Asili ya Israel

Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi. Akamuumba mtu akamweka katika nchi hiyo, akakubaliana naye kuwa ailinde, aitunze, tena aweze kuimiliki. Mtu huyo akakiuka Makubaliano yake na Mungu ambayo walikubaliana.

Mtu huyo alifukuzwa na kuondolewa katika nchi ile aliyokuwa amewekwa ndani yake ili aweze kuitunza.

Baada ya Mwaka elfu moja ya mtu huyo kufukuzwa kutoka katika nchi ile Mungu alimtafuta mtu miongoni mwa wanadamu atakaye mtumia kutimiza kusudi lake la moyoni mwake.

Katika mpango huo akampata mtu ambaye aliitwa Abramu, ambaye baadaye alimbadlisha kutoka Abramu maana yake Kuhani wa Mungu akawa Abrahamu, baba wa Mataifa, Kuhani wa Mungu aliye hai. Ilikuwa imepita miaka elfu moja mpango wa kwanza uliposhindwa wa kumpata mtu huyo.

Abrahamu alipewa masharti  ambayo akiyakubali ndipo akubaliwe kutumiwa na Mungu. Tunasoma katika kitabu cha Mwanzo  Sura ya Mwanzo 12: 1-3.

BWANA akamwambia  Abrahamu, Toka wewe katika nchi yako  na jamaa zako, na nyumba ya baba yako uende mpaka nchi nitakayo kuonesha, nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako nawe uwe Baraka, Nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani, na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.

Mungu alimwaahidi huyo mtu mambo makuu yafuatayo, akikubali kufanya kama anavyomwagiza Kwanza: Atampa nchi, Pili: Atamfanya kuwa Taifa kubwa, Tatu: Atamfanya kuwa Baraka , Nne: Jamaa zote za dunia watabarikiwa kupitia yeye, Tano:  Atawabariki wambarikio na kumlaani Yule Atakaye mlaani.

Mtu huyo alikubali masharti hayo yote ambayo Mungu alimpa Mwanzo 17:6-7.

Nitakufanya uwe na Uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa taifa, na wafalme watatoka kwako. Agano langu nitalifanya kuwa imara kati ya mimi na wewe, na Uzao wako baada yako na vizazi vyao kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa Uzao wako baada yako.

Nami nitakupa wewe na Uzao wako baada ya yako nchi hii unayo ikaa ugeni, nchi yote ya kaanani, kuwa milki ya milele, nami nitakuwa Mungu wao.

Mungu alimpa Abrahamu nchi ya Kaanani kuwa Milki yake, yeye na Uzao wake. Kaanani lilikuwa ni jina la nchi ambayo leo hii inaitwa Israel, kwa sasa.

Mjukuu wa Abrahamu ambaye jina lake lina maana ya mtu mdanganyaji, mtu aliye tumia mabavu kupata anacho kitaka, mtu ambaye ni mavumbi.  Kwa kuwa Mungu alitaka kubadilisha jina la Yakobo, kumpa jina jipya, mpango wake Mungu ukamleta Yakobo kukutana na Malaika ambaye walishikana mieleka usiku kucha. Mwanzo 32:24-28

Yakobo akakaa peke yake, na mtu mmoja akashindana naye mweleka hadi alfajiri. Naye alipoona ya kuwa hamshindi akamgusa panapo paja lake, akateguka uvungu wa paja lake. Yakobo alipokuwa akishindana naye akasema  Niache, niende maana kumepambazuka. Akasema sikuachi  usipo nibariki. Akamuhuliza jina lako nani? Akasema Yakobo. Akamwambia jina lako hutaitwa tena  Yakobo ila Israeli maana umeshindana na Mungu, na watu nawe ukawashinda.

Kuanzia hapo Yakobo akaitwa Israeli, Jina Israeli linahusu mtu aliyeitwa hapo mwanzo Yakobo mwana wa Isaka, mjukuu wa Abrahamu.

Nchi ya Israeli ilipata jina kutoka kwa mtu huyo ambaye ni Yakobo.

Asili ya Taifa la Israel

Tuangalie mwanzo wa taifa hili la Israeli. Yakobo alizaa watoto kumi na wawili ambao wanaunda kabila kumi na mbili za Israeli, mtoto mmoja wa Yakobo aitwae Yusufu, alikuwa mtoto wa pekee katikati ya ndugu zake,  walimuita muota ndoto. Kwa kuwa hizo ndoto zake alipozisimulia kwa kaka zake zikawafanya wamchukie. Siku moja aliota ndoto kuwa ndugu zake wangeishi maisha ya kumsujudia.

Kwa hiyo ndugu zake walipokuwa malishoni Yusufu akawaletea chakula, wao wakaamua kumuuza kwa wafanya biashara ambao nao wakamuuza kwa mtu mmoja potifa aliye kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Misri.

Huyo Yusufu aliishi kama mtumwa wa mtu huyo, alipewa kuangalia mali zote za Yule  bwana. Mashamba ya mtu huyo pamoja na mifugo yake ikaongezeka maradufu kwa sababu yake. Lakini mwanamke wa Yule bwana alimtamani Yusufu akataka kulala naye na kufanya uzinzi lakini Yusufu akakataa maana alikuwa mtu mwaminifu kwa Mungu. Mwishowe Yule mwanamke akamsingizia kwa mumewe kuwa mtumwa wako alitaka kunibaka nikakataa.

Huyo bwana Mmisri akamtupa Yusufu jela akafungwa kifungo kisichojulikana muda gani angeliweza kufunguliwa.

Humo gerezani Yusufu aliendelea kuishi Maisha ya Uadilifu na Uaminifu kwa Mungu wake. Siku moja mfalme Farao wa Misri akaota ndoto iliyoshindikana kutafsiriwa. Akaitwa Yusufu, aliyekuwa mfungwa akatoa tafsiri yake ambayo ilikuwa ni ya muhimu sana.

Mfalme Farao akaamuru Yusufu afanywe Waziri Mkuu wa Misri ambaye alisaidia nchi hiyo kukusanya chakula na kukiweka akiba kwa miaka ya njaa itakayo kuja baadaye.

Misri ilikuwa na miaka saba ya Mavuno makubwa sana. Yusufu akasimamia Ukusanyaji wa hicho chakula na kukihifadhi katika maghala kwa nchi nzima.

Wakati Misri inashibe ya chakula huko nchi ya Kaanani kulikuwa na njaa kali , Misri ilikuwa na miaka saba ya Mavuno makubwa sana. Yusufu akasimamia Ukusanyaji wa hicho chakula na kukihifadhi katika maghala kwa nchi nzima.

Wakati Misri inashibe ya chakula huko nchi ya Kaanani kulikuwa na njaa kali hata Mzee Yakobo akawatuma  kuja Misri kununua  chakula. Mwanzo 42:1-3

Basi Yakobo akaona ya kuwa kuna nafaka katika Misri, Yakobo akawaambia wanawe kwa nini mnatazama? Akasema, angalia nimesikia  ya kuwa nafaka iko Misri, Shukeni mkatununulie chakula tupate kuishi wala tusife.

Basi ndugu kumi wa Yusufu, wakashuka Misri ili wanunue nafaka. Walipofika Misri walikutana na Yusufu ambaye alikuwa mtu mkubwa lakini hawakumtambua kama ndugu yao.

Yusufu aliamuru wauziwe chakula walichotaka. Njaa ilikuwa nzito huko Kaanani, mwisho wao walirudi Misri kununua nafaka kwa mara nyingi, mwishowe Yusufu alijitambulisha kwao kuwa mimi ni Yusufu mliye niuza huku Misri Mwanzo 45:3-4

Yusufu akawaambia ndugu zake mimi ndimi Yusufu, baba angali hai?  Wala ndugu zake hawakuweza kumjibu, maana waliingiwa na hofu mbele zake. Yusufu akawaambia ndugu zake karibuni kwangu, basi wakakaribia. Akasema mimi ni Yusufu, ndugu yenu ambaye mliniuza Misri. Yusufu aliwasamehe hakujilipiza.

Baadae Mzee Yakobo Israeli alihamia Misri na watu wa nyumba yake wapatao sabini. Yakobo akaungana na Mwanawe Yusufu wakakaa Misri.

Baada ya miaka 430 hao watu 70 walioingia nchini Misri waliongezeka hadi kufikia jumla ya watu 25,000,000 wakawa tishio katika nchi ya Misri. Tunasoma Kutoka 1:7

Na wana wa Israeli walikuwa na Uzazi sana, na kuongezeka mno, na kuzidi kuwa wengi, nao wakaendelea kuongezeka nguvu na ile nchi ilikuwa imejawa na wao.

Kwa sababu hiyo Wamisri walipoona ya Yusufu amekufa ambaye alikuwa ndugu yao, tena kiongozi katika serikali. Wamisri waliwachukia Waisraeli na kuwa tesa sana. Lakini walivyo watesa ndivyo walivyoongezeka  na kuzidi sana.

Mwisho wa mateso yao Mungu alimtuma mtu mmoja aitwaye Musa, ambaye aliwaongoza Waisraeli kwenda nchi yao ambayo ndiyo Israeli ya sasa.

Safari yao iliwachukua muda wa miaka 40 kuhifikia nchi yao ya ahadi. Katika miaka hiyo 40 Mungu akafanya agano pamoja nao ambalo liliwatofautisha na mataifa mengineyo. Mungu akawapa amri kumi,  Mungu akawapa alama yao juu ya miili yao tohara. Mungu akawapa siku ya kupumzika Sabato.

Kwa hiyo hakuna  nchi au taifa ambalo linaweza kuwa juu ya Israeli, maana Israeli ni nchi takatifu kwa Mungu. Mfalme wake Daudi aliuteua mji wa Yerusalemu kuwa makao makuu ya nchi ya Israeli miaka 3,000 iliyopita. Nao utaendelea kuwa mji wake Mkuu hata Kristo atakapo kuja kutawala tena.

KWA NINI ISRAEL.
Kuzungumzia taifa la Isreali, Kumbumbuku La Torati 7:7-9 yatuambia, “BWANA hakuwapenda ninyi, wala hakuwachagua ninyi, kwasababu mlikuwa wengi kuliko
mataifa yote, maana mlikuwa wachache kuliko watu wote; bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu, ndiyo sababu BWANA akawatoa kwa mkono wa nguvu,
akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri. Basi jueni ya kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kusika amri zake, hata vizazi elfu.”

Mungu alilichagua taifa la Israeli kuwa watu ambao kupitia kwao Yesu Kristo atazaliwa- mwokozi kutuokoa katika dhambi na kifo (Yohana 3:16). Mungu kwanza aliahidi Masihi baada ya Adamu na Hawa kuanguka katika dhambi ( Mwanzo mlango wa 3). Mungu baadaye alithibitisha kuwa Masihi atakuja kutoka kwa uzao wa Abrahamu, Isaka, na Yakobo (Mwanzo 12:1-3). Yesu Kristo ndiye sababu kuu ya Mungu kuichagua Israeli kuwa watu wake malaamu. Mungu hakustahili kuwa na watu wateule, lakini aliamua kufanya namna hiyo. Yesu alistahili kuja kutoka kwa taifa la watu fulani na Mungu akachagua Israeli

Ingawa, sababu ya Mungu kulichagua taifa la Israeli halikuwa peke lengo la kumtoa Masihi. Nia ya Mungu kwa Israeli ilikuwa kwamba wataenda na kuwafunza wengine kumhusu. Israeli ilikuwa liwe taifa la makuhani, manabii na wamisionari kwa ulimwengu. Nia ya Mungu ilikuwa, Israeli iwe na watu wa kipekee, taifa ambalo lingeelekeza wengine kwa Mungu na ahadi zake, kutolewa kwa mkombozi, Masihi na mwokozi. Kwa sehemu nyingi Israeli ilikosea katika jukumu hili. Hata hivyo lengo lake kabisa kwa Israeli- lile la kuleta Masihi katika ulimwengu- lilitimizwa kikamilifu katika Kristo Yesu.