunganishwa na maagano

Kuna mtu aliota kang’atwa na nyoka ktk ndoto na alivyoamka akajikuta damu inatoka sehemu hiyo. Hivyo alikuwa kaachiwa roho ya mauti na ile sumu iliharibu maisha yake kabisa kwani familia yao ilikuwa imeingia ktk maagano hivyo ingawa alikuwa kaokoka hakufanikiwa kwa sababu yalikuwa na uhalali nae

*MAOMBI*

?Fanya Toba

?Ita Damu ya Yesu itakase popote ambapo uling’atwa na ng’e,mbwa,nyoka, mende n.k katika ndoto ili kukuondolea uhalali wa shetani kukutesa

?Tubu kwa kuachia mlango uliochilia mashambulizi ambayo yanamiliki mwili wako

?Futa sumu yoyote iliyoachwa kupitia ndoto na ondoa jina lako kwenye maagano kwa kujua au kutojua kwa jina la Yesu

Amen na ubarikiwe sana._

 

*SIKU YA NNE*

 

SEMINA YA NENO LA MUNGU DODOMA UWANJA WA BARAFU NA MWL MWAKASEGE*

SOMO: *YAFAHAMU YAFUATAYO KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI UFANIKIWE KIMAISHA*

LENGO: _kuhakikisha uhusiano wako na Mungu unaimarishwa ,pia tuendelee kumtegemea yeye katika mafanikio_

Jambo 1,2 na 3 (tumeyaona kwenye masomi ya siku zilizopita Leo tuendelee na Jambo LA NNE)

*JAMBO 4*
Imarisha IMANI yako inayohusu kutumia Damu ya Yesu ili ikusaidie kushughulikia Ndoto zilizobeba vitu vinavyokwamisha maisha yako

⏩Tofauti katika kuombea Ndoto ni ile imani uliyonayo kwenye Kutumia Damu ya Yesu
⏩Ndoto pia huwa zina vipindi vyake, unapoota ndoto angalia muda uliyoota ndoto hiyo na chiki huwa unaota muda gani. *Kuna vipindi 4 vya muda – SAA 1-3, SAA 4-6, SAA 7-9 na SAA 10-12*
check ndoto zako unaota ktk kipindi gani

Waebrania 11:1,10:17
⏩Imani chanzo chake ni kusikia sio Neno. Ni lazima usikie kwanza .Unaweza kusikia ila usisikie na unaweza kusikia na usielewe

Yakobo 2:20,26
20″… Imani pasipo matendo haizai
26″… Imani pasipo matendo imekufa
Unaweza kuwa na Imani na isikusaidie kitu
⏩Wakristo wengi wana Imani ya Damu ya Yesu ila wengi hawana Imani katika kuitumia hiyo Damu ya Yesu.
✍✍
*HATUA ZITAKAZOWEZA KUIMARISHA IMANI YAKO*

*HATUA 1*
_Uwe na Mistari ya Neno la Mungu katika Biblia juu ya Damu ya Yesu_
Kutoka12:21-23 na 12:12-13, 1 kor 5:7
Unapotumia na mstari katika Agano la kale uwe na unaofafana nao katika agano jipya. Tafuta mstari utakaokupa uhalali wa kuitumia katika MAOMBI yako.

*HATUA 2*
Tafakari hayo maneno?? hadi uone ile Waebrania 11:1 na Yakobo 2:20 itokee moyoni mwako

⏩Mistari ya HATUA ya kwanza ina mambo yatarajiwayo. Mungu aliwaambia wana Wa Israel watapona tu kwa sababu ya Damu ikiwepo juu ya miimo ya milango yao, nao waliyasikia hayo na kupata uhakika wa kuwa yaliyosemwa yatatokea

Yakobo 2:20
Imani pasipo matendo haizai
⏩Suala la kuweka kwenye matendo ni la muhimu sana katika utumiaji wa Damu ya Yesu. Musa nae aliweka kwenye matendo kwa kutii ndio maana hawakuangamizwa ( Kutoka 12:21-23)

*HATUA YA 3*
Wana wa Israel kushiriki kwa matendo kuitumia Damu ya Pasaka ili Mungu aweze kuitumia kama wao walivyoitumia.

*Kumbuka:* Mungu haitumii Damu ya Yesu ambayo wewe huitumii ni lazima kwanza uikubali kuitumia ndipo naye ataitumia kama waisrael walivyofanya huko Misri

⏩Mungu anatazama Damu uliyoitumia kwanza kwani inaonyesha Imani yako ipoje

⏩Mungu hutafuta Damu iliyofanyika Ishara ili yeye naye aone Imani yako

⏩Mfano : kuna tofauti ya kupanda bus na kujifunza kuendesha bus, hii itakusaidia hata dereva akishindwa kuendesha wewe unaweza kuendesha. Hiyo pia ipo ktk utumishi wetu kuna watu wanajua kuombewa tu ila kujiombea hawawezi.
Mfano mwingine ni pale unaponunua simu itategemea unataka kuijua kwa kiwango gani, kama unataka kujua kupiga na kupokea uwezo wako utaishia hapohapo. Hivyo kama una kiu ya kutaka kujua zaidi utajifunza zaidi ili kupanua uelewa wako

⏩Vivyo hivyo kama Damu ya Yesu unaitumia kwa ajili ya kwenda mbinguni tu au kujifunika tu, itaishia kufanya kazi hiyohiyo unayoiamuru, ila kumbuka Damu ya Yesu inatumika popote unapoihitaji alimradi uwe na imani katika kuitumia.
Kumbuka Damu ya Yesu unaweza kuimwaga, inanyunyuziwa pia unaweza kunywa hivyo usikariri kazi moja tu,

⏩Kama hulitumii Jina au Damu ya Yesu jua nae Mungu hatalitumia kwako.

NB:
Kuna walioota wakifanya mapenzi kwenye ndoto, wengine wakifunga ndoa ktk ndoto au unakuta upo kwenye ndoa ila unaota unafanya mapenzi na mke/ mumeo hizo ndoto sio nzuri. Kwani unakuwa tayari umeingia katika Agano la kwanza katika ulimwengu wa roho. Ndio maana unakuta binti au kijana wanachelewa kupata wenzi kwani wanakuwa tayari wameshaingia Agano ktk ulimwengu wa Roho. Au ndoa INA mafarakano au zinavunjika kwa ajili ya hayo maagano. Hapo inabidi uitumie Damu ya Yesu ili uvunje hilo Agano la kwanza

*MAOMBI*
⏩. Kama umeota hayo?? shika kitovu chako alafu ingia kwenye:
?
*1.* Toba, rehema na utakaso.
Tubu popote ulipoacha mlango hadi hiyo roho ya uzinifu ikaingia kwako, pia Toba kwa ajili ya UOVU wa wazazi wetu vizazi vya nyuma
*2.* Ondoa Agano la kwanza kwa kutumia Damu ya Yesu
*3.* Jitenge na huyo uliezini nae ktk ndoto na uliefunga nae ndoto , jitenge na Pete, mavazi, zawadi,nk. kwa Damu ya Yesu

*4.*Pia tulifanya MAOMBI ya kujiweka WAKFU kwa Bwana
– Wakfu Nafsi,mwili na roho
– Uongozwe na Bwana ktk mambo yako
– Usonge mbele kimwili na kiroho
– Utumie mapenzi ya Mungu katika maisha yako na sio akili yako.
??
*Amen*

 

 

 

 

 

 

*SIKU YA TANO*

 

*SEMINA YA NENO LA MUNGU DODOMA UWANJA WA BARAFU NA MWL MWAKASEGE*

SOMO *FAHAMU YAFUATAYO KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI UFANIKIWE KIMAISHA*

*TAR MARCH 6, 2017*
Lengo ni kuimarisha uhusiano na Mungu ili umtegemee na kumtumini ili yakisaidie.

Baada ya semina Mungu akusaidie kukupa maarifa ya ndoto na uelewe.

Jambo la 5.Vijue vyanzo vya ndoto ili ujue kuviombea ipasavyo.
Ni rahisi kufuatilia na kuombea ndoto ambayo unajua chanzo chake.

1.Chanzo cha kwanza ni Mungu.

Usingizi mzito

2.Shetani..
Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda BWANA, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. Tembeeni kwa kumfuata BWANA, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.
KUM. 13:1-4 SUV
Haijalishi ndoto ina mbwembwe kiasi gani au ishara kiasi gani kuna zingine sio za Mungu. Hivyo kuwa makini sana.

3.Shughuli nyingi.
*Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi*; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno.
MHU. 5:3 SUV
-ndoto zingine huja kwa sababu ya shughuli nyingi.

4.Hali ya Kiroho ya mahali ulipolala.
_Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani. Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale. *Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa. Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia. Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli BWANA yupo mahali hapa, wala mimi sikujua. Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni.* Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake. Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu._
MWA. 28:10-19 SUV
? lile eneo lilikuwa ni madhabahu ya Mungu hapo mahali alipolala yakobo.

?jua hivi vyanzo maana itakupa mtaji wa kuomba na tutapita kwenye mifano hapa ili kuomba.

MFANO.
ndoto kutoka kwa Mungu angalia Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,
AYU. 33:14-16 SUV
http://bible.com/164/job.33.14-16.SUV

Omba Mungu akupe neema ya kusikia sio kupuuzia lakini kuna kitu kipo anataka upate. Omba Mungu akupe hiyo neema maana hataki upoteze muda.

Na omba Mungu akupe.. neema ya kujua.. kufungua masikio lengo Mungu afungue masikio yako maana mchana unaweza ukawa busy..

Omba Mungu akusaidie kusikia kilichoko ndani ya ndoto ili afungue masikio yako ya ndani. Angalia 16. Muhuri Mafundisho yao. Kama umepata Mafundisho na hujui kuwa ni ya Mungu atakuja kwenye ndoto kuthibisha au kubatilisha kwa ndoto.

Mfano kuna mtu alikuwa kaokoka na anenda mahali kupata neno la Mungu. Na alienda mahali hapo mara kwa mara na mwishoni akaamua kuhamia. Na usiku aliota ndoto Mchungaji wa mahali hapo anawaongoza kwenda porini na wakapotea njia. Na yeye alikuwa anaowaona.

Na alipoamka . Alikuja nisikia nikifundisha na akajua kuwa kuwa Mungu amkataza.

Na angali 17 .. alikuwa anamtoa kwenye makusudi yake.

Na usipuuzie ndoto na Mungu alinisukuma kulifuatilia somo la ndoto lea sababu Mungu alisema nami kwa ndoto.

Siku nataka kuacha kazi kabla ya wakati maana wito uliwaka ndani sana.. na hali hii unaweza dhaniwengine wanatania.. na elia alisema nimenaki peke yangu Mungu alimwambia kuwa wapo watu 700 Kwa hiyo usiwaze kuwa wewe tu ndio mtenda kazi.

Basi niliona watu ng’ambo wako kwenye senyenge na kuna mto na mimi niko upande mmoja. Akaja mtu mweusi ananiambia ruka ruka. Nikasema ngoja nitafute pa kupitia.

Ghafla nikaona mwamba nikasema si uneona nikapata kupitia. Na nilipoamka Roho mtakatifu akiniambia kuwa hiyo pressure ya kuacha kazi sio yangu. Tukia hadi upate pakukanyaga.

Hivyo inahitaji utulivu.

Mfano 2.
Mwanzo 41. Farao alipoota ndoto za njaa na ndoto zile haikuwa kwa taarifa bali alikiwa na maelezo ya kipindi cha maandalizi ya kuweka akiba.

Na angepuuzia ina maana dunia nzima na yeye mwenyewe angepata hasara.. na ndio maana Mungu aliweka ishara.

Maisha ya Yesu alipokuwa mdogo yamefuatiliwa na ndoto. Yusufu alipotaka kukuacha Mariam na Mungu alisema nae kwa ndoto ili asimuache. Wakati nawaza namna ya kumuacha Malaika akaongea nae. Na Yusufu alikubali.. maana haikuwa rahisi kuamino kuwa mimba ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

Quote. Herode.. na mamajusi na jinsi Mungu alivyongea nao..

Na ilipita muda herode alijua kadangangwa.

Quote. Ndoto ya kwenda misri.. tena ndoto ya kurudi misri.

Search akisha kuonywq kwenye ndoto litimie neno la kuitwa mnanazayo.

Kama angepuuzia ingukwa hasara sana.. hivyo ndoto itakusaidia kupata utulivu ndani.

Mungu alisema nami mengi sana.

Nilikuwa eneo la kijinini eneo la migomba na kuna mtu alinipeleka pale. Na mchungaji wa pale kila akihubiri wanakufa. Na akatoka na mimi niliingia na hap kanisa lote watu wamekufa na yule mtu kanipa nguo nyeupe na mimi nikaanza kufundisha watu wakaamka wote na mara 3 kwa theluthi.

Na nikaamka.

1.Nilijuq wito wangu ni kwa ajili ya kanisa na kuwqkwqmua mahali walipokwama.. ndio maana utaona. Mafundisho ya kukuwqmua.

Mfano wa ndoto Kutola lwa shetani.
Ziba lango la ndoto ili lisipitishe mambo ya shetani maana za shetani ndoto zake zinakuharibu Kutoka 12:21-23. Nanyi twaeni tawi la hisopu, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu ye yote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi. Kwa kuwa BWANA atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, BWANA atapita juu ya mlango, *wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi.*
KUT. 12:22-23 SUV
http://bible.com/164/exo.12.22-23.SUV

Waliziba kwa damu ule mlango ndio maana aliwaambia waweke damu katika vizingiti vya mioomo ya malango.

Muhimu. Damu itamila kuziba mlango na omba. Kwa damu ya Yesu Kristo nafunga mlango shetani asipitishe ndoto zake. Omba mara kwa mara.

Mungu hatumii damu iliyopo kwenye bakuli ambayo haitumiki. Weka neno kwenye matendo kwa upande wako na yeye anafanya kwa upande wake.

Ombea na wototo wake na semea neno eneo la ndoto. Ombea watu na ombea sana watoto ili shetani asipitishe vitu vyake. Na kuanza kupitisha ombea sana hili jambo.

Yule dada anazini na mtu kwenye ndoto na alikuwa anaomba na nilipoomba kwa damu ya Yesu zile ndoto zilikatika.

Na endelea kusoma ili imani yako ijenge na kristo ni pasaka wetu na inaziba.. hii ni siri sana..

3.Ndoto zinazokuja kwq sababu ya shuguli nyingi

Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake; naye alipokuwa akizipanda, nyingine zilianguka karibu na njia, zikakanyagwa, ndege wa angani wakazila. Nyingine zikaanguka penye mwamba; zilipoanza kumea zikakauka kwa kukosa rutuba. Nyingine zikaanguka kati ya miiba, na miiba ikamea pamoja nazo ikazisonga. Na zilizoanguka penye miiba ni wale waliosikia, na katika kuenenda kwao husongwa na shughuli na mali, na anasa za maisha haya, wasiivishe lo lote.
LK. 8:5-7, 14 SUV
http://bible.com/164/luk.8.5-14.SUV

Shughuli nyingi maana yake kutumia muda bila kufuata mapenzi ya Mungu. Yesu alisema sifanyi neno ila lile baba analofanya.. search kuiimiza kazi yake.

Haya sio kwa ajili ya Yesu tu bali hata wewe.. (tangu sasa hatumtabui mtu kwa ajili ya mwili…kwa ajili yake yeye.. tumesulubiwa pamoja na Kristo.. Yesu alisema mimi ni mzabibu nanyi ni matawi) search.

Matunda anayotaka.. matunda yape kukaaa.. matunda yake yanayotokana na mbegu maana Mungu ndiye akuzaae. Na anakuja kuona kama kila mwaka kama kuna mtu ana matunda na kama huzai Mungu anasema ukate.

Mungu hatazami maisha bali anaangalia matunda kila siku .wiki mwezi.. Mungu antaangalia.. search matendo yao yabawtabgulia..

Mungu anakusidia na anangalia na kuwa je unafanya.. na kuna watu wapendwa kwenye miba.. omba Mungu maisha yako yasikae kwenye miimba.. miimba imekuja kwa ajili ya adhabu.. jifuze kitembea katika toba..

Omba toba.. mahali ukifika.. Mungu akusamehe.. fanya hilo.. kila wakati.

Aliyoko kwenye miimba haivishi kitu na maana kuna mahangaiko huko.. kasome kwenye biblia. Maana yake kuna watu hawataki wakuzungike na akasemw kaa nao mbalo lakini wewe unawang’ang’ania..

Kama marafiki hawakusaidiii kaa nao mbali fika ng’ambo nyingine fika mbali.. *watakuwa miimba search)

Huwa nawaambia wanafunzi usikae na watu ambao hawasomi.. na wengine wanasema hela ya baba ipo kama hujui alipataje.. maana ulirithi tosha ni kukuambia kuwa alipate huo utajiri.. au mali.. maana mali ni fikra.

Ikawa katika kuenenda kwao aliingia katika kijiji kimoja; mwanamke mmoja jina lake Martha akamkaribisha nyumbani kwake. Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake. Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie. Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi; lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.
LK. 10:38-42 SUV
http://bible.com/164/luk.10.38-42.SUV

?Maneno magumu sana.. na fikiria unachaharika kumtumika Yesu na anasema unapoteza muda.. na niliomba Mungu anisaidia nisitumike kwa hasara..

?Unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya utumishi mwingi.. na unapomtumika Mungu una utulivu kiasi gani.. na usihangaike.. na usifutahie unavyomaliza kilomita.. je unakimbia kwenye utumishi wa kwako.

?Unajua kwanini Yesu hakuenda kumponya Lazaro, lakini yeye aliona baba yake aliona kuwa anamfufua.. japo alipelekewa taarifa.. kwa emergence..lakini hakwenda.

?Yohana 17 Yesu anasema kazi uliyonipa nimemaliza.. na mbona dodoma hajafika.. alifanya alichotumiww kufanya.. na lengo kubwa sio kuponya magonjwa bali ni kufa msalabani.

Mungu anatafuta vipaumbele na huna muda wa kufanya kila kitu. Na hakuna mwalimu atake fundisha kila kitu..

Na mungu hawezi kukupa kufundisha kila kitu. Sasa wewe umefundisha hesabu unataka kufundisha physics.. na wewe ndio utanata uonekane.. na utajimini wewe mwenyewe…

Na anasema fundisha na hili na hili huwa nasema nasubiri Mwalimu mkuu ndiye anipangie kipindi…

Na nikisema namwaga zege.. najua kabisa shetani hawezi bomoa.. kazi ya mtu itapimwa.. na jenge akisema itakuaje.

Yesu akija wakati tunajenga hema anatafuta nini, na kati kati ya semina anangalia nini.. au baada ya semina..

Na jion na asubuh omba Mungu akuongoze hatua kwa hatua.. na usifurahie njia bali hatua ambazo Mungu atakupeleka..

Na mbinguni utaenda na utumishi sahau
Omba Mungu akusaidie…

Ndoto kwa shuguli nyingi zitakuonesha na watu uliokwama nao na Mungu anasema kaa nao mbali.. na omba kwa Mungu usilale kwenye adhabu.. omba toba na Mungu analisamehe tu..

Hamna sababu ya kulala kwenye adhabu walayi damu ya Yesu ipo.. na shughuli nyingi zinakusaidia..

Anasa za dunia hii ni vile vitu vinakuvuta na sio vya Mubgu kwako.. enenda sawa sawa na wenye haki.

Mtu yeyete aliyoko kwenye utumishi na kijana aliyoa mtu na vitu visivyo vyake..

Kuna mahali ukiona utashtuka.. na utanishangaa mimi na mwakasege yuko hapa.. na kwa sababu ya nafasi niliyonayo.

Omba kwa Mungu vipaumbele vya kwako.. na vipaumbele na mke wangu nae ananfasi yake na kuombeana na na huyu abebe hiki na huyu abebe hiki.

4.Mazingira ya kiroho.
Mambo 4 muhimu
1.Ombea chumba unacholala.. funika kwa damu ya Yesu. Kama ni hotel omba toba kwa kila kilichofanyika nje ya mapenzi ya Mungu.

Nguo zinabeba roho ombea kwa damu ya Yesu.

Nilikiwa nchi moja na nilifika kwenye hotel na alikuwa anatufuatilia kila hotel tunayolala.na alikuwa analal baada ya sisi kutoka

Na akawa anasema nawahi upako, nikalala nalia usiku kucha.. na yeye atalia..

Ombea nyumba nzima.. na ombea ardhi unayolala..na kama kuna madhabahu nyingine na ombea hili jambo mara kwa mara.

Mtu mmoja alipita kwenye Ardhi anasikia vitu vinagonga chini…

Na aliomba Mungu naomba ardhi kama imebeba kitu kicho cha kwako.. na akasema naomba itapike kila kitu hapo na akatoka nyoka.

Ombea mbingu iliyoko juu maana ina sauti ya kiroho.. na Yesu alipotoka juu ya maji na mbingu zilifunika zina siri ya ajabu sana.. mbingu zinatatandaza utukufu wa Bwana.

€Ombea watu wanaoingia mahali hapo.. Tamari alipobakwa alienda mahali kwa kaka yake.. na ukiwa wa tamari ulishika kaka yake ulileta hasira ya kuua. unaua hali ya kiroho.. omba Kama Ayubu.. aliwaombea watoto wake.

Kama ni mgeni omba kwa ajili yake na vichujwe.. na ombea hili jambo.

Kama uombea nyumba yako.. hiyo hamu inaisha hata kama anavuta sigara.. na omba sana hivi vitu.

Ni vitu vya kawaisa kabisa.. na anakuja mtu kuwatembelea nyumbani na mnaanza kuota ndoto ngumu ngumu.

Walikuja watu kuniona na mtoto wakasema kuna vitu vinaruka.. na wakasema kuna vitu vinaruka na kumpiga mtoto. Na walisema mama mkwe akuja nyumbani, na alikuja na mambo yake.

Na niliwaambia kuwa either mumuwekee kikao au mwombee rehema.. na usione aibu. Mweleze ukweli.

Mtoto katoka shule kafundishwa hadi kwenda kuzimu.. na anataka kugeuza chumba chao kuwa kama lango la kuzimu. Na ujue hamtalala salama.

Funika macho yako tuombe

 

*SIKU YA SITA*

 

 

*SEMINA YA NENO LA MUNGU DODOMA UWANJA WA BARAFU NA MWL MWAKASEGE*

SOMO: *FAHAMU YAFUATAYO KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI UFANIKIWE KIMAISHA*

*APRIL 7, 2017*

Kama hukuwepo hakikisha unapata kanda na tumekwenda hatua kwa hatua. Sikiliza na sikiliza itakusaidia sana..

tembelea www.mwakasege.org kupata malelezo namna ya kupata kanda.

Jambo la

*YAJUE MAENEO MUHIMU YATAKAYO KUSAIDIA KATIKA KUFASILI NDOTO.*

?LENGO LA SOMO: Kuimarisha uhusiano wako na Mungu katika Kristo Yesu. Na usiishie kujua tu mambo ya ndoto bali uhusiano wako na Mungu uimarike.

?Katika biblia unaona Yusufu na Daniel wakifasili ndoto. Sasa sio mara zote utakutana na Yusufu au Daniel lakini ndoto utaendelea kuota hiyo. Kwa hiyo fahamu wewe mwenyewe kwa kuomba Mungu na akupe ufahamu wa kufasili ndoto na kumjua Mungu katika Kristo Yesu.

? Maeneo haya yanafanya kazi pamoja.

ENEO LA  *UWE NA KIU YA KUTAKA MUNGU AKUSAIDIE KUJUA TAFSIRI YA NDOTO HIYO.*

_Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, *Kufasiri si kazi ya Mungu? Tafadhalini mniambie*_.
MWANZO. 40:8

?kufasili ndoto ni kazi ya Mungu. Kwa hiyo na wewe jua kufasiri ndoto ni jukumu la Mungu na wewe weka Imani yako kwa Mungu ili afasiri ndoto yako

_Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, *Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.* Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa._
YOHANA. 7:37-39

Kila aliye na kiu aende kwa Yesu na sio kwa mtumishi. Japo Mungu anaweza kukufungulia mlango wa kwenda kwa mtumishi hakikisha unamtukuza Mungu. Na hakikisha imani yako hakikisha imani yako inaenda kwa Mungu.

Pia kuwa Mwangalifu na watumishi *Kumbu kumbu 13:1-4* inasema kuna watumishi wanamtumikia *mungu* lakini sio *Mungu* wa Kwako yaani katika Kristo Yesu.

_Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni._
1 WAKORINTHO. 2:10, 13

?Ndoto inakupa picha ya vitu vulivyoko Katika ulimwengu wa Roho mwenyeji wetu ni Roho Mtakatifu.

?Hakikisha unakuwa na *kiu ya kutosha*

Hapa nakufundisha namna ya kuonesha kiu kwa Mungu.

_Basi Danieli akaingia, akamwomba mfalme ampe muda, kisha yeye atamwonyesha mfalme tafsiri ile. Ndipo Danieli akaenda nyumbani kwake, akawapasha habari kina Hanania, na Mishaeli, na Azaria wenzake; ili waombe rehema kwa Mungu wa mbinguni kwa habari ya siri hiyo, ili kwamba Danieli na wenzake wasiangamizwe pamoja na wenye hekima wa Babeli. *Ndipo Danieli alipofunuliwa siri hiyo katika njozi ya usiku. Basi Danieli akamhimidi Mungu wa mbinguni*._
DANIEL. 2:16-19

?Nabukedreza aliota ndoto na alisahau na aliita watu wote wakaldayo na wachawi na wenye hekima.

?Na waliposhindwa kumkumbusha ndoto yake alitangaza kuwaua wote. Na taarifa alipelekewa Daniel. Na Daneil aliomba Kwa Mungu na akampa ile ndoto na tafsiri yake.

*Namna ya kuwa na Kiu*

*1. Tenga muda wa kuombea hiyo ndoto kwa msukumo*

Maana ilikuwa ni ngumu kwao wasingeshughulikia ile ndoto ya mfalme kwa maana Mungu wao asingejibu maombi yao wangeuawa.

?Weka msukumo ndani yako wa kutaka kuombea na weka msisitizo ndani yako ya kuomba na ndio maana *Yesu alisema kila aliye na kiu aje kwangu*. Na Roho Mtakatifu anajua siri za Mungu na atakupa kujua.

*Tenga muda wa kuombea ndoto*

?Masomo kama haya yanakusaidia usipuuzie ndoto maana Farao alitaka kupuuzia ndio maana akisema kumbe ni *ndoto tu* alidharau na alitaka kuiacha.

Kile kiashiria kilimpa kumbana na alitafuta tafsiri. Kwa hiyo unapoota ndoto mahali pa kwanza ni *kwenda kwenye maombi*.

Ndoto ikikuondolea usingizi ombea muda huo huo. Mke wa Pilato alipewa muda mfupi na hakuomba kuhusu mateso ya Yesu na hakuomba _Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na yule mwenye haki; *kwa sababu nimeteswa mengi leo katika ndoto kwa ajili yake*._Mathayo 27:19

Ukiota ndoto na unaomba kwenye ndoto endelea kuomba na wewe kama umeshtuka kutoka usingizini hiyo ni ishara ya hiyo ndoti inahitaji kushughulikiwa saa hiyo.

ENEO LA  *UWE NA NENO LA KUTOSHA LA BIBLIA MOYONI MWAKO ILI USIKIE MUNGU AKISEMA NA WEWE*

Kuna hekima ya Mungu, na mwanadamu na shetani. Maana yake kwa hekima yote *tumia neno la Mungu kwa hekima ya Mungu ili Mungu apate utukufu.*

Uwe na utaratibu wa kujijaza neno la Mungu la Kutosha moyoni mwako.

Kwa sababu Ayubu 33:14-15
_14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. 15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;_
*Ayubu 33 :14-15*

Mungu anasema kwa ndoto kwa mambo mengi..

_*Warumi 10:17* Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa *neno la Kristo.*_

_Zaburi 103:20 20 Mhimidini Bwana, enyi malaika zake, Ninyi mlio hodari, *mtendao neno lake, Mkiisikiliza sauti ya neno lake*_

?Ndoto ni neno katika picha. Hii ni tafsiri nyingine.. maana ya kwanza nilikuambia kiwa ndoto ni picha ktk ulimwengu wa Roho.

Kwa hiyo kama huna neno la Mungu huwezi kuelewa na kusikia huja kwa neno la Kristo kwa hiyo ili upate ujumbe unahitaji neno.

Ndani yako kama una kiu lazima Mungu atasema na wewe na kukuhimiza ujaze neno lake.

Hivi umewahi jiuliza kwanini hujasoma biblia yote.Maana usisingizie muda kwa sababu uko mda mwingi online whatsap na kwenye mitandao na unasema huna muda. Kwani waatumishi wanajuaje kwa sababu wanasoma neno.

Weka utaratibu soma sura 3 agano la kale na 1 agano jipya kila siku utamaliza. Au nenda kwenye simu yako weka utaratibu wa kusoma biblia mara moja kwa mwaka.

? The One Year ® Bible
http://bible.com/r/y

?Naona mtu anaota ndoto yuko chini ya mlima na unazungua huo mlima na hujajua maana yake.

Biblia inasemaje kuzunguka mlima huu umetosha.

_*Mlivyouzunguka mlima huu vyatosha; geukeni upande wa kaskazini.Kumbukumbu la Torati 2:3*_

Mungu anasema saa yako ya kutoka imefika lakini hujajua kwa sababu huna neno la kutosha.

Ndoto zingine zina ujumbe moja kwa moja

Nilipokuwa chuo SUA (wakati ule ilikuwa Faculty of Agriculture chini ya chuo Kikuu cha Dar es Salaam) Morogoro nikaota ndoto niko ndani na ikaja karatasi nyeupe ikashushwa na kunyanyuliwa juu mara tatu. Na nilishindwa kusoma na ukaja ujumbe na sauti ikasema hiki ni kitabu cha Joshua .

Na kumbuka nilikuwa sijaokoka nikamwambia Marehemu baba yangu na alisema Mungu anakumbia somakitabu cha Joshua .

Baada ya mwaka kupitia nilipokuwa nakarabia kuokokaa na nikaona katika macho haya na nikaoneshwa kitabu cha Joshua tena

Na nikaonesha na historia na Mungu akisema nani atakaye pokea koleo ya Musa . Na nguvu za Mungu zilinishukia na nikawa nanena kwa lugha nikijua naumwa nimeanza kuchangangikiwa maana nilikuwa sijui kitu cha kunena kwa lugha.

Kwa hiyo nikafunga mdomo lakini huku ndani (moyoni) nasikia Bwana Yesu asifiwe.

Nilijua hapa nimechanganyikiwa.. marehemu mama alikuwa anawahi kuja kunitazama maana alijua saa yoyote nakufa kwa namna nilivyokuwa naumwa

Na baba yangu nilipomueleza alisema Mungu kasema na wewe mwaka jana kwenye kitabu cha Joshua soma na sasa anakuuita kuanza kazi.

_2 Musa mtumishi wangu amekufa; *haya basi, ondoka,* vuka mto huu wa Yordani; wewe na watu hawa wote, mkaende hata nchi niwapayo wana wa Israeli. Yoshua 1 :2_

Na baba yangu alisema rudi chumbani kwako kaongee na Mungu niliokoka mwenyewe kitandani kwangu na si kuongozwa na mtu na nilikuja hata sijui nini maana ya sala ya toba na Mungu alinisaidia na *nikaweka agano na Mungu kuwa sitaenda kuhubiri bila uwepo wake*.

Na baada ya hapo nikasoma tena kitabu cha Joshua na nikapata ujumbe na kitu cha kifanya.

Habari za Nebukadreza .. alitaka tafsiri na hakutafuta ujumbe. Usifanye kosa hilo la *kufurahia tafsiri ya ndoto na kuacha ujumbe*.. si siuala la kusoma neno tu bali hakikisha unapata unachotafuta.

Kama ni uponyaji utaona uponyaji.. nuru neno ni taa litakuongoza, hakikisha unapata kitu cha kukusaidia katika neno.

Nimeona watu wanatafsiriana ndoto na unaona hawako sahihi.. na nagundua kuwa hawana neno la kutosha.

ENEO LA  *Omba Mungu akupe ufahamu wa kudumu juu ya ndoto*

_17 Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; *Danielii naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto*. Danieli 1 :17_

Paulo aliwaombea waefeso ufahamu

_17 Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, *awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye;18 macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;* Waefeso 1 :17- 18_

Na usiombe kujumla omba specific kuwa Mungu naomba uafahamu wa kufahamu ndoto.

Mungu anahamu ya wewe uwe na ufahamu maana yeye ndiye aliyetengeza hiyo njia ya kuwasiliana na wewe kwa ndoto

_6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. Waebrania 11 :6_

_1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Waebrania 11 :1_

_17 Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. Warumi 10 :17_

Mungu ni mzazi anataka aongee na wewe kwa lugha ya kawaida. Kama wewe hukai na watoto wako atajua sana ile lugha ya ya mlezi wake kama ni hause girl au house boy au bibi. Na ndio maana Mungu anataka kukupa njia ya kudumu ya kusema na wewe maana ni mzazi wako

Tokea Mungu ananifundisha jambo hili naona moja kwa moj ndoto nyingi sana.mimi naona urahisi kwa sababu niliamua kujifunza lugha ya Mungu ya ndoto.

Kama Mungu alisema na mimi kwaa njia ya ndoto na kama nilielewa basi ujue na wewe atakusaida.

ENEO LA  *Kumbuka ulichokuwa unawaza au kukiombea kabla ya ndoto*

_20 aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; Waefeso 1 :20_

?Mungu anajibu ndoto na mawazo yako

_18 Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.19 Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. *20 Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu*.21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.22 Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema,23 Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.24 Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe; *Mathayo 1 :18-24*_

Ina maana alikuwa anawaza kumwacha Mariam na Mungu alijibu moja kwa moja na angalia _16 Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao *17 Ili amwondoe mtu katika makusudio yake*, Na kumfichia mtu kiburi; 18 *Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga. Ayubu 33 :18*_

?Kagua ulikuwa unawaza nini na hiki ndicho unakipata kwenye Mathayo _Kisha Herode akawaita wale mamajusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota. Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia, mkaulize sana mambo ya mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende nimsujudie. Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane. *Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine*_.
MATHAYO . 2:7-8, 11-12

Na Mungu aliwaonya walipotoka tu kwa Herode kwa njia ya ndoto na Mungu aliwakataza. Kitu cha muhimu kwenye ndoto ni ujumbe. Maana hatujaambiwa ndoto hapa ila ni *ujumbe ndio muhimu*.

Nebukadreza alipotukuka na alimsahau Mungu na aliota ndoto na akaona mti mkubwa.. na ndege wapo hapo na aliona mlinzi akija kuuagiza mti ukatwe na Daniel akaja kumfasiria na alifadhaika moyoni na yeye.

Na Daniel alimwambia
_Ndipo Danieli, aliyeitwa jina lake Belteshaza, akashangaa kwa muda, na fikira zake zikamfadhaisha. Mfalme akajibu akasema, Ee Belteshaza, ndoto ile isikufadhaishe wala tafsiri yake. Belteshaza akajibu, akasema, *Bwana wangu, ndoto hii iwapate wao wakuchukiao, na tafsiri yake iwapate adui zako*. ni wewe, Ee mfalme, uliyekua, na kupata nguvu; maana ukuu wako umekua na kufika mpaka mbinguni, na mamlaka yako yamefika mpaka mwisho wa dunia. ya kuwa utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni, nawe utalazimishwa kula majani kama ng’ombe, nawe utatiwa maji kwa umande wa mbinguni, na nyakati saba zitapita juu yako; hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa yeye amtakaye, awaye yote. *Hayo yote yakampata mfalme Nebukadreza. Baada ya miezi kumi na miwili, alikuwa akitembea ndani ya jumba la kifalme katika Babeli. Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee mfalme Nebukadreza, maneno haya unaambiwa wewe;*Ufalme huu umeondoka kwako. Nawe utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni; utalishwa majani kama ng’ombe, na nyakati saba zitapita juu yako, hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yote. *Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadreza; alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng’ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege*_.
DANIEL. 4:19, 22-22, 25, 28-29, 31-33

Na amri ya walinzi ilikuja na kumundoa kwenye nafasi yake na alisema tengeza mambo yako na Mung *Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha.DANIEL. 4:27*

?Na yote yalitokea baada ya miezi 12. ? *Na hakujali na alipewe tafsiri na ujumbe*

ENEO LA ⃣. *Ikiwa umeota ndoto na umesahau omba Mungu akukumbushe. Na akupe tafsiri yake na ujumbe.*

Daniel 2:1-29. Nabukadreza aliota ndoto na alisahau. Ndani yake alisahau kabisa. Wachawi nao walisahau. Akina Daniel waliomba kwa Mungu awakumbushe na walipewa na tafsiri yake na ndoto aliyoota.

Na nebukdreza hakubisha maana alikumbushwa yote.

?Kuna miaka kadhaa mama yangu alikuwa anasumbuliwa jambo fulan na kitu kilichokuwa kina namsumbua nilishuhuduwiwa kuwa kuna ndoto aliota lakini nilipomuuliza alisahau. Na niliomba na Mungu alimkumbusha na nilijua namna ya kuombea.

Kama Mungu anaweza zuia usisahau mwombe Mungu usisahau kwa sababu ulisahau kuomba ili usisahau.

Omba Mungu akusaidie.. na ndio maana andika ndoto zako. Hakikisha unaandika ndoto andika wakati huo huo.

Na ukiota ndoto na ukawa unakumbuka kijumla itakupa shida kutafsri .. na wengine wameandika wamesoma shule uliyoota. Sio sawa uko chuo kikuu unaota uko primary au kindergarten.

Hakikisha cheki akina nani wanakuzunguka na ni nani na mtihani huo ni nini.. kesho tutapita..

Na kesho ntaanza kukufundisha namna ya kutumia vipengele fulani fulani.

?Maombi: Hakikisha unaokoka na Mungu anakuita uokoke msalaba ni kwa ajili yako na Roho Mtakatifu afungue mlango wa Kuokoka maana kuokoka sio dini mpya bali ni kuhamishwa kutoka ufalme wa giza kwenda ufalme wa mwana wa Pendo lake.

Mapepo yote achia watu hawa tunafuta laana zote za ukoo na kila kinachozuia usiokoke kwa damu ya Yesu Mungu wafungulie mlango kama Seth na muokoke . Na Mungu mpe neema ya wokovu mtu anayesoma somo hiki katika Kristo Yesu.

?Nazungumza na wewe kama hujaokoka na unatamka huyu Yesu. *Au ulirudi nyuma njoo kwa Yesu na neema ipo rudi kwa Yesu*.
***********************?**************
Soma sala hii
? *Sala ya Toba*

? Inawezekana kabisa ya kuwa wewe unayesoma ujumbe huu hujaokoka – yaani hujampokea Yesu Kristo ndani ya moyo wako kama Bwana na Mwokozi wako. Lakini sasa umeona umuhimu wa kumpokea Yesu Kristo katika maisha yako.

Naamini Roho Mtakatifu ameweka fursa hii mikononi mwako kwa mpango maalum wa Mungu ili ufike mahali pa kutubu na kuokoka. Inawezekana kabisa, pia ya kuwa hujawahi kuambiwa juu ya umuhimu wa wewe kuokoka. Lakini napenda kukuambia ya kuwa ni mpango wa Mungu uokoke. Soma Wakolosai 1:13,14 na Yohana 1:12-14 na 1 Timotheo 2:3-6 na Warumi 1:16,17 na Yohana 3:7. Ni vigumu kuona baraka za Damu ya Yesu bila ya kuokoka.

Kwa hiyo kama unataka kuokoka – tafuta mahali palipo na utulivu, na usome kwa sauti sala ifuatayo: *(ukiweza unaweza kupiga magoti unapoomba sala hii)*

_*“Ee Mungu wangu ulie Mtakatifu. Ninakuja mbele zako. Mimi ni mwenye dhambi. Naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizokukosea katika maisha yangu. Ninatubu kweli. Naomba damu ya Yesu Kristo iliyomwagika msalabani kwa ajili yangu initakase sasa katika roho yangu na nafsi yangu na mwili wangu. Nimefungua moyo wangu. Bwana Yesu Kristo nakukaribisha ndani yangu. Ingia kwa uwezo wa Roho wako – uwe Bwana na Mwokozi wangu kuanzia sasa na siku zote. Ahsante kwa kunisamehe na kwa kuniokoa. Nimejitoa kwako nikutumikie katika siku zote za maisha yangu. Shetani hana mamlaka tena juu yangu katika jina la Yesu Kristo. Amina.*

Ikiwa umesoma sala hii kwa kukusudia kabisa na kwa imani, basi wewe umeokoka na dhambi zako zimesamehewa na kusahauliwa na Mungu sawasawa na alivyoandika katika neno lake. Damu ya Yesu iko juu yako sasa.

??‍♀ *Baada ya kuokoka*

Unapoanza maisha haya mapya katika Yesu Kristo nakushauri mambo yafuatayo:

 1. Zungumza na Mungu kwa maombi kila siku (Yohana 15:7)
 2. Soma Neno la Mungu (Biblia) kila siku (Matendo ya Mitume 17:11)
 3. Mruhusu Roho Mtakatifu akutawale (Wagalatia 5:16-25; Warumi 8:14-17)
 4. Umtumaini Mungu kwa kila jambo katika maisha yako (1Petro 5:7; Zekaria 4:6)
 5. Usiache kukusanyika na kushirikiana na wengine waliompokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wao kama wewe ili uimarike zaidi (Waebrania 10:25)
 6. Soma jarida la “Hongera kwa Kuokoka.??

Ukipenda unaweza kuniandikia kwa anwani yangu http://www.mwakasege.org/mawasiliano.htm juu ya uamuzi uliofikia leo wa kuokoka, ili tumshukuru Mungu pamoja, na tuzidi kukuombea; na pia, tukutumie maandiko mengine ya kukusaidia:

*Soma kitabu cha Hongera kwa kuokoka*

???????

 

*SIKU YA NANE*

 

SEMINA YA NENO LA MUNGU DODOMA UWANJA WA BARAFU NA MWL MWAKASEGE*

SOMO: *FAHAMU YAFUATAYO KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI UFANIKIWE KIMAISHA*

*APRIL 9, 2017*

DOWNLOAD KITABU CHA HONGERA KWA KUOKA https://drive.google.com/…/0BxdP6mgDJWByVERtampLTGZWR…/view…

SALA YA TOBA http://www.mwakasege.org/mafundisho/okoka.htm

Lengo: Kuimarisha uhusiano wako na Mungu ili ufanikiwe kimaisha.

Ndoto ni njia ambayo Mungu anatumia kuongea na mtu, na kwa wakati ule wetu ilikuwa shida sana kupata masomo haya ya ndoto. Kwa hiyo hii ni neema kusikia masomo haya kwa wakati huu. Tafsiri za ndoto zipo kwenye biblia kwa hiyo fuatilia hatua kwa hatua.

*Na nilikuambia tunaandika kitabu cha Ndoto na tunaomba Mungu atusaidie kitoke mwaka huu.*

*Summary*

_Kwa kuwa Mungu husema, wakati huu kwa njia moja, au wakati mwingine kwa njia nyingine, ingawa mwanadamu anaweza asielewe. Mungu husema na mwanadamu katika ndoto, katika maono ya usiku, wakati usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu wasinziapo vitandani mwao,Ayubu 33:14-15 NEN_

?Ndoto ni njia ambayo Mungu anatumia ili uweze kusikia kitu ambacho Mungu anataka kukuambia

_Ikawa, mwisho wa miaka miwili mizima, Farao akaota ndoto; na tazama, amesimama kando ya mto. Na tazama, ng’ombe saba wazuri, wanono, walipanda kutoka mtoni, wakajilisha manyasini. Na tazama, ng’ombe saba wengine wakapanda nyuma yao kutoka mtoni, wabaya, wamekonda, wakasimama karibu na wale ng’ombe wengine ukingoni mwa mto. Kisha hao ng’ombe wabaya waliokonda wakawala wale ng’ombe saba wazuri, wanono. Basi Farao akaamka. Akalala, akaota ndoto mara ya pili. Tazama, masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa, mema. Na tazama, masuke saba membamba, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao. Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. *Basi Farao akaamka, kumbe! Ni ndoto tu*.MWANZO. 41:1-7 SUV_

?Farao aliposema kumbe ni ndoto tu ina maana alikuwa anataka kudharau. Na naamini wewe sasa hutaweza kudharau ndoto .

Na ndoto zina vyanzo mbali mbali japo Mungu anaweza tafsiri ndoto zote.

 1. Mungu

2.Shetani

3 Shuguli nyingi unapokosa vipaumbele vya kutumia muda vizuri unakuwa na shughuli nyingi maana yake hazina mpangilio

4.Hali ya Kiroho ya mahali unapolala.

Mungu ndiye aliyetengeneza lango la ndoto na kwa kuwa hatujui namna ya kulinda shetani nae analitumia. Na nilikufundisha kuwa linalindwa kwa kwa damu ya Yesu. Ndio inatumika kuziba lango la ndoto

Kama hukuwepo hakikisha unapata kanda na sikiliza itakusaidia sana.

Jana nilipitia baadhi ya ndoto na nyingi sana ni ndoto za shule. Na jana nilikupa mtaji wa kuanzia kufanya maombi

*UMUHIMU WA KUFANYA MAOMBI YA KUONDOA KINACHO KUFUATILIA KWA NJIA YA A NDOTO TOKA KWENYE ENEO UNALOLALA AU ULILOWAHI KULALA*

*SEHEMU YA KWANZA*

*.Kutoka eneo unalola*.
Nyumbani kwako, hotelini, kazi, nyumba ulipanga

_Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani. Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale. *Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako*. Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa. Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia._

_*Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli BWANA yupo mahali hapa, wala mimi sikujua. Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni*.MWANZO. 28:10-17 SUV_

Yakobo alipolala na aliota ndoto na kazi ya ile ndoto ilikuwa na kazi kubwa ya kumtaarifu juu ya mahali alipolala.

Na Mungu alikuwa anajitambulisha kwake na ndio maana yako alisema hapa ni nyumba ya Mungu. Ina maana mahali pale palikuwa uwepo wa Mungu.

Jambo lingine ni lango ina maana kuna vitu vya kiroho vinapita pale kutoka katika ulimwengu wa roho kuja ulimwengu wa mwili.

Tulikuwa mkoa mmoja na tulikuwa tunajenga hema, na kuna watu walikuja na wakasema hapa mnapojenga hema mnakata network zetu. Na walisema tutaona nikasema haisha shida. Na tulijua kabisa ni wachawi.

Baada ya siku 2 mchawi wa kwanza aliokoka na wakaenda kutafuta mchawi mwingine mkubwa maana na wao wana ngazi zao.

Jumamosi alikuja kupambana na sisi. Alijaribu kila kitu na alishindwa na akarudi nyumbani kwake na anakaandika bango lake na kuwa mganga wa kienyeji.

Na alikuwa na uwezo wa kujigeuza umbo lolote na anaingia chumbani kwake na anafungua hata Ardhi. Na alishangaa aliporudi nyumbani kwake alijaribu kila kitu alishindwa.

Na ilibaki moja na alikuwa na kadi ya ATM, na alikuwa anatumia kila mahali maana alipewa kuzimu. Na alipewa masharti kuwa hela atakayochukua lazima aitumie yote . Sasa jumapili alipoenda benki kutoa hela kadi yake ilimezwa.

Na aliona sasa kapatikana alinyoosha moja kwa moja uwanjani aliwakuta wenzangu na alijitambulisha kuwa anaenda kijisalimisha kuwa anataka kuokoka. Na wakamhoji maswali na walienda nae nyumbani kwake.

Na walienda nae nyumbani kwake, na gari zinapiga nyimbo za injili na walishangaa kuona mganga anakuja na nyimbo za injili maana pale kwake walikuwepo watu waliokuwa wanahitaji wake na magari yao.

Na bango la mganga walilitoa na kila kitu chake wakaondoa kila kitu wakachoma uwanjani. Na tukaomba nae na alipokuwa kwenye madhababu wenzake walishindwa kuingia ndani.

Na hii iwasaidie wahudumu na alikuwa haoni mtu na alikuwa anaona miali ya moto. _Na kwa habari za malaika asema, Afanyaye malaika zake kuwa pepo, Na watumishi *wake kuwa miali ya moto*.Waebrania 1:7_

Na hata mapepo yanakuwa hayaoni watu yataona moto tu. Hata wachawi walipokuwa wanatafuta kuingia walishindwa. Kwa hiyo biblia inaposema kuwa hili ni lango ina maana ni eneo maalumu la kuingilia.

Kwa hiyo hadi sasa huyu ni mtumishi wa Mungu na mchungaji sasa. Sasa turudi kwa Yakobo, chukulia huyu Yakobo angekutana na miungu mingine ingekuaje?

Sasa twende kwa mtoto Samuel na nafuatilia kwenye maandiko na sijaelewa bado kwanini aliwekwa karibu na sanduku la agano. Maandiko yanasema alipompeleka hekaluni na Kuhani Eli alimpeleka karibu na Sanduku la agano sasa kama unalala karibu na sanduku la agano utalala kweli? Biblia inasema kuwa akaanza kusikia sauti, maana kuna watu huwa usiku wakilala wanasikia sauti. Sasa ile sauti ilikuwa ni ya Mungu.

Sasa fikiria unaenda kulala hotel na unalala sehemu mtu kasahau hirizi yake hapo na wewe unakuja speed kuwa na hujaombea hapo. Sasa lazima utaota ndoto ngumu ngumu ivi.

_Na Babeli, huo utukufu wa falme, uzuri wa kiburi cha Wakaldayo, utakuwa kama Sodoma na Gomora hapo Mungu alipoiangamiza. Hautakaliwa na watu tena kabisa, wala watu hawatakaa ndani yake tangu kizazi hata kizazi. Mwarabu hatapiga hema yake huko, wala wachungaji hawatalaza makundi yao huko. Lakini huko watalala hayawani wakali wa nyikani; na nyumba zao zitajaa bundi; mbuni watakaa huko; na majini watacheza huko. Na mbwa-mwitu watalia ndani ya ngome zake; na mbweha ndani ya majumba ya anasa; na wakati wake u karibu kufika, na siku zake hazitaongezeka.ISAYA. 13:19-22 SUV_

?Hii ni adhabu iliyotolewa katika mji wa Babeli na Mungu Mungu aliweka zuio na aliweka na wanyama wakali na majini yacheze ndani yake na mbwa mwitu walie huko ndani.

?hujawaji jiuliza kwanini mtu anaota ndani kwake kuna nyoka au jogoo au myama yoyote? Na ukiamka ni unasema ni ndoto tu na Mungu anakuambia kuwa hapa kuna shida.

Kuna mtu aliota mbwa kalala kwenye kitanda chake. Na majini yapo pale kisheria na huwezi nyamazisha maana wapo pale kihalali na ukitaka kuwatoa pale lazima uwe na *eviction order* ya mahakama ya mbinguni. Kwa hiyo lazima utumie neno la Mungu kisheria.

Na nilikuambia kuwa kila picha unayoota ina maana yake. Ukiona nyoka kuna maana yake ukiona mbuni kuna maana yake.

Kuna mtu alikuwa anaombea nyumba yake na kila akilala alikuwa anaona nyoka kweye ndoto na akimka anawakuta kweli mara mlangoni na akiamka anakutana na nyoka kweli. Na aliua zaidi ya nyoka 30 na wote wana rangi ya kufanana. Nenda kwenye biblia kuna mifano na mifano.

Kuna wakati wana wa Israel walitolewa Samaria.

_Naye mfalme wa Ashuru akaleta watu kutoka Babeli, na Kutha, na Ava, na Hamathi, na Sefarvaimu, akawaweka katika miji ya Samaria badala ya wana wa Israeli; wakaumiliki Samaria, wakakaa katika miji yake. Basi ikawa, wakati ule walipoanza kukaa huko, hawakumcha BWANA; kwa hiyo BWANA akapeleka simba kati yao, nao wakawaua baadhi yao. Kwa hiyo wakamwambia mfalme wa Ashuru, wakasema, Wale wa mataifa uliowahamisha, na kuwaweka katika miji ya Samaria, hawaijui kawaida ya Mungu wa nchi; kwa hiyo amepeleka simba kati yao, na tazama, wanawaua, kwa sababu hawaijui kawaida ya Mungu wa nchi. Ndipo mfalme wa Ashuru akatoa amri, akasema, Mpelekeni mmojawapo wa makuhani, mliowachukua kutoka huko; aende akakae huko, akawafundishe kawaida ya Mungu wa nchi. Basi mmoja wa makuhani waliochukuliwa kutoka Samaria akaenda akakaa katika Betheli, akawafundisha jinsi ilivyowapasa kumcha BWANA. Lakini pamoja na hayo watu wa kila taifa wakajifanyia miungu yao wenyewe, wakaiweka katika nyumba za mahali pa juu, walipopafanya Wasamaria, kila taifa katika miji yao walimokaa.2 WAFALME. 17:24-29_

Baada ya kuraruliwa na simba walisema kwa sababu hatujui kawaida ya Mungu wa eneo hili. Ndio maana kuna wengine wanaota wanakimbizwa na nyoka au mbwa au wanyama wakali hivi.

Cha kufanya ni ombea kwanza mahali pako pa kulala na Mungu anakuambia kuwa mungu wa eneo hili ana alama hii. Na kama wewe ni mpangaji na hujafuatilia uwe na uhakika kuwa utaondolewa hilo eneo kama ni kwako patakukinai na uwe na uhakika kuwa utahama.

*MAMBO YA KUFANYA KAMA UMEKUTANA NA HALI YA NAMNA HIYO*.

?1.Omba toba kama kuna kitu kiko mahali hapo na hakimpendezi Mungu. Omba toba . Na nilikufundisha namna ya kuzia ndoto mbaya kuwa ombea

?Nyumba unayolala
?Ombea mbingu
?Au mtu huyo a aingia kwako.
?Secure chumba cha kwako. Ombea hicho tu.
?Ombea ardhi ya hapo.
?Zuia kwa damu ya Yesu ndoto mbaya

Kama uko hotel ombea mahali pako tu usianzishe ugomvi bila sababu.

Siku moja tulikuwa Calfonia kwenye mkutano wa uchumi. Na sisi tuliwahi siku nne kabla. Sasa tulifika eneo la hollywood nadhani mnajua. Sasa unaweza kuelewa Mhubiri anaingia holly wood.

Na kama hujawahi muona shetani akitembea nenda pale. Na tukamuuliza Mungu tunafanyeje hapa. *Mungu alituambia jifunike kwa damu yangu.*

Si unajua hata Yesu alikwepa vita, na sisi tulijiombea wenyewe. Sasa kama hujui namna ya kufanya mazingira ya namna hiyo unaweza kwama.

Mahali popote pale watu hawakai au nyumba au chumba ina maana kuna ukiwa na ukiwa ni adhabu. Unasafiri muda mrefu hata kama ni kwako jifunze kuomba maana unaweza kutana na vitu vigumu.

? *2.Mwaga damu ya Yesu kwenye eneo unalokaa au unalolala*

Damu ikimwagika huwa inaondoa kila kilichoko hapo.fanya zoez nyumbani kwako. Na kuna kijana mmoja alisikia hili somo na yeye akaenda akamwaga damu ya Yesu nyumbani kwake na aliweza kuomba maana mara ya kwanza alikuwa hawezi.

Mwingine alikuwa anashindwa kulala lakini baada ya kumwaga damu ya Yesu eneo lake aliwaza kulala vizuri.

*3.Hakikisha unakemea nguvu za giza zilizoko mahali pale*

Kama watu wamelala hapo na wamefanya uasherati na eneo hilo hilo, juzi nilikuambia sabuni haiondoi nguvu za giza. Na unashangaa unalala hapo na mapepo yanaanza kukusumbua.

Kwa hiyo ombea na mashuka kwa damu ya Yesu maana damu ya Yesu hua
safisha kabisa.

*4 Ombea uwepo wa Roho Mtakatifu na malaika zake*

Neno la Mungu linasema _*Malaika wa Bwana hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.Zaburi 34:7*_

Kwa hiyo malaika wanaweza kukufanyia ulinzi.

*SEHEMU YA PILI*
*ENEO ULILOWAHI KULALA NA UKAONDOKA KATIKA HIMAYA YA MAPEPO*

_Biblia inasema Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni *juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho*.Waefeso 6:12_

?Hiyo ni hirach yao sasa jeshi la pepo wabaya wana vikosi vyao. Na nilishangaa siku moja niliona makundi Tofauti Tofauti ya malaika. Na wanakuwa miili Tofauti wale wa kuligana na kazi iliyopo. Wale wapiganaji hawana mabawa ila wanakuwa na Farasi weupe. Na wengine wana maumbo ya kwao. Na wale wanaoimba nao wana sura tofauti. Ni mara chache huwa nawaona , na muda mwingine na wao wanakuja kuimba na sisi.

Ukisoma Mwanzo 28:10-17☝angalia 28?

_Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake. Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu. Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu. Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.MWANZ. 28:18-22 SUV_

_Na malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, Yakobo! Nikasema, Mimi hapa. Akasema, Inua, basi, macho yako, ukaone; mabeberu wote wanaopanda wanyama wana milia, na madoadoa, na marakaraka; maana nimeona yote aliyokutendea Labani. Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa.MWANZO. 31:11-13 SUV_

_Mungu akamwambia Yakobo, Ondoka, panda uende Betheli, ukakae huko; ukamfanyie Mungu madhabahu huko; yeye aliyekutokea ulipomkimbia Esau, ndugu yako. Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake, na wote waliokuwa pamoja naye, Ondoeni miungu migeni iliyoko kwenu, mjisafishe mkabadili nguo zenu. Tuondoke, tupande kwenda Betheli, nami nitamfanyia Mungu madhabahu huko; yeye aliyenisikia siku ya shida yangu, akawa pamoja nami katika njia yote niliyoiendea.MWANZO. 35:1-3 SUV_

Sasa kwanini Mungu alitaka kumkubusha kuwa Mungu wa Betheli. Na kila mahali nilienda na wewe na malaika wangu. Sasa fikiria Yakobo angekutana na mapepo?

Mungu anataka kuingia kwenye agano. Mara nyingi huwa nawaambia watu kuwa kama unaota ndoto unakula na watu waliokufa kwenye ndoto usiowajua au unakula nyama ambayo sio kawaida kula. Maana yake ni kuwa unaingizwa kwenye agano na mapepo yako pale

Kama Malaika alimfuata Yakobo kwa Labani na alimkumbusha kurudi Betheli. Na kama ulikutana na mapepo yaani ulilala shule na hapakuwa pazuri kuna mapepo yataanza kukufuatilia. Kuna mapepo yanaitwa Demon monitors na kila mahali yanakufuatilia. Miaka na miaka na unaota ndoto uko shule. Sasa kumbuka kukata kitu cha kiroho ulicho kutana nacho mahali hapo maana itakutesa.

Jifunze namna ya kujikung’uta maana unaweza ukaokota kitu hotelini na inaanza kuhamia kwako. Cheki unamtembelea mwenzio na unakuta ugomvi wa nyumbani kwa rafiki yako na unahamia kwako na unaanza kufanana fanana na kule.

Kwa hiyo hakikisha unakata hiyo connection kwa damu ya Yesu. Jikung’ute kila mahali ulipotoka hata kama mtu amekuja kukutembelea kwa kwako hakikisha unaomba na kung’uta kila kitu anachokuja nacho.

Hujawahi ona umeota ndoto katika mazingira mbali mbali na uko sehemu tofauti tofauti. Mara uko Morogoro na Dar es Salaam au Dodoma. Hiyo ni Mungu anataka kukumbia kuwa kata hiyo connection.

Ninaona mtu aliachiwa alama mkononi kwenye ndoto na nyoka ulipolala. Na kuna pepo lipo linakufatilia na kila ukienda mahali popote una tembea nalo. (Mwl alifanya maombi ya mtu huyo na kukata hiyo network.) Na pepo lilipuka na kumtoka huyo mtu.

Hili lilikuwa ni zoezi ili kuthibitisha kitu alichokuwa anafundisha. Kwa hiyo jifunze namna ya kuomba toba. Na sasa nakata connection ya hilo pepo na baada ya maombi mtu alifunguliwa.

Tunakwenda sawa sawa.?

WEKA MKONO WAKO JUU YA MAGOTI NA MAHALI ULIPOLALA NA ARDHI INAKUMBUKA.

NA NAOMBEA ENEO LOLOTE AMBALO UNALALA NA UKIWAHI KULALA NA NAACHILIA DAMU YA YESU.

KAMA KUNA KITU NYUMBANI KWAKO CHA KAMBI NYINGINE KAKITOE MAANA NAMWAGA DAMU YA YESU SASA HIVI KWA KILA ANAYEFUATILIA SOMO HILI

MAOMBI NA BARAKA.

Pia kama hujampokea Yesu hakikisha unaokoka na kumpata Yesu. Soma kitabu pale juu cha hongera kwa kuokoka

Ubarikiwe sana sana na tuonane tena semina ijayo