HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO

SOMO:   HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO

MWALIMU   CHRISTOPHER  MWAKASEGE  (Mana Ministry)

ENEO:  TANGANYIKA PAKERS – KAWE,   DAR ES SALAAM

TAREHE:  5th hadi 12th MARCH  2017

Siku ya kwanza

LENGO YA SOMO:

Kuhakikisha ya kwamba Mafanikio yako yaliofungwa kwenye hali ya kiroho ya ardhi yanafunguliwa

➡Leo tuangalie jambo moja tu kufungua mafanikio yako yaliyofungwa na hali ya kiroho ya ardhi inayofanya mahali unapoishi pawe nyumba ya utumwa

Kumbukumbu 6:12

✅Angalia vizuri sana haya maneno Nchi ya misri, nyumba ya utumwa

➡Angalia haya mambo vizuri kwa kutazama mambo yafuatayo

1 Kufuatana na 2nyk 7:14 nchi maana yake ni ardhi yenye mipaka halali ya kuumiliki. Biblia ya kiingereza maneno ya mwisho inasema kuiponya nchi yako (I will heal their land)

➡Taifa ni tofauti na nchi linahusisha mkusanyiko ya watu hasa linapozungumza maswala la uongozi waliokubaliana, lina mlolongo wake utegemea nchi na nchi na katiba waliyo nayo.

➡Ukitoka kwenye taifa utakuta kabila, kabila utakuta jamaa, ndani ya taifa kuna lugha.

➡Nchi imegawanywa tofautitofauti na mipaka yake.

➡Kiblia Taifa linaweza kuwepo lakini lisiwepo kwenye nchi yake. Wana wa Israeli walikuwa Taifa lakini si kwenye nchi yao

2 Ukilinganisha mstari huu wa 2nyk 7:14 na ile Kumb 6:12 utaona ya kuwa hali ya kiroho ya ardhi inaweza ikageuza eneo kuwa nyumba ya utumwa

Kumb 6:12

➡Nchi maana yake=2nyk 7:14 nchi hiyo inaitwa Misri

Nchi ya Misri nyumba ya utumwa kwa hiyo ardhi imefanyika nyumba ya utumwa au ardhi ina uwezo wa kufanya eneo likawa nyumba ya utumwa

3 Utumwa wa wana wa Israeli ulikuwa ni wa kiroho lakini ulijitokeza katika maisha yao ya kila siku

Sababu 3 zinakazokusaidia kueleza jambo ili

MOJA

Shida haikuwa kazi waliyokuwa wanafanya lakini ni hali/mazingira ya kiroho ambayo walikuwa wanafanya hiyo kazi

Kut 1:11-14

➡Kazi walizokuwa wanafanya Misri walizifanya pia Kaanan. Walifanyishwa kazi ngumu

➡Sasa si kila kazi ngumu ni kazi ya utumwa. Walishughulika na chokaa, matofali na kujenga miji na mashamba

➡Swala si aina ya kazi ndo iliwafanya kuwa watumwa bali mazingira ya kiroho

➡Walipokuwa wanamlilia MUNGU hawakumlilia sababu ya kazi walizokuwa wanafanya bali sababu ya utumwa Kut 2:23

➡Utumwa si kazi ni hali ya kiroho/mazingira ya kiroho yanayotengeneza aina fulani yamaisha ambayo:-

✅Ubana fikra za watu,

✅Ubana maamuzi yao,

✅Uweka mipaka kwenye maisha yao na kwenenda kwao

➡Si watu wengi sana wanaweza kujua wako kwenye hali ya utumwa sababu ya kazi wanayofanya maana kazi hiyo hiyo mwingine anaomba kufanya

PILI

Walishindwa kujitoa

➡Kama ingekuwa ni swala la kazi kwanini wasiache?

➡Kila siku walalamika kazi ngumu kazi ngumu kwanini usiandike barua ya kuacha? Utafute iliyo nyepesi?

➡Unapokuwa mtumwa kwenye mazingira ya nyumba ni tofauti nay ale ya gerezani

➡Yule aliyekwenye nyumba inamchukua mda mrefu sana kujua kama ni mtumwa

Kama MUNGU asingewatangazia kwamba wako utumwani wasingejua.

➡Walipokuwa wanalia MUNGU awaondolee uchungu wa ule utumwa MUNGU akaondoa utumwa maana huo ndio uliosababisha uchungu ndani yao

TATU

MUNGU aliwatoa kwa nguvu

Kumb 7:8

➡Swala alikuwa kazi bali ni ile hali ya mazingira ya kiroho iliyowafunga kwenye utumwa

 

4 Waishio ndani ya nyumba wanatambuliwa kiroho kwa kuangalia jina la mmliki wa nyumba hiyo

Esta 8:1-2

Soma ile Esta 7:10

➡Amani hayupo, nyumba yake kapewa Esta

➡Katika ulimwengu wa roho nyumba zinatazamwa tofauti na tunavyotazama, angalia na Modekai naye akapewa pete ya Amani na Esta akamweka Modekai juu ya mlango wake amani

Kumb 6:12

➡Nchi ya Misri nyumba ya utumwa weka misri haijalishi uko nchi gani kama wewe ni Mmisri uko duniani unatambulikana kama mtu wanyumba ya misri au nchi ya misri kuna alama inayokutambulisha

Nyumba ya Israeli na nchi ya Israeli, wana kitambulisho katika ulimwengu wa roho kinachofanana

➡Amani alikufa na aliyepewa mamlaka juu ya nyumba yake alipewa Esta haijalishi walikaa kikao cha kuchagua msimamizi

Modekai alipewa mamlaka kwenye lango la nyumba ya amani, haijalishi hawako nyumbani wakati huo lakini wako na alama waliuwawa wote

➡Ukiwa na alama kwa ajili ya uangamifu utapata shida sana. Kama nyumba ya baba yako inamilikiwa na adui utapata shida sana

Math 12:29

➡Nani anayemiliki nyumba na uzao wako?

➡Uwezi kuwafungua waliofungwa kabla ya kushughulika na Yule aliye juu yao

5 MUNGU aliwatoa wana wa Israeli toka kwenye nyumba ya utumwa kupitia kwenye mlango wa nyumba ya utumwa

Kut 12:13-23

➡Alitumia kitu gani?… Jibu ni DAMU YA AGANO

➡Hakuwapitishia dirishani bali mlangoni lakini ilikuwa lazima DAMU YA AGANO itumike kuwatoa

➡Nchi ya Misri kipindi kile yote ilikuwa chini ya mazingira ya utumwa iliitwa nyumba ya utumwa na MUNGU alikwenda kuwafuta uzao wa Ibrahimu, Isaka na Yacoko sababu ya kiapo alichowaapia kwamba kuwatoa wana wa Israeli utumwani (walikuwa na alama) hakwenda kumfungulia kila mtu atoke

➡Mafanikio yao na kukua kwao kulikuwa kumefichwa na kukamatwa na mazingira ya ardhi ya Misri na walikuwa hawajui

➡Angalia ardhi ya nyumbani kwenu ama mahali ulipo kama ina mtawala anayetumia ardhi hiyo kama nyumba ya utumwa kuwa na uhakika utapata shida sana kutoka

➡Mfano nyumba ina vijana wana akili sana wana uwezo wa kufanya biashara, ana uwezo wa kufundisha na kufanya kazi lakini wako nyumbani na wale wajirani hawana hata shule lakini wako kazini.

➡Wakati mwingine unafikiri ni sawasawa sababu yuko kwako au nyumbani ujajua kuwa ardhi imegeuza nyumba yako kuwa nyumba ya utumwa

➡Kama baba yako alisimama na MUNGU mahali akaweka agano usifiriki shetani atakuachia kirahisirahisi katika mambo yako ama kuamua kwako.

➡Utashangaa kwako tu mambo hayaendi lakini kwa wengine yanaenda…hii yote ni yale mazingira ya kiroho yakibadilishwa na mambo yote yanabadilika

➡Ujawahi kuona mtu anahama kutoka kwenye nyumba ya kupanga kwenda kwenye nyumba yake gafla mambo yake yanasimama kiroho hata kiuchumi?

➡MUNGU aliwapitishia wana wa Israeli langoni ili kujua kuwa walikuwa kwenye nyumba.

➡Wengi wamefungwa:-

✅Kufikiri kwao

✅Kutokupata msaada mahalipopote pale

✅Wasipate kazi

✅Wakae tu nyumbani

✅Kitu cha imani wakifikiri wako kiroho. Hawafanyi kazi na ni watumishi wanatakuishi maisha fulani ya kiutumishi hivi, hawafanyi biashara wala kazi yoyote, wengine wameacha masomo yao

➡YESU anasema nyumbani mwa BABA yake, na pia anasema kanisa ni nyumba yake kwa hiyo, alama ya kiroho ya kanisa inategemea jina la kanisa.

➡Kama unasali kanisani hujui jina la mchungaji wako basi ujue alama yako ya kiunganiko chini ya mchungaji imepotea

➡Ardhi ni kama kompyuta kubwa ukikanyaga ardhi inafahamu na kama haikufaamu upeleke taarifa kwenye system yake kujua background yako na ndiyo maana ukikataliwa mjini hata mashambani utakataliwa na ukibarikiwa mjini na mashambani umebarikiwa

MAOMBI

#UFALME_KWANZA

 

……”Jesus Up”……

*************** ENDELEA  SIKU YA PILI  ***************

LENGO YA SOMO:

Kuhakikisha ya kwamba Mafanikio yako yaliofungwa kwenye hali ya kiroho ya ardhi yanafunguliwa

Kumb 6:12, 2Nyk 7:14

✅Pitia somo la jana ili kujua tulipotioka nay ale mambo ya msingi 5 juu ya kufungua mafanikio yako yaliyofungwa na hali ya kiroho ya ardhi inayofanya mahali unapoishi pawe nyumba ya utumwa

✅Kumbuka jambo la msingi utumwa wa wana wa Isareli haukuwa sababu ya kazi walizokuwa wanafanya bali ni kwa ajili ya hali ya kiroho ya mazingira ya kazi walizokuwa wanafanya

✅Walimlilia MUNGU juu ya uchungu moyoni mwao wakati wanafanya kazi wala si kwa sababu ya kazi kuwa ngumu

➡Leo tuangalie NAMNA YA KUJIONDOA KWENYE MADHARA YA LANGO YA ARDHI YA NYUMBA UNAYOISHI INAPOMILIKIWA KIROHO YA NGUVU ZA SHETANI

➡Ni jambo pana na jipya kwa watu wengi neema ya MUNGU na iwe juu yako kuweza kuona na kufahamu jambo hili maana kujua na kufunguliwa katika jambo hili utafunguliwa katika mambo mengi sana

Esta 8:1-2, 13-14

Mwz 22:17

Math 12:29

Kut 12:12-23

Tuangalie vipengele vichache vya jambo hili ili iwe rahisi kuelewa

1 Ardhi na nyumba iliyojengwa juu yake vina uhusiano wa kiroho

➡Unasema unajuaje…..?

➡Kufuatana na Kumb 6:12 MUNGU amelinganisha nchi na nyumba kwa hiyo ardhi ile ambayo ina mipaka halali inauhusuano wa kiroho na nyumba inayojengwa

2 Mlango wa nyumba una uhusiano na mlango wa ardhi

➡Kwanini? sababu kama ardhi ina uhusiano wa kiroho na nyumba basi na milango yao ina mahusiano

3 Ukigusa mlango wa ardhi kiroho unagusa pia mlango wa nyumba kiroho

Matendo 16:26

➡Tetemeko lile halikuwa la kawaida lile la kuangusha nyumba bali lilikuwa lile la kushughulika na ardhi ambayo juu yake gereza lilikuwa lipo

➡Sababu walikuwa wapo gerezani kwa jinsi ya mwili isingekuwa rahisi wao kutoka maana hawakufungwa kimwili bali kesi yao mpaka kufungwa kwao ilikuwa kiroho

➡Ndiyo maana MUNGU alileta tetemeko akatikisa misingi ya gereza na Biblia inasema milango ya gereza ikafunguka haisemi ikavunjwa na vifungo walivyokuwa wamefungwa vikaachia

➡Yule askari alipoona milango iko wazi alitaka kujiua maana alijua wametoroka lakini walimwambia asijiue akawakaribisha kwake akawanawisha miguu na kuwatayarishia chakula na baada ya hapo walirudi gerezani

➡Kulipokucha asubuhi wale makadhi waliowafunga walitoa order ya wakina Paulo kuachiliwa.

➡Nini nataka uone hapa gereza halikuvunjwa wala kuwa na nyufa hata moja kutoka kwenye lile tetemeko

MUNGU hakuwa na shida na gereza la nje bali alikuwa na shida na gereza la kiroho ambalo kwa jinsi ya nje watu wanaona kama vile kuta tu na linaweza kuwa sehemu yoyote ile

➡MUNGU alikuwa anashughulika na ardhi  ili kushughulika na nyumba iliyo juu ya ardhi akafungua milango ya ardhi ili kufungua milango ya gereza iliyoko juu yake

➡Kama nyumba yako ni ya utumwa imezungukwa na mazingira ya utumwa usiangaike kuombea nyumba bila kuombea ardhi ya nyumba hiyo maana mlango wa ardhi una uhusiano na mlango wa nyumba yako

➡Vita ya ardhi si vita ya kumshirikisha kila mtu maana ina mapamabano yake mabaya kama ujajipanga

➡Kama huna NENO la kutosha ndani yako MUNGU akikusemesha uwezi kusikia maana kusikia huja kwa NENO la KRISTO maana waweza kushughulika na ardhi MUNGU akikwambia shughulikia mlango la ardhi

➡Wakina paulo walienda kuhubiri wakatengeneza mahali pa kusali bila kucheck na kushughulikia nani anamiliki lango la ardhi/nani ni mmiliki wa lile eneo

➡Waulize watu wa nyumba ya amani maana kiroho nyumba yake ilikabidhiwa Esta na Modekai sasa haijalishi kikao cha milathi kimeamua nini maana wamiliki ndio wanaoamua na kutoa ruhusa hali ya kiroho na hali ya maisha ya nyumba hiyo inaendaje

➡Unaanzisha kanisa/fellowship mahali badala ya kuangalia na kucheck nani ameshikiria lango la roho nyingine inayopingana na kitu unachofanya na ambaye ameshikiria lango la ardhi ambalo pia ndilo limeshirikia lango la nyumba ya sehemu hyo na msingi wa kiroho unayotumia kusali sasa kama vifungo hivi vimefungwa kwenye ardhi na vikaja kuonenakana mpaka kwa nje usipojua namna ya kuvifungua kwenye ardhi uwezi kufunguka

➡Angalia habari ya kina paulo kama waliendele na maombi kikundi cha cha ibada kikavurugika wakafungwa jera hata baada ya kutolewa gerezani walifukuzwa kutoka nje ya mji sababu walianzisha huduma mjini bila kusimamia malango ya ardhi ya mji

Matendo 16:39-40

➡Walipotoka gerezani walienda kwa Lidya na kukutana na ndugu/wapendwa tu na wale wapendwa waliwafariji tu hawakuwa wa msaada nao wakaenda zao

➡Ndiyo maana chunga sana watu wanaokushabikia huduma wakati hawajui vita unayopitia, chunga sana watu wanakusumizia front line wakati hawajua kupigana sababu ukifungwa gerezani watakufariji na kukupa pole na kusema tunakuombea na wakati hawajui hata wanachoomba

➡Mji ule ulikuwa na wapendwa lakini hawakuweza kuwasaidia kina Paulo sababu inategemea ni nani aliyeshirikia lango la ardhi kiroho la mji ule.

➡Maana walioshirikilia kama hawaitaki huduma kuwa na uhakika itafungwa na watu kuamia kwenye huduma ama kanisa jingine hata kama wapendwa wapo na usije fikiri watakusaidia watakufariji tu

➡Vikundi vingi sana vya maombi watu hawajui ni kwanini gafla vimechanua na gafla vimekufa sababu ni moja tu ulianzisha kikundi cha maombi bila kushughulikia lango la ardhi ambalo Modekai ndiye aliyeshikiria lango hilo na kama uko kinyume naye kuwa na uhakika kikundi hicho kitafungwa kabisa

➡Ndiyo maana unaweza kukuta makanisa mengine yanapata shida eneo hilo lakini nyumba nyingine hazipati hiyo shida ama kanisa moja linapata shida na jingine walaa sasa ni mambo mawili au moja lina operate kwa viwango vya juu sana au siyo tishio

➡Ndiyo maana watu wengi wanapata shida kwenye nyumba zao Biblia inaita nyumba za kitumwa na wako kwao.

➡Umewahi kufikiri kwa mfano hicho kiwanja ulichonunua ni nani anamiliki lango la hicho kiwanja katika ulimwengu wa roho?

➡Nani amepewa kumiliki ardhi uliyojenga? Wengine alipewa marehemu sasa ukichanganya jambo hili kiroho kuwa na uhakika kama usipojua namna ya kutengeneza kisiwa cha ardhi ya kwako utapata shida sana kuvuka na vita yake si nyepesi

4⃣Kama vile nyumba ilivyo na mlango zaidi ya mmoja vile vile na ardhi ina milango zaidi ya mmoja inayoweza kutumika kumfunga mtu

Isay 26:1-2

➡Nchi ili kurikaribisha taifa, taifa lazima lipite kwenye lango.

➡Anapozungumzia lango kwenye nchi anazungumzia lango la kwenye ardhi linaloruhusu watu kupitia, kuingia na kutoka

Matendo 16:26-27, 24

➡….milango… Biblia haituambaii milango ilikuwa mingapi mlinzi alipoamka alikuta milango yote imefunguliwa na funguo anazo yeye.

5⃣Kila lango la kiroho katika ardhi au nyumba lina walinzi wa kiroho

Matendo 12:6,10

➡Kuliwa na walinzi kwa ajili ya petro na kulikuwa na walinzi kwa ajili ya mlango/nyumba

➡Kuna mapepo unapewa wewe ukitoka nyumbani unakuwa nayo na kuna yale yamepewa kulinda ardhi ya nyumba yako hayatoki.

➡Alipofika kwa wapendwa waliokuwa wanaomba aligonga mlango (maana yake wakikupa kibali na kukufungulia ingia) malaika alazimishi wapendwa kufungua, wakati huku pengine malaika alimpitisha na milango kufunguka yenyewe. Swala ni kwanini hawakumfungulia? maana yuke dada hakufungua mlango baadaye walikuja wakamfungulia

➡Ardhi lile lilikuwa na malango 4, walipita lindo la kwanza na la pili hata mlango wa chuma na wa kuingilia mjini na mpaka kwa wale wapendwa waliokuwa wanamwombea kuna watu amabo wamefungulia lakini wako gerezani.

➡Fikiri Petro kama malaika alipomtokea angemwambi avae nguo na viatu kisha akapotea maana yake nini yuko huru keshavaa nguo na viatu lakini yuko gerezani kafungwa hana uhuru tena

➡Ndiyo maana tuna watu wengi sana tunawaombea na inapofika kwenye kufunguliwa kwako tunafunga mlango tunatamani kuwaomba kwenye chumba cha maombi lakini kuwafungulia hatufanyi hivyo.

➡Wengi tunawaombea halafu tukikutana nao tunakumbuka na kuona lile tatizo bado kwako hata kama wamebadilika kwa hiyo tunajikuta bado hatujawafungulia gafla wanarudi gerezani

6⃣Omba kwa imani na kwa juhudi hadi aliyefungwa apite milango yote iliyomkwamisha

Matendo 12:5

Waamuzi 5:8

➡Kati ya eneo la uwanja la mapambano la MUNGU ni langoni

➡Petro ililazimika avuke geti 4, mbili ndani ya gereza, moja ndani ya mji na nyingine kwa waliokuwa wanamwombea hivyo MUNGU akikupa eneo la kuwavusha watu na kukupa namna ya kuomba omba mpaka uwavushe geti zote

➡Wakati mwingine unapohitaji msaada wa vita unahitaji watu ambao wanajua kupigana uhitaji msaada wa pole hata kama ni pole bali hawata nyamaza mpaka umetoka

➡MUNGU atakupa mamlaka ya kukanyaga na kukika malangoni na kuachilia DAMU YA YESU hapo maana hii ni ahadi ya MUNGU kwa Ibrahimu

#UFALME_KWANZA

……”Jesus Up”……

 

*************** ENDELEA  SIKU YA TATU  ***************

 

SOMO: HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO

LENGO YA SOMO:

Kuhakikisha ya kwamba Mafanikio yako yaliofungwa kwenye hali ya kiroho ya ardhi yanafunguliwa

Kumb 6:12, 2Nyk 7:14

SUMMARY YA SIKU 2

✳Pitia somo la siku ya kwanza na siku ya pili ili kujua tulipotoka maana kuna yale mambo ya msingi 5 juu ya kufungua mafanikio yako yaliyofungwa na hali ya kiroho ya ardhi inayofanya mahali unapoishi pawe nyumba ya utumwa siku ya kwanza na vipengele 6 vya namna ya kujiondoa kwenye madhara ya lango ya ardhi ya nyumba unayoishi inapomilikiwa kiroho ya nguvu za shetani kwa siku ya pili

✳Somo hili halifundishwi kama ile kawaida ila kila siku MUNGU anampa kitu kipya ili yule atakayesikiliza kwa siku hiyo atapata jibu lake

✳Si watu wengi pia wanalipokea kwa haraka sana mioyoni mwao somo hili na kwa sababu hiyo ROHO MTAKATIFU anarirudia na kurirudia ili lizidi kujengeka ndani yetu

➡Leo tuangalie KUFUNGULIWA TOKA KWENYE KIAPO KILICHOIFUNGA NAFSI YAKO NA HALI YA KIROHO YA ARDHI

➡Na katika kulitazama jambo tuangalie mambo kadhaa ambayo MUNGU ameachilia ndani ya kichwa cha Mtumishi ili yamkini yatufikishe mahali pa kuweza kuingia kwenye maombi na wale ambao kuna viapo vimewafunga wapate kufunguliwa

1⃣Njia mojawapo inayounganisha mafanikio yako kimaisha na hali ya kiroho ya ardhi ni maagano

Mwz 9:13

2Nyk 7:14

➡Anazungumzia juu ya kuiponya nchi yao na kumbuka nchi ni ardhi lenye umiliki halali na ina mipaka kabisa. Biblia ya kiengereza imewaka wazi kabisa inazungumzia juu ya ardhi

➡Sasa tazama kitu ambacho MUNGU alifanya wakati Nuhu ametoka kwenye safina wako watu wachache waliojulikana kama wapo na wanyama na ndege, ukisoma ile sura ya 8 na 9 na alipozungumza nao kwa habari za agano

➡..Anasema ni ishara ya agano kati yangu na nchi na hasemi ni ishara ya agano kati yangu na wewe bali ni ishara ya agano kati yangu na ardhi

2⃣Ishara ya agano hilo juu ya ardhi husika kazi yake ni hizi zifuatazo:

MOJA (i)

Kazi kubwa mojawapo ni kukumbusha kuwepo kwa agano

Mwz 9:13-16

Tazama maneno haya….nami nitalikumbuka agano langu lililoko kati yangu na ninyi…..

➡Kukumbusha kwa watu wote waliohusika na maagano, kiswahili kinakosa lugha iliyo nyepesi sana juu ya neno agano maana tukisema ni mapatano halitoshi au mapatano ya kimkataba linasogea kidogo maana agano ni pana kidogo

➡Jambo ambalo watu wengi hawafahamu Agano haliwezi kuwa Agano isipokuwa kuna kitu cha kiroho kati yake, kunaweza kuwa na mapatano lakini hakuna kitu cha kiroho kati yake

MBILI (ii)

Kukumbusha kuwepo kwa kiapo kwa sababu ishara ni alama ya uhaminifu kwenye kiapo husika

Yosh 2:11-13-19

➡Rahabu alipokuwa amegundua ukombozi wake umekaribia, kivipi ni kwa imani kama Waebrania isemavyo, kwa hiyo hakuangamia pamoja na waovu wengine sababu aliwakaribisha wale wa pelelezi kwa furaha, kwa shukrani na kwa imani

➡Swali la msingi kwanini MUNGU asiwapitishe pembeni ya mji wa Yeriko kwa safari yao ya kwenda Kaanani? Maana mji ule uliangamizwa wote na watu wakao humo isipokuwa Rahabu na familia yake na hata wakati wanaondoka Joshua aliachilia laana ili asiwepo mtu wa kujenga hapo

➡Fahamu ili kilichomfanya MUNGU aende Yeriko ni Rahabu peke yake hakuna kitu kingine chochote kilimpeleka kule maana Rahabu alikuwa na destiny, alikuwa na kitu katika maisha yake na shetani alifikiri akiachilia uasherati ndani yake na kumfunga katika ardhi ya mji wa yeriko hakuna atakaye mkumbuka. Ukitizama utaona tokea pale MUNGU alimwamisha na kumwingiza katika familia ya wayahudi yeye pamoja na familia yake na kumjengea maisha yake ya baadaye

➡Mji waYeriko ulifungwa wote kwa jinsi ya kiroho si ya mwili na ndiyo maana ilifunguliwa kwa jinsi ya kiroho. Gharama zote za kuuzunguka mji ule siku zote 7 kama angeulizwa angejibu ni Rahabu ndiyo maana walinyamazishwa

➡Kuna kitu MUNGU anaweka katika maisha yako na shetani anajaribu kukuzamisha kabisa, haijalishi mahali ulipo, haijalishi shetani amekufunguka kwa namna gani kama ni katika uasherati ama wizi au shida ili kusudi ile ndoto MUNGU aliyoweka ndani yako isije kuchipua SIKIA NENO LA BWANA MUNGU ATAKUFUATILIA NDANI YA YERIKO NA ATAKUTOA NA SI TU KUKUTOA YERIKO NA ATAKUTOA KATIKA UASHERATI atakuweka katikati ya watu amabo kila mtu atashangaa umetokea wapi na hawataacha kusema IMANI yake imemtoa pale na kumfikisha hapa na kusema yuko MUNGU ambaye anaweza kushughulika na ukahaba

➡Ilichukua jeshi lote la Israeli kumtoa mtu mmoja

“Ndiyo maana saa nyingine ninaposimama kwenye madhabahu huwa sijaribiwi kufikiri na wingi wa watu nafikiria kuangalia mtu mmooja ambaye MUNGU amemkusudia”

➡Rahabu aliwaapisha kwa kusema ninawaapisha kwa BWANA, maana yake ninawafunga kwa MUNGU wenu alafu akasema wampe alama ya uhaminifu, wakasema tusije tukaingia hatia ya kiapo ulichotuapisha…funga kamba hii, wale wapelelezi walikuwa wanatembea na kamba nyekundu ni kamba waliyokuwa wanatembea nayo ili ijulikane ni watu wa agano.

TATU (iii)

Kukumbusha masharti yaliyoambatanishwa na kiapo

➡Hakuna kiapo kisichokuwa na masharti ili kuonyesha hakuna agano lisilokuwa na masharti na ni masharti ya kisheria na kihalali ile roho iliyowaunganisha kwenye agano kazi yake ni kufuatilia masharti

➡Ndiyo maana alipowaapisha kwa BWANA walimpa masharti:

✅Uruhusiwi kusema

✅Hakikisha ndugu zako unaowataka waje aje

✅Hawaruhusiwi kutoka nje

3⃣Kiapo cha agano kinabeba wahusika wakufuatiliwa

Yosh 2:12-13

➡Rahabu wakati anazungumza na wale wapelezi hata kuingia kwenye kiapo ndugu zake hawakuwepo lakini aliingiza jina la baba, mama yake na ndugu zake na listi ya vitu walivyokuwa navyo kwa hiyo kila kilichitajwa hakikurusiwa kuwa nje ya nyumba

➡Kuna watu ndani yamioyo yao MUNGU amewabebesha familia, wengine kampuni, wengine kanisa unamwona yuko peke yale lakini hayuko peke yake ndani yake amebeba majina ya watu na vitu vyao na kila mahali anawakumbuka kwamba anao.

➡Kumbuka habari ya yule tajiri aliwabeba ndugu zake aliokuwa anawabeba kwenye pesa na alijua watapita na kuja njia hii hii wale ndugu watano akataka wapelekewe taarifa mapema

➡Joshua alipewa watu wa kusafiri nao na watu wote wale urithi wao ulikuwa kwa Joshua

➡Watu wa namna hiyo katika ulimwengu wa roho wana alama zao ambazo zinafuatailiwa kila wakati na unapoingizwa kwenye kiapo haijalishi kwamba umekubali ama hujakubali swala ni kwamba aliyekuingiza kwenye kiapo ana sauti gani juu yako..kupitia kwenye kizazi, uhalali wa kukaa mahali pamoja

➡Kama mwenye nyumba ameapa kwa mungu wake juu ya ardhi ya hapo kwake ambayo na wewe unakaa maana yake amekuingiza kwenye kiapo

➡Ndiyo maana vipao vya maagano vinasumbua sana maana vinafunga watu hata kama hawajui kama wamefungwa

4⃣Kiapo kinafungamanisha nafsi ya mtu na alichojiapiza

Hes 30:2 (Mahusiano ya kiroho kati ya baba na binti yake)-Daka hiyo ilikuwa aja ya Mtumishi akafundishwa na MUNGU

➡Kwa hiyo kiapo ni kifungo na kiapo kinafunga nafsi na kitu ambacho mtu ajiapiza nacho

➡Rahabu alipowaambia niapie kwa BWANA alikuwa anafunga nafsi za wale wapelelezi kwa kitu watakacho kisema, walijua kabisa huyu anazungumza kitu cha kiagano

Math 5:33-36

➡YESU alizuia viapo mahali ambapo havitakiwi kuwepo, kuna vitu alivitaja kwa maskudi kabisa:-

✅Usiape kwa kichwa chako

✅Usiape kwa mji wa Yerusalem

✅Usiape kwa mbingu na

✅Usiape kwa mji

✅Usiape kwa ardhi

➡YESU kwa lugha nyingine alikuwa anatufundisha kuwa waangalifu katika kuapa maana kuapa ni kuifunga nafsi yako na ardhi na roho iliyoko mahali pale inabana hayo maneno uliyotamka mahali hapo

5⃣Ishara ya agano inafanya wahusika wafuatiliwe katika ulimwengu wa roho kujua ikiwa masharti ya kiapo yanazingatiwa

➡Ukisoma habari za MUNGU na agano lake la ibeahimu, isaka na yakobo utakuta anasema …kile kiapo nilichowaapia baba zako…MUNGU anamwambia mussa sijakufuata kwa ajili yako ila jina lako kwenye kiapo, nifuatilie toka ukiwa tumboni, nicheck utavyoishi na kula saa ikifika nijifunue kwako, nataka kucheck kama unafuata masharti

➡Wewe unaweza kusahau juu ya masharti ya kiapo lakini MUNGU hawezi kusahau

➡Miungu inaingia mikataba katika ardhi kwamba ikufanikishe ama isikufanikishe katika ardhi kwa nini sababu kwenye ardhi ndiko kulikowekwa siri ya mafanikio ya hapa duniani.

➡Ulimwengu mwingine wowote hauna udongo kasoro ardhini na mbegu zote za kiroho ziliwekwa ardhini kwa sabu Sura ya kwanza inasema kila kilichoumbwa kilikuwa ni neno na neno ni mbegu na sura ya pili kila kilichochipuka kilichipuka kutoka kwenye udongo kwa hiyo lile neno lilikuwa mbegu lilivyotamkwa MUNGU akaliweka kwenye udongo kwa hiyo udongo una mbegu za kiroho

➡Siri ya mavuzo yako iko kwenye ardhi, siri ya hali ya hewa iko kwenye ardhi na hii ni ishara ya agano MUNGU aliyoweka na Nuhu kwamba katika vitu alivyowekeana naye na ardhi ipo na kama ipo kuwa na uhakika na mbingu yake ipo maana utegemea na kufanya kazi pamoja

6⃣Badala ya kukimbilia kuvunja agano badilisha na tangua kwanza kiapo ili kuliondoka jina lako na nafsi yako kwenye kifungo

Hes 30:2,10-15

➡Usipotangua kiapo yote yaliyosemwa kwenye kiapo yatatokea

➡Rahabu aliwaapisha kwa BWANA hakulijua agano likoje lakini alijiingiza kwa njia ya kiapo na kuvunja lile agano ilikuwa kutengua kile kiapo kwamba watu wale/ndugu zake wasikae ndani ya ile nyumba/ ndani ya lile agano.

➡Sasa kiapo kile hakitawafunga hata kama agano lipo

➡Shida watu wengi sana wanakimbilia kuvunja agano wasilolijua limefungwaje na limefungiwa wapi na vitu gani vimehusika kwenye agano.

➡Usijaribu kumkwamua mwingine wakati wewe umekwama toka wewe kwanza

 

➡Joshua aliwaambia watu chagueni hivi leo ila mimi na nyumba yangu tutamtumikia MUNGU wakasema nasi tutamtumia huyo MUNGU akawaambia kwanza ondoeni alama za miungu yenu kwanza

➡Ukifunga nafsi kwa kiapo usipotangua kila ulichokisema kitatokea na kinaweza kukusumbua miaka na miaka. Unatangua kwa kutumia DAMU YA YESU maana ni DAMU ya AGANO na ni DAMU BORA kuliko damu zozote zile

7⃣Miguu yako ni lango rahisi la kutumia kuifunga nafsi yako na ardhi katika kiapo cha kiroho

Zab 56:6

Zab 57:6

➡Shetani anatumia nyayo kushika nafsi yako kwa hiyo anaotea nyayo zako. Shetani amekuwekea nyavu kwenye miguu lakini usikii nyavu unasikia moyoni mwako kukata tama, kila ukiganyaga usogei mpaka umeacha kutembea

➡Sasa unaweza kujua kwanini Rahabu alipokuwa anataka kutolewa kule ilibidi wazunguke kwa miguu siku zote zile, sababu miguu ya watu wa MUNGU inaweza kuachilia nguvu za MUNGU inapokanyaga mahali

➡Walipokuwa wanazunguka walikuwa wanatafuta misingi ya ile kuta zile hazikuwa kuta zimejengwa kawaida bali zilikuwa kuta za kiroho, sababu ile ardhi ilikuwa na misingi ya kiroho 7 na ule wa 7 ulifungwa mara 7. Kile kitu na kila mahali kulianguka chini kasoro nyumba ya rahabu misingi mingine yote ilibomoka

➡Kuokoka kwako na kupona kwako si sababu ya matendo yako bali ALAMA YA DAMU YA YESU moyoni mwako

#UFALME_KWANZA

……”Jesus Up”……

*************** ENDELEA  SIKU YA NNE  ***************

SOMO: HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO

 

LENGO YA SOMO:

Kuhakikisha ya kwamba Mafanikio yako yaliofungwa kwenye hali ya kiroho ya ardhi yanafunguliwa

Kumb 6:12, 2Nyk 7:14

SUMMARY YA SIKU 3

✳Pitia somo la siku ya kwanza mpaka siku ya tatu ili kujua tulipotoka na yale mambo ya msingi 5 juu ya kufungua mafanikio yako yaliyofungwa na hali ya kiroho ya ardhi inayofanya mahali unapoishi pawe nyumba ya utumwa siku ya kwanza na vipengele 6 vya namna ya kujiondoa kwenye madhara ya lango ya ardhi ya nyumba unayoishi inapomilikiwa kiroho ya nguvu za shetani kwa siku ya pili na kwa siku ya tatu tulijifunza mambo 7 juu ya kufunguliwa toka kwenye kiapo kilichoifunga nafsi yako na hali ya kiroho ya ardhi

➡Leo tuangalie HATUA ZA KIMAOMBI KWA AJILI YA KUJITOA KWENYE KIFUNGO CHA KIAPO KILICHOUNGWA NA ARDHI

➡Ziko hatua nyingi lakini tujifunze kama mtaji wa kukutoa

1⃣Omba MUNGU akupe kujua eneo la ardhi lililotumika/tumiwa kukufunga nafsi yako kwa njia ya kiapo

Yosh 6:22-23

Yosh 2:8-18

➡Kiapo hiki cha sura ya 6 kilifanyika sura ya 2

➡Kuna maneno ya msingi mawili katika sura ya 2 nataka uone

i)mstari wa 12…..Niapieni kwa BWANA

ii)mstari wa 17….. Sisi tunataka tusiwe na hatia kwa ajili ya kiapo hiki tulichokuapia

➡Sasa mambo mawili ya msingi

i)Kile kiapo kilifunga pande zote mbili kilimfunga Rahabu na kiliwafunga wale wapelelezi

i)Kile kiapo walikiweka kianze kufanya kazi namna gani na katika eneo lipi

➡Walimpa alama ya uhaminifu kuweka katika dirisha na ikashirikia nyumba yake na ule ukuta ulipoanguka lile eneo la nyumba lilipbaki pale pale na Rahabu hakutoka mpaka ametolewa na kwa sababu hiyo kile kipindi cha kiapo kufanya kazi maana alisema mtakapoingi kwenye mji huu mtakapo kaa kwenye nyumba hii waliweka eneo la kiapo

➡Kabla hawajaingia katika ile inchi kile kiapo kilikuwa akiwasumbui maana Rahabu alikuwa anaweza kutoka na kuingia lakini wakikanyaga wana wa Israeli Yeriko kiapo kinaanza kufanya kazi na kiapo kile kilikuwa kinawafunga mpaka maelekezo ya kuwatoa yalipofika

➡MUNGU alijifunga kwenye kiapo na Ibrahimu kuwafanikisha wana Israeli katika nchi ya kaanan wala si misri na akajiwekea na muda miaka 400 na alipowafuata alisema amekumbuka agano langu, alitaka kutimiza kiapo alichomwapia ibrahimu.

➡Misri awakufungwa na kiapo huku kanan kiapo cha ndipo kilifanya kazi ya kuwafanikisha maana kuwafanikisha Misri ni nje ya agano

➡Yusufu alikuwa na upako nje ya agano alibarikiwa nje ya agano, hata ishmail alibarikiwa nje ya gano, essau alipewa eneo la kukaa, ruthu alipewa eneo la kukaa, pamoja ya kwamba MUNGU amewapa lakini alikuwa la kiapo alikuwa na Baraka ya kiagano ndani yake

➡Msihi MUNGU sana akuonyeshe kama ipo ardhi yoyote ambayo imekufunga kwa kiapo, unaweza kufungwa kwenye eneo unaloishi, unalofanyika kazi ama ibada ama kwenye eneo la familia yenu.

2⃣Omba maombi ya TOBA kwa ajili ya mambo mawili makubwa

MOJA

Maovu ya wazazi ya kukufunga kwenye kiapo kinachounganisha ardhi na miungu yao

MBILI

Kwa ajili ya dhambi yaw ewe mwenyewe kujifunga kwenye kiapo cha ardhi..waweza usijue lakini kama umefika katika kiwango fulani cha kutafuta msaada utaelewa

➡ Dan 9,10 TOBA kwa ajili ya dhambi zao na uovu za wazazi wao.MUNGU anaweza kukupa si tu kuombea uovu wa wazazi hata kama hukufanya wewe maana TOBA inakazi nyingi sana

✅Ina zaidi ya kusamehe

✅Kubwa zaidi nataka uone hapa ni kumfungulia MUNGU uhalali wa kisheria kushughulika na kesi yako

➡Baada ya mwanadamu kumkorofisha MUNGU na dhambi kuingia ikaleta mauti mahusiano ya mtu na MUNGU yalikatika ndiyo maana kuna vitu MUNGU hawezi kujibu wala kukupa bila kusema na kuhitaji usiposema hawezi kukusaidia lazima ufanye TOBA na kumwamini YESU kama BWANA NA MWOKOZI wako halafu umfungulie mlango kukusaidia yaani maombi ya TOBA

3⃣Batilisha kiapo hicho juu yako

Hes 30:2,14-15

➡Biblia inapozungumza juu ya kubatilisha kiapo au batili inazungumza juu ya kuondoa uhalali wa hicho kitu juu yako ambayo ni kukuondoa kwenye ushiriki kama jina lako lipo na umeingizwa kwenye kiapo hujui. Mfano kama una cheti batili na ndicho umekitumia kupata kazi anapotokea mwenye nacho na kusema hicho ni batili jua umepoteza kazi

➡Kubatilisha kiapo ni swala la kiroho ambalo unaweza kulitumia kwa DAMU YA YESU KRISTO kwa hiyo unapoanza ngazi ile ya maombi ya toba inakuweka mahali pazuri kwa kuwa na msaada wa MUNGU kuwa upande wako kwa ajili ya kubatilisha maana kama MUNGU hayupo upande wako usijaribu kubatilisha kitu ambacho shetani alishirikiana na watu wengine kuingiza jina lako halafu kwa nguvu zako unasema hii ni batili

➡Bibilia inasema kuna sheria ya ROHO WA UZIMA, sheria ya ROHO WA UZIMA ufanya kazi chini ya DAMU YA YESU, sheria hii ukuacha mbali na sheria ya dhambi na mauti

4⃣Tangua kiapo

➡Kutangua kiapo inahusisha kuondoa uhalali wa vifungo kuendelea kukufunga au kukuzuia

➡Kutangua kunahusika na vifungo

Kubatilisha kunahusika na ushiriki

➡Mfano mtu gari yake ni mbovu unaipeleka garage na fundi anasema kaa chini nikufundishe kutengeneza gari ili ukipata breakdown njiani utengeneze mwenyewe kwahiyo mafundisho haya ni kutaka kukufundisha jinsi ya kutengeneza gari. Na watu wengi awana uvumilivu kupata maarifa ya kutengeneza gari wengi utaka kuacha gari garage na kusema nirudi saa ngapi kuchukua, utafikiri anajua hatua za utengenezaji wa icho kilichoharibiga

5⃣Futa kwa DAMU YA YESU alama za uhaminifu zinzofanya ufuatiliwe na utambulike

➡Na mara nyingine ukitambulika unatambulika kabisa wewe ni wa agano lipi maana kuna mahali wataangalia hadi alama

Yosh 2:17-18

➡Walimwambia weka kamba hii nyekundu maana aliwaambia nipeni alama kiapo tu peke yake hakitoshi, kiapo kinaambatana na alama, ile alama ya kamba nyekundu ina maana fulani. Kamba ikikosekana na nyumba ya Rahabu inaenda chini maana kamba inafanya ufutailiaji uwe mwepesi

➡Alama inaweza kuwa imewekwa ndani ya damu yako, ndani ya mwili na nafsi kuweza kutoonekana kirahisi kwa macho ya nje na alama nyingine ziko kwa jinsi ya nje kama mavazi, pete n.k sasa uzifuti tu wa jinsi ya kawaida kama kuchoma na kutupa ukifikiri umefuta rohoni, bali ni DAMU YA YESU pekee inaweza kuingia ndani na kufuta kabisa

6⃣Kemea mapepo yanayotumia kiapo kukwamisha maisha yako

➡Mahali popote penye kiapo pana agano, mahali popote penye agano pana kitu cha kiroho na ngazi tofautitofauti

➡Na unapo kemea, kemea kwa kutamka kabisa “mapepo mnaofanya kazi kwa uhalali wa kiapo hicho kiapo nimebatilisha, nimetangua, nimefuta alama za uhaminifu hamna uhalali wa kuendelea kukaa ninawahamuru katika JINA LA YESU achia nyumba yake, mafanikio yake, maisha yake, biashara zake…utaongozwa na ROHO MTAKATIFU kutamka ni eneo lipi huyo mtu kabanwa”

➡Ndiyo maana unahitaji kusimama kwenye nafasi yako vizuri maana mapepo yaliyokaa sehemu kihalali uwa yanatafuta kukata rufaa, huwa yanatafuta kukusumbu na kucheck kama unajua kitu unachofanya. Mfano mzuri ni Paulo na Silla walikemea pepo la kijakazi wakaishia jera

7⃣Omba uponyaji wa nafsi hasa eneo la akili ili ziweze kukusaidia zaidi ya mipaka ya kiapo kilichokufunga

Ayubu 32:8

…Na pumzi za mwenyezi uwapa akili

Mwz 2:7

➡Akili ziko kwenye nafsi, akili zimeletwa ndani ya mtu na pumzi ya MUNGU wakati anamuumba mtu. Njia mojawapo ambayo ulimwengu wa roho unatumia kushika nafsi za watu ni kwa kutumia nyazo zao na miguu yao na kwa ajili hiyo kwa sababu miguu ugusana na ardhi maagano mengi na vaipo vingi vilivyopo ndani ya ardhi vinaelekezwa kwenye nafsi na vikifika kwenye nafsi uenda kwenye akili na akili zinakuwa blocked huwezi kufikiri zaidi ya mipaka ya kiapo. Mfano wastaafu akisha staafu kama hajatoka na kufunguliwa kwenye kiapo

Ez 21:21-23

➡Mtu alienda kufanya uganga kwenye njia panda na anawafunga watu kwenye kiapo kwenye njia panda, shetani anaweka jina lako kwenye njia panda kukumaliza kwenye maamuzi, watu wengi wanaenda mpaka njia panda wanashindwa kuamua wanakuwa na mawazo mengi, mipango mingi na ukiwauliza wanakwambia hawajui wafanye lipi maana kimawazo wana mambo mengi

➡Rahabu ilibidi atolewe ili kutekeleza mawazo yake nje ya kiapo. Hujatoka basi umebanwa hapohapo hutatoka. Mfano mtoto amemwamisha shule gafla matokeo yake yanashuka

8⃣Pokea jibu la maombi kwa IMANI ndipo upokee kwa kuona

Mark 11:23-24

➡Kuna mahali pa kusema na kuomba

✳23: Kama unasema sema kwa Imani ukiamini kwamba hayo usemayo yametukia

✳24: Kama unaomba omba amini ya kwamba ulichoomba MUNGU amesikia na kujibu

➡Pokea kwa imani kwanza maana ukishaamini MUNGU amefanya kuna hatua ROHO MTAKATIFU atakupelekea hatua kwa hatua hata kukwambia ulichokiomba kimefika madhabahuni na kimejibiwa kwa hiyo utabadili maombi na kuanza kushukuru

➡Kuna mwingine hatoki pana umemtangazia kufunguliwa kwake…Paulo na Sila waligoma kutoka mpaka walipoambiwa wamefunguliwa kwa hiyo kama unamuhudumia Paulo na sila uwatangazie kufunguliwa kwao

 

#UFALME_KWANZA

……”Jesus Up”……

 

*************** ENDELEA  SIKU YA TANO  ***************

 

SOMO: HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO

 

LENGO YA SOMO:

Kuhakikisha ya kwamba Mafanikio yako yaliofungwa kwenye hali ya kiroho ya ardhi yanafunguliwa

Kumb 6:12, 2Nyk 7:14

SUMMARY YA SIKU 4

✳Pitia somo la siku ya kwanza mpaka siku ya tatu ili kujua tulipotoka na yale mambo ya msingi 5 juu ya kufungua mafanikio yako yaliyofungwa na hali ya kiroho ya ardhi inayofanya mahali unapoishi pawe nyumba ya utumwa siku ya kwanza na vipengele 6 vya namna ya kujiondoa kwenye madhara ya lango ya ardhi ya nyumba unayoishi inapomilikiwa kiroho ya nguvu za shetani kwa siku ya pili, siku ya tatu tulijifunza mambo 7 juu ya kufunguliwa toka kwenye kiapo kilichoifunga nafsi yako na hali ya kiroho ya ardhi na kwa siku ya nne tulijifunza hatua 8 za kimaombi kwa ajili ya kujitoa kwenye kifungo cha kiapo kilichoungwa na ardhi

➡Leo tujifunze JINSI UKIWA ULIOPO KATIKA ARDHI UNAVYOWEZA KUZUIA MAFANIKIO YA MTU ANAYEHUSIKA NA ARDHI HIYO

➡Na tutazame katika mtiririko ufuatao

1⃣Ukiwa maana yake nini Kibiblia?

➡Ni hali ya kiroho inayojidhihirisha katika maisha ya mtu ili kuonyesha ya kuwa eneo hilo la ardhi limo katika adhabu

Ez 15:8

➡Kumbuka tulipotoka 2Nyk 7:14

➡Nchi maana yake ni ardhi yenye mipaka halali, kwa hiyo anavyosema nitaifanya nchi kuwa ukiwa MUNGU anazungumza ardhi yenye mipaka halali kuwa ukiwa

Mwz 1:1-2

➡Hapo mwanzo MUNGU aliziumba mbingu na nchi, nayo nchi ilikuwa ukiwa, utupu na ina giza na kile kitabu cha isaya anasema MUNGU hakuimbua dunia iwe ukiwa bali ikaliwe na watu. Kwahiyo kama MUNGU hakuumba ukiwa na wakati wa uumbaji ukiwa ulikuwepo kumefichika vitu fulani acha nisiseme leo nilitaka tu ujue maana ya ukiwa

2⃣Utaitambuaje ardhi yenye ukiwa?

➡Kwa kuangalia unavyojisikia moyoni mwako unapokanyaga ardhi ya eneo hilo

Yer 4:27-28

..Kwa ajili ya ukiwa nchi itaomboleza..

Yosh 5:14-15

➡unatuonyesha jinsi Yoshua alivyoukabiri Yeriko akatokea jemedali wa BWANA akapopoma kiusouso na kuuliza BWANA aniambia nini mimi mtumishi wake? Malaika alimwambia vua viatu vyako maana hapo unaposimama ni nchi takatifu..maana kuna mahusiano kati ya miguu yako mahali inapokanyaga na uwezo wa kusikia ndo maana Biblia inasema tuvae utayari miguu mwetu

➡MUNGU anaposema nchi takatifu maana yake ameisafisha, ameitenga haina sauti za kukuchanganya tena amekutengenezea mazingira ya kukusikilizisha jambo! Wajengao makanisa wanaweka wakfu ile ardhi maana yake wanaitenga ili iweze kutumika kwa makusudi ya MUNGU na wale wanaokuja pale waweze kumsikia MUNGU akisema bila kusumbuliwa na sauti zingine zilizoko ndani ya ardhi

➡Lile eneo lilikuwa limesafishwa lakini shida ilikuwa Yoshua alichovaa, aliambiwa vua viatu vyako maana yake nini ..Joshua kuna kitu nataka kukusemesha cha kukusaidia juu ya Yeriko lakini huna utayari kuna kitu ulichovaa, kuna mipango uliyonayo, kuna makusudi uliyonayo ambayo hauko tayari kuyaachia lakini unataka nikusaidie..

➡Tatizo si kusikia tu peke yake bali ni ule utayari wa kutekeleza unachosikia. Ndiyo maana wengi husema MUNGU hajanisemesha siyo kweli bali ni wewe umekataa kusikia kuna vitu umeshajiamulia jinsi gani MUNGU aseme kwako

➡Kama ukienda eneo ambalo lina ukiwa utasikia moyoni mwako kuomboleza gafla na huoni kitu kwa jinsia ya nje kinachokusuma kuomboleza

Yer 4:23

➡Ukikanyaga mahali peke ukiwa gafla utasikia upweke moyoni hata kama umezungukwa na watu au utasikia upweke sababu hakuna watu wakati unajua unaweza kukaa bila upweke hata kama hakuna watu

Yer 4:31

Yer 51:29

➡Ukikanyaga eneo lenye ukiwa si tu utasikia kuomboleza ama upweke bali saa nyingine utasikia kuomba maombi ya kuomboleza maombi ya kuzaa kitu, maana utasikia mzigo wa kuomba

Ez 26:20

➡Anazungumzia juu yakusikia moyoni mwako mauti, mahali palipo na ukiwa utasikia mauti ndani yako au kusikia kama umefiwa hata kama hujafika ndiyo maana mtu akifa kinachokuja ni ukiwa na ukiwa ni adhabu kwa hiyo adhabu inapokuja namna hiyo inatuonyesha kwamba haukuwa mpango wa MUNGU mtu afe bali tunakufa kwa sababu ya dhambi zilizokuwa zimeingia kwenye Bustani ya Eden

2Sam 13:20-22

➡Ukiwa wakati mwingine unaunganisha huzuni yenye uchungu ambayo ndani yake inakuwa na hasira na chuki

➡Si kila ukiwa unakaa juu ya ardhi bali kuna ukiwa unaokaa juu ya

✅Mtu

✅Tukio

✅Kikao

✅Mkutano

✅Ardhi

➡Unaweza ukaenda kwenye ardhi ambayo haina ukiwa lakini ameenda mtu mwenye ukiwa kama tamari ukiingia pale anaingia na ukiwa wake na ule ukiwa unafunika ardhi yote ile na kuwaambukiza wote waliokule ndani na wote wanasikia ukiwa

➡Saa zingine unakuta mtu akiwa ofisini anacheka na kutabasamu na kila mtu sasa subiri akifika nyumbani, ni hasira, aongei wala hana utulivu hata yeye hajui shida ni nini maana akitoka gafla eneo la nyumbani unaona anaongea na kila mtu hata wale wa nyumbani wakiwa eneo jingine. Wengine wakiwa kwenye biashara ni ugomvi lakini wakirudi nyumbani ni salama

3⃣Nini matokeo ya ukiwa katika ardhi juu ya maisha ya watu wanaohusika na ardhi hiyo

➡Matokeo kwa ujumla

Jambo kubwa sana utakaloona na kuligundua kwenye mistari ihusuyo ukiwa ni kwamba ukiwa unaweka zuio eneo hilo lisiendelezwe bila kumaliza au kuondoa tatizo lililo fanya ukiwa ukawepo..ukiwa hauji peke yake bali uweka na zuio.

➡Mfano una kiwanja lakini umeshindwa kukijenga au kukiendeleza, kuna sababu nyingi tu za kimsingi lakini sehemu kubwa sana iliyowakwamisha watu ni zuio linalotokana na ukiwa ulioko pale.

Ez 48:8-14

➡Wana wa Israel walikuwa wakipewa maelekezo na nabii Ezekiel kwamba mahali popote pale wanapokuwa kwenye maeneo ya kuishi lazima watoke maeneo mengine kama sadaka kwa MUNGU na hilo eneo linawekwa na kutengwa kwa ni mahali pa ibada na hilo eneo wanapewa makuhani na walawi kujenga

➡Inawezekana umenunua shamba au kiwanja ambacho kina zuio kisiuzwe, katika ulimwengu wa roho kina zuio kisiuzwe, sasa mtu anataka kukiuza wewe mnunuzi ukienda pale ukikanyaga tu unajisikia ukiwa, unajisikia kuomba. Hii ndiyo imewapata watu wengi sana walionunua ardhi za kurithi ambazo familia ziliweka zuio zisiuzwe..Mnunuzi anashangaa sasa kawekeza pesa gafla anaona eneo halisogei na kuendelea tena

Ez 35:9

➡Inawezekana umenunua kiwanja ambacho ukiwa umepewa zuio haruhusiwi mtu kukaa hapo, sasa na wewe unanunua kujenge nyumba gafla wazo la kuendeleza linapukutika hata kama fedha unazo za kufanya hivyo

Zak 7:14

Sef 3:6

➡Kuna zuio si tu kwamba usikae bali kuna zuio eneo hilo usitembelee, unapanga kwenda kwenye shamba ama eneo ulilonunua unajikuta umeshindwa kwenda…Wangapi wamenunua viwanja na mashamba na hawajayatembelea mwaka mzima?

Yer 9:11

➡Magofu…si kwamba watu hawana hela bali kuna zuio la kuendelea kujenga. Katika ulimwengu wa roho kuna kibao kwenye ardhi kikisema uruhusiwi kujenga hapa njoo kwa MUNGU uambiwe ni kwanini

Yer 51:26

➡Umekwama kwenye msingi..jiwe la pembeni anazungumzia majengo ya ibada unachukua kiwanja kwa ajili ya kujenga jengo la ibada inagomea kwenye msingi si kwamba watu hawana pesa bali kuna zuio kwenye kiwanja maana MUNGU hawezi kuagiza kazi akashindwa kulipia, si maskini akageuka ombaomba. Ukiona unafanya kazi ya MUNGU na pesa inakupa shida rudi kwa MUNGU kwa TOBA usijaribu kujihesabia haki, usijaribu kumkemea shetani yawezekana akasema ninakibali cha MUNGU wako kukaa hapa lazima MUNGU akupe kibali na uhalali wa kumtoa

➡Kesho ntazungumza nawe na kukupa mistari yake kwanini ukijenga nyumba inabomoka au kwanini ukijenga nyumba unashindwa kukaa ndani yake au kwa wale wanaofanya biashara bila kujua eneo hilo lina zuio la uzalishaji.

➡Leo tuangalie kwa wale ambao wanaishi ndani ya nyumba iliyowekewa zuio watu kuishi lakini umeng’ang’ana kukaa na huna raha

Isy 13:20-22

➡Saa nyingine MUNGU anaweka zuio na anajua kuna watu wengine watalazimisha kukaa kwa hiyo anaweka vitu vingine ndani kukuzuia..Ukitaka kuona tafuta nyumba yoyote mtaani ambayo haijakaliwa na watu mda mrefu kuwa na uhakika utakuta majini, bundi, mbuni na mbwea..Sasa si kwambii uogope kununua maana si wajua YESU ni mkuu kuliko majini.

➡Sasa wengi ununua tu ama na kukarabati unafanya maombi tu kirahisi rahisi bila kujua namna ya kufanya na MUNGU anajaribu kukusemesha na kukuwekea ishara mahali pale kwamba kuna kitu hajika kaa sawa wewe unalala, uwe na uhakika yale majini yaliyopo mahali pale yamepata nafasi ya kusherekea

➡Yakobo wakati anamkimbia Esau akafika eneo moja linaitwa luzu baadae alipaita betheli akalala gafla aliota, alipoamka alisema kumbe hapa MUNGU yupo, kumbe hili ni lango la mbinguni, alilala mahali ambapo kuna madhabahu chini. Sasa fikiri unauziwa nyumba ambayo ndani yake mtu aliweka madhabahu ya mungu wake halafu unalala ukiota unafikiri utaota nini miungu ya pale na kukupa utaratibu wa kukaa hapo

➡Kuna wakristo wengi sana ambao wanashindwa kukaa kwenye nyumba zao hawalali na hawapati msaada wanaomba na kuomba na kujikuta wanaenda kwa waganga wakipewa pua ya nguruwe wakifiri shetani anaogopa nguruwe wakati mapepo yalimwomba YESU yawaingie wale nguruwe sasa unadanganywa tu. Na wakati mwingine unajikuta unaota ndoto mbaya sababu ni eneo ulilolala

MAOMBI

➡Masomo kama haya ndiyo maana nang’ang’ana kupeleka mstari kwa mstari ili ujue yako kwenye Biblia MUNGU anahitaji kukupa macho ya kuona na kuweza kuweka haya mambo sawasawa. Haya mambo ni halisi kuliko unavyofikiri na yanatesa watu wengi sana

#UFALME_KWANZA

……”Jesus Up”……

 

*************** ENDELEA  SIKU YA SABA  ***************

SOMO: HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO

LENGO YA SOMO:

Kuhakikisha ya kwamba Mafanikio yako yaliofungwa kwenye hali ya kiroho ya ardhi yanafunguliwa

Kumb 6:12, 2Nyk 7:14

SUMMARY YA SIKU 6

✳Pitia somo la siku ya kwanza mpaka siku ya tatu ili kujua tulipotoka na yale mambo ya msingi 5 juu ya kufungua mafanikio yako yaliyofungwa na hali ya kiroho ya ardhi inayofanya mahali unapoishi pawe nyumba ya utumwa siku ya kwanza na vipengele 6 vya namna ya kujiondoa kwenye madhara ya lango ya ardhi ya nyumba unayoishi inapomilikiwa kiroho ya nguvu za shetani kwa siku ya pili, siku ya tatu tulijifunza mambo 7 juu ya kufunguliwa toka kwenye kiapo kilichoifunga nafsi yako na hali ya kiroho ya ardhi na kwa siku ya nne tulijifunza hatua 8 za kimaombi kwa ajili ya kujitoa kwenye kifungo cha kiapo kilichoungwa na ardhi na pia siku ya sita tulijifunza

Leo tuzungumze juu ya HATUA ZA KIMAOMBI ZA KUCHUKUA ILI KUONDOA TATIZO LA UKIWA KATIKA ARDHI ILI UFANIKIWE

Ez 15:8

➡Ukiwa ni adhabu ni hali ya kiroho inayoashiria kwamba eneo hilo liko kwenye adhabu. Shetani aleti ukiwa bali utumia ukiwa kusumbua watu. Ukiwa ni adhabu halali kabisa ambayo MUNGU anaichachilia kufuatata na maandiko kwa sababu kuna kosa kwenye hilo eneo

➡Si mapenzi ya MUNGU mahali pawe na ukiwa maana MUNGU aliumba dunia ikaliwe na watu pasipo ukiwa. Ukiwa ni adhabu

➡Hatua hizi zitakuwa mtaji kwako angalau utapata mtaji mkubwa sana wa kuomba utakapotaka kuomba

1⃣Omba MUNGU akupe ufahamu ikiwa ardhi inayohusika na nyumba inayokuhusu inayo tatizo la ukiwa

Yer 4:27-28

2Nyk 7:14

➡Nchi ni ardhi yenye mipaka halali ya kiumiliki kwa hiyo unaposoma kwenye Biblia juu ya nchi itakufungulia macho kwenye vitu vingi

➡Si kila ardhi yenye matatizo ina ukiwa na si kila mahali penye ukiwa huo ukiwa uko kwenye ardhi unaweza ukawa juu ya mtu kama ilivyokuwa kwa Tamari. Unaweza kuombea hiyo ardhi mpaka ukachoka maana ukiwa haupo kwenye ardhi bali mtu aliokuja nao ameambukiza eneo hilo

➡Ukishajizoeza kumsikiliza MUNGU juu ya kukusemesha kwenye ukiwa utajua tu ukiwa huu unasababishwa na nini je ni ndani ya mtu ama ndani ya ardhi

➡Kiroho moyo wa mtu umeumbwa kama ardhi, Biblia inasema NENO ni mbegu linapandwa katika ardhi na linapandwa katika moyo, moyo ambao hauwezi kupokea NENO linapandwa pembeni shetani anakuja kulichua, udongo tifutifu unafananishwa na moyo ambao uko tayari kwa ajili ya kupokea. Kwa hali ya udongo inavyofanya kazi kiroho na hali ya moyo au ya kiroho katika nafsi yako kuna vitu ambavyo vinafanana ambavyo ukifuatilizia vinaweza kukusaidia. Ni rahisi sana kwa moyo wako kudaka kitu ambacho ardhi inasikia, inaposikia moja kwa moja kama ardhi iliyiopo mahali hapo ina maombolezo ndani yake kule kuomboleza utakusikia ndani, yaani ukisha kuja na kukanyaga utasikia maombolezo ndani yako

➡Wapo watu wanakaa bila kumalizia nyumba miaka 10 na hana maelezo kwanini hawezi maliza, sasa si kila mtu aliyeshindwa kumalizia nyumba na kujenga swala ni ardhi, sasa tatufa kiwakilishi chochote iwe ramani, hati halafu omba mpaka MUNGU aseme ndani yako na utasikia tu.

➡Utakapoanza kusikia hali ya ukiwa usikimbilie kuomba maana lazima ujue hiyo hali ina ujumbe gani ndani….unasema nitajuaje? Jana tulisoma Mwz 1:2

➡ROHO WA MUNGU alitulia pale hakufanya kitu chochote hakubadilisha mazingira yaliyokuweko kazi yake ilikuwa kufunua kilichopo pale, kulikuwa na ukiwa, kulikuwa na utupu

➡Nguvu za MUNGU zinaweza kushuka mahali hazibadilishi kitu zinakueleza shida iliyoko, kwa hiyo ile kukanyaga na ukasikia ukiwa haina maana ROHO MTAKATIFU amemaliza kukusemesha lazima uwe na UTULIVU kama ROHO MTAKATIFU ametulia na wewe unapaswa kutulia ili amalize kukukamilishia kilichoko ndani sababu inawezekana kati ya hivi

CHA KWANZA

Unapewa taarifa na ROHO kuwa eneo hilo liko chini ya adhabu ya MUNGU iitwayo ukiwa

➡Ukiwa kwenye sura ya kwanza ya mwanzo ulichanganyika na utupu na giza, ukiwa ule wa Tamari ulichanganyika na hasira na uchungu na kulipiza kisasi, unaenda ukiwa mwingine umenyanganya furaha ndani, mwingine una maombolezo, ukiwa mwingine unanyang’anya utoaji sadaka kanisani.

CHA PILI

Unataka kukuonyesha kwamba kuna kosa lililofanywa na mtu au watu waliomiliki au waliokaa eneo hilo kabla yako lililosababisha hiyo adhabu

Ez 15:8

✳Vipengele unavyoona hapa

✅Inakuonyesha wazi kabisa nchi itakuwa ukiwa sababu imekosa hivyo ukiwa ni adhabu

✅Kuna kosa limefanyika na mtu aliyekuwa anamiliki kabla yako au ni kosa lako wewe mwenyewe, maana kuna adhabu za kimaonezi katika ulimwengu wa roho na kuna adhabu za kihalali na zote hushughulikiwa tofauti

✅Kosa hilo liwe limefanywa na wewe au mtu mwingine linatakiwa kurekebishwa kwa TOBA la sivyo eneo hilo la ardhi haliwezi kuendelezwa ipasavyo

➡Ukikanyaga eneo ukasikia hiyo hali hizi taarifa tatu huwezi kuzikosa ndani ya ROHO MTAKATIFU

Pana

✅Adhabu

✅Kosa

✅Hilo eneo lirekebishwe au hilo tatizo lirekebishwe la sivyo haliwezi kuendelezwa kabisa

➡Kwa hiyo taarifa hizi unapopewa zinakusaidia namna ya kujipanga. Saa nyingine unapoenda kuomba MUNGU anaweza kusema na wewe kwa njia ya ndoto kwa sababu kwa njia ile ya kawaida ndivyo Biblia inavyotaka uwe na uwezo wa kumsikia MUNGU kwa njia ya ROHO MTAKATIFU maana yeye ni muhusika Mkuu wa kukushirikisha mambo ya MUNGU na mambo yote katika ulimwengu wa roho sasa si kila mtu anauwezo wa kumsikia maana wengi wetu hukosa utulivu au si wengi wanaweza kudaka ndiyo maana MUNGU husema mara nyingi kwa njia ya ndoto kama alivyosema na Yakobo alipolala eneo liitwalo luzu baadaye akaliita betheli aliota ndoto na ishara katika ile ndoto MUNGU alimwonyesha kwamba chini ya ardhi ile kulikuwa na madhabahu

➡Sasa eneo ulilolala je linamilikiwa na nani ama kuna madhabahu ya nani chini ya ardhi. Mara nyingi sana watu wanapoota hawafuatilii hizo ndoto kujua maana yake nini lakini mara nyingi unataarifiwa kujua kilichopo

2⃣Omba TOBA kwa MUNGU kwa ajili ya maeneo yafuatayo:

2Nyk 7:14

➡Haisemi na kuwaponya wao, wataomba TOBA wao lakini MUNGU ataiponya nchi, hazungumzii juu ya Taifa bali ni ardhi, anazungumzia juu ya kuiponya ardhi inayoombewa. Huwezi kuponya kitu ambacho hakijaugua ama hakiko sawasawa.

➡Kuna aina fulani ya maombi yanaruhusiwa kupita na kuna aina fulani ya maombi hayaruhusiwi mpaka ardhi inayohusika imepokea uponyaji.

➡Unapoomba TOBA lazima uombe kwa IMANI si kwa mazoea, kwa Imani maana yake lazima uwe na mstari wa kusimamia kwenye Biblia na kujua ni kitu gani unachotaka kwenye huo mstari

Ebr 11:1

➡Huwezi kuomba kitu kwa IMANI bila kuwa na uhakika na kitu unachokitarajia

Rum 10:17

➡Unapewa mstari usitumie mstari sikia kilichoko ndani ya mstari tumia ulichosikia maana wengi sana wanatumia mstari hawatumii wanachosikia kwenye ule mstari halafu wanashangaa kwanini hawapati kilichoko ndani ya mstari sababu MUNGU hajasema IMANI inakuja kwa NENO lililoko pale bali huja kwa kusikia na kusikia huja kwa NENO  la KRISTO.

➡NENO lina sauti ndani yake ile sauti inapoachiliwa inakuachilia kitu kinaitwa ufahamu, kwa IMANI twafahamu, inaachilia kitu kinaitwa uhakika sababu IMANI ni uhakika, imani huachilia picha ndani yako katika ulimwengu wa roho kwa jinsi ya kawaida usingeona

➡Kuna TOBA za aina nyingi ndani ya Biblia na zina kazi yake tofauti tofauti kwa mfano kuna TOBA ya kuingia kwenye UFALME WA MUNGU na kuna TOBA ya kukaribisha UFALME WA MUNGU mahali ulipo

➡Watu wengi ukiwaambia tubu wanaanza kujihesabia haki kwa sababu wao wana aina moja tu ya TOBA, unatubu kama fire escape ili usiende motoni kwa hiyo wao wana aina moja tu ya TOBA, kukwepa jehanamu lakini ni kwa sababu hawajajua uwanja mwingine wa TOBA

Math 4:17

➡Hakusema tubuni kwa maana safari ya kwenda mbinguni imekaribia kwa hiyo huwezi simamia huu mstari kwa ajili ya kwenda mbinguni unasimamia huu mstari kwa ajili ya mbinguni kuja mahali ulipo

➡TOBA inakupa maandalizi ya ndani, badilisha mtazamo wako na kuwa tayari kuupokea mfumo mpya unaokuja

➡Lakini pia kuna TOBA ya kukuingiza kwenye UFALME WA MUNGU, kuna TOBA ya kuombana msamaha ninyi kwa ninyi.

➡Hapa tunazungumzia si watu walioko juu ya ardhi bali shida ya watu walioko juu ya ardhi wanazopata kutoka kwenye ardhi na MUNGU anadai TOBA ya hao watu itakayomfanya aponye ardhi yao ili apate kuwasikia zaidi ya kiwango walichokuwa wanaomba aponye ardhi yao ili maisha yao yabadilike, aponye ardhi yao ili waweze kufuga bila shida, aponye ardhi yao ili ardhi iwaruhusu kumalizia nyumba zao na kujenga lakini lazima ardhi ipokee uponyaji na huu uponyaji MUNGU anadai uje kwa TOBA

➡Kwa hiyo unapoingia kwenye TOBA ndani yake angalau kuna vitu 3 unapaswa kukumbuka

MOJA

Omba toba kwa ajili ya kuvunja au kutofuata masharti ya MUNGU yanayohusu ardhi hii

➡MUNGU anapokupa eneo la kukaa lina masharti na katika mazingira ya Agano jipya watu hawajajua namna ya kuunganisha kati ya Agano la kale na jipya. Mfano kuna ardhi imewekewa zuio isiuzwe, MUNGU anaweka masharti katika eneo unalokaa haruhusu madhabahu ya miungu mingine, sasa usijaribu kuweka madhabahu za miungu mingine gharama yake ni kubwa sana. Na ROHO MTAKATIFU anakuwepo mahali hapo kukusadia na kuelewa masharti ya MUNGU

➡Si watu wengi wanaelewa kwamba wanaweza kukorofisha masharti na ukakwama, maana hakuna eneo lisilokusudiwa kitu, maana yake usinunue kiwanja bila kuwauliza watu wa mpango miji kuna nini wamepanga kwenye eneo hilo

MBILI

Unaweza kuomba TOBA kwa kuchanganya MUNGU na miungu

Wakristo wengi wana shida ya kuchanga MUNGU na miungu mahali wanapoishi na mahali wanapofanyia biashara na kazi, leo wanasali kanisani kesho wameenda kwa waganga

➡MUNGU ni MUNGU mwenye wivu anataka heshima yake peke yake ukimchanganya namna hiyo ananyamaza kwa sababu hawezi kupokea utukufu na mapepo, kwa manana haitajulikana nani kafanya kwa hiyo anaamua kunyamaza na kuweka pingamizi kwamba huwezi kufanikiwa kwa stahili hiyo kama hujafanya TOBA hutafanikiwa

TATU

Kuomba kilichosababisha shetani akapata nafasi ya kumiliki eneo hilo na kuweka masharti yake haijalishi wewe umehusika au amehusika mwingine

3⃣Omba MUNGU aondoe zuio, sababu ukiwa ni adhabu kutoka kwa MUNGU

Popote ulipokwama omba MUNGU akuondolee zuio yaani pale ulipozuiliwa

Malaki 1:3-4

➡Si shetani anaangusha bali MUNGU anaangusha ndiyo maana anasema ondoa zuio ukishatubu mwambie MUNGU aondoe zuio

4⃣Kemea viondoke vyote vilivyokaa kwenye eneo la ardhi hiyo unayoiombea iliyoshindikana kuindeleza

Isaya 13:19-22

➡Kuna vitu ambavyo vinapata nafasi kihalali kabisa kukaa mahali hapo ambavyo vinaweza kukutesa sana kwa hiyo lazima uweke eviction order

5⃣Omba madhara yaliyotokea kwenye eneo lile yaishie

Sababu umeomba

✅Toba,

✅zuio likaondoka,

✅umekemea nguvu za giza zilizokuwepo ndani

✅sasa omba uponyaji upite maana kuna madhara yaliyotokea, uzalishaji umepotea MUNGU arudishe tena, madhara kwenye ndoa MUNGU aweze kuiponya ndoa, huduma yako imeharibika MUNGU aweze kurudisha kibali tena, omba uponyaji kwenye kila eneo ufugaji wako na kila madhara yaliyotokea

➡Kama ni mwombaji utajua ya kwamba unahitaji kuomba na kuomba na kuomba na kuomba mpaka ndani yako usikie umevuka kumbuka MUNGU alipokuwa anamtoa Rahabu walilazimika kuzunguka siku 6 sababu kulikuwa na misingi kwenye ardhi ile ambayo ilitakiwa kushughulikiwa kila siku

➡ROHO MTAKATIFU atakusukuma kama unaona ile hali uliyoikuta wakati unaoomba ya kuomboleza ukirudi kwenye lile eneo hali haijaondoka maana yake hujamaliza kazi endelea kuomba mpaka ile hali imeachia maana utaona kuna mabadiliko ndani

 

#UFALME_KWANZA

……”Jesus Up”……

*************** ENDELEA  SIKU YA NANE  ***************

 

LENGO YA SOMO:

Kuhakikisha ya kwamba Mafanikio yako yaliofungwa kwenye hali ya kiroho ya ardhi yanafunguliwa

Kumbu kumbu la torati  6:12, 2 Nyakati  7:14

SUMMARY YA SIKU 7

✳Pitia somo la siku ya kwanza mpaka siku ya tatu ili kujua tulipotoka na yale mambo ya msingi 5 juu ya kufungua mafanikio yako yaliyofungwa na hali ya kiroho ya ardhi inayofanya mahali unapoishi pawe nyumba ya utumwa siku ya kwanza na vipengele 6 vya namna ya kujiondoa kwenye madhara ya lango ya ardhi ya nyumba unayoishi inapomilikiwa kiroho ya nguvu za shetani kwa siku ya pili, siku ya tatu tulijifunza mambo 7 juu ya kufunguliwa toka kwenye kiapo kilichoifunga nafsi yako na hali ya kiroho ya ardhi na kwa siku ya nne tulijifunza hatua 8 za kimaombi kwa ajili ya kujitoa kwenye kifungo cha kiapo kilichoungwa na ardhi na pia siku ya sita tulijifunza, na mwisho siku ya saba tulijifunza  hatua 5 za kimaombi za kuchukua ili kuondoa tatizo la ukiwa katika ardhi ili ufanikiwe

➡Kuna mistari michache nataka nikupe halafu tutaingia kwenye maombi,na mistari hii pia ni sehemu ya somo tulilonalo hali ya kiroho ya ardhi inavyohusika na kufungwa au kufunguliwa kwa mafanikio yako

➡Leo kuna jambo ninalotaka kwenda nalo na kusimama nalo kwenye maombi nalo ni KUFUTA MANENO YALIYOPO KWENYE ARDHI YANAYOKWAMISHA MAFANIKIO YAKO

2Kor 3:12-18

➡Alimuuliza MUNGU maswali na majibu yake alipelekwa Agano la kale, alikuwa anamwambia sisi ni wa Agano jipya kwa hiyo nijibu kwenye Agano jipya usinipeleke kwenye Agano la kale huko si kwetu lakini kila akiomba MUNGU alikuwa anampeleka kwenye Agano la kale, akaomba tena MUNGU ndipo akamleta kwenye mistari hii

➡Nguvu za MUNGU zilipokuwa zinapungua katika maisha ya Mussa na kung’aa kwake kwenye sura kunapungua waisraeli walikuwa hawajui kwa sababu ule utaji umefunika, hawawezi kuona mabadiliko yaliyoko, naye alikuwa akirudi kwenye uso wa BWANA anaondoa ule utaji anakaa na MUNGU akitoka huko uso unarudi umeng’aa halafu anarudi tena kujifunika

➡Kwa lugha iliyonyepesi kabisa ukitaka kusoma Agano la kale usisome kwa jicho la Agano la kale hutaelewa soma Agano la kale kwa jicho la Agano jipya

➡Biblia inasema ukisoma Agano la kale kwa jicho la Agano la kale utaji utakukalia na fikra zinakuwa nzito huwezi kuelewa kilichoko ndani…Biblia inasema lazima kwanza utizame kutoka kwenye sura ya KRISTO

➡Unaposoma Biblia usiisome kwa kuigawa maana Biblia ni kitabu kimoja ila ndani yake kuna maagano yako ndani yake ambayo yanaweka nyakati na mitazamo ya MUNGU kwa kuwaangalia wanadamu na mitazamo waliyonayo. Agano lililo bora na lililo kubwa zaidi kuliko yote ni Agano Jipya na ndiyo maana baada ya hapo hakuna Agano jingine lakini kabla ya hapo kuna maagano mengi sana, Agano jipya halikuja kufuta maagano yaliyotangulia bali kukamilisha na kuturahisishia kuelewa vitu maana tunatizama kwa sura ya msalaba maana katika Agano la kale vilikuwa vivuli na katika Agano jipya tunaviona kuwa halisi

➡Ndiyo maana DAMU YA YESU katika Agano jipya inaenda kushughulikia mpaka makosa yaliyofanyika katika Agano lililotangulia. DAMU YA YESU inajibu ndani yake

Yer 22:29-30

*2Nyk 7:14….*Kumbuka tafsiri ya nchi…ni ardhi yenye mipaka halali ya kiumiliki

➡Yule mtu kakataa kusikia sauti ya MUNGU kwa sababu amefanikiwa, yuko vizuri sasa MUNGU anasema ngoja niseme na ardhi iliyoko chini yako. MUNGU aliiambia ardhi iandike

Kumb 31:28

Kumb 32:1

➡Anasema niitieni wazee katika kabila zenu na viongozi wa kijeshi-maakida nikutanisheni sababu kuna vitu nataka kuviweka kumbukumbu kwenye mbingu na nchi kwenye ardhi wasikie na wao ili ardhi iwe shahidi na mbingu iwe shahidi

➡Ni maneno alitaka yakae kwenye ardhi kama kumbukumbu

Yoh 6:63

➡YESU anasema roho ndiyo ijuayo uzima mwili haufai kitu. Maneno niliyowaambia ni roho tena ni uzima, maneno ni roho yanabeba kilichoko ndani ya neno, maneno ya YESU yamebeba uzima kwa hiyo ni roho inayobeba uzima kwa hiyo kama ni maneno ya mauti ni roho iliyobeba mauti

➡Kwa maneno yakikaa kwenye ardhi uhai wake, kudumu kwake kunategemea roho iliyoambatana na hayo maneno. NENO la MUNGU li hai maana limebeba uzima wa MUNGU ndani na ROHO MTAKATIFU anapeleka kile MUNGU alichokusudia

Uf 12:15-17

➡Siyo Taifa ni nchi=ardhi ikamsaidia mwanamke.

MUNGU aliweka ardhi kazi yake mojawapo ni kumsaidia mtu anayekaa juu yake afanikiwe, kumsadia mtu yuko juu yake ashinde vita. Ardhi ni uwanja wa mapambano lakini ni mpiganaji hodari sana. Mtu akiamua kupigana na wewe na ardhi ikakaa upande wake utapata shida sana kushinda lazima  uwe unajua kitu cha kufanya, na ukijua hiyo vita hatakushinda. Wachahe sana wanaojua vita inaweza kupelekwa katika ardhi na hawajua kwamba ardhi iko pale kukusadia

➡Mwanamke ni kanisa, maana kuna kitu anachotakiwa kuzaa kuna kusudi la MUNGU kwa ajili ya kanisa kuwa pale na shetani kila wakati yuko hapo kutaka kumeza kitu kinachotoka, ndiyo maana kila aliye okoka ndani yake amebeba NENO la BWANA ana mimba ya ROHO MTAKATIFU ndani yake anatakiwa kuzaa kitu katika maisha yake na ardhi iko hapo kwa ajili ya kumsaidia

➡Biblia inasema kaeni vizuri ardhi=nchi isije kuwatapika, maana yake inauwezo wa kumeza kitu bila kukiharibu na inauwezo wa kukitapika

Math 26:28

➡Maana yake mojawapo check DAMU ilivyoandikwa na ndivyo inavyotumika kwa hiyo wakisema inamwagika maana yake unaweza kuimwaga, wakisema DAMU ya kunyunyiza maana yake unaweza kuinyunyiza. Kwa hiyo inategemea MUNGU anakupa mstari gani wa kusimamia

➡Unapomwaga Biblia inasema inaondoa/inasafisha na kila kitu ambapo kimeambatana na hayo maswala kinaondoka.

➡Humwagi DAMU ya YESU kutoka kwenye nafasi yoyote tu, nafasi unayokuwa nayo katika ulimwengu wa roho lazima ujifunze kusimama nayo kwa IMANI, nafasi ambayo unaweza kumsaidia mtu ambaye hamjui YESU hataki kwenda mbunguni, hajaokoka, amezungukwa na dhambi na bado MUNGU anaweza kuingilia kati na kumsaidia ni nafasi ya kikuhani

➡Tumenunuliwa kwa DAMU YA THAMANI na MUNGU ametufanya kuwa makuhani na wafalme kwa MUNGU wetu nasi tunamiliki juu ya nchi. Unamiliki juu ya ardhi kwa kutumia nafasi mbili kubwa nafasi ya Kikuhani na nafasi ya Kifalme. Kuingia huko unabadili tu nafasi kwa kinywa chako, unasoma NENO la MUNGU mpaka imani yako inakaa sawa

➡Wana wa Israeli walikuwa wanamkorofisha MUNGU na wanaanza kupigwa na tauni ila Mussa alikuwa anasimama kama kuhani na tauni inakoma si kwa sababu wale watu wametubu bali sababu kuhani ameomba TOBA

➡MUNGU anatafuta mtu ambaye atasimama kama kuhani, na ukisimama kama kuhani una ruhusa ya kuchukua na kuitumia DAMU YA YESU maana iko kwenye madhabahu. Kwa hiyo ukipaka DAMU, DAMU ni uhai, uhai wa ile DAMU unatokea saa hiyo hiyo kwa hiyo ukimwaga DAMU YA YESU uhai wa YESU unatokea maana yake ROHO MTAKATIFU anatokea saa hiyo hiyo

➡Wapo wengi ambao wanashindwa kulala vizuri ila wakiachilia DAMU YA YESU wanalala bila shida. Jifunze kufanya mazoezi binafsi achilia DAMU YA YESU kwenye ardhi kwa kutunza kumbukumbu kwa kutofanikiwa kwako

#UFALME_KWANZA

……”Jesus Up”……