Iraq kwenye Biblia

Israel ni taifa ambalo limetajwa sana kwenye Biblia kuliko taifa lingine lolote, je! Unajua ni taifa gani ambalo linatajwa sana kwenye biblia badala ya Israel?, ni Iraq; Majina yaliyotumika kwenye Biblia ni Babeli, Shinari na Mesopotamia.

 • Bustani ya Heden ilikuwa Iraq.
 •  Nuhu alijenga safina nchini Iraq.
 • Mnara wa Babeli ulijengwa Iraq.
 • Ibrahimu alitoka Uru wa wakaldayo, ambayo iko kusini mwa Iraq.
 • Rebeka mke wa Isaka alitoka Nahori ambayo ni Iraq.
 • Yakobo alikutana na Raheli nchini Iraq.
 • Yona alihubiri Ninawi ambayo iko Iraq.
 •  Ashuru ambayo ni Iraq iliyashinda makabila kumi ya Israel.
 • Amos aliililia Iraq.
 • Babeli ambayo ni Iraq iliharibu Yerusalemu.
 • Danieli alitupwa kwenye tundu la simba huko Iraq.
 • Meshack, Shedrack na Abednego walitupwa kwenye moto huko Iraq.
 • Belshaza mfalme wa Babeli aliona maandishi ukutani huko Iraq.
 • Nebukadreza mfalme wa Babeli aliwapeleka utumwani Iraq Wayahudi.
 • Ezekieli alihubili huko Iraq.
 • Petro alihubili Iraq.