Kabila 12 za Israel

Ibrahim alimzaa Isaka, Isaka akamzaa Yakobo, Yakobo naye akazaa watoto 12 ambayo ndiyo makabila 12 ya Israel.

NA.   JINA MAANA
MZAZI MSTARI WA BIBLIA
1 Reubeni Ona Lea Lea akapata mimba akazaa mwana, akampa jina lake, Reubeni, maana alisema kwa kuwa BWANA ameona teso langu; sasa mume wangu atanipenda. (Mwanzo 29:32)
2 Simeoni Sikia Lea Akapata mimba tena akazaa mwana, akasema kwa kuwa BWANA amesikia, ya kwamba mimi sikupendwa, amenipa na huyu; akamwita jina lake Simeoni. (mwanzo 29:33)
3 Lawi Ungana Lea Akapata mimba tena, akazaa mwana, akasema, Basi wakati huu mume wangu ataungana nami, kwa sababu nimemzalia wana watatu. Kwa hiyo akamwita jina lake Lawi. (mwanzo 29:34)
4 Yuda Sifu Lea Akapata mimba tena, akazaa mwana. Akasema, mara hii nitamsifu BWANA; kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; akaacha kuzaa. (mwanzo 29:35)
5 Dani Haki Bilha(mjakazi  wa Rahel) Rahel akasema, Mungu amenipa haki yangu, naye amesikia sauti yangu, akanipa mwana. Kwa hiyo akamwita jina lake Dani. (Mwanzo 30:6)
6 Naftali Mashindano Bilha(mjakazi  wa Rahel) Bilha, mjakazi wa Rahel, akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa pili. Rahel akasema, kwa mashindano makuu nimeshindana na ndugu yangu, nikashinda. Akamwita jina lake Naftali. (Mwanzo 30:7,8).
7 Gadi Bahati njema Zilpa(mjakazi wa Lea) Lea akasema, Bahati njema! Akamwita jina lake Gadi.(Mwanzo 30:11)
8 Asheri Heri; Furaha Zilpa(mjakazi wa Lea) Mtumishi wa kike wa Lea akamzalia Yakobo mwana wa pili. Ndipo Lea aliposema, “Jinsi gani nilivyo na furaha! Wanawake wataniita furaha.’’ Kwa hiyo akamwita Asheri. (mwanzo 30:12-13)
9 Isakari Ujira; Zawadi Lea Ndipo Lea akasema, “Mungu amenizawadia kwa kumpa mume wangu mtumishi wangu wa kike.” Kwa hiyo akamwita Isakari. (Mwanzo 30:18)
10 Zabuloni Zawadi ya thamani sana Lea Ndipo Lea aliposema, “Mungu amenizawadia kwa zawadi ya thamani sana. Wakati huu mume wangu ataniheshimu kwa sababu nimemzalia wana sita.’’ Kwa hiyo akamwita Zabuloni. (Mwanzo 30:20)
11 Yusufu ongeza Raeli Ndipo Mungu akamkumbuka Raheli, akasikia maombi yake na akafungua tumbo lake. Akapata mimba na akamzaa mwana na kusema, “Mungu ameniondolea aibu yangu.’’ Akamwita Yusufu na kusema, “BWANA na anipe mwana mwingine.’’ (mwanzo 30:22-24)
12 Benjamini Mwana wa mkono wa kulia Raeli Hapo alipopumua pumzi yake ya mwisho, kwa maana alikuwa akifa, akamwita mwanawe Benoni. Lakini babaye akamwita Benjamini. (Mwanzo 35:18)