KUOMBA KWA KUNENA KWA LUGHA KUNAVYOMSAIDIA KIJANA KUISHI MAISHA YA MAFANIKIO YENYE FAIDA

Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu. Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.RUM. 8:26-28

UJUMBE.

  1. Jizoeze kutathimini maisha yako yana faida kwa kiwango gani.

Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida. Ila ikiwa kuishi katika mwili, kwangu mimi ni matunda ya kazi; basi nitakalolichagua silitambui. Ninasongwa katikati ya mambo mawili; ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo maana ni vizuri zaidi sana; bali kudumu katika mwili kwahitajiwa zaidi kwa ajili yenu. FLP. 1:21-24.

Tathimini maisha yako ukiwa bado na nguvu ya kupokea tathimini yako usisubiri mambo yaharibike ndipo ufanye tathimini. Kwa hiyo jitathimini mara kwa mara ili upate kufanyia kazi tathimini yako.

Katika wafilipi tuliyosoma, Paulo katathimi maisha yake na kaona ana faida lakini hata akifa atakaa na Bwana kwa hiyo anaona kila mahali kuna faida.

Vijana wanataka kutathimini maisha yao wakiwa watu wazima ila nakushauri jitathimini sasa.

Vijana wanaokunywa sumu wamejitathimini na kujiona hawana faida. Kwa hiyo anajiona ana hasara na ndio maana anajiua. Kama uko kazini na hauna faida  uwe na uhakika kwa utapunguzwa kazi.

Je tokea umekuwa ndani ya Yesu je anapata faida kwako, je ufalme wa Mungu baada ya wiki au mwezi au mwaka una ingiza faida gani?

Kened raisi wa Marekani alisema  usiwaze kuwa taifa litakufanyia nini bali wewe utalifanyia nini taifa lako?

Nchi yetu ina vijana wengi sasa kama hawana faida kwa nchi ina maana wanaingiza taifa hasara. Je kufanikiwa kwako wewe kuna faida gani.

2.Mungu anao mpango aliokupangia kwa ajili ya maisha yako

Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.YER. 29:11

Mungu hakuleti duniani ili akutafutie mpango wa kufanya balikuna mpango wake unaohitaji mtu kama wewe na ndio maana kakuleta duniani.

Tatatizo kubwa ni kuwa watu wanashindwa kuunganisha maisha yao na mpango wa Mungu.

Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.EFE. 2:10

Sasa unganisha na ile Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

RUM. 8:28.

Kama unasoma vizuri biblia utaona maneno haya

?Mpango au mawazo.

?Kusudi au shauri.

?Utakuta hatua

?Utakuta njia

Kusudi linaeleza sababu  na mpango unajibu swali la kwa namna gani.

Swali la kwanini linajibu maono au kusudi.

Mpango unajibu swali la kwa namna gani.

Unaweza ukawa na mpango na usijue njia na unaweza ujue njia  pia hakikisha unajua na hatua maana maandiko yanasema hatua za mwenye haki zaongozwa na Bwana. Hakikisha hatua za kusogea mbele unazijua.

Mungu ndiye anajua kwanini alikuleta. Hivyo muulize Mungu

?Mpango

?Njia

?Hatua.

Somo hili litajibu maswali mengi sana waliyouliza vijana Facebook na email.

Kitu chochote ambacho mtu hajui kwanini kipo uwe na uhakika anakitumia vibaya.

Mfano. Wangapi wanajua bangi ni mbaya na wangapi wanajua kwanini iliumbwa. Maana ukisema mwanzo unaona Mungu katika uumbaji aliumba vitu na akasema kila kitu ni vema

Sasa kwa kuwa bangi inatumika vibaya sasa Mungu anaweka sheria kwa kutumia  vyombo vya dola kuzuia bangi.

Hadi siku tukijua vizuri  ndipo ataondoa katazo hilo.

  1. Maombi yanakusaidia kupambana na vikwazo katika maisha yako

Hamna kitu kibaya kama kutokujua kwanini upo duniani.  Mungu alipokuwa anasema na mimi kwenye huduma nilianza kumuuliza Mungu inatakiwa nifanye kitu gani.

Sasa baada ya kuokoka lazima ujue kuna kazi yako ya kufanya hapa duniani na si suala la kwenda mbinguni tu ila pia kuna kazi ya kufanya hapa na ndio maana upo duniani.

Kwa hiyo Mungu akipiga hesabu na anaona una faida hapa duniani. Sasa shida inakuja ambapo hujui kusudi lako hapa duniani na unaanza kuishi kwa kuiga au unaenda kwenda kwa mkumbo. Na mimi wakati ule nilijua kumtumikia Mungu ni kuwa  Mchungaji mchungaji hivyo nikaanza kujiandaa kuwa mchungaji.

Sasa kumtumikia Mungu lazima uwe Mhubiri kuna kazi nyingi sana ndani ya Mungu  za kufanya. Sasa kuhubiri au kushuhudia kila mtu anajua maana biblia inasema kila aliye na mwana anao ushuhuda.

Basi nikaenda kwenda chuo cha biblia ila ahsante Yesu sikuanza Mungu alinizuia. Ahsante Yesu hata mke wangu alinisaidia kupiga breki.

Maana wakati ule nilijua kazi nyingi ya Uinjilist lakini Mungu aliniita kuwa Mwalimu. Na mke wangu alikuwa anchunga sana utumishi wangu. Maana nikipata mialiko alikuwa anauliza kuwa je ni semina au mkutano wa injili. Akiona tofauti anasema hapana hatukuitwa kuwa wainjilisti. Kwa kweli namshukuru sana kwa kunishauri na kulinda utumishi huu.

Biblia inasema  Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana Bwana ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume. Yeremia 31 : 22

Na  na Mungu alipomuumba mwanamke toka kwa mwanaume alitumbia mbavu maana yakekazi ya mbavu kulinda vitu vya thamani katika mwili yaani moyo na mapafu Na vingine. Kwa sababu hiyo kama mbavu ambavyo hulinda vitu vya thamani katika mwili mdivyo hata mwanamke anamlinda mume wake.

Sasa ndio tunaona huduma ya ualimu sasa inapata heshima yake.

Kujua mpango wa Mungu  ni hatua ya kwanza ila kutembea ni hatua nyingine

VIKWAZO KATIKA KUTEMBEA KATIKA KUSUDI LA MUNGU.

  1. Tabia yako

Mfano wa Rahabu.

Kwa imani Rahabu, yule kahaba, hakuangamia pamoja na hao walioasi; kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi kwa amani. EBR. 11:31

Rahabu alikuwa kahaba  ila hakuangamia kama wengine ya Yeriko. Na hela alikuwa nayo maana alifanikiwa sana na alikuwa na mafanikio na hayana faida katika ufalme wa Mungu.

Lakini alikuwa na imani na aliweza kuwatambua kuwa hawa ni wapelelezi walipokuja kwake maa a wengine waalijua ni watu wabaya lakini yeye aliona ni watu ambao wamebeba future yake.

Na aliomba kuwa watakapomtoa yeye alisema watoke na wengine wanaoambatana nae.

Tabia inaweza kukukwamisha katika kmtumikia Mungu. Lakini iko dawa katika maombi ya kuondoa

  1. Ugonjwa pia ni kiwakwazo kwako kumtumikia Mungu.

Siku hizo Hezekia aliugua, akawa katika hatari ya kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, BWANA asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona. Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba BWANA, akasema, Ee BWANA, kumbuka haya, nakusihi, kwamba nimekwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana.

ISA. 38:1-3 SUV

Ukisimama kwenye kusudi la Mungu. Lazima Mungu atapangua ugonjwa uliomo ndani yako

Warumi 8:28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. RUM. 8:28 SUV

  1. Maaumzi ya kwako binafsi.

Kuna kijana alianza kuvuta sigara na kunywa pombe alipokuwa form three.  Na alipokuja kwangu nilimuuliza nani kakufundisha , alisema baba yangu maana alikuwa anamtuma kununua sigara na pombe na yeye alikuwa anaonja. Baba yake alikuwa anasema mwanangu usinywe pombe wala kuvuta maana ni mbaya. Lakini yeye alikuwa anaonja kidogo kabla ya kupeleka kwa baba yake.

Maandiko yanasema Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya.Kwa maana agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya.Waebrania 9:16-17

Kwa  hiyo ile tabia yake ilipata nguvu  baada ya baba yake kufariki

Ahsante Yesu alikubali na alianza hatua kwa hatua na nilijua iko mbegu katika neno la Mungu. Ambayo mama yake alikuwa anapanda na ilikuwa bado.

Nilienda mahali nilikuta mama analia sana na baada ya mtoto wake kapata ugonjwa na akafa. Mama yake alisema Mungu si ungenichukua mimi aliona ni harasa sana kwa mtoto wake kufa akiwa bado mdogo.

Uhusiano wa Daudi na Mungu. Na alikuwa anamuuliza kila jambo.

2 Samwel 2:1-4 Ikawa baada ya hayo, Daudi akauliza kwa BWANA, akasema, Je! Niupandie mji wo wote wa Yuda? BWANA akamwambia, Haya! Panda. Daudi akasema, Niupandie mji upi? Akasema, Hebroni. Basi Daudi akapanda aende huko, pamoja na wakeze wawili, Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili, mkewe Nabali, wa Karmeli. Daudi naye akawapandisha watu wake waliokuwa pamoja naye, kila mtu na watu wa nyumbani mwake; wakakaa katika miji ya Hebroni. Basi watu wa Yuda wakaenda, wakamtia Daudi mafuta huko, awe mfalme juu ya nyumba ya Yuda. Wakamwambia Daudi wakasema, Watu wa Yabesh-gileadi ndio waliomzika Sauli.

Daudi alikuwa na utulivu wa kumuuliza  Mungu. Sasa punguza hiyo gharama ya kufanya maamuzi mabovu sasa ukiharibu ndipo  una muuliza Mungu. Sasa muulize kabla hujafanya maamuzi.

Hata katika masuala ya kuoa na kuolewa mshirikishe Mungu kabla na sio baada  ya kumpata mtu ndipo uulize, sisemi kuuliza ni vibaya ila . Hakikisha unamshirikisha Mungu kabisa.

D Mwili  unaweza ukawa kikwazo

Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.MATHAYO. 26:41.

Yesu alipokuwa anaomba bustani ya getsmane alisema kikombe kiniepuke. Yesu alikuwa na upako  lakini mwili ulitaka kumkamisha maana ulikuwa unagoma asipite msalabani.

  1. Mapokeo ya dini yako

Galatia 3:1-3 Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa? Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili?

Walianza katika Roho na walipotea njiani.

Vitoto vyangu, ambao kwamba nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu; GAL. 4:19

Paulo anasema mpaka Kristo aumbike ndani yao ina maana wanahitaji kutifuliwa. Kuna ardhi ndani yake iko kama mwamba ukipanda mbegu haizai. Kwa hiyo inahitaji kuendelea kutifua na kutifua ili kitu kiumbike ndani yao

Na ndio maana tunakuwa na watu wengi wanaokoka na lakini wanashikwa na dini na kutegemea watumishi badala ya kumtegemea Yesu. Na jua kuwa  watumishi wanafahamu kwa sehemu.

Hakikisha unapima kile kilichosemwa na watumishi maana na sisi ni binadamu

F .Wazazi wako

Akamchagua Daudi, mtumishi wake, Akamwondoa katika mazizi ya kondoo  Nyuma ya kondoo wanyonyeshao alimwondoa, Awachunge Yakobo watu wake, na Israeli urithi wake.   Akawalisha kwa ukamilifu wa moyo wake, Na kuwaongoza kwa busara ya mikono yake.

ZAB. 78:70-72 SUV

Wazazi wake Daudi waliona kama ni mchungaji wa kondoo na wakati Mungu kamtengenezea mazingira ya kuwa mchungaji wa taifa la Israel.

Na hata Samuel alitaka kukosea  lakini Mungu alimsaidia. Na Mungu alisema ni huyu. Na maisha ya Daudi yalibadilika kuanzia pale.

Na kuna wazazi wanainvest kwa watoto sana maana hawakujua mpango wa Mungu kwa watoto wao na wanakuta baada ya muda wanahama kabisa kwenda kufanya vitu vingine.

Wakati Mungu ananifundisha hili jambo alinipa Warumi 8:26-27     Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.RUM. 8:26-27_

na  tutakuombea na wewe ujazo wa Roho Mtakatifu.ili unene kwa lugha.

Tunaomba japo hatufiki vile viwango ambavyo Mungu anataka kwa hiyo tunakuwa wadhaifu. Udhaifu maana yake ni kutokuwa kama vile Mungu anataka.

Sasa udhaifu mmoja wapo ni kutokujua namna ya kuomba ipasavyo. Mstari wa 27.. husaidia kuwaombea wengine.

Rahabu aliomba lakini muujiza haukuja kwa sababu wana wana Israel kuzunguka ukuta. Na waliomba kwa mzigo zaidi kuliko Rahabu na alivuka.

Pia angalia habari za Paulo na Sila  waliomba kwa mzigo mkubwa sana Mungu aliwasaidia waliomba hadi milango ya gereza ilifunguliwa na vifungo vikalegezwa.

Petro alikamatwa na aliweka jela na alilala hakupata nguvu za kuomba ila kanisa  liliomba kwa mzigo sana.

Mungu aliweka mzigo mkubwa sana ndani ya kanisa na liliomba hadi alivuka.

Pia nilikuwa naomba kwa watoto wangu walipokuwa ndani ya tumbo la mama yao. Na nilikiwa naomba kwa kunena kwa  lugha sana hadi naona mzigo uliopo ndani yangu unaisha.

Sasa mpaka leo nawaombea na nazidi kuwaombea ili Mungu awasaidie. Kitanda cha mtoto hakiondoki kwa sababu wanahama nyumbani. Huwa nawaombea sana na naenda kwenye viumba vyao. Na naomba sana. Naomba hadi mzigo unaokuwa ndani yangu hadi uishe..

Na hata katika maisha yako ombea mambo yako hadi uvuke. Na kama unaona nguvu ndani yako inapungua omba Pendo la Mungu lijae ndani yako.1 Wakorintho 13. Maana Paulo anasema usipokuwa na upendo unakuwa kama debe tupu yaani huna kitu cha ndani. Kwa hiyo ni dalili ya kutokuwa na upendo ndani. Omba huo upendo uje ndani yako

Kama unaomba kwa kunena kwa lugha  usiombe kwa mazoea bali omba kwa Mungu hadi uvuke.

Mambo mengi hapa nayaona kwa vijana kuna wengine hapa wana magamba kama Paulo  ila Mungu atayatoa.

Kama unasumbuliwa na tabia ya ukahaba kama Rahabu yuko Mungu atayake kusaidia kuvuka hapo.

Wimbo wa ni salama Rohoni Mwangu.

Pia mwl aliita vijana kuokoka. Sasa hakikisha unaokoka ili umpate huyu Yesu na soma kitabu cha Hongera kwa kuokoka .

NA MWL MWAKASEGE

DIAMOND JUBILEE HALL DSM

TAR 14 MAY 2017