MAMBO YA KUFANYA ILI FIKRA ZAKO ZITUMIKE KUFANIKISHA MAISHA YAKO

MWAL.  CHRISTOPHER MWAKASEGE

UKUMBI:  VIWANJA VYA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
TAREHE:  18th hadi 25th SEPTEMBER 2016

Lengo   la Somo:
Kutambua maarifa  ya kutumia fikra zako kupata Mafanikio maishani.

MSINGI WA SOMO.

Mithari 23:7a
Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.

NB; Neno Fikra na Fikira ni neno moja kwenye Biblia. Usipate shida ukiona yameandikwa tofauti.

Fikra
Kwanza, ni mkusanyiko na mtiririko wa mawazo unaotengeneza msimamo  wa  kiutekelezaji ndani ya mtu.

Kwahiyo fikra sio tu tunavyowaza au kufikiri. Ni zaidi ya hapo. Ni matokeo ya jinsi uonavyo kwa namna na jinsi ulivyo. Au jinsi uonavyo. Au unavyotafakari nafsini mwako.

Pili, fikra inaonyesha ulivyo kimaisha. Inaonyesha kiwango chako cha kufikiri kilipo au kilipofika.

Tatu, fikra ziliumbwa zikae ndani ya nafsi ili zitumike kuweka aina na kiwango cha maisha ya mtu  katika kila eneo linalomhusu. Unaposoma Biblia utagundua MTU ni ROHO inayokaa ndani ya MWILI.

Kazi ya nafsi ni kiungo kati ya Roho na Mwili ili kuwasiliana baina yao. Roho na Mwili haviendani lugha zao. Ndipo nafsi ikawepo kuleta mawasiliano. Nafsi huunganisha ulimwengu wa kiroho na wa kimwili.

Ndani ya nafsi ndiko kwenye fikra. Nafsi ina akili. Mwili una ubongo.

3 Yohana 1:2
Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.

Tofauti ya aina ya viwango vya maisha haina ya MTU na MTU inatokana na namna wanavyofikiri. Hajalishi mpoje,namna zenu za maisha zinategemea tofauti zenu za kufikiri.

2 Wakorintho 11:3
Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.

Shetani akitaka kuharibu maisha yako ya kiroho huanza kwenye nafsi. Kwenye fikra. Fikra ni mpango mkubwa sana. Kama alivyowaharibu Adamu na Eva pale bustanini Eden. Hata MTU akitaka kuokoka vita huwa kwenye fikra. Mungu wa ulimwengu huu hushambulia fikra.

HATUA ZA KUFUATA ILI KUTUMIA FIKRA ULIZONAZO ZIKUSOGEZE VIWANGO ALIVYOKUSUDIA MUNGU.

1. TATHMINI NI MAISHA YAKO ILI UJUE KIWANGO CHAKO CHA KUFIKIRI KWAKO KILIVYO

Hii haijalishi upo kwenye hali gani.  Hii itakusaida kujua unaanzia wapi ili kushughulikia na kufikiri kwako. Unajua ni kwanini unaweza kwenda kwenye chuo ukapewa mtihani tena ingawa ulifaulu? Huwa wanachek fikra. Hata kusaidiwa huja baada ya kujua fikra zako. Shule inapaswa ikupe MAARIFA SIO ELIMU

Biblia iliweka MAARIFA ili uweze kufanikiwa. Mfano kwenye kina Daniel walipotakiwa kuwekwa ili kutumika na mfalme walipimwa maarifa sio elimu zao.

Kwahiyo unapoenda mbele za Bwana kwanza ni lazima ujitathmini. Vigezo vya kujitathmini ndivyo hufanya uweze kujitathmini. Mfano,kuwa mzima unatembea barabarani sio kigezo cha kwamba u mzima. Kapime kwanza vipimo ndio utajua kweli. Kwenye mambo ya kiroho inakuwa shida sana. Kwa wakristo vigezo ni Agano letu ndani ya Kristo Yesu. Vigezo hivi ni vikubwa. Sana

2 Wafalme 4:1-7
Basi, mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wana wa manabii alimlilia Elisha, akasema, Mtumishi wako mume wangu amekufa; nawe unajua ya kuwa mtumishi wako alikuwa mcha Bwana; na aliyemwia amekuja ili ajitwalie wana wangu wawili kuwa watumwa.2  Elisha akamwambia, Nikufanyie nini? Niambie; una kitu gani nyumbani? Akasema, Mimi mjakazi wako sina kitu nyumbani, ila chupa ya mafuta.3  Akasema, Nenda, ukatake vyombo huko nje kwa jirani zako wote, vyombo vitupu; wala usitake vichache.4  Kisha uingie ndani, ukajifungie mlango wewe na wanao, ukavimiminie mafuta vyombo vile vyote; navyo vilivyojaa ukavitenge.5  Basi akamwacha, akajifungia mlango yeye na wanawe; hao wakamletea vile vyombo, na yeye akamimina.6  Ikawa, vilipokwisha kujaa vile vyombo, akamwambia mwanawe, Niletee tena chombo. Akamwambia, Hakuna tena chombo. Mafuta yakakoma.7  Ndipo akaja akamwambia yule mtu wa Mungu. Naye akasema, Enenda ukayauze mafuta haya, uilipe deni yako; nayo yaliyosalia uyatumie wewe na watoto wako.

Vitu ambavyo utaviona kwa mwanamke huyu mfiwa ni…..

i. Fikra zake za kimaisha mama huyu mjane zilikwamia mahali zilipokwamia fikra za mume wake. Maadamu mume alikuwa hai na Mke aliegemea anapoishi mumewe. Mume alipokufa mke hakujua la kufanya. Hakuwa na namna za kuendeleza fikra za mumewe mbele zaidi. Alikwenda kwa Elisha kwakuwa hakuwa na cha kufanya.Kufa kwa mumewe kuliua sehemu ya maisha ya yule mama. Ukiolewa sio kwamba akili yako isifanye kazi. Mnapaswa kuungalisha fikra zenu. Ndio mana mali za wengi hupotea mume akifariki.

ii. Hali ya maisha na kiwango cha maisha cha mama huyu kilitokana na ulipofika mtiririko na mkusanyiko wa fikra za mume wake. Ukiangalia maisha ya baba yule angalia maisha ya familia yake. Mtiririko wa fikra za mume ndio ulileta kiwango cha maisha ya familia ile. Angalia wengi wakiacha kazi. Maisha yao husimama. Kwakuwa wengi huwa na fikra za kampuni sio zao.

iii. Fikra za mume wake zilitengeneza viwango  vya maisha yake na ya familia yake kutoka kwenye maeneo yafuatayo.

A. Utumishi aliokuwa nao kwa Elisha. Haitajwi allowance wala chochote alikuwa akipata lkn familia ilikuwa inafaidika kwa namna flani

B. Kumcha Bwana pia ilikuwa kigezo kingine. Maisha yakawa ya naenda.

C. Alikuwa anaishi kwa mkopo. Mama anakiri kuwa walikuwa wanakopa na mume amekufa kabla ya kulipa. Hii maana yake muulize mumeo anatoa wapi hela kabla hujaanza kudaiwa. Huyu mama walichukua mpaka watoto. Biblia haikatai mikopo lkn inakataa riba.

Huyu baba alikuwa ni mcha Mungu lkn alikuwa na maisha ya shida. Kama uchaji wako haujacharge fikra zako hutaenda kokote hapa duniani ingawa utaenda mbinguni. Tukitaka kujua fikra zako tunaangalia maisha yako.

D. Mume wa mjane alimjengea Mke wake kufikiri kuwa maisha yao yalitokana na ushauri na muongozo wa Elisha na kumbe sivyo.  Ndio mana mama alipofiwa tu na mume moja kwa moja alienda kwa Elisha. Kwanini huoni kwenye Biblia mama huyu akienda kwa mmoja wa ndugu wala marafiki? Anaenda kwa Elisha.

Elisha hakumwambia kuwa atamkopesha. Au atamuajiri. Akampa maagizo mengine.

E. Mama mjane hakujua cha kufanya juu ya fikra za mume wake kuwa kawaweka watoto wao rehani. Yani hakuandaliwa na mazingira hayo. Hakujipanga. Aliona kama mumewe ataishi milele. Mume alikopa yeye lkn aliweka rehani watoto. Kwa namna hii alikuwa anawawekea watoto wake fikra za KITUMWA.

Biblia haisemi yule baba alipokuwa anapata pesa alikuwa anapeleka wapi? Lkn tunawaona watoto wanawekwa rehani. Watoto wakikua watafikiria deni aliloacha baba yao. Na huu ni utumwa. Masharti ya mikopo huwa yanakufunga fikra za kufikiri. Unakuwa unawazia deni tu. Huu ni utumwa. Ni fikra za kitumwa.

F. Fikra zake na za mume wake hazikuwa na uwezo wa kutumia walichokuwa nacho ili kuwatengenezea maisha mazuri. Mama anapojibu kuwa sina kitu inaonyesha namna alivyokuwa anafikiri. Hakuitaja kwanza chupa ya mafuta. Hakuiwazia hiyo. Fikra zake zilikuwa haziwazii chupa ya mafuta. Alikuwa na watoto ambao walishiriki kubeba chupa za mafuta. Walitaka kupelekwa utumwani,maana yake walikuwa na uwezo wa kufanya kazi nyingine kuleta kipato nyumbani. Sio kufa njaa.

Unaweza ukawa na kipawa au cheti au chochote lkn huna fikra za kujitoa kwenye hali uliyonayo.. Tatizo ni fikra. Fikra ni pesa. Fikra ni kila kitu. Biblia inasema tutumie akili lkn tusitegemee akili zetu.

Home Work!
1. Chanzo cha mapato yako kinatoka wapi?

2. Na je kikifika mwisho au kufa utafanyaje?

3. Fikra zako zinahusika kwa kiwango gani katika upatikanaji wa mapato yako

Mungu ametuita kuishi kwa NENO na sio MUUJIZA.

*************** ENDELEA  SIKU YA PILI  ***************

▶Lengo
Kuweka maarifa ya Kiblia ndani yako yatakayokuwezesha kutumia fikra zako ili ufanikiwe ktk maisha yako

Mith 23:7(a)
H/W ya jana ulifanya?
✅ Wapo wanaofikiri kuwa hili somo ni la wajane, sawa na huko ni kufikiri pia japo utaachwa
✅ Wapo wanaofikiri kuwa ili somo ni la wastaafu sawa nao vile vile

HATUA AMBAZO UNAHITAJI KUZIFUATA KAMA UNATAKA KUTUMIA FIKRA ZIKUSOGEZE KIMAISHA…..[Zinaendelea…]

2. Tathimini kufikiri kwako ili uweze kushirikiana na MUNGU anapotaka kukusaidia kimaisha.

⚫Haifanani na hatua ya kwanza
⚫Tafsiri nyingine ni kama ifuatavyo Mith 23:7
….aonavyo nafsini mwake…
➡Biblia haisemi *aonacho* bali *aonavyo* si *afikiricho* bali *afikirivyo* si *anachotafakari* bali *anavyotafakari*

✅ Kumbuka alichosema YESU kwenye *Math 13:13-14*

➡Biblia haizungumzi tu juu ya aonavyo, bali anaonavyo anachoona
➡Kinachomsaidia kuona anachoona si swala la kufikiri bali jinsi ya kufikiri
➡Ni kitu gani kinachokusukuma kufikiri na kuja na jibu ulilonalo?

*Kumbuka habari ya wale wapelelezi 12*
10:- waliona majitu
2:- waliona chakula

➡Walitazama lakini hawakuona
➡Ndivyo ilivyo wengi usoma NENO kumbe hawasomi, wengi usikiliza kumbe hawasikilizi

⚫Shida ni nini??
➡Nafsi=FIKRA zimefungwa!

*Rum 1:28*
✅ Ufahamu ulioko ktk nafsi ni tofauti na ufahamu ulioko ktk roho
✅ Unasema najuaje…ndiyo maana anazungumzia.habari za akili hapa…na akili haipo rohoni bali kwenye nafsi
✅ Ukimkataa MUNGU kwenye fahamu zako ama kumuacha, basi utafuata akili zisizofaa, zako na za wengine!
✅ Kwa sababu hyo utajikuta unafanya mambo usiyotaka kufanya
✅ Kwa lugha rahisi kumwacha MUNGU huwezi tembea ktk mpango wake juu yako
✅ Ukimkubali KRISTO hawezi kukuacha utembee nje ya mpango wa MUNGU

*Akili zisizofaa ni nini*
Unachotakiwa wewe kukijua/kukifuata wewe kama wewe!

Na wala si maana yake kwamba ni *akili mbaya*❌

✅ Maana yake ni FIKRA ambazo kwa mtu mwingine si zake mwingine ni zake. Mfano mfanyabiashara astahili kumwona mfanyakazi ofisini anafanya kisicho sawa na vivyohivyo mfanyakazi kumtazama mfanyabiashara kuwa amepotea!

✅ Ukiruhusu na kukubali MUNGU akutawalate anakupa FIKRA za kusimama alipokusudia hata kama akikuletea washauri watakushauri ktk FIKRA za MUNGU juu yako na wala hawatatumia akili mbaya

✅ MUNGU anataka kutusaidia ili tuishi maisha ya kiwango cha Ki-Agano maana huko ndiko kwenye kusudi la kila mmoja!
✅ Viwango vyetu vya maisha vimefungwa ktk Agano(kwa sasa twatumia Agano jipya ila tusisahau na kuliacha maana ktk lile la kale MUNGU alishaweka maagano pia)

*Hebr 8:8-10*
*Hebr 4:12-13*
➡MUNGU akitaka kukufanikisha utuma NENO ktk nafsi yako(FIKRA) ili nafsi iweze kutafsiri lile NENO kati ya roho na mwili

➡MUNGU anapotuma NENO lile NENO lina uwezo wa kutambua mawazo na makusudi ya nafsi

➡NENO ukagua aina ya FIKRA au mawazo uliyonayo ktk kuendesha maisha yako.

*Zab 117:19-20*
✅ Ukimlilia MUNGU utuma NENO lake na NENO ukagua mambo haya:-
1. Aina ya FIKRA na akili unazotumia
2. Pia imsaidie maamuzi ndani yake aina gani ya akili(FIKRA) unazihitaji mahali ulipo
3. NENO la MUNGU linampa MUNGU nafasi ya uhalali/kibali kwako

*Isaya 55:8-11*
▶kuna pointi kama 4 hapa muhimu uzidake
*WAZO*:- MUNGU utuma wazo ndani ya mtu
*NJIA*:- Ukisha tafakari wazo ukupa njia(MIKAKATI)
*MVUA*:- Uachiliwa mvua kuzidi kunyeshea listawi na kukua hilo wazo
*NENO*:- kwa hiyo NENO ufanikiwa hakika

➡Usishtuke litakapokuja wazo tofauti na ulilonalo hyo ni ishara ya kuambiwa jipange ili utoke mahali ulipo

➡Kumbuka kama nafsi yako haitakuwa tayari kupokea hata YESU asimame mbele yako utamgomea tu, sababu ni nini mafundisho tunayopokea. *Yoh 8:31-59*

▶Ukikataa msaada wa maelekezo yake utakuwa na maisha ya kuishi jangwani tu(maisha ya mzunguko tu usijue ushike nini uache nini) na mbinguni ila jiulize Airport yako itakuwa wapi? Jangwani au Kaanani?

*TURUDI KWA MAMA MJANE TUJIFUNZE KITU*

*2Falm 4:1-7*

*MASWALI AMBAYO YANAWEZA KUKUSAIDIA KATIKA KUTATHIMINI KWAKO*

1. Je ninajua ni aina gani ya masaada ninaohuitaji ili niwe na maisha mazuri kuliko niliyonayo sasa?

✳Swali hili tunalipata kwa mama mjane baada ya kujieleza Elisha akamuuliza swali *nikufanyie nini*

✳Mama hakujibu lile swali hakusema anahitaji msaada gani bali alipekeka ripoti ya hali yake ya maisha aliyokuwa nayo baada ya kufa mumewe.

✳Alishindwa kujibu yawezekana kwa mambo haya:-
-FIKRA zake hazikuwa na jibu ya swali hilo
-FIKRA zake zilikuwa zimeishiwa mawazo ya kumtoa ktk shida hyo
-FIKRA zake zilikuwa zinataka kutua mzigo bila kujua atabebeshwa mzigo wa lile swali *unataka nikufanyie nini*

*MUHIMU SANA KUFAHAMU SIRI ZILIZOKO KTK MASWALI YA NAMNA HIYO*
✳ Kushindwa kujibu maswali/swali la Elisha maana yake au inaonyesha
✳Matatizo yake yalikula muda wake wa kufikiri kiasi ambacho hakubakiza muda wa kufikiria jibu

✅Muda wako ukiliwa na kukatawaliwa na matatizo huwezi fanya maamuzi, unapigwa bumbuazi huwezi pata hata wazo la kufanya ndani yako. Utabaki kukaa na hasira na huzuni

✅Usikubali mazingira yakuwekee ngome inayokwamisha/kuzuia kufikiri kwako zaidi ya mawazo uliyonayo sasa

*Mwz 26:1-14*
✳MUNGU aliisemesha FIKRA yake isitazame mazingira bali aangalie Agano

*2Kor 10:3-5*
➡Shetani upambana na kuvuruga sana FIKRA ndani ya mtu

*2Kor 11:3*
✳Unapoona mapambano ya FIKRA ndani yako usiruhusu kabisa matatizo kuyaona ni makubwa kuliko NENO ndani yako

✳Shetani uleta hila ndani ya mtu kwenye FIKRA ili kukuvuruga

*HILA MAANA YAKE NINI*
1. Wazo linalokuja kukuzuia uwezo wa FIKRA zako kupokea cha MUNGU na kama ulikuwa umekipokea unakikataa

2. Ukweli+Uongo=Usipovitenga jibu ni Uongo. Jiulize pale Edeni mti wa mema+mabaya=mabaya

✅Cheki wazo linapokuja ndani yako ROHO MTAKATIFU anasemaje? Kama si la kusudi la MUNGU utakosa amani, utapata huzuni(maana yake change your mindset fanya TOBA)

✅Uhitaji kufikiria mtu anayekuja na wazo fikiria na sikia wazo la MUNGU pekee

✅Ukikosa amani usiendelee na hilo wazo
-Cheki ndoto unazoota kama ni
✳Nyoka=kuna hila inakuja kuvuruga FIKRA zako kama kakung’ata ujue kaacha sumu na kama la jua kaacha hofu!

✳Ngome=kuna kizuizi umefungiwa ndani, ulitakiwa kutoka

✳Stendi=Kufikiri kwako kumekwama

*Unapoomba ombea sumu kuondoka na kama kuna roho ya kufuatilia utekelezaji bado ipo kemea*

*Teka kila nyara na kila FIKRA=zilizimishe kufikiri ki FLAME na KI AGANO

*HOME WORK*
✳YESU akisimama mbele yako leo akikusemesha unataka nikufanyie nini utajibu nini??

✳Ukishindwa kujibu ni wazi kufikiri kwako kumekwama!

*KWANINI MUNGU ANAULIZA MASWALI HAYA*
1. Kumlazimisha aliye uliza alazimishe FIKRA zake kufikiri mahali zilipokwama

2. Anatafuta uhalali/kibali cha kuingilia kufikiri kwako maana anaweza kuja na wazo jipya ukakataa

***************  ENDELEA  SIKU YA TATU  ***************

LENGO LA SOMO.
KUWEKA MAARIFA YA KIBIBLIA ILI KUPATA MAFANIKIO KWA KUTUMIA FIKRA ZAKO.

MSTARI MKUU

Mithari 23:7a
Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.

2 Wafalme 4:1-7

Hatua ya *kwanza* ilikuwa kutathmini maisha yako.

*Pili* kutathmini kufikiri kwako

Naamini Home Work ya Jana mlifanya.

Je? Unajuaje kuwa unachomuomba Mungu akufanyie ndicho mapenzi yake?

*Warumi 8:26-28*
Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.
27  Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

Roho Mtakatifu ni Mungu ndani yako. Ni muwakilishi wa Mungu ndani yako. Muulize Roho Mtakatifu nini uombe. Roho Mtakatifu ataweka neno ndani yako. Yeye huomba sawa na mapenzi ya Mungu. Kama una neno ndani yako utajua tu. Kwenye nafsi kuna nia,hisia  nk. Roho Mtakatifu atakusaidia.

*Funzo la kwanza*
Usizuie fikra zako kushughulika na swali ambalo hujui kwanini limeulizwa. Swali la Elisha na jibu la yule mama yalikuwa tofauti kabisa. Mama hakujua kwanini swali limeulizwa na hilo likamuwekea mama ukuta ili fikra zake zisifike mbali. Ndio mana wengi wakiwa kwenye hali hii hupenda zaidi ya kuombewa kuliko kuelewa tatizo. Unapoulizwa maswali na mtumishi usimkatishe kuuliza. Huwa kuna sababu. Unapoulizwa swali ambalo Mungu tayari ana majibu nalo tatizo lipo kwenye fikra zako.

*Funzo la Pili.*
Swali la pili liliulizwa kwakuwa swali la kwanza halikufaulu kuamsha fikra za mama mjane kufikiri zaidi ya pale zilipokomea kufikiri. Mama alieleza shida zake lkn sio anataka nini! Kazi ya swali la kwanza lilikuwa kwa ajili ya kuamsha fikra za yule mama ndio mana likaulizwa la pili. Fikra zilizochoka kufikiri unazipa mzigo kufikiri kitu cha pili. Haijalishi unajaza mafuta kiasi gani kwenye gari engine ikiharibika ni kazi bure. Wazo jipya kwenye fikra zilizochoka ni kazi sana. Inawezekana Mungu anataka kuyapekeka maisha yako kiwango kingine lkn wewe unaona umechoka.

Fikra za Yesu zilichoka kabla ya kusulibiwa ndio mana wakaja malaika kumtia moyo. Mwili ukiwa umechoka akashuka mlimani. Mungu alimtia nguvu Yesu ili amalizie safari yake atakutia moyo na wewe. Ndio mana misuli ya anayepanda lift na anayepanda ngazi huwa ni tofauti. Mungu anatafuta  kinachopatikana kwako pale anaposhughulika na wewe

*Mithali 3:5*
Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

Kuna tofauti ya kutumia akili zako na kuzitegemea akili zako mwenyewe. Yani usiziache akili zako zikafanya kazi zenyewe. Akili zako hazikuumbwa zifanye kazi zenyewe. Angalia mwanadamu anapoumbwa anapuliziwa pumzi ya Mungu. Ukiwa mwanasayansi unaona oxygen lkn kiroho ni pumzi ya Mungu. Ni zaidi ya pumzi ya kawaida. Akili ziliumbwa zifanye kazi na Roho Mtakatifu na neno

*Luka 24:45*
Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.

Yesu alizifungua akili zao ili wawe mashahidi wake. Wasingeweza kufanya kazi bila Roho Mtakatifu na neno ambalo lilikuwa kwa ajili ya kuwasaidia.

*2 Timotheo 3:16-17*
Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
16  ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.

Isaya 55:8-11(isome )

Akili zetu hazikuumbwa kutumia neno na roho nyingine zaidi ya ile ya Mungu.  Ili shetani aweze kutumia akili zetu aliharibu fikra kwanza. Tushindwe kutambua tubebe tu hata mabaya. Ndio mana swali la pili lilikuwa muhimu sana ili kuamsha fikra. Ndio mana unapopita kwenye magumu mengi unakuwa na maswali mengi kuliko majibu. Mengine huwa ya Roho Mtakatifu. Ndio mana hata kama anajua unachotaka bado alikupa akili zitumike. Usitumie akili bila roho wa Mungu. Ndio mana tunakwama maishani. Kuna waliookoka wamekwama na wasiookoka wanafanikiwa mbele.

*Funzo la Tatu.*
Angalia/Orodhesha vitu ulivyonavyo hata kama unaona havina thamani.

Yule mama alipoulizwa ana nini cha kwanza alisema hana kitu. Hakujua kwanini swali linaulizwa. Kwa lugha nyingine alikuwa anamwambia Elisha nilivyonavyo havina thamani ya kunitoa nilipo.

*Mathayo 14:13-21*
Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao.15  Hata kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na saa imekwisha pita; uwaage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula.
16  Yesu akawaambia, Hawana haja kwenda zao, wapeni ninyi vyakula.
17  Wakamwambia, Hamna kitu hapa ila mikate mitano na samaki wawili.
18  Akasema, Nileteeni hapa.
19  Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi, wanafunzi wakawapa makutano.20  Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, vikapu kumi na viwili, vimejaa.21  Nao waliokula walikuwa wanaume wapata elfu tano, bila wanawake na watoto.

Yesu anawauliza wanafunzi wake. Kwanini mnataka watu hawa waondoke? Yesu anataka kushughulisha fikra zao. Alipowaambia kuwa wawape chakula akili yao ikaweka defence kuwa hakuna Chakula. Lkn Yesu anaona kuwa wanafunzi hawana Neno wanaangalia nje na sio ndani. Mungu ametuumba kwa namna ambayo msaada utaanzia ndani. Hata wewe orodhesha una vitu vingapi hata kama vya kurithi? Usiseme huna kitu. Hata kama ni pikipiki mbovu. Ndivyo hata kwenye kampuni yoyote wanavyofanya INVENTORY. Unahesabu vyote. Kisha angalia vipawa ulivyonavyo. Mfano unachekesha wenzio kijiweni bure lkn wenzako wanatumia huo uchekeshaji wanapata hela. Andika vyote! Usiangalie thamani

*Funzo la nne*
Unahitaji kujua kwa msaada wa Mungu kwanini unacho ulichonacho? Kwanini? Kwasababu thamani yake inategemea uhitaji wake. Yule mama alijua ana chupa ya mafuta lkn hakujua kwanini anayo. Kwahiyo hakutumia alichokuwa nacho ipasavyo?

*2 Wakorintho 9:10*
Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu;

Je,ulichonacho ni mbegu au mkate. Anayeamua ulichonacho kiwe mkate au mbegu ni Mungu. Anakupa mbegu na mkate. Nani anayeamua mbegu iwe mbegu au mkate kama mkate sio Mungu bali Fikra zako. Haijalishi amekupa mbegu au mkate anategemea ushirikiano wako. Ukitumia vibaya unavuruga utaratibu. Ndio mana usipoona vile ulivyonavyo kwenye fikra zako utapata shida. Kila alichokupa Mungu kina thamani ila fikra zako ndio huondoa thamani yake.

Yesu alipowaambia nileteeni hapa wale wanafunzi wake alikuwa anamaanisha peleka kwake kwa njia ya *Maombi.* Chochote ulichonacho au unachoona hakina thamani kwako mletee kwake. Kubariki ni kuvipa nguvu ili vifanikiwe. “To Empower and Prosper”. Mfano,Isaka wa baada ya kupelekwa madhabahuni alikuwa ni tofauti na Isaka wa kabla ya kupelekwa madhabahuni. Alipopelekwa madhabahuni fikra zake ghafla zikapanuka na kuona possibilities *Oooh Hallelujah……!*.

Chochote ambacho hakiendi mpelekee Yesu kwa njia ya maombi. Mwili wako ukiuweka kwenye madhabahu ya Bwana huwa unageuzwa nia. Mungu ana mipango mikubwa kuliko gari unayotembelea. Ana mipango mikubwa kuliko chochote ulichonacho. Ndio maana ni vizuri kuweka akili zako kwa Bwana.

*Funzo la Tano*
Ukomo wa kufikiri kwako kusizuie kiwango cha utii wako katika kutekeleza wazo ulilipewa na Mungu

*2Wafalme 4:6*
Ikawa, vilipokwisha kujaa vile vyombo, akamwambia mwanawe, Niletee tena chombo. Akamwambia, Hakuna tena chombo. Mafuta yakakoma.

Mwisho wa kufikiri kwa mama mjane lilikuwa ndio mwisho wa mafuta kupatikana. Thamani ya mafuta haikuwa kwenye mafuta bali kwenye fikra zake. Vyombo alivyoleta kwa mtumishi Elisha ndio ukawa mwisho wa kupatikana kwa mafuta. Unapomuwekea Mungu mipaka unajiwekewa mipaka wewe mwenyewe. Hii ni muhimu. Mungu hukuletea Neno na Roho wake vikusaidie lkn utekelezaji wa akili (fikra zako) huwa una maana sana kwenye utekelezaji wa namna Mungu anavyokusaidia.

Fundi akiharibu kitambaa chako cha suti thamani ya Fundi ipo kwenye;
1. Kusikiliza vizuri
2. Kufikisha ukomo wa namna anavyopaswa kukitumia kitambaa.

Wengi wanaishi maisha “substandard.” Wanapopata maisha ya *mtumba* “wanaridhika”. Lkn Mungu ana maisha *mapya* anayotaka uwe nayo. Fikra zako ndio mwisho wako. Suleiman alipomjengea MUNGU nyumba aliijenga vizuri sana na kabla Mungu hajaingia aliridhika nayo kwanza.

Kwanini unataka Mungu aingilie maisha yako wakati ulivyojiweka mbele za Mungu ni kiholela holela tu. Haiwezekani.  Ukishinda vita kwenye fikra utashinda maisha kwenye mwili. Kiongozi yoyote ni lazima awe trained fikra zake. Uongozi sio cheo ni mtazamo wa kifikra. Pressure ikija fikra zitakuumbua kwakuwa huna utulivu wa fikra.  Ni lazima ujiweke kwenye madhabahu ya Bwana usafishwe. Mungu atakupa akili kwakuwa alikuumba yeye.

*Glory to God ……. Glory to God!*

Kama mpo Partnership ni lazima muwe na nia moja. Ndio mana ni lazima kwenda mbele za Bwana kuomba ili muwaze na kunia mamoja. Kama mwenzako anasema 3 na wewe unasema 5 lazima mtagombana. Mnapaswa kunia mamoja. Muombe Mungu upate partner ambaye mtania mamoja…

Mungu alipotuumba alitaka tufike mbali sana. Dhambi ikaharibu. Pata picha pamoja na dhambi zetu bado tunarusha madege makubwa angani je kusingekuwa na dhambi tungefanya nini? Akili ni fursa.  Unaona pale mwingine asipoona. Kuna fikra nyingine hazioni kesho. Zipeleke fikra kwenye madhabahu ya Bwana.  Naye atafanya.

Tuombe….

*************** ENDELEA  SIKU YA NNE  ***************

▶Lengo
Kuweka maarifa ya Kiblia ndani yako yatakayokuwezesha kutumia FIKRA zako ili ufanikiwe ktk maisha yako

*Mith 23:7(a)*

*Summary*
➡Tuliangalia maana nzima ya FIKRA
➡Tuliangalia hatua ya kwanza
➡Tukafahamu na ya pili
➡Tukapena na H/W, jitahidi sana kuomba mara kwa mara juu ya hizi H/W hasa ile ya jana maana ni mtaji kwako na usifanyie utani
➡Tukaangalia jana na mafunzo kadhaa kama 5 hivi

*LEO*
✅ Tunaendelea na ule mstari wa *7*
*2Falm 4:1-7*
✅ kipengelea cha muhimu au nataka uone hapa ni pale Biblia inaposema……. *enenda ukayauze mafuta haya*………

✅ Ningekuwepo kipindi hiki ROHO MTAKATIFU anamvuvia upako mwandishi wa kitabu hiki ningemwambia aongeze kidogo hii habari ya mama mjane kujua *jinsi alivyouza mafuta haya* maana Biblia haikuendelea kusema

✅ Maana hakuwa mfanyabiashara, alikuwa mgeni sokoni, ni mara yake ya kwanza kuuza

✅ Je somo la kuuza alipata wapi? Je aliuza? Kwa shs ngapi?

✅ Maana waweza kuwa na vitu na usiuze pia maana si kitu chepesi atii, wafanyabiashara wanaelewa. Jiulize Mama mjane hakuwa na hata na lebo kwenye mafuta yake, packing ilikuwa na kumbuka vyombo vilikuwa vya kuazima maana yake mafuta yako kwenye vyombo tofauti tofauti, alifungajefungaje?

*JAMBO LA MSINGI*
✅Ni kuwa Elisha alitumika kumtengenezea kuandaa FIKRA zake zaidi kwa habari ya soko.

*FUNZO LA 6*
Jifunze na jizoeze kulitafuta na kuliona na kuliingia soko kiroho kwanza kwa njia ya FIKRA zako kabla ujaliona soko hilo iwe kimwili ama kiuchumi

➡Utekelezaji wa mstari wa 7 unategemea sana utekelezaji wa ile mistari.kuanzia wa 3-6

➡mistari ya 3-6 Alitekeleza kwa kiwango gani maagizo aliyopewa

➡Maana 3-6 maagizo haya yalikuwa ya kujenga FIKRA zake ziweze kuona thamani ya chupa ya mafuta kwa jicho la FIKRA zake.

➡Ndani ya FIKRA zake lazima uhitajiwa (soko) wa chupa ya mafuta

➡MUNGU alimtengenezea ya kuwa kama ulichonacho hakina thamani kwenye FIKRA zako hakiwezi kuwa na thamani kwenye soko

*SABABU HIYO*
✅FIKRA lazima zione thamani ya kitu(uhitajiwa wake) ndiyo kitakuwa na thamani sokoni

✅Wengi wamekufa na kuviacha vitu vingi sana sababu ya kushindwa kitambua uthamani wake hata hivi leo kupotea bila faida

✅Soko linaonekana kwanza kwenye FIKRA kabla ya nje

*Wakati mama mjane anapewa maelekezo aliambiwa*

*I).* Nenda, halafu koma(,)
Maana yake fikra zake ziwe na utayari wa kutafuta soko. Yalikuwa maamuzi ya ndani

*II).* Nenda ukatake vyombo kwa jirani zako wote
✅Alikuwa anaambiwa panua wigo wa vyombo vitupu
✅MUNGU alitaka aone uhusiano wa chupa ya mafuta na FIKRA zake pamoja na soko la mafuta
✅Kati ya chupa ya mafuta na soko la mafuta katikati yake kuna FIKRA
✅FIKRA zikigoma soko la mafuta limegoma

✅Kwa hiyo uhusiano kati ya chupa ya mafuta, FIKRA na soko ni wa *KIROHO KWANZA.*

✅Kwa lugha nyepesi Soko ni mkutaniko wa wauzaji na wanunuzi

✅Mtu anayeuza anategemea soko kuuza, soko kumkutanisha na mnunuzi, soko kumpa bei, soko kumwandalia auze lini kwa kiasi gani

✅Anayenunua naye anategemea soko limkutanishe na bidhaa anayoitahi, soko limpe bei, limkutanishe na muuzaji, limwekee utaratibu wa kununua

*SOKO LINAANDALIWA NA NANI*
➡Wauzaji/muuzaji
➡Mununuzi
➡Wote kwa pamoja
➡Yule ambaye upata faida kwa Mnunuzi na Muuzaji kukutana (Serikali)

✳Soko linatakiwa kutawalina na nani? Na linatawaliwa na nani?

✅Soko uandaliwa kwenye FIKRA (msukumo wa kuhusisha ulichonacho na soko)

✅Soko ni la KIROHO KWANZA
*Isaya 24:1-2*
✅Adhabu ya kiroho ilienda kugusa maeneo tofautitofauti imegusa mpaka soko
-Muuzaji na Mnunuzi wanafanana
-Mkopaji na Mkopeshaji wanafanana

*Eze 7:12*
➡Muuzaji na Mnunuzi kuna adhabu mjini

*Neh 13:15-22*
➡Viongozi kutumia misingi yao ya imani kubana aina fulani ya soko
➡Kiongozi alifunga milango kuzuia biashara sababu ya misimamo yake ya kiimani

✅Kwa hiyo nguvu ya hilo soko halipo ktk vitu vinavyouzwa bali ktk ulimwengu wa roho

✅Imani kuanza kuingia kidogo kidogo kwenye uchumi kuwa na uhakika utegemea ni imani ipi na ina ingiza nini ndo maana soko uanzia rohoni kwanza.

*Uf 13:1-7*
➡Roho ya mpinga kristo ukimbilia kushambulia kwenye eneo la soko

➡Ndo maana watu.wenye haki/walokole wengi wanapambana hapa shetani anajaribu kuwazuia kwenye eneo hili ili wasifanikiwe na wengine hawajui kwanini kila biashara kwako inagoma au yeye auzi na wale wenzake wa mataifa wanauza kweli. Shida ni kutokujua na kutofundishwa kuona soko rohoni kwanza.

*SWALI*
Wangapi hawana Akaunti Benki? Ila wengi hawajui kwanini hawataki kugungua akaunti benki. Sasa sikwambii huna pesa au napigia debe Benki noo
Mfano Mfanyakazi unapokea mshahara ukatoa sadaka zako na kilichobaki kikarudi benki uwe na uhakika kimerudi na ROHO wa MUNGU kwenye mzunguko wa fedha yako

➡Pesa haina dini bali ina Roho.

*Uf 18:1-3,9-13*
➡Hakuna mtu anayenunua bidhaa yao tena si kwamba soko halipo

➡Si kila mfanyabiashara utafuta msaada sehemu nzuri

➡Kuna anaye amua kipi kinunuliwe na kipi kisinunuliwe usipoweza kujua hapo na kutengua hapo utateseka

*NANI ANATAWALA SOKO LA AJIRA?*
➡Ulimwengu wa roho utawala soko hili

Jifunze kwa kina Daniel walikuwa bora mara 10 ya wale waliomzunguka mfalme! Maana mfalme hakuwa na kauli ya mwisho na sababu kina Daniel walikuwa bora zaidi kilimbana mfalme kuwaondoa wale wachaw na nafasi hizo kupewa kina Daniel.

*Uf 5:9-10*
*….ukamnunulia MUNGU…..*
✅DAMU YA YESU ina ruksa kuingia sokoni sababu kuna kitu kilichokuwa kinauzwa kimewekwa bei ya juu ili kisinunuliwe

✅YESU alijua thamani ya DAMU yake na alitununua kwa cash.

✅Kwa kutumia DAMU ya YESU waweza ingia kama mfalme sokoni
✅Usijizuie omba kila ufikapo dukani kwako anza kwa maombi
✅mahali ambapo soko halina haki kuna dhuruma na mambo si ya KIFALME achilia DAMU ya YESU isemeshe ardhi ya mahali hapo

✳Usiende kwenye soko bila DAMU ya YESU
✳Hakikisha FIKRA zako zimepata kibali cha NENO la MUNGU na ROHO MTAKATIFU
✳Ombea kibali juu ya Biashara yako
✳Hakika ROHO MTAKATIFU anajua anayehitaji bidhaa unazouza

*Math 6:33*
➡Hakikisha mfumo wa UFALME wa MUNGU umekaa juu ya soko

➡Mfumo.unatengenezwa, tafuta haki mfumo wa Kiblia wa Biashara (soko) uliopotea

➡Maana bila mfumo hakuna uwajibikaji. Mfumo.wahitajika kila mahali iwe kanisani mpaka kwenye familia..

*HOME WORK*
✳Unaona soko kwenye FIKRA zako kwa kiwango kipi?
(Fursa zako za kuuza na kununua na kuuza tena)

✳Cheki mahali unapofanyia Biashara kama kuna umiliki wa KIROHO/KIFALME

*MAOMBI*

*************** ENDELEA  SIKU YA TANO  ***************

▶Lengo
Kuweka maarifa ya Kibiblia ndani yako yatakayokuwezesha kutumia FIKRA zako ili ufanikiwe ktk maisha yako

*Mith 23:7(a)*

*HATUA AMBAZO UNAHITAJI KUZIFUATA KAMA UNATAKA KUTUMIA FIKRA ZIKUSOGEZE KIMAISHA*

➡Tumeshaangalia hatua 2 tuko tumeanza seminar. Leo tuendelee na ya 3

3⃣Panga FIKRA zako kwa upya ili zisikupitishe tena mahali pabaya ulipokwisha pitia.

✅FIKRA zinapangika
✅Mfano kwa mama mjane baada ya kusaidiwa na Elisha akitaka hali ile ya mwanzo isijirudie tena lazima abadiri kufikiri kwake la sivyo ile hali atarudi tu

*2Falm 5:7*
Mama mjane alipanga FIKRA zake kwa upya..lazima ujifunze kupanga FIKRA zako kwa upya
Tuonaona mstari wa 7

➡…Nenda kauze mafuta…
Si FIKRA tu kutumika bali MUNGU alitaka Mama mjane ajuaje na akubali ndani yake kuwa MUNGU ndiye amfundishaye kupata faida.

*Isy 48:17*
✅MUNGU hakufunsidhi tu kuhubiri au kuimba bali pia hukufundisha na hupanga FIKRA zako ili zipate kujua MUNGU ndiye akupaye faida

✅FIKRA lazima zipate msaada wa kufundishwa jinsi ya kupata faida

✅Pata tofauti sana kati ya kufundishwa kupata faida na kufundishwa Biashara. Ni sawa na ilivyo tofauti kati ya kufundishwa kufaulu mtihani darasani na kufundishwa juu ya kufaulu mtihani wa kimaisha

✅Maana si kila mtu aliyeko darasani atafaulu maisha, na si kila afanyaye Biashara atapata faida..lazima ujifunze kuvuka hapa

*MAENEO MUHIMU YA KUTAKIWA KUBADILIKA*

*1).* Weka FIKRA zako zikubali MUNGU ndiye anayekufundisha kupata faida

▶Watu wengi wakikwama kiroho hukimbilia kanisani ila uchumi wao ukikwama huwaoni kanisani hukimbilia Benki, sasa sisemi Benki ni mbaya au usiende Benki ila wanasahau kuwa

▶ROHO MTAKATIFU ni mwalimu mzuri sana wa kukufundisha ujasiriamali wenye kupata faida

*2).* Lipa Deni
✅Elisha alimwambia Mama mjane ….kauze kisha lipa deni….

✅Alikuwa anatafuta kitu gani?
▶Alikuwa anapandikiza nidhamu za kutumia fedha ambazo MUNGU amempa kwa sababu zake alizokupa au ulizomwomba tena kwa mwongozo wake!

▶Mama mjane alikwenda kutaka msaada wa watoto wake kutokuchukuliwa watumwa(Alitaka kupata fedha za kuwakomboa watoto wake)

▶Hakuwa na FIKRA zilizojengeka kulipa deni maana Biblia haituonyeshi aliwahi kukopa. Kama huna FIKRA za kukopa huwezi ukawa na (nidhamu) FIKRA za kulipa deni.

*Mama mjane alikabidhiwa matumizi ya fedha ktk maeneo haya*
⚫Kulipa deni
⚫Gharama za kwake na zile za baadaye
⚫Gharama za watoto na za wakati ule wa baadaye
⚫Kuhakikisha ya kwamba hamalizi faida lazima abaki na mtaji.

✳Je unamwomba MUNGU pesa kwa ajili ya nini au kwa ajili gani?
▶Kumbuka pesa huyumbisha mawazo na kujikuta watumia nje ya lile kusudio

▶Ukikorofisha hapo MUNGU hukaa pembeni. FIKRA zinahitaji nidhamu kwenye matumizi ya pesa. Kama MUNGU anakupa kwa ajili ya kitu fulani hakikisha unaielekezea hyo pesa kwenye hicho kitu.

▶Tofauti na hapo utaona ROHO MTAKATIFU anakuhimiza TOBA

*Mith 13:22*
▶Watu wengi wana FIKRA za kujitazama wenyewe tu kwenye upande wa pesa wanajikuta kusahau kuwa wana familia na watoto!

▶Biblia inatuhimiza kuweka akiba mpaka za wajukuu!

▶Usitazame kukwama kwa mme/mke wako ama wazazi wako, usifike mahali hata pa kuwakasirikia badili FIKRA zako ili wewe uvuke hapo kisha mrushie kamba naye atoke hapo oooh hallelujah Hallelujah

*HOME WORK*
➡Orodhesha madeni yako

*Zab 37:21*
✳Umuhimu wa kuorodhesha madeni

▶ Usipolipa mikopo MUNGU haji kukupigania katika haki zako.
▶ Unapoteza haki katika haki
▶ Mikopo isiyolipwa ugeuka deni
▶ Deni ubeba vitu (rehani) ili akili zako ziamke. Na baada ya kutaka kuja kuvichukua ndipo akili zako zitaamka
▶ Si kila ambaye anashindwa kulipa deni hana hela bali hana mpangilio mzuri wa matumizi na ulipaji

*Yer 22:21*
✅ Si kwamba hapendi kusikia bali hataki kusikia maana yake hataki kutekeleza alichoambiwa

✅ Gharama kubwa ya kutokufaulu mipango yako ni kupoteza utulivu wa MUNGU kukusemesha

✅ Wengi wakisha kopa kwenye kulipa hulipa nusu na nusu wanaweka mfukoni wanasahau MUNGU ndiye aliwafundisha kupata faida na au walipewa kibali cha kupata mkopo

✅ Usije ukasahau na kusema huu utajiri ni nguvu zangu wakati ni MUNGU ndiye aliyekupa nguvu za kupata utajiri

*UNAFIKIRI KWANINI MUNGU ALILETA SADAKA*
▶ Si kwamba ana shida na pesa yako
▶ Lengo la kwanza lilikuwa kutumia sadaka kukutengenezea FIKRA sahihi ndani yako
✳Tazama maana ya
⚫ Malimbuko=MUNGU anataka umfikirie yeye kwanza
⚫ Zaka ya kwanza=MUNGU anataka kupewa heshima ktk maisha yako

✅ Watu wengi kwenye kipindi kigumu na chenye kibano wako tayari kutafuta hela kulipa Benki lakini si kwa MUNGU. Kwa MUNGU excuses zitakuwa nyingi sana na hata kusema “MUNGU we si unajua nilivyobanwa”

✅ MUNGU hana maana wala hataki kukufirisi bali anataka kukutengenezea FIKRA zenye Nidhamu

✅Jifunze kumpa MUNGU 100% naye anakurudishia 100%

✅Muulize MUNGU kwanza kwenye kila kitu, ratiba zako, muda wako na mambo yako mkabidhi na mfikirie MUNGU kwanza

✅Usitamani kuiga maisha na FIKRA za mtu mwingine hakikisha MUNGU anakupa mbinu za kujenga FIKRA za kwako mwenyewe.

✅FIKRA zenye kujenga nidhamu ndani yako.zitakufanya utende haki wala hazitakupeleka kwenye kupokea rushwa

✅FIKRA hizi zitakuwekea unyenyekevu ndani yako, kujishusha na kujifunza kutoka kwa wengine

✅Usijaribu ku copy na ku paste kutoka kwa mtu mwingine BWANA atakupa mikakati sahihi ndani yako

*MAOMBI*

*************** ENDELEA  SIKU YA SITA ***************

▶Lengo
Kuweka maarifa ya Kiblia ndani yako yatakayokuwezesha kutumia FIKRA zako ili ufanikiwe ktk maisha yako.

*Mith 23:7(a)*

▶Tunaendelea na *HATUA….*

4⃣Omba MUNGU akusaidie uweze kupata kutoka kwenye vitabu maarifa yanayohitajika ili uhitajike

*Dan 12:4*
✅Tutazame hatua kwa hatua ktk mtirirko ufuatao:-

*1).* Ni vyepesi mtu kuhitajika akiwa na maarifa yanayohitajika ktk kipindi husika

*Dan 1:17-21*
➡Watu hawakuajiri sababu ya Cheti bali ujajiri maarifa uliyonayo

➡Wakikuajiri sababu ya Cheti na kukaa nawe muda wakagundua una Elimu lakini huna maarifa utashushwa cheo

➡Hatuambiwi kina Daniel walikuwa wangapi, ila walisomeshwa na kupimwa ktk mtihani. Kuanza kwako chuo walikuwa tayari na mtaji..swali la kujiuliza kile walichosomea kiliwasaidia kupata maarifa?

*Dan 1:3-4*
➡Walikuwa na Elimu pamoja na maarifa kwa kiwango fulani.

➡Ilibidi wakae darasani miaka 3 wapate maarifa juu ya maarifa. Haijalishi Elimu na maarifa waliyokuwa nayo awali.

*Mwz 41:37-40*
➡Yusufu alipewa nafasi ya Uwaziri Mkuu akiwa jera baada ya kugundua kuwa ana maarifa

➡Haijalishi uko wapi, jera? Umefunikwa? Umefungiwa au wapi lakini ROHO MTAKATIFU ni mwaminifu atakukutanisha tu na kusudi kama una maarifa yanayohitajika

➡Usiende shule au usisome kwa ajili ya kupata.Cheti bali soma ili upate maarifa. Maarifa yatakusaidia kutoka maishani ila si cheti

*2).* Kuna Vitabu vilivyobeba maarifa yanayotakiwa kwa muda husika

*Dan 12:4*
➡Muda ndiyo unaodai aina ya maarifa

➡MUNGU aliumba kwanza nyakati(muda) kisha mtu

*Mwz 1:1*
➡NENO mwanzo=aliumba muda kwanza kisha mbingu na nchi

➡Muda na maarifa zinaenda pamoja

➡Daniel aliambiwa yatie muhuri= Mtu yeyote akisoma asipate maarifa yaliyomo ndani yake kwa sasa mpaka kwa muda ulioamriwa. Hata yeye kwa kipindi kile asingeelewa hata kama angesoma

*Dan 1:4*
➡Mfalme aliagiza wafundishwe Elimu ya wakaldayo maana yake walikuwa tayari na kiwango fulani cha uelewa.

➡Ni sawa na kuchukua mtoto wa darasa la kwanza kumpeleka Chuo Kikuu haiwezekani maana kuna ngazi tofauti tofauti maana *Umri uenda na aina fulani ya kufikiri*

➡Ni hatari sana kusoma na kuwa na Elimu halafu huna lugha ya kutafsiri maarifa hayo(Wasoma kiswahili halafu interview kichina)

➡Kumbuka lugha inakunyima kazi

➡Njia yako uendana na lugha vilevile yaani kuchukua maarifa Ujerumani siri imefichwa kwenye kitabu hicho cha lugha ya kijerumani. Lazima usome mwaka mzima kijerumani kwanza kuweza kutoa maarifa yaliyoko humo.

*Ayb 35:16*, *34:35*
➡Kuna maneno hayana maarifa.
➡Si kila kitabu chenye maarifa chaweza kukusaidia isipokuwa kwa wakati sahihi na muda ulioamriwa!

*3).* Vitabu vilivyobeba maarifa uwa vingine vinafungwa visitoe maarifa hadi muda/wakati wa kuhitajika kutoa maarifa au muda umekaribia au umewadia

*Dan 12:4*
*Dan 9:1-3*
➡Kitabu chochote chenye sababu hii ya (3) lazima ukishakisoma utapata msukumo wa kuyaweka kwenye matendo yale yote uliyoyasoma

➡Nunua Vitabu Chini ya msaada wa ROHO MTAKATIFU, mwombe MUNGU akupe hekima kununua vitabu ambavyo.vina maarifa unayoyahitaji. Hii ni nidhamu unahitaji kujiwekea

➡Kumbuka kitabu chichote kilicho na maarifa ya wakati huo na sahihi kinakupelekea kupata msukumo ndani yako kuweka kwenye matendo hayo uliyosoma na kupata msukumo wa kuyaombea.

*4).* Ni muhimu kwa kitabu kufunguliwa na akili ya msomaji kufunguliwa kwa pamoja ili maarifa yaliyomo ndani ya kitabu yawe msaada ktk muda husika kwa ajili ya msomaji huyo

*Luk 24:44-49*
➡Kitabu kilikuwa kimefunguliwa lakini akili zao zilikuwa zimefungwa

➡Kitabu kilifunguliwa kwa ajili yao na YESU alijua akisema nao waweze kuoanisha kutoka kwenye vitabu vya torati na zaburi ndiyo maana akili zao zilifunguliwa na kufunuliwa wapate kuelewa walichokisema manabii waliotangulia kinatimia sasa

*5).* Mwombe MUNGU akukutanishe na Vitabu vilivyobeba maarifa unayoyahitaji na avifungue kama bado vimefungwa ili upate maarifa unayostahili kama hayo

*Uf 5:1-5*, *10:1-11*
➡Simba wa Yuda (YESU) alipata nafasi ya kukifungua kitabu.

➡Kitabu kinaweza kikawa kimefungwa ukaomba kifunguliwe

➡Pia kinaweza kikawa kimefunguliwa, sasa omba maarifa ukifunguliwa akili uweze kukielewa

➡Tazama Biblia ni kitabu bora na ni ileile inabeba maarifa ya kukusaidia bila kujali muda uliowekwa maana muda ukifika unafunguliwa tu

➡Jiulize ni kwanini watu wengi wanasoma shule lakini si wabunifu? Mfano waliosoma Administration waambie waanzishe ofisi binafsi uone..wanasubiri ku copy na ku paste ila leo MUNGU anakutafuta kukupa maarifa ukagunguliwe akili…oooh hallelujah!

*MAOMBI*
Orodhesha madeni yako maombi yataendelea siku ya 7(leo)

✅Maelfu ya watu walimpokea YESU pia

*************** ENDELEA  SIKU YA SABA  ***************

▶Lengo
Kuweka ndani yako maarifa ya Kiblia yatakayokuwezesha kutumia fikra zako ili ufanikiwe ktk maisha yako

*Mith 23:7(a)*

*Summary*
✅Kubadili maisha yako badili kufikiri kwako
✅Maana ya fikra…rejea day 1
✅Hatua ambazo unahitaji kuzifuata kama unataka kutumia fikra zikusogeze kimaisha..rejea day 1-6
✅Jana tuliangalia mtiririko wa mambo kama 5 hivi, lile la 5 tuliangalia; uhusiano kati ya maneno na Vitabu maana kitabu kimebeba maneno, muda na maarifa *Dan 12:4*
✅Maarifa ndani vitabu uachiliawa kufuata na uhitajika wake kipindi husika
✅Wazo la vitabu lilianzia rohoni si mwilini

..Tuendele na mtiririko huo..

*6).* Zijue njia za kupata maarifa kutoka ndani ya maneno yaliyomo ndani ya kitabu

*Josh 1:8-9*
▶Maneno ya MUNGU alizungumza na Joshua baada ya Musa kufa

▶Alikuwa akimtia moyo kuendelea mbele na watu wake ili kusudi litimie.

▶Joshua alitazama kazi aliyopewa na kuangalia kufanikiwa pamoja na kustawi kwake pamoja na watu wake hakika kwake halikuwa jukumu jepesi ndiyo maana alipewa njia ya kunsaidia…mstari wa 8

▶Aliambiwa chukua kitabu maana humo ndiko kuna maarifa ya kushinda kwako.

▶Maana miaka 400 walikaa bila kuwa na utaratibu wa KIMUNGU, MUNGU baada ya kukumbuka Agano alilofanya na Ibrahim na Yacobo akawatoa utumwani, walipofika Sinai akatengeneza utaratibu ambao utafananafanana na yeye ili kukaa nao. Lilikuwa jambo jipya sana kwako

▶MUNGU akija na kuamua kukaa mazingira take ubadilika kabisa ndo maana akatengeneza kitabu na ndani yake kuna maarifa, kuna masuala ya ujenzi, kilimo, uchumi, mahusiano ya kila aina, kitabu kukusaidia kustawi sana na uweze kuishi pamoja naye

*JOSHUA ALIAMBIWA VITU 3 VYA MUHIMU ILI UWEZE KUTOA MAARIFA NDANI YA KITABU, NA NI KITABU CHOCHOTE KILE*

1. Kisiondoke kinywani mwako
✅Jifunze kufikiri kila ambacho unakiona na kukisoma ndani ya kitabu na kutaka kitokee kwako

✅Jifunze kusema kila unachokiamini ndani ya kitabu *Mark 11:23*

✅Yale uliyonayo utegemea sana kile unachosoma na kukisema

*Rum 10:8-10*
✅Ukitaka kupata kilichopo kwenye kitabu lazima ukiri. Ukikuta mtu anapinga kilichopo ndani ya kitabu jua hakitatokea kwake

*Zab 45:1*
✅Ulimi unaandika
✅Kuzungumza ni kuandika kwenye mioyo na vibao vya nyama kwako.

✅Ndiyo maana ni rahisi tukikutazama tukajua nani kaandika ndani yako

✅Unaposema unaandika kwenye nafsi yako
✅Haitoshi kusoma jifunze kusema maana uanzia kuandikwa ndani. Maana sauti ninayoisikia kuongea si sauti ninayoisikia kuongea

2. Yatafakari maneno take mchana na usiku
✅Ni zaidi ya kusoma, kukariri
✅Tamka kutoka moyoni. (Meditation)

✅Tafakari=Tafuna
✅Kukariri=Kumeza na hii so guarantee zitafanya kazi

✅Huwezi ukatoa maarifa ndani ya kitabu bila kutafakari= fikra na akili zako kuchanganya ili utakapotembea utakuwa neno linatembea. Maana NENO alifanyika mwili akaa kwetu

✅Kutafakari NENO kuna kupa nafasi ya kutafuna na kupata nafasi ya kuwa na maswali mengi sana utakuwa mtu wa kutembea na note book na kalamu Mara nyingi si Ku copy na kupaste bali utapata maarifa zaidi

3. Upate kuangalia na kutenda sawasawa na maneno yaliyoandikwa humo
✅Utendaji unahitaji nidhamu ya kiwango cha juu sana

✅MUNGU anapoachilia wazo la biashara ndani yako usiwe na haraka kushirikisha watu maana kufanya hivyo kesho utamkuta mwenzako katekeleza..unahitaji nidhamu ktk hili

✅Swala si wazo au utekelezaji bali anahitaji kukuweka utaratibu wenye nidhamu kwanza

*Muh 12:9*
Tuongezee jambo jingine
4⃣Tafuta waalimu ambao wanakufundisha upate maarifa si wale watakaokufundisha upate darasa=cheti

✅Hata ktk vyuo vya kuandaa walimu lazima waandaliwe kutoa maarifa ndani ya Vitabu na si tu wawafundishe wanafunzi kunaliza shule

✅Binafsi nitamsikiliza na kumfuatilia mwalimu yule kesho na kesho kutwa kila nikimsikiliza nitapata maarifa=lugha ya mjini ninamwelewa sana

✅Paul alipokuwa na kiu ya kumtumikia MUNGU alipata waalimu walikuwa wanatoa maarifa ya Dini si maarifa ya KRISTO

✅Jiulize kwanza waalimu gani wanakufundisha? Unapeleka watoto shule jiulize ina walimu wa namna gani

*7).* Uwe mwangalifu na Vitabu unavyosoma

✅Si kila Vitabu vina uwezo wa kutoa maarifa
✅Kuna vingine haviendani na njozi yako. Hivyo usipoteze muda mwingi kusoma visivyo vya kwako maana muda hautoshi na huna muda wote ukifikiri ni wa kusoma

*Muh 12:12*
✅Vutabu ukisoma vinakuchosha
✅Usijaribukushindana na watunzi wa Vitabu ktk kusoma maana utakufa na wataendelea kutunga tu

✅Pia kuwa mawangalifu sana na Vitabu vya hadithi maana hutoa maarifa ndani ya mtu na pia utoa maarifa kwa njia ya hadithi *1Tim 1:3-4*

*Matendo 19:19*
✅Vilichomwa Vitabu hivyo maana maarifa yake yalikuwa hayatakiwi

✅Kama Vitabu vimepitwa na wakati wasomaji wakisoma fikra zao urudishwa nyuma ila vipo vile Vya zamani ambavyo maarifa yake ni ya mbele

*8).* Jizoeze kwa maombi kunyunyizia DAMU YA YESU juu ya kitabu unachosoma

*Ebr 9:19-22*
✅Maana si kila kitu unachosema kitakuzalishia jambo ulitakalo

*Ayb 38:2*
✅Maneno yasiyokuwa na maarifa uachilia giza

✅Mfano angalia ukitaka kusoma Biblia sekunde chake umechoka, umelala, uelewi lakini tazama ukitaka kusoma msg kwenye Simu au gazeti, waweza soma msg zote na magroup yote bila kuchoka na kuwa active zaidi

✅Ukigundua hili unajua ni vita na DAWA YAKE NI DAMU YA YESU PEKEE

✅Kabla ya kusoma achilia DAMU ya YESU kuondoa Giza na kufunga fikra usielewe

✅Jifunze kuombea miguu ya waalimu
✅Jifunze kuombea eneo unalopatia elimu. Mussa aliambiwa vua viatu

✅Kuna uhusiano mkubwa kati ya miguu na sikio na kichwa pia

✅Hatua unazokanyaga na jinsi unavyofikiri kuna uhusiano mkubwa sana

✅Miguu lazima ifungwe utayari maana waweza pata maarifa halafu ukapata uzito kutekeleza.

✅Shetani akiweza kukubana kwenye miguu yako na masikio yako huwezi kufanikiwa hata kidogo.

✅Jiulize Mara ya mwisho kusoma Biblia tena unayo kwenye Simu yako ni lini? Ila Mara ya mwisho kusoma msgs ndani ya Simu ni lini?

*MAOMBI*
✳Masikio yako vs Simu yako

*************** ENDELEA  SIKU YA NANE  ***************

▶Lengo
Kuweka ndani yako maarifa ya Kiblia yatakayokuwezesha kutumia FIKRA zako ili ufanikiwe ktk maisha yako

*Mith 23:7(a)*

*HATUA…..*
5. Jiulize maswali yanayofanya FIKRA zako zifikiri kiubunifu

*MAENEO MACHACHE UNAYOHITAJI KUFUATILIA*

1) Kufikiri juu ya soko kwanza kabla ya kitu ulichonacho kuuza

➡Wengi ulima kwanza,ufuga kwanza, uanzisha duka kwanza kisha ndo wanatafuta wateja na soko..Anza kwanza na soko na wateja ndipo uende kwenye kufuga, kulima na n.k

➡FIKRA zako zifikiri soko kwanza kabla ya chupa ya mafuta
➡Hata kama una pesa zako ukipeleka mradi wowote Benki wakiukataa usiutekeleze hata kama unapesa zako maana wao ufikiri kama ulipa au la!

2) Zizoeshe FIKRA zako kufikiri kiubunifu maana ichi ndicho kinazaa viwanda

➡Soma na jifunze uchumi wa Japan, South Africa, Marekani n.k

3)Tafuta mahitaji ya muda

➡Muda una mahitaji yake
➡Fikiri kwa namna ya kutafuta majibu ya mahitaji ya muda

✳Hayo ni masomo tosha ila leo nimepanga tujifunze kwa habari ya

*KUJIBU MALALAMIKO*

*Jizoeze FIKRA zako kujibu malalamiko*

➡Zifanye FIKRA zako zifikiri kiubunifu

✅Unaposikia mahali popote pale pana malalamiko usiziamshe FIKRA zako nazo kulalamika

✅Haijalishi malalamiko hayo ni halali kiasi gani

✅Zizoeshe FIKRA zako kufanya utafiti ktk malalamiko hayo,
⚫Nani analalamika andika, ⚫wanalalamika sababu gani andika,
⚫juu ya nini andika!
⚫Muda gani wanalalamika

*MIFANO KADHAA YA KUJIFUNZA KUTOKA KWENYE BIBLIA*

1. Wapelezi 12

*Hes 13,14*
✅Walipewa kazi ya kwenda kufanya utafiti ktk nchi ya Kanani na utafiti ule ulikuwa ulikuwa wa kiuchumi mno tazama maswali ya utafiti wao.

✅Kuleta ushahidi kuwa walienda huko ni kurudi na kichanja cha Zabibu.

✅Kazi ya utafiti ni kusaidia watu kufikiri zaidi.

✅Wale 10 FIKRA zao zilijioanisha na walichokiona kule na kujiona ni mapanzi, waliandika FIKRA zao zilichokiona *Hes 13:33*

✅Wengine baada ya kusikia habari hizo nao wakaanza kulalamika hata kusema kwanini tulitoka Misri. *Hes 14*

✅Joshua na Kareb wakasema tunaye MUNGU tutasonga mbele na kuingia kanan. FIKRA zao zilifikiri ubunifu na jibu la kulalamika kwa wengine

*TUNAJIFUNZA NINI HAPA KWA JOSHUA*

*1)* MUNGU akikuonyesha tatizo ina maana anataka kuamsha FIKRA zako zijiandae kutatua tatizo hilo pamoja naye

*Mith 3:5-6*

✅Akili hazikuumbwa zifanye kazi zenyewe bali na NENO LA MUNGU na ROHO MTAKATIFU

✅MUNGU anataka akili zako zikae mkao wa kutatua tatizo

✅MUNGU aliijua Kanani na hivyo kuvuka kuingia ilikuwa ni hatua lazima FIKRA zao ziwaze majibu na zione chakula na si majitu

*2)* Kulalamika ni ishara ya kuwa FIKRA hazioni jibu la tatizo na zinalitafsiri kuwa ni tatizo

✅Ndiyo maana walijona kama mapanzi na ndivyo walivyowaona

*3)* FIKRA ziliumbwa zione na kutafsiri changamoto zilizo katika FIKRA ya mtu na kuzitolea ufumbuzi

✅ FIKRA ziliumbwa ili zione

*2Kor 4:3-4*
✅FIKRA kama hazioni haziwezi kutafsiri ilivyo sahihi na sawasawa

✅NENO NURU tafsiri yake ni MAENDELEO KIBLIA
✅Hapo mwanzo kulikuwa na giza MUNGU akasema na iwe NURU=MAENDELEO

✅Mahali popote alipo mtu wa MUNGU mwenye HAKI lazima awasaidie wengine kufikiri. Sisi ni changamoto na chachu ya maendeleo.

*4)* Ile kwamba mtu amekutanguliza ktk jambo haina maana unafikiri vizuri kuliko wewe

✅Wapepelezi 12 walipewa nafasi na kutangulia kufikiri kabla ya wenzao lakini FIKRA zao wale 10 zilikwama na kushindwa kuona

✅Ukifuata FIKRA za mtu aliyekwama na wewe utakwama

✅Usiruhusu FIKRA zako kulalamika pamoja na walalamikao

✅Ukifuata FIKRA za kiongozi aliyekwama utakwama na wewe

*PALIPO NA MALALAMIKO NI ISHARA YA KUWA HAPO KUNA FURSA YA CHAKULA*

Daka hiyo

✅Kwa hyo fanya utafiti mahali hapo

✅ROHO MTAKATIFU anakupa fursa namna ya kujibu kulalamika kwako au sehemu hyo

✅Kalisha FIKRA zako ktk mkao wa kiutafiti. Tafuta chakula kati ya walalamikao, tafuta ndani ya nchi,mkoa,wilaya,kanisa,familia,umoja tafuta walalmikao we kaa hapo fanya utafiti

✅Tofauti ya Joshua na Kareb na wale wengine ilikuwa ni kutafsiri kwao

✅Ilihitaji ubunifu kuyageuza majitu kuwa chakula. Maana katikati ya jangwani na Kanani kuna FIKRA

✅We zipe kazi FIKRA zako utaona

*MFANO WA PILI*
*Hes 11:11-15*

✅Mussa alimlalamikia MUNGU
✅Kulalamika kwa Mussa kulitoa ajira kwa watu 70

✅Kiongozi anapolalamika ama kazi imemzidia jua kuna fursa ya ajira inakuja jipange, jiandae

✅Usimsaidie kiongozi ktk kulalamika maana atakapochagua wale 70 hatakuchagua, atakuacha

*MFANO WA TATU*
*Habakuki 1,2:1*

✅MUNGU alijibu kulalamika kwake, hakujibu kilichomfanya alalamike maana hakujua kuwa hicho kilichomfanya alalamike kinajibiwa na FIKRA

✅Kualamika kwenye maombi hakusaidii, maana njozi imebeba jibu na njozi bila matatizo haina thamani

✅Maono bila kujibu matatizo na maswali ya watu hayana thamani. _”Vision must has problems to solve otherwise has no value”_

✅Kulalamika kwenye maombi hakusaidii ikiwa uwezi kiunganisha njozi na jibu

*HOME WORK*
✳Tafuta mahali penye malalamiko utapata chakula

 

*************** MWISHO  ***************