MBINU ZA KUOMBEA NDOTO ILI USIKWAME KIMAISHA

SEMINA YA NENO LA MUNGU NA MWL MWAKASEGE.

UWANJA WA TANGAMANO TANGA 5 JUNE 2017

SOMO MBINU ZA KUOMBEA NDOTO ILI USIKWAME KIMAISHA.

Siku ya Kwanza.

Hii ni semina ya neno la Mungu kwa hiyo kaa mkao wa kujifunza. Hakikisha unakuwa na Biblia na daftari yako. Uwe kama watu wa Beroya waliokuwa wanayachunguza maandiko.

Lengo: Kuimarisha uhusiano wako na Mungu katika Kristo Yesu.

Lengo la kukutangazia somo si suala la kufundisha kuhusu ndoto bali ni kutumia somo la Ndoto ili kuimarisha uhusiano wako na Mungu katika Kristo Yesu uwe mzuri

Mungu hana dini na hili somo halina dini haijalishi wewe ni mkristo sio mkristo unaota ndoto. Kwa hiyo fuatilia hili somo vizuri kabisa na Mungu akusaidie kujua namna ya kuombea juu ya ndoto unazoota.

NDOTO INA VYANZO VISIVYOPUNGUA VINNE

Ndoto ninayosema hapa si ile vision yaani kile unachokiona kwa ajili ya hali yako ya baadae. Nazungumza ndoto unayoota usiku ukiwa umelala.

1.CHANZO CHA KWANZA NI MUNGU

Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.   Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;AYU. 33:14-15 SUV

Mungu huleta Ndoto mara moja au mara mbili na utaona akirudia hata zaidi ya mara moja japo watu hawajali na wengine husema ni ndoto tu.

 1. CHANZO CHA PILI NI SHETANI.

Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda BWANA, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote.KUMBU KUMBU. 13:1-3

Si ndoto zote anazoota mtu huwa zinatoka kwa Mungu bali pima vizuri kwa neno la Mungu kile ulichoambiwa kutoka katika ndoto hizo  haijalishi kimetokea kiasi gani,usitishike sana bali angalia sana matokeo yake yaani mwisho wake unakupeleka wapi

Angalia kama hicho kilichosema kama kinakutoa kwenye maombi au kukuweka mbali na Mungu.  Shetani naye anaweza sema vitu na vikatokea  kwa hiyo isikupe shida ila pima na neno la Mungu utajua ukweli.

3.SHUGHULI NYINGI.

Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno.

MHUBIRI. 5:3.

Mtiririko wa shughuli nyingi huleta ndoto za aina fulani. Na shughuli nyingi kwa Biblia maana yake ni Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai.Mathayo 13:22

Maana yake ni masumbufu ambayo hayapo katika mapenzi ya Mungu.  Mungu anatumia ndoto kukuambia kuwa hukutumia vizuri siku yako na hujamzalia Mungu matunda ndio maana Mungu atasema na wewe kwa njia ya ndoto ili kukuonesha kuwa unavyotumia muda wako si sawa.

4.MAZINGIRA YA KIROHO YA MAHALI UNAPOLALA

_Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani. Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale. Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa. Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.   Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli BWANA yupo mahali hapa, wala mimi sikujua. Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni.

MWANZO. 28:10-17_

Sasa fikiria hapa Yakobo alilala mahali ambapo pana miungu mingine maana tunaona alipolala Mungu wa eneo lile alijifunua katika Ndoto.  Na yule Mungu akasema mimi ni Mungu wa baba yako na akasema atamfuatilia kila mahali.

Sasa geuza upande wa pili. Mtu kajenga hapo ambapo kuna madhabahu ya miungu au  kaweka kitu kibaya na wewe hujajua hata namna kuombea eneo unalola maana kuna vitu vingine ni vigumu na angalia namna ndoto unazoota hapo ukilala ( kama ni nyumba uliyopanga au uliyonunua au nyumba ya kulala wageni). Angalia aina ya ndoto unazoota ukilala hapo utajua hiki ninachokuambia

Mtu mmoja alisema Mwalimu napata shida kulala kwa sababu ndoto ninazoota ni ngumu. Na alipokuwa anaomba Mungu  amsaidie  ili kumfanikisha, akilala hapo nyumbani kwake usiku alikuwa anaona nyoka kwenye ndoto. Na saa nyingine akitaka kuingia katika baadhi ya vyumba katika nyumba yake anaona kama kuna mtu anamzuia kuingia na akuchungulia katika chumba alichotaka kuingia anaona nyoka kajiviringisha hapo  kwa hiyo haingii katika hicho chumba maana nyoka anatumika kama zuio kwenye hicho chumba.

Na alikuwa hajui maana yake nini, nikamuuliza  hii nyumba ulijenga au ulinunua akasema nilinunua na haikukaliwa na watu muda mrefu kwa hiyo nikamuambia namna ya kuomba na akaomba na ile shida yake ikatoweka siku hiyo hiyo.

MAENEO MUHIMU MATATU.

 1. Kuombea Ndoto zile ambazo umeota na usingependa yatokee kama ulivyoota.

Unaombaje….

Si kila  unachoota lazima kitokee kama unajua maandiko unaweza zuia kisitokee.

Mimi, Nebukadreza, nalikuwa nikistarehe katika nyumba yangu, nikisitawi katika nyumba yangu ya enzi. Nikaota ndoto iliyonitia hofu; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa changu, zikanifadhaisha. Basi nikatoa amri kwamba wenye hekima wote wa Babeli, waletwe mbele yangu, ili kunijulisha tafsiri ya ndoto ile. Ndipo wakaingia waganga, na wachawi, na Wakaldayo, na wanajimu; nikawahadithia ile ndoto; wao wasiweze kunijulisha tafsiri yake. Bali hatimaye Danieli akaingia mbele yangu, ambaye jina lake ni Belteshaza, kwa kufuata jina la mungu wangu; tena ndani yake inakaa roho ya miungu watakatifu; nikamhadithia ile ndoto, nikisema,DANIEL. 4:4-8

Wale wachawi wakashindwa kutafsiri ndoto ndio maana jifunze  kutotafuta tafsiri yake  nje ya neno la Mungu bali fuatilia katika biblia .

Ile miaka ya 85 / 86 na Mungu aliposema na Mimi kwa njia ya ndoto  na zilikuwa zinakuja miaka ile ya 82 /83 (nilikuwa bado sijaokoka) na nilikuwa naenda kwa waganga kutafuta tafsiri na nilikuwa chuo kikuu. Na walitafsiri  wanavyojua wenyewe katika miungu yao  na hawakunipeleka kwenye tafsiri halisi kama  Mungu   alivyo maanaisha.

Angalia tena mstari wa 17    Hukumu hii imekuja kwa agizo la walinzi, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge.DAN. 4:17

Sasa ile ndoto iliishia kutangaza hukumu ile hukumu iliyotangazwa ilikuwa kwa nyakati saba tunaweza sema kwa miaka 7. Swali la kujiuliza  je kwani ilikuwa lazima itokee? Maana tunaona Nebukadreza akiondolewa kwenye nafasi.

Kama unasoma Biblia yako vizuri ilikuwa si lazima itokee maana kuna vitu kama vitatu hivi unaviona hapo

1.Aliambiwa kwanini adhabu imekuja (hakumpa Mungu heshima) kwa hiyo alihitaji kutambua tu na kutoa heshima kwa Mungu.

2.Mstari wa 26-27

Na kwa kuwa waliamuru kukiacha kisiki cha shina lake; ufalme wako utakuwa imara kwako, baada ya wewe kujua ya kuwa mbingu ndizo zinazotawala. Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha.DAN. 4:26-27

Na ile Ndoto ilimwambia na kitu cha kufanya ili asiingie kwenye shida na ili jambo  lisitokee lile lilotabiriwa kwenye ndoto.

Kulikuwa na faida gani akapokea tafsiri na kupuuuzia ujumbe  uliokuwemo kwenye ndoto.

Watu wengi sana wanapokea tafsiri na wanapuuzia ujumbe.  Hawafuatilii kilichomo ndani ya ndoto.

3.Hayo yote yakampata mfalme Nebukadreza. Baada ya miezi kumi na miwili, alikuwa akitembea ndani ya jumba la kifalme katika Babeli.DAN. 4:28-29

Mungu alimpa miezi 12 ili kutambua mambo yale mawili yaani kutambua kuwa Mungu  ndiye anayetawala na kufuata ushauri aliopewa na Daniel.

Na mambo yote yaliyotokea ni kwa sababu alipuuzia ujumbe uliokuwa kwenye ndoto  alyopewa na Mungu.

Nebukadreza alikuwa mtumishi wa Mungu  kama askari magereza wa kuwafunga wana wa Israel miaka 70 na apewe na vyombo vya hekaluni ili avitunze

Baada ya miaka 70 Mungu alikuwa anadai na vyombo alivyotakiwa kutunza. Na mtoto wake Nebukadreza alivunja mashart na ndio maana alipigwa Mene mene ….  kiti cha enzi cha Nebukadreza kilikuwa na pingu kwa sababu kilikuwa kiti cha askari magereza.

Kwa hiyo katika siku kadhaa tutajifunza  namna ya mambo haya. Na nia ya Mungu sio kukupeleka jela anakupa taarifa ili huenda ukabadilika na ukabadilisha msimamo wako ili utende mema.

Katika Daniel 3   Nebukadreza unaona  alipewa na Mungu   nafasi ya kuwa mfalme na alitengeneza sanamu. Mungu alisema naye kwa njia ya ndoto  kuwa Nebukadneza umeenda mbali unahitaji kutengeneza (sura ya nne) na Mungu anasema nao kwa njia ya ndoto lakini wengi sana wanapuuzia. Wanasema ni ndoto tu ndoto tu. Hakikisha hufanyi kosa la aina hiyo.

 1. YALE ULIYOOTA YAMETOKEA KAMA ULIVYOOTA LAKINI UNATAKA KUYABADILI YASIENDELEE KAMA YALIVYOTOKEA.

Hayo yote yakampata mfalme Nebukadneza. Baada ya miezi kumi na miwili, alikuwa akitembea ndani ya jumba la kifalme katika Babeli. Mfalme akanena, akasema, Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe kao langu la kifalme, kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu? Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee mfalme Nebukadneza, maneno haya unaambiwa wewe; Ufalme huu umeondoka kwako. Nawe utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni; utalishwa majani kama ng’ombe, na nyakati saba zitapita juu yako, hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yote. Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadneza; alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng’ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege.   Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadneza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi; na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe? Basi wakati uo huo fahamu zangu zikanirudia, na kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu, enzi yangu na fahari yangu zikanirudia; na mawaziri wangu, na madiwani wangu, wakaja kunitafuta; nami nikathibitika katika ufalme wangu, nikaongezewa enzi kupita kiasi. Basi mimi, Nebukadneza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili.DAN. 4:28-37

Ina maana alikuja kuwa kichaa na alipewa taarifa mwaka mzima na ile hukumu ilimpata na alifungwa porini.(sababu kuu alipuuzia ndoto aliyoambiwa)

Na kulikuwa hamna sababu ya kukaa nyakati saba  maana aliambiwa tu hadi atakapotambua ina maana asingetambua hizo nyakati, miaka ingeongezeka ya kukaa jela ( porini) na angetambua mapema ina maana hizo nyakati zingepungua.  Katika kipindi hiki cha agano jipya ni bora sana maana hamna sababu za kukaa utumwani au jela miaka 7 wakati una nafasi ya kupunguza au kuombewa kufutiwa  hicho kipindi.

Fikiria Nebukadneza   hana uwezo wa kujiombea mwenyewe  je watu wake wa karibu kwanini hawakuomba kwa ajili yake?.. omba kwa Roho  Mtakatifu atajua umuombee kwa namna gani. Angalia

Yakobo 5:15 Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.

Kwa hiyo unaweza ukaomba toba kwa ajili ya mtu mwingine hata kama yeye hataki kufanya toba ila kwa sababu wewe umeomba Mungu atakusikia na kumsamehe. Na hii ndio nafasi ya kikuhani ndani ya kanisa na kuomba kwa kanisa kama kuhani  ili mwenye dhambi aponywe na asamehewe.

A.Kwa hiyo kama Daniel angeweza omba kwa imani kama Yakobo 5:15 uwe na uhakika Nebukadneza   angetoka mapema kwenye adhabu.

Lakini sijajua kwanini Daniel hakumuombea Nebukadneza  .  Katika Biblia sijaona katazo lolote ila Samwel aliambiwa asimuombee Sauli *Bwana akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli?*1 Samweli 16:1a

Ila tunaona Daniel akitoa  Ushauri kwa Nebukadneza   lakini hakufanya maombi ya rufaa. Kwa  mwombaji yoyote  lazima ajue namna ya kutumia neno la Bwana kama sheria kwenda  nalo kwa Mungu kwa ajili ya kukata rufaa ili utoke kwenye adhabu.

B.NJIA NYINGINE NAMNA YA KUFANYA

26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.

Warumi 8 :26

27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.

Warumi 8 :27

Mstari wa 26 ni wa wewe kujiombea wewe mwenyewe na mstari wa 27 wa namna ya kuwaombea wengine.

 1. KUOMBA KWA KUSIMAMIA KUSUDI LA MUNGU.

Angalia Warumi 8: 28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

Kwa hiyo Daniel angeomba kwa Mungu juu ya kusudi alilomsimamisha Nebukadneza   kwa nafasi yake. Na kama unaomba juu ya kusudi la Bwana.. na katika matendo ya mitume tunaona  Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu.Matendo ya Mitume 13:36

Ina maana hakulisimamia kusudi la kwake bali alisimamia kusudi la Bwana. Hujiulizi kwanini Sauli alifukuzwa kazi na aliendelea kupata mshahara wake na kwanini Nebukadneza hakufukuzwa moja kwa moja. Daniel angeendelea kuomba na Mungu angeweza msamehe Nebukadneza

22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.

Mathayo 24 :22

Watwule ni waliotengwa kwa ajili ya kusudi la Mungu, kutengwa maana yake kuweka maalum au wakfu kwa ajili ya kazi ya Mungu  (kusudi) kwa hiyo ukiomba kufuata kusudi la Mungu utaona hata shetani kama alikusudia kukukwamisha Mungu atakupromote.

Mteule anayesimia kusudi la Bwana utaona Mungu anamsaidia kwa hiyo shetani asikutishe ukiona umechafuka nenda katafute damu ya Yesu kukusafisha. Akikuangusha inuka.endelea mbele.. usishindwe na shetani pambana hadi mwisho.

Mtu mmoja alinijia na kusema  alipokuwa anamuomba Mungu ili amfanikishe basi aliota ndoto na akaona yupo nyumbani kwao na katika uwanja wa kwao  mara akamwona nyoka kasimama usawa wake na alijaribu kumkemea kwa jina la Yesu lakini akawa haondoki na Mara akamuuma kidole chake na alipoamka toka usingizini  akaona kidole chake kinatoa damu. Na kesho yake alienda kanisani kwake maana alikuwa kaokoka na alipoulizwa na mchungaji wake hata kabla hajamiliza kueleza akaanguka chini  wakakemea pepo lilitoka pepo la mauti  lakini baada ya pale uchumi wake ukawa mbaya sana na kila alipokuwa anapanga nyumba alikuwa anafukuzwa.

Akaniuliza sasa hapa Mwakasege ndio nafanyeje sasa.  Nilielewa moja kwa moja unapoona umetumia jina la Yesu  unashindwa hakikisha damu ya Yesu inafanya kazi kwanza kabla ya jina la Yesu.  Damu ya Yesu ndio ilifunuliwa kwanza maana jina la Yesu ni la agano kwa hiyo ukiona kitu katika ulimwengu wa roho kimetokea hakijakaa sawa usijaribu kukemea kama hauko sawa sawa bali tubu kwanza.( kama hujakaa vizuri na Mungu wako)

Kaangalie kwa wana wa Skewa walikemea pepo lakini walishindwa na pepo liliwavuruga sawa sawa. Walikuwa hawanajulikani katika ulimwengu wa Roho maana unapewa authority na damu ya Yesu kutumia jina la Yesu. Wenyewe walikuwa hawana hiyo authority siku hiyo ya kutumia jina la Yesu

Na Mungu  alikuwa anamuambia kuwa kuna kitu cha kushugulikia  ambacho hakijakaa sawa sawa. Na japo aliombewa ila walisahau kuondoa  ile sumu ambayo iliingia na yule nyoka maana ilikuwa ni sumu ya Kiroho ndio maana iliua uchumi wake na kumletea roho ya kukataliwa.

 1. KUOMBEA NDOTO AMBAZO UNALETEWA TAARIFA ZA MAMBO YAJAYO AMBAYO UNAHITAJI KUJIANDAA NAYO NA HUWEZI KUYABADILI.

Mwanzo 41:1-37  Ndoto za farao za masuke saba na ng’ombe saba. Yananza masuke mazuri yanaliwa na mabaya na ng’ombe hivyo hivyo.

Wachawi walishindwa kutoa tafsiri na Yusufu ndio alikuja kutoa tafsiri  Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi.MWANZO. 41:32 .

Sababu ya kuleta ndoto mara mbili Mungu amelikusudia ili kulitimiza kwa hiyo yalihitajika maandalizi. Ya kujiandaa na alikwambia na kitu cha kufanya.

Ndoto kama hiyo uwe na uhakika kuna maandalizi ya muhimu unayotakiwa kuyafanya ili uvuke hapo.

Farao alitii na hakupuuzia, maana nae alitaka kupuuzia kwa kusema ni ndoto tu . Basi Farao akaamka, kumbe! *Ni ndoto tu.*MWANZO. 41:7b

Alitaka kudharau lakini Mungu alimuongezea kitu kingine  Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo.MWANZO. 41:8

Ndipo alianza kufuatilia.

Kuna watu wanaohitaji  kufanikiwa na wanaota wako shuleni  unakuta mtu yuko chuo kikuu ila anaota yuko primary maana yake kuna  mahali umekwama  na unahitaji maandalizi maana shule ni sehemu ya maandalizi. Kwa hiyo  hapo usitafute muujiza bali fanya maandalizi

Kuna mtu mmoja alinisikia nilikufundisha  na akaweka kwenye matendo  mara akaanza kuota yuko primary nikaomba na akasema akaota yuko secondary na akaona tena yuko chuo kikuu   na basi nikasema  na yule mtu endelea kuomba hadi uone graduation yako .

Tufanye zoezi hapa.  Wangapi hapa wanaota wanakula chukula kwenye  ndoto? Na hizi ndoto sio nzuri kutegemea na umeota nini. Mfano ukiota ndoto unakula na mzazi wako na unampa Chakula na anasema nimeshiba maana yake ni _Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu.

ZAB. 91:16_

Ina maana yuko tayari kuondoka (kufa) sasa kama unakula chakula kwa jinsi ya kawaida  na watu waliokufa ni chakula cha miungu. Wana wa israel walitengeneza ndama na wakala na kunywa (sakrement)

Ukila namna hiyo unakula na kushirikiana na mapepo.  Na kuna agano unaingia hata kama hujazaliwa miungu huwa inaingia agano ndio maana Mungu aliwafuatilia watu ambao walizaliwa kwa uzao wa Ibrahim.  Yesu alimfuata Zakayo kwa sababu ya agano maana Biblia inasema nae ni mwana wa Ibrahimu.

Kuna maagano yapo kwenye ulimwengu wa Roho Mungu anataka kukuweka sawa upate kufuatilia na kuvuka

Maombi kama kuna watu wamekula chakula kwenye ndoto haijalishi ni kizuri kibaya Ngoja  tupime na neno la Bwana kwa maombi. Kama ni uwe na uhakika kitatoka tu. Baada  hapo Mwl alifanya maombi sana na nguvu za Mungu zilishuka na kuwafungua watu.

Ni siku ya kwanza ya semina na   hakikishag unampata huyu Yesu maana ni mtaji muhimu sana katika maisha yako maana bila Yesu semina hizi hazitakuwa na msaada kwako hivyo basi hujaokoka hakikisha unaokoka au uliokoka ukarudi nyuma tengeneza na Mungu. Hamna sababu ya kuendelea kukaa dhambini wakati msahama upo msalabani rudi kwa Bwana.

Baada ya hapo nenda pale juu bonyeza kile kitabu cha Hongera kwa kuokoka kisome kitakusaidia pia kuna sala ya toba mule (hatujaandika hapa ili kwenye kile kitabu kipo.

Ubarikiweee sana na YESU  mkaribishe na mwingine kwenye semina hii kwa njia redio au mtandao au kufika moja kwa moja kwenye semina (Tangamano Tanga)

==Glory to God, Glory to God==

 

SEMINA YA NENO LA MUNGU NA MWL MWAKASEGE

UWANJA WA TANGAMANO TANGA 6 JUNE 2017

SOMO MBINU ZA KUOMBEA NDOTO ILI USIKWAME KIMAISHA.

Siku ya Pili.

Hakikisha unapata DVD au CD na kusikiliza na kusikiliza na utaona unapata kitu cha kukusaidia.

MAMBO YA KUZINGATIA

1.Katika ndoto unawezafanya agano na Mungu.

Katika biblia neno ndoto kuna mahali limetumika kama Njozi au maono ya usiku lakini maana yake ni Ndoto.

Tunaona Ibrahimu aliongea na Mungu kwenye  ndoto.

 

Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana. Abramu akasema, Ee Bwana MUNGU, utanipa nini, nami naenda zangu hali sina mtoto, na atakayeimiliki nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski? Abramu akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtu aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu.   Nalo neno la BWANA likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali atakayetoka katika viunoy vyako ndiye atakayekurithi. Akamleta nje, akasema, Tazamay sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. Akamwamini BWANA, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki.  Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,MWA. 15:1-6, 18 SUV

Pia tunaona katika mstari wa 18 Bwana  alifanya agano  na Ibrahim  katika ndoto.

Agano  walilofunga katika ndoto liliwafanya wana wa Israel kuishi misri miaka 400.

Na waliomba waondolewe uchungu wa kazi lakini Mungu aliliangalia agano ndio maana utasema Mwl mbona biblia inasema ombeni lolote?  “ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.”YOHANA. 15:7.

Lakini nakuambia omba kwa kufuata agano maana kuna tofauti ya maombi ya mtu wa chekechea au primary na secondary na maombi ya University.

Mungu ametoa  nafasi ya kumsikiliza kila mtu maana kila mtu kwa ngazi yake karuhusiwa kuomba. Sasa Biblia inasema “tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.”1 Yohana 5:14b

Ndio maana nakuambia omba kwa kufuata mapenzi ya Mungu. Kwa5 kila jambo lina utaratibu wake. Huwezi endesha gari kwa utaratibu wa Marekani ukiwa hapa Tanzania lazima ufuate taratibu wa hapa Tanzania

2.Kukujulisha kuwepo kwa agano

Habari za Yokobo kuota Ndoto.

10 Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani. 11 Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale.

12 Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake.

13 Na tazama, Bwana amesimama juu yake, akasema, Mimi ni Bwana, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako.14 Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa.

Mwanzo 28 :14

15 Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.

16 Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli Bwana yupo mahali hapa, wala mimi sikujua.

17 Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni.18 Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake.

19 Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu. 20 Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae;

21 nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu.22 Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.

Mungu hakufunga agano na Yakobo bali alifunga na Ibrahim babu wa Yakobo  na alimuambia Yakobo kuwa nitakuwa Mungu wako. Maana yake kuna mahusiano tumekubaliana na baba yako yanayotaka nikufuatilie  katika maisha yako.

Yakobo alikuwa hamuamini Mungu na ndio maana alisema “Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; 21 nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu.22 Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.”

Alisema hivyo kwa kuwa hajawa bado my personal God na tunaona hapa njia ya ndoto ilimjulisha kuwa Mungu   alifunga agano na baba yake. Ndio maana alisema Mimi ni Bwana, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako

3.Unaweza kukumbushwa kwa njia ya Ndoto juu ya kuwepo kwa agano linalohusu

Ikawa, wakati wale wanyama walipochukua mimba, naliinua macho yangu nikaona katika ndoto, na tazama, mabeberu waliowapanda hao wanyama walikuwa na milia, na madoadoa, na marakaraka. Na malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, Yakobo! Nikasema, Mimi hapa. Akasema, Inua, basi, macho yako, ukaone; mabeberu wote wanaopanda wanyama wana milia, na madoadoa, na marakaraka; maana nimeona yote aliyokutendea Labani. Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa.

MWANZO. 31:10-13

Mungu anamkubusha kwa njia ya ndoto kuwa kuna agano linalokuhusu na anamwambia kuwa ni Mungu wa Bethel na kulikuwa na alama kuwa maana kulikuwa na jiwe na akalala.

Halikuwa jiwe na kawaida  maana alipolala na Mungu alijifunua na ukifikiri natania jaribu kuchukua jiwe na uweke kama mto uone kama utalala. Ndio maana unaona hilo hilo jiwe Yakobo alimina mafuta na akaweka kama nguzo ili iwe alama ya nadhiri yake.

_Akasafiri Israeli, pamoja na yote aliyokuwa nayo, akaja Beer-sheba, akamchinjia sadaka Mungu wa Isaka babaye. Mungu akanena na Israeli katika ndoto ya usiku, akasema, Yakobo, Yakobo. Akasema, Mimi hapa. Akasema, Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako, usiogope kushuka mpaka Misri; maana nitakufanya uwe taifa kubwa huko. Mimi nitashuka pamoja nawe mpaka Misri; nami nitakupandisha tena bila shaka; na Yusufu ataweka mkono wake juu ya macho yako. Yakobo akaondoka kutoka Beer-sheba; wana wa Israeli wakamchukua baba yao na watoto wao wadogo, na wake zao katika magari aliyoyapeleka Farao ili kumchukua.

MWANZO. 46:1-5.

Alitoa sadaka kwa Mungu  wa baba yake nat kama wewe umetoa sadaka kwa Mungu wa baba yako unakuwa unaamsha agano lililopo na kama unaenda nyumbani kwenu ujue atakutembelea kwa njia ya ndoto.

Na Mungu alisema nae kwenye ndoto na alimkumbusha kuwa niko pamoja na wewe.

Na alipotoa sadaka ina maana alikuwa anahitaji msaada na kwa sababu alikuwa na agano na Mungu.

_Nikusanyieni wacha Mungu wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu.

ZABURI. 50:5 _

Kwa hiyo agano huwa linafanywa kwa sadaka.

 1. Atakujulisha ujumbe wa agano lilopo.

Kwa ishara au wazi wazi.

Na ukitaka kutafsiri Ndoto za kwako hakikisha unasoma biblia maana mwenye kutafsiri Ndoto ni Mungu.  Na tafsiri ya Mungu ipo kwenye biblia.

Mifano.

Nabukedneza  aliota mti mkubwa una ndege na chini kuna wanyama.. na akasema ukatwe.

Ukiona namna hiyo Mungu anasema na wewe kwenye ndoto kuwa kuna agano Lipo. Maana agano haliwezi kukuruhusu ufanikiwe zaidi ya kiwango kilicho kwenye agano.

Watu wanaotumia “vigoda” ina maana ni kiti cha enzi.

Kwa hiyo katika ndoto utaona.. na damu inatumika kuzungumza na miungu maana  dhambi iliua mawasiliano na Mungu katika agano la kale Mungu aliruhusu damu za wanyama na ndege ili ziongee.

Biblia inasema damu ni uhai sasa ukitumia damu ya mbuzi kwenye agano utakuwa unaona mbuzi kwenye ndoto zako kama unaomba Mungu akutoe ulipokwama.  Ina maana mbuzi ndio ilitolewa sadaka kwa ajili yako ndio maana Mungu anakusisitiza  kuwa fuatilia hiyo alama ili uipangue  kwa kutumia damu ya Yesu  .

Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng’ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili;

basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?Waebrania 9:13- 14

Kama ni sadaka ya jogoo utaona jogoo katika  Ndoto zako utaona jogoo kila ukiomba Mungu akufanikishe.

Haijalishi umefungwa kiasi gani Mungu atakuja kukufungua. Kama alivyomfungua punda aliyepandwa na Yesu.

Kuna watu wanaota ndoto wako njia panda na hawajavuka hapo  katika biblia katika njia panda kuna kiapo.

21 Maana mfalme wa Babeli alisimama penye njia panda, penye kichwa cha njia hizo mbili, ili atumie uganga; aliitikisa mishale huko na huko, akaziuliza terafi, akayatazama maini.

Ezekieli 21 :21

22 Katika mkono wake wa kuume alikuwa na kura ya Yerusalemu, kuviweka vyombo vya kubomolea, kufumbua kinywa katika machinjo, kuiinua sauti kwa kupiga kelele sana, kuweka vyombo vya kubomolea juu ya malango, kufanya maboma, na kujenga ngome. 23 Jambo hili litakuwa kwao kama uganga wa ubatili, mbele ya macho yao waliowaapia viapo lakini ataufanya uovu ukumbukwe, ili kwamba wakamatwe.

Ezekieli 21 :23

Ukiona namna hiyo ujue kuna kiapo hapo  mambo hayo yapo kwenye biblia.

Kusikia huja kwa neno la Kristo maana lazima usome biblia maana kusikia huja kwa neno la Kristo.

Kuna watu wanaota wanafunga ndoa kwenye Ndoto. Angalia vizuri hiyo Ndoto sio nzuri

Mwaka wa 1984  niliota ndoto upinde wa mvua na ulikuja mara nyingi nikitembea na nao unatembea.

Pia niliona katika nyumba yetu upo juu na umeishia mbinguni.  Na nilianza kuomba na kusoma biblia na nakagundua.

Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele; Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi. Hata itakuwa nikitanda mawingu juu ya nchi, upinde utaonekana winguni, nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili. Basi huo upinde utakuwa winguni; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi. Mungu akamwambia Nuhu, Hii ndiyo ishara ya agano nililoliweka kati yangu na wote wenye mwili walioko katika nchi. MWANZO. 9:12-17

Kwa hiyo upinde ni alama ya agano.

Mungu alisema muulize mama yako. Na bahati nzuri mama yangu alikuja kunitembelea kwetu .

Na mama aliniambia alipokuwa anasoma  kule Tosamaganga katika shule ya Wakatoliki aliyokuwa anasoma  walitaka asomee usista maana walimpenda.

Mama yangu alikuwa anataka kuolewa maana angesomea usista asingeolewa. Kwa hiyo alienda porini na kuanza kuomba kwa Mungu maombi ya nadhiri. Na alisema watoto nitakao zaa hao nimekupa Mungu watumie ila mimi niolewe.

Basi nikaelewa Mungu aliniambia kuwa kabla hujazaliwa wewe ulikabidhiwa kwangu.

Na nilijua kuwa kuna agano ila sio maisha mepesi maana  inabid niishi kwa kufauata agano.

Namshukuru Mungu aliyeniongoza kunipeleka kwenye biblia. Na nikaelewa.

Kama unaota ndoto na mtu aliyekufa nyumbani kwenu angalia vizuri.  Na ukiota Ndoto unavaa mavazi au bibi Harusi ina maana umeolewa kwenye ulimwengu wa roho check vizuri.

Mbaya sana ukiota ndoto unazini ni mbaya sana. Mtu mmoja alisema anazini na mnyama maana yake unatengwa na jamii na mauti.

Mtu awaye yote alalaye na mnyama sharti atauawa.

Kutoka 22:19

Na alaaniwe alalaye na mnyama wa aina yo yote. Na watu wote waseme, Amina.

Kumbukumbu la Torati 27:21

Na mwingine  alisema anazini na mtoto wake ina maana utatengwa na jamii.

20 Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa amefunua mavazi ya babaye. Na watu wote waseme, Amina.

Kumbukumbu la Torati 27 :20

Unahitaji kujua namna ya kutoka mahali hapo unapoota Ndoto za namna hiyo kwa njia ya neno  Mungu ( neno kukunasua mahali ulipokwama)

Mwingine aliota Ndoto kazini na mtu kwenye ndoto na baada ya muda ndoa yake ilipata shida.

Mwingine aliota Pete ya ndoa imekatika ina maana  agano limevunjwa  na baada ya miez 6 mume wake alihama chumbani.(hakuomba mapema na alipata madhara)

Mwingine aliota nyoka kapita tumboni kwake baada ya hapo ndoa yake ikafa. Na nyoka ina maana ni miungu ya ukoo

Ukiota ndoto za aina hiyo uwe na uwe speed kuomba na kufutilia

Kuota unazini kwenye ndoto sio sahihi haijalishi unamfahamu huyo mtu unayezini nae au humfahamu ila sio ndoto nzuri hata kidogo  Angalia pia alama iliyopo hapo unapoota  mfano umeona gauni la harusi limechanika.

Sauli alishika vazi la samwel lilichanika.

_27 Naye Samweli alipogeuka, aende zake, Sauli akaushika upindo wa vazi lake, nalo likararuka.28 Basi Samweli akamwambia, Leo Bwana amekurarulia ufalme wa Israeli, naye amempa jirani yako, aliye mwema kuliko wewe.

1 Samweli 15 :28_

Yesu aliposema damu ya agano  “Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.Luka 22:20”

Tumia damu ya Yesu kupangua vitu vibaya vilvyoletwa na ndoto

5 tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake,

Ufunuo wa Yohana 1 :5

 

basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?Waebrania 9:14

Niliposikia hili somo la Ndoto  miaka ya nyuma Mungu aliponifundisha . Nilisikia sana kumshukuru Mungu maana ilikuwa ni neema . Na endelea kumshukuru Mungu kwa kuweka wazi mambo haya ya Ndoto.

Ndio maana naimba wimbo wa ni salama rohoni mwangu kwa sababu ya neema ya Mungu iliyofunguliwa sasa inayotupa kujua mambo haya kwa uwazi.

Baada ya hapo yalifanyika maombi sana kwa ajili ya watu waliopata shida kwenye ndoto na Mungu aliwafungua sana watu wake.

Ubarikiweeee na Bwana Yesu tuonane tena kesho..

==Glory  to God Glory to God==

 

SEMINA YA NENO LA MUNGU NA MWL MWAKASEGE.

UWANJA WA TANGAMANO TANGA 7 JUNE 2017

SOMO MBINU ZA KUOMBEA NDOTO ILI USIKWAME KIMAISHA.

Siku ya Tatu.

 

Kitabu cha Hongera kwa kuokoka.

https://drive.google.com/file/d/0BxdP6mgDJWByVERtampLTGZWRms/view?usp=drivesdk

Hakikisha unatafuta kanda na sikiliza na kusikiliza. CD au DVD  za mahali kama Mbeya na Dodoma na Dar es Salaam na maeneo mengine hapa nchini tuliyofundisha habari za ndoto. Tuliangalia kwa sehemu na sina uhakika sana kama ntaweza pitia maeneo yote kwa siku hizi chache.

Pia kama unaweza nenda kwenye ukurasa wetu wa Facebook Christopher & Diana Mwakasege (MANA MINISTRY). Au bonyeza hii link https://www.facebook.com/Christopher-Diana-MwakasegeMana-Ministry-132462780111984/ Tayari tumeshatuma masomo kumi kuhusu ndoto bado masomo kama mawili matatu kabla hatujahamia somo lingine.

Kwa hiyo pitia hilo somo utapata kitu cha kukusaidia maana hatuwezi pitia somo lote kwa siku chache hapa Tanga.

Lengo la somo ni kuimarisha uhusiano wako na Mungu.  Ndio maana nakusisitiza si suala la kujifunza habari za ndoto bali ni kuimarisha uhusiano wako na Mungu katika Kristo Yesu.

MBINU ZA KUFANYA

1.Tumia damu ya Yesu ili kujiondoa kwenye maagano ya kiroho uliyojulishwa kwa njia ndoto juu ya kuwepo kwake na kufanyika kwake

Maana yake maagano yanatumika kuweka aina na kiwango cha maisha haijalishi linatoka kwa Mungu au Shetani.

Kama ni Mungu anahusika basi kutakuwa na msaada wa Mungu katika kuishi katika kiwango cha maisha. Na katika agano jipya utapata na neema yake na atakuwezesha kufika pale anapotaka ufike.

Jana tuliangalia mambo manne makubwa.

1.Agano linaweza kufungwa kwa njia ya ndoto na linaweza kuwa halisi na halali  Kiroho.

Na mfano Mwanzo 15:1-15 (Ibrahimu alifunga agano kwenye ndoto na Mungu)

2.Unaweza kujulishwa kwa njia ya ndoto juu ya kuwepo kwa agano katika maisha yako. Inawezekana si wewe uliyefunga au umeingizwa tu na unaona limekubana. Na Mungu atasema na wewe kukuonesha kama kuna agano linalokukwamisha.

Mwanzo 28: 10-16 (Yakobo alikumbushwa na Mungu kuwepo kwenye agano na Mungu  kwenye ndoto)

3.Unaweza kukumbushwa kwa njia ya ndoto kuwa kuna agano.  Mungu anakujilisha kuwepo kwa agano.

Mwanzo 31:10-13 (Mungu alimwambia Yakobo kuwa Yeye  ni Mungu wa Bethel. Mwanzo 46:5 hapa alisema Mimi ni Mungu wa baba yako.

4.Ujumbe wa agano linalokuhusu unaokujia katika ndoto unaweza ukawa wazi au ukakujia kialama au kiishara.

Kuna baadh ya ndoto zinakuja moja kwa moja. Mfano Yusufu alipotaka kumuacha Mariam (mama yake Yesu) alipotaka sasa kumwacha Malaika alimjia kwa njia ya ndoto na kusema nae kumwambia asimwache. Hii ndoto ilikuwa wazi kabisa. Na Yusufu baada ya pale alienda kumuoa yule dada.

Sasa kuna baadh ya ndoto zinakuwa na mafumbo hadi ujue namna ya kutafsiri.

Zingine zinakuja na ishara na wazi wazi yaani mchanganyiko. (Mwanzo 15:1-18) Mungu alijifunua kwa Ibrahimu kwa njia ya ndoto juu ya mambo yake. Ni mazungumzo yaliyokuwa wazi wazi na kuna ishara ndani yake. Fuatilia hiyo habari.

Na tunaona alitoa na sadaka na wale wanyama walikuwa na maana yake kwa hiyo unahitaji kufuatilia vizuri.

Hata kama kuna agano na shetani Mungu ni mzuri atakuambia kila kitu kwa ishara ili  ujue cha kufanya. Kwa hiyo hakikisha uwe na neno la kutosha maana kila jambo lina maana  ndio maana katika Ayubu unaona Mungu akisema na mtu kwenye ndoto mara mbili mara tatu  lakini japo mtu hajali.

Natamani kusema na wewe namna ya kutafsiri ndoto ili uelewe hata kama hatutaenda kila eneo ila nataka ujue kwa sehemu ndio maana nakusisitiza uwe na neno la kutosha.  Biblia inasema mwenye  kutafsiri ndoto ni Mungu.

Jana tuliangalia vitu vingi kidogo bila kukutajia mstari

Ndoto nyingi  za kiagano zinakuwa na mambo mengi kidogo  unahitaji kujua.

Yaani kuna agano ndani ya agano. Na nilikuwambia kuwa  mama yangu aliingia agano na Mungu na lilibana maisha yetu kutuwekea utumishi.

Mfano Mimi nilipokuwa mdogo nilikuwa sio muongeaji kabisa maana nilibadilishwa na agano kuwa mhubiri haikuwa rahisi maana sikuwa hivyo.

Nimesoma masuala ya uchumi darasani kwa hiyo lazima uwe updated sasa sikutarajia kama  naweza soma biblia mara kwa mara. Baada ya kuokoka maisha yamebadilika. Maana maisha yalibadilika kabisa. Maana nilianza kutokaaa na watu. Na nilikuwa naomba sana kila nikitoka kazini lazima niombe kwanza ndio nenda kula  lazima niombe hata saa moja ndipo narudi sebuleni..

Nilishangaa sana kwanini maisha yangu yamebadilila hivyo. Kati kati ya jambo hilo niliota ndoto nikaona kuna upinde wa mvua.

Sasa Upinde wa mvua maana yake nini  angalia  _”Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi. Hata itakuwa nikitanda mawingu juu ya nchi, upinde utaonekana winguni, nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili. Basi huo upinde utakuwa winguni; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi. Mungu akamwambia Nuhu, Hii ndiyo ishara ya agano nililoliweka kati yangu na wote wenye mwili walioko katika nchi.

MWANZO. 9:13-17.

Ujumbe huu ulikuwa na ishara angalia huo upinde  unaenelekea wapi au upo sehemu  gani.

Niliona pinde 3 zimeelekea kwenye nyumba tuliyokuwa tunaishi na kuelekea mbinguni.

1.Niliona upinde ukiwa juu ya Nyumba na kuelekea mbinguni.

2.Upinde  mwingine ulinizunguka na kila nikitembea zinatembea. Kwamba zimekuja 3 zina maana yake.

Mungu alikuwa ananiambia kuwa maisha yako yamefungwa na agano alilofunga na mama yangu. Kwa hiyo ndio maana maisha yangu yalibadilika kuanzia miaka ile ya 80 Mungu alipojifunua kwangu.

2.Unaweza ota mti mkubwa au kisiki au kiti cha enzi

Njozi za kichwa changu kitandani mwangu zilikuwa hivi; naliona, na tazama, palikuwa na mti katikati ya nchi, urefu wake mkubwa sana. Mti ule ukakua, ukawa na nguvu, urefu wake ulifika mpaka mbinguni, na kuonekana kwake mpaka mwisho wa dunia. Majani yake yalikuwa mazuri, na matunda yake mengi, na ndani yake chakula cha kuwatosha watu wote; wanyama wa kondeni walipata uvuli chini yake, na ndege wa angani walikaa katika matawi yake; kila kitu chenye mwili kilipata chakula kwake. Nikaona katika njozi za kichwa changu kitandani mwangu, na tazama, mlinzi, naye ni mtakatifu, alishuka kutoka mbinguni. Akapaza sauti yake, akasema, Ukateni mti huu, yafyekeni matawi yake, yapukusieni mbali majani yake, na kuyatawanya matunda yake, wanyama na waondoke hapo chini yake, na ndege katika matawi yake. Walakini kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya kondeni; kikapate maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na wanyama katika majani ya nchi;DANIEL. 4:10-15

Lakini moyo wake ulipoinuliwa, na roho yake ilipokuwa ngumu akatenda kwa kiburi, aliuzuliwa katika kiti chake cha enzi, nao wakamwondolea utukufu wake. Akafukuzwa mbali na wanadamu, moyo wake ukafanywa kuwa kama moyo wa mnyama, na makao yake yalikuwa pamoja na punda-mwitu; akalishwa majani kama ng’ombe, mwili wake ukalowa maji kwa umande wa mbinguni; hata alipojua ya kuwa Mungu Aliye juu ndiye anayetawala katika ufalme wa wanadamu, na ya kuwa humweka juu yake yeye amtakaye, awaye yote.DANIEL. 5:20-21

Ukiona kiti cha enzi katika ndoto ujue kuwa kina kitu cha kiroho. Sasa mfano fuatailia mtu aliyeingia kazini kwa kiapo maana kuna kazi lazima uape sasa mara nyingi baada ya hiyo kazi kufanya kazi nyingine au kuajiriwa mahali pengine inakuwa tabu sana. Na wakitaka kufanikiwa lazima kwanza watangue hicho kiapo.

Nilikuwa mahali fulani  na vijana waliniuliza swali gumu kidogo kwa vijana juu ya kuomba mchumba.

Katika biblia hamna kitu cha namna hiyo cha kuomba mchumba. Omba mke ngoja tuzungumze neno la ugumu kidogo.

Sasa mfano mkaingia kwenye uchumba na mkavalishana pete hilo ni agano na mchungaji akaja hapo akasemea na baraka. Sasa mfano mchumba siku chache kabla ya harusi anakukimbia. Sasa kama alifanya engagement kwanini asifanye disengagement.  Kwa maana hiyo kama  umeachwa na mchumba au umeacha mchumba uliefanya nae  engagement mara nyingi sana hili agano litakutesa na kukusumbua kwa sababu hilo litakuwa linabana sana maisha yako.

Uchumba wako utakuwa na shida, maana uchumba ni probabition maana kila mchumba atakuwa anakaa mbali na kusema huyu ni wa fulani kwa hiyo itakuwa shida. Mungu akufungue hapo, mtu akikuacha mwambie sana kama unataka tufunge uchumba siku ukiniaacha  lazima twende kwa mchungaji tukafanye disengagement ili kutangua hilo agano uwe huru.(ukifanya namna hiyo ujue wababishaji watakimbia hawatakusumbua na kukupotezea muda)

Neno la BWANA likanijia tena, kusema, Tena, mwanadamu, ujiwekee njia mbili, upanga wa mfalme wa Babeli upate kuja; hizo mbili zitatoka katika nchi moja; ukaandike mahali, upaandike penye kichwa cha njia iendayo mjini. Utaagiza njia, upanga upate kufikilia Raba wa wana wa Amoni, na kufikilia Yuda katika Yerusalemu, wenye maboma. Maana mfalme wa Babeli alisimama penye njia panda, penye kichwa cha njia hizo mbili, ili atumie uganga; aliitikisa mishale huko na huko, akaziuliza terafi, akayatazama maini. Katika mkono wake wa kuume alikuwa na kura ya Yerusalemu, kuviweka vyombo vya kubomolea, kufumbua kinywa katika machinjo, kuiinua sauti kwa kupiga kelele sana, kuweka vyombo vya kubomolea juu ya malango, kufanya maboma, na kujenga ngome. Jambo hili litakuwa kwao kama uganga wa ubatili, mbele ya macho yao waliowaapia viapo lakini ataufanya uovu ukumbukwe, ili kwamba wakamatwe.EZEKIEL. 21:18-23

Hapa nataka uone kitu kinachotokea njia panda na tunaona ameenda njia panda na alienda na sadaka zake yaani terafi na maini na alikuwa na majina ya miji na watu.

Tunaona Mungu  akiingilia kati ili kubatilisha kiapo maana kama mtu hujabatilisha kiapo ataishi sawa sawa na hilo neno  Mtu atakapomwekea BWANA nadhiri, au, atakapoapa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa kifungo, asilitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake.HESABU. 30:2

Mungu anasema hatamsahau katika uovu wake. Sasa jana nilikuambia kama umeota uko njia panda  ina maana maamuzi yako yamekwama. Ndio maana nakuambia andika hizo ndoto zako maana huwezi kumbuka kila kitu. Unaandika kwa ajili ya kufuatilia kwa ukaribu.

Sasa mwingine anaweza ota kakwama kwenye daraja au kila akitaka kuvuka hapo anakuta limevunjika na daraja lina maana yake.

Na niliona mwingine kakwama airport au kiwanja cha ndege na siku ya kwanza niliona hana passport na kaota tena yuko airport na kapoteza board pass  na aliamka kabla hajapita kwenye security  (ukaguzi).

Siku nyingine aliota yuko kwenye chumba cha kusubiri ndege na ndege ya kwake haijaitwa na akaamka. Akaniuliza Mwl sasa hapa ndio nafanyaje?

Nikamwambia kuwa umekwama na lazima utakuwa umekwama kimaisha. Na  nilimwambia namna ya kuomba na aliomba na akavuka. Kwa hiyo usipojua namna ya kuomba itakusumbua sana na utakwama.

Akasema, Ee Bwana MUNGU, nipateje kujua ya kwamba nitairithi? Akamwambia, Unipatie ndama wa miaka mitatu, na mbuzi mke wa miaka mitatu, na kondoo mume wa miaka mitatu, na hua, na mwana njiwa.MWANZO. 15:8-9

Utaona ishara za wanyama na kila mnyama ana kazi yake kibiblia. Maana ndiko utapata usahihi.

Ikawa Daudi alipokwisha kusema na Sauli, roho ya Yonathani, ikaambatana na roho ya Daudi, Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe. Sauli akamtwaa siku ile, wala hakumwacha arudi tena nyumbani kwa baba yake. Nao Yonathani na Daudi wakaahidiana, kwa kuwa alimpenda kama roho yake mwenyewe. Ndipo Yonathani akalivua joho alilokuwa amelivaa, akampa Daudi, na mavazi yake, hata na upanga wake pia, na upinde wake, na mshipi wake.

1 SAMWEL. 18:1-4.

Walifunga agano Daudi na Yonathani ni maagano ya ajabu sana. Sauli alipoondoka kwa sababu mrithi wa Sauli alikuwa ni Yonathan na Mungu alikuwa anataka kumwepusha Daudi katika ngome  ya ugomvi ndio maana Mungu alitaka waingie patano.

Na alimkabidhi na vazi lake maana yake chukua na nafasi niliyokuwa nayo. Katika ulimwengu wa roho kilikuwa ni kitu Halisi.

Katika kabila zingine unaweza pewa kiti,  au chungu au koti au fimbo zina maana Kiroho.  Nilienda eneo fulani niliona akina mama wakipeana hirizi wanasema hirizi ya uzazi na walikuja kwangu na niliwaeleza kitu cha kufanya.

Ukiota ndoto unapewa kitu cha kifamilia mfano koti au fimbo au viatu na mzazi wako ina maana anaelekea kuondoka  ndio maana nakuambia unahitaji kufuatilia katika maandiko na kujua namna ya kuomba.

Wale wanaume wakamwambia, Sisi tunataka tusiwe na hatia kwa ajili ya kiapo hiki ulichotuapisha. Angalia, tutakapoingia katika nchi hii, funga kamba hii nyekundu katika dirisha hili ulilotutelemshia; nawe uwakusanye kwako nyumbani mwako, baba yako, na mama yako, na ndugu zako, na watu wote wa nyumba ya baba yako.YOSHUA. 2:17-18

Hicho kiapo unakiona  mistari ya juu 13 na 14   ya kwamba mtawaponya hai baba yangu na mama yangu, na ndugu zangu wanaume na wanawake, na vitu vyote walivyo navyo, na kutuokoa roho zetu na kufa.   Wale wanaume wakamwambia, Uhai wetu badala ya uhai wenu, ikiwa hamwitangazi habari ya shughuli yetu hii; kisha itakuwa, wakati BWANA atakapotupa nchi hii, tutakutendea kwa ihisani na uaminifu.YOS. 2:13-14

Rahabu aliwaingiza ndugu zake ndani ya agano kwa kiapo na maisha yao kuanzia pale yalibanwa kabisa.  Na walikuwa na kamba nyekundu  ambayo ni ishara ya agano.

Ndugu zake walikusanywa nyumbani kwa Rahabu  na maisha yao ya kawaida yalikufa hapo na wakawa na maisha mengine.

Sasa sikia wale wapelelezi hawakumfuata Rahabu kwa kumtazama bali walifuata kamba nyekundu kama alama. Endapo ile kamba ingeondolewa ina maana hata nyumba yake  ingebomolewa. Kwa hiyo lazima ujue kuwa alama ambazo zinawekwa zinakuwa zinakufuatilia.

Katika ndoto Mungu akikuonesha alama fuatilia kwenye biblia  maana yake   ” Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu? Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu? Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye?1 KORINTHO. 10:18-22

ukiota ndoto unakula chakula kwenye ndoto angalia nani unayekula nae  na unashirikiana na nani.

Wala hawatatoa tena sadaka zao kwa wale majini, ambao huwafuata ili wafanye uasherati nao. Sheria hii itakuwa sheria ya milele kwao, kizazi baada ya kizazi.

LAW. 17:7

Kuna majini yanapokea sadaka na kufanya uzinzi (hili suala ni kipepo)

Na mtu yule atakayewaendea wenye pepo, na wachawi, ili kuzini pamoja nao, nitakaza uso wangu juu ya mtu yule, nitamtenga na watu wake.

LAW. 20:6

Ukiota ndoto unazini  ina maana shetani anapandikiza roho ya kukataliwa na ndugu zako ndio maana Mungu anataka ufuatilie hapo.

Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye. Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo. Kwa maana kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, mimi mwenyewe nimekwisha kumhukumu yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo. Katika jina la Bwana wetu Yesu, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na uweza wa Bwana wetu Yesu; kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu.1 KORINTHO. 5:1-5.

Katika kanisa la Korintho kuna watu walikuwa wanazini  na mama zao (mke wa baba yake). Sasa angalia adhabu yake hapo juu ina maana shetani anapandikiza mateso katika maisha yako.

Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti, na wa mataifa BWANA aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda. Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo.   Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa BWANA, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake.

1 FAL. 11:1-4

Mungu haruhusu watu wake kuolewa au kuoa  watu wa Imani nyingine.sasa sio kuwa Mungu analeta ubaguzi wa kidini ila anajua kuwa kuna mbegu mbaya inapandwa.

Biblia inasema Sulemani hakuwa mkamilifu tena kama baba yake Daudi alivyomwelekea Bwana.

Ukiota ndoto unazini na mtu mwingine ina maana kuna vitu vitaanza kuharibika kwako mfano vita kwako itakuja. Na hali yako ya Kiroho inapoa kwako.

Fuatilia watu walioana na wana dini tofauti kidogo waangalie wote wamepoa kiroho hii ni sababu Mungu anakuonya mapema kuwa hili si suala zuri maana gharama yake ni kubwa sana.

Na mmoja kati yao akipata moto wa kiroho ndoa inapata shida au mtu mmoja akubali kukaa chini ya imani ya mtu mwingine.

Tena mwanamke akimkaribia mnyama ye yote, na kulala pamoja naye, mtamwua huyo mwanamke, na mnyama pia; hakika watauawa; damu yao itakuwa ni juu yao.

LAW. 20:16

Kuna watu wanaota ndoto wanazini na wanyama ina maana shetani anapandikiza roho ya mauti kwako.

Kuna mtu alisema yuko uchi kwenye banda la ng’ombe na anazini na ng’ombe ina maana Mungu anamwambia kuwa kuwa shetani analeta roho ya mauti.

 

Hivi ndivyo tunavyotafsiri ndoto katika biblia. Lazima ndoto itafsiriwe na biblia ndio utapata maana na kitu cha kufanya.

Ni neema sana kujua hizi siri.

Naona miguu ya kuku ikijengwa juu ya meza. Miguu yako imepata shida kwa sababu ulishiriki kula chakula kilichotolewa sadaka kwa miungu.

Naona mtu alifungwa kitambaa kwenye kifua na alama  hii iliwekwa kwa njia ya ndoto. Nakiyeyusha kwa damu ya Yesu.

Naona jiwe na lina majina ya watu wote na nafuta hilo jina kwa  damu ya Yesu na kufuta hilo jina lako kila lilipoandikwa  kwenye hilo jiwe na nguvu za giza achia maisha ya mtu huyu kwa jina la Yesu . (Na ni jiwe lao la ibada)

Naona sadaka ya jicho la ng’ombe na kila anae toa sadaka nae   anapata shida. Nafuta hilo agano kwa damu ya Yesu.  Na hilo jicho la ng’ombe. Pepo achia kwa jina la Yesu na nafuta hilo agano kwa damu na Yesu na achia ufahamu wake wewe pepo uliopita hapo.

Baada ya hapo Mwl aliita watu kuokoka na kama hujaokoka hakikisha unaokoka mpokee Yesu awe Bwana na mwokozi wa maisha yako au uliokoka ukarudi nyuma njoo kwa Yesu maana Mungu anakuwazia mawazo mema juu yako na kila nguvu zinazokukwamisha zikuachie sasa kwa jina la Yesu.

Bonyeza  link pale juu ili kusoma kitabu cha Hongera kwa kuokoka na fanya sala ya toba.

Wimbo wa nasikia kuitwaaa..

Jina la Bwana libarikiwe sana. Tuonane tena kesho.

Kumbuka kumkaribisha mwingine semina hii kwa njia ya mtandao au kufika moja kwa moja uwanjani au kwa njia ya redio.

==Glory to God Glory to God==

 

SEMINA YA NENO LA MUNGU NA MWL MWAKASEGE.

UWANJA WA TANGAMANO TANGA 8 JUNE 2017

SOMO MBINU ZA KUOMBEA NDOTO ILI USIKWAME KIMAISHA.

Siku ya nne

 

Hili somo la Ndoto  kama unaona linakusaidia basi usisahau kumueleza mwingine. Haijalishi dini yake anahitaji kufuatilia hili somo la ndoto.

Somo hili la ndoto Mungu alinifundisha mimi mwenyewe kutokana na hali niliyokuwa napita nayo ile miaka ya 80. Maana kuna ndoto niliota wakati sijaokoka na sikuelewa maana yake na nilipookoka pia niliendelea kuota. Namshukuru sana Roho Mtakatifu kwa kunifundisha hili somo hatua kwa hatua.

Sasa nakushirikisha kile ambacho Mungu kanifundisha na kanipa kukueleza. Siwezi kukueleza kila kitu maana biblia inasema tunafahamu kwa sehemu.

Pia nakukumbusha lengo la somo kuwa ni Kuimarisha uhusiano wako na Mungu Katika Kristo Yesu. Si suala la kujifunza tu kuhusu ndoto bali jenga uhusiano wako na Mungu.

UMUHIMU WA KUIMARISHA IMANI YAKO JUU YA  DAMU YA YESU KATIKA KUSHUGULIKIA MAMBO YALIYOMO KWENYE NDOTO.

Niliwahi kwenda kwenye mji mmoja na kuna msichana nilikutana na akanieleza baba nina shida katika ndoto maana kuna mwanaume mmoja alinijia wa dini nyingine anataka  kunioa na ana mke wake lakini alitaka niwe mke wa pili.  Nilikataa moja kwa moja lakini cha kushangaza ni kuwa ananijia kwenye ndoto na kuzini na mimi. Nimeomba na kukemea lakini bado naona tu anazini na Mimi katika ndoto na nikijiangalia naona kuna alama katika mwili zinazonesha nimezini nae kabisa.  Nilimuuliza unapolala je unajifunika kwa damu ya Yesu akasema ndio.  Basi nikaomba nae pale na kuondoa pandikizi la adui na kukata ule muunganiko wa kipepo kwa Damu ya Yesu . Baada ya maombi nikamuacha akaenda zake.

Baada ya siku chache akaja kuniambia baba ile ndoto haipo tena. Lakini akaniuliza swali je mbona mimi niliomba kwa damu ya Yesu hiyo hiyo lakini bado ndoto ilinisumbua. Kwanini?

Na nilimwambia Tofauti ni imani katika damu ya Yesu  na si imani tu katika damu bali matumizi ya hiyo damu ya Yesu.  Wengi wana imani katika damu ya Yesu  ila hawana imani katika matumizi ya hiyo damu.

25 ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake,ili aonyeshe haki yake ,kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa MUNGU dhambi zote zilizotangulia kufanywa. Warumi 3 :25

Na kufuatana na Ebrania  1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Waebrania 11 :1

Sasa imani kwa mujibu wa mstari huu ni mawili katika moja.

1.Ni hakika ya mambo yatarajiwayo.

2.Ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

Kwa hiyo huwezi kuona kitu katika ulimwengu wa roho ambacho hakijatokea. Kwa hiyo ni lazima ndani yako kuwe na uwezo wa kusikia . Na wengine wanasema kwa kuwa wana imani na Yesu usiwe na imani na damu ya Yesu. Unaweza ukawa na imani na jina la Yesu ila usiwe na imani katika neno lake unaweza ukawa na imani  katika neno la Mungu fulani lakini sio lote unaamini na unaweza  ukawa na  imani ya damu ya Yesu lakini usiwe na imani katika  kuitumia damu ya Yesu.

Ngoja nikusomee ndoto za watu.

 1. Niliota kijana ameajiriwa kuniua na nilimkemea kwa jina la Yesu lakini alinizidi nguvu nikasema damu ya Yesu inenayo mema kwa ajili yangu inisaidie. Ghafla akaniachia na nikashtuka usingizini.

Wiki iliyofuata  niliota niko msituni  nimeshikwa na walizi, akaja mdada ili anichome na kisu nikakumbuka kilichotokea katika ndoto ya kwanza na nikaita damu ya Yesu ghafla yule dada akimbia na kile kisu kilidondoka. Na nikashtuka usiningizini. Tokea siku hiyo natafuta sana kujua uweza wa damu ya Yesu. Na ahsante kwa somo.

Sasa unaweza ukaona huo mtiririko hapo juu,  wa namna alivyotumia damu ya Yesu.

2.Mwl tatizo ni nini mbona natumia damu ya Yesu  katika ndoto lakini bado nazini kwenye ndoto na mambo mengi yanatokea sijui tatizo ni nini.?

Leo nataka uelewe juu ya mambo haya  juu ya imani yako katika damu ya Yesu.

7 Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo; 1 Wakorintho 5 :7

Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu. Luka 22 :20

Shika lile neno pasaka na neno agano Jipya na tunapoendelea hatua kwa hatua

28 Kwa imani akaifanya Pasaka, na kule kunyunyiza damu, ili yule mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao. Waebrania 11 :28

Wote tunajua walichinja kondoo lakini hapa tunaona  ya kuwa ametumia neno pasaka Na maandiko yanatuambia . _Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;_1 Wakorintho 5:7b

Kwa hiyo lazima tutafute neno Pasaka lilitokea wapi. Ili kujua Yesu kwanini anaitwa Pasaka Chanzo chake ni  ule usiku wakati wana wa Israel walipotolewa katika nchi ya misri. Angalia Kutoka 12 :1-33.

Sasa nataka tuangalie mistari michache hapa ili tuelewe.

11 Tena mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya Bwana. Kutoka 12 :11

Sasa hapa tunaona ya kuwa Mungu anataka kutufundisha kuwa kama alivyomtumia Pasaka wa kwanza ndivyo anavyomtumia na sasa pasaka wa pili

Pasaka ni jina la sadaka  kwanza kabla haijawa sikukuu. Yesu alikufa kipindi cha sikukuu ya Pasaka maana wengi  wanajua kuwa chanzo cha Pasaka ni siku Yesu alipokufa msalabani.  Na walikuwa wanahesabu siku kwa siku 7. Na ilikuwa na siku 14 na wayahudi wanasherehekea mpaka leo.

Mungu sasa anatufundisha kuwa damu ya Yesu itatumika kama alivyotumia damu ya mwana kondoo ndivyo atatumia damu ya Yesu kwa viwango vya juu zaidi sasa.

Hamna kitu kibaya kupigana vita kwenye ndoto na ukashindwa maana hiyo ni vita halisi. Na unapolala unaomba damu ya Yesu ikufunike lakini bado unazidi kwenye ndoto. Inasumbua sana.

Mwingine aliniambia kuwa aliota ndoto  kaumwa na nyoka kwenye kidole chake cha mguuni. Na alimkea yule nyoka kwa Jina la Yesu lakini bado alimuuma.

Sasa ukishindwa vita kwenye ndoto ujue hata katika ulimwengu huu wa kawaida huwezi vuka hapo.

Mwingine aliniambia kuwa aliota ndoto yuko msituni na alikutana na bibi kizee na akampa karatasi iliyoandikwa vitu. Na aliposhtuka kutoka usingizini aliona mkononi mwake anayo ile karatasi lakini kapewa kwenye ndoto.

Kuna wengine wanasema kila ninachoota mimi kinatokea jana nilikuambia sio lazima kitokee na unahitaji kujua namna ya kutumia damu ya Yesu katika ili kubadilisha mambo hayo uliyoyaona.

Na usiku ukilala unalala mwili tu na ndio maana nafsi yako na roho yako haitakiwi kulala. Wanafunzi walipo uliza saa ngapi shetani kapanda magugu Yesu aliwaambia  “lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.Mathayo 13:25”

Hapa sio usingizi wa kawaida ni jambo la Rohoni ina maana katika maisha yako kama una miaka 60 unakuwa umelala miaka 20. Sasa kama Mungu kasema na wewe miaka 20  lakini hujasikia itakuwa tabu sana kwako maana  wastani wa kulala ni masaa 8 kwa siku. Sasa kama nafsi yako iko macho mchawi akija kwako utamuona. Maana akija kama ng’ombe utaona na akija kama nyoka utaona akija nyumbani kwako na utajua cha kufanya.

Na ndio maana unaona Yule ndugu aliyekamatwa porini katika ile ndoto niliyokuwambia  alipokemea kwa jina la Yesu aliona hii silaha haifanyi kazi na akabadilishia hapo hapo akatumia damu na na Akasema Damu ya Yesu inene mema juu yangu  “na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.Waebrania 12:24”

Na hata alipoota ndoto nyingine alitumia damu ya Yesu na aliona ushindi. Na sababu ni kuwa huyu ndugu roho yake imetengenezewa msuli na ndio maana ameshinda.

TUANGALIE MAMBO KADHAA KATIKA PASAKA

Sasa linganisha na Pasaka ya  Kutoka 12 na Kristo Yesu.

1.Walielekezwa kuitumia damu bila kusema neno.

Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu,g katika zile nyumba watakazomla. Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri. Nanyi twaeni tawi la hisopu, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu ye yote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi. Kwa kuwa BWANA atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, BWANA atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi.

KUT. 12:7, 13-13, 22-23f

Na tunaona hapo Mungu akisema kuwa atakapoiona damu na hasemi atakaposikia maneno.

Na aliwapa maelezo namna ya kuitumia ile damu kwa kupaka kwenye miimo ya malango

11 Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi. 14 Kwa maana kuliko huo uhai wa mnyama, hiyo damu yake ni moja na uhai wake; kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Msile damu ya mnyama wa aina yo yote; kwa kuwa uhai wa wanyama wote ni katika hiyo damu yake; atakayeila awaye yote atakatiliwa mbali. Mambo ya Walawi 17 :14

Mungu alikuwa anataka tuone namna  damu inafanya upatanisho na kusema badala ya mtu, kwa hiyo lazima waweke imani kwenye hiyo damu. Na alitaka wajue kuwa hiyo ni damu ya agano.

Wana wa Israel walipolia Mungu hakuwatoa kwa sababu walilia bali biblia inatuambia kuwa aliwatoa kwa sababu  alilikumbuka agano alilofanya na Ibrahimu. Kwa hiyo na wewe jifunze kuachilia na kuamini damu isimame badala yako.

24 na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili. Waebrania 12 :24

Damu ina uwezo wa kuongea kwa hiyo ipe damu nafasi ya kuongea. Kama biblia inasema paka basi uwe na uhakika damu itafanya kazi.

Mungu hakutaka waunganishe na maneno kwa sababu wengi walizaliwa Misri.  Walikuwa wanafundishwa namna ya kuweka imani kwenye damu.

Unafikiri kwanini waganga wanatumia damu na wanamwaga. Na saa ingine hawasemi wanaimba nyimbo au namna yoyote ile. Sasa kama wanamwaga ina maana yale majini yanasema hatuwezi kumsikiliza huyu mtu ila hiyo damu iongee badala yake.

Ukiota ndoto unaona kuku maana ndio alikuwa msemaji wako kwenye ile kambi. Sasa kama unaweza amini damu ya kuku amini damu ya Yesu.  Maana ndio damu bora zaidi.

Wangapi hapa wana smartphones, kwanini baada ya muda unaupdate programs au applications? Kama hufanyi hivyo ujue kuwa baadh ya vitu havitafanya kazi vizuri.  Sasa kwanini utumie damu ya kuku wakati kuna update s mpya ya damu ya Yesu.  Geuza sasa imani yako hamia kwenye damu ya Yesu achana na hizo damu za wanyama.

 1. Damu ya Yesu ina nguvu katika ufalme wa Mungu na katika ufalme wa shetani.

23 Kwa kuwa Bwana atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, Bwana atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi. Kutoka 12 :23

Hawa watu walikuwa na pigo la Mungu kwao na hasira ya shetani. Hawa watu walimuuza Yusufu aliyekuwa amebeba baraka zao  na alikaa utumwani na Mungu aliwasaidia waende Misri wamfuate aliyebeba baraka zao. Na hawakutakiwa kukaa misri maana Mungu anaita Misri nyumba ya utumwa

Kwa hiyo kazi ya damu ilikuwa ni kuomba toba  kwao kwa kuomba toba kwa ajili  uovu wa wazazi wao waliomuuliza Yusufu.

Ndio maana damu ilimwagika ya kondoo ilikufanya upatanisho.na Damu ya Yesu imeachiliwa kwa lengo la kuomba toba na ukiita damu ya Yesu imebeba roho ya Kristo.

Damu ya Pasaka ilipewa nguvu za

i.Kuzuia pigo kutoka kwa Mungu  (Damu ilinena mema)

ii) Kuzuia hasira ya shetani.(mharibu) baada ya miungu kuhukumiwa

Hii ilikiwa damu ya kondoo na ilikuwa na nguvu sana kiasi hicho je damu ya Yesu ni bora sana.

Sasa haijalishi ndoto inakuja toka wapi damu ya Yesu inajua namna ya kuongea na kupambana kwa niaba yako.

Glory to God Glory to God.

3.Mungu haitumii damu ya Yesu ambayo haijatumika.

Angalika Kutoka 12:7, 13, 22 ☝

Damu iliyokuwa ndani ya mwana kondoo na ilikusanywa kwenye bakuli haikuwa na faida kwao. Na aliwaambia wapake kwenye milango yao ndipo ingewasaidia bila hivyo damu ilikuwa haina kazi.

1.Atakapoiona hiyo damu atamzuia mharibu.

2.Atahukumu miungu ya Misri.

Na kwa maana hiyo alikuwa anawaambia kuwa kama hamtumii hiyo damu basi ujue hayo mambo ya kuzuia pigo na kuhukumu miungu hamtayaona kwenu.

Kuna mashahidi watatu mbinguni.

A.Baba

B.Neno

C.Roho Mtakatifu

Kuna mashahidi 3 duniani

1.Roho

2.Damu

3.Maji.

Wanaosema kuwa wewe ni Mkristo na  hao ndio mashahidi. Na Maana yake Damu kama huitumii  haikusaidii maana ili uone nguvu ya Mungu lazima tumia damu kwa maelekezo yake.

Akisema tumia damu inayomwagika kwa ajili ya dhambi tumia hivyo hivyo (mwaga) tumia damu kama biblia inavyosema.

Damu ya Yesu ambayo huitumii na Mungu nae haitumii. Imani bila matendo imekufa. Lazima tafuta mstari unaosema kwenye hiyo damu. Tumia hivyo hivyo damu ya Yesu inaondoa dhambi.

Damu inasafisha hadi dhamiri yako.

Damu inafuta hata jana nilitumia damu kufuta lile jina  lilioandikwa kwenye jiwe.

Tumia hivyo damu ya Yesu. Lakini lazima uingize damu kazini. Nenda kwenye biblia jifunze kutumia damu ya Yesu katika maisha.

Jina la Yesu ni jina la agano na alijifunua hatua kwa hatua. Kwa hiyo lazima damu itumike na ndipo upate nguvu ya kutumia Jina la Yesu.

Na ndio maana utanisikia nasema namwaga damu ya Yesu na utaona hata moto ukiwaka na mapepo yanalipuka. Na siri kubwa ni kuwa natumia damu kama biblia ilivyosema na naamini hivyo.

Na unaposhiriki meza ya Bwana unapokula chakula cha Bwana maana kuna kunywaa damu ya Yesu ina maana unakula uhai wa Yesu. Hakikisha unakunywa damu na kupata faida

4.Damu ina uwezo wa kulidhibiti lango la muda linalotumika kiroho linakwamisha maisha yako.

Kuna mmoja aliniandikia hii ndoto  “Niliota nimeona mtu  kavunjika mguu na mfupa unaonekana hadi nje na kila mara usiku maono ya yale ndoto yakawa yananijia.

Mwezi huu niliugua sana na nikilala usiku saa saba nashtuka mwili unapata moto  hapo nakuwa macho hadi asubuhi. Na nilipoanza kukemea hiyo Ndoto ndipo nilipata ahueni. Maana hospitali sikupata nafuu kabisa.

Huyu mtu aliota ndoto lakini mwezi mmoja baadae alipata shida . Na ndoto ile ya kwanza ilimjia saa saba ndio maana  kila ukifika saa hizo ile hali inarudi.

Sasa kuna ndoto huwa zinakuja usiku saa saba au zingine alfajiri na cheki kama huwa unaota sana ndoto mida hiyo kila muda zitakuwa zinakuja masaa hayo hayo. Na wengi sana huwa wanakwepa kulala akijua kabisa muda huu ndio huwa anaota zile ndoto.

Hilo ni lango na inabidi ushughulike kwa damu ya Yesu.  Sasa kwa kuwa ndoto ni lango nayo hufungua lango lingine la muda ambao katika huo muda ndoto zitakuwa zinakujia. Na utasema nimeipata wapi ipo kwenye Kutoka 12:2 Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu.

Ina maana damu ya Yesu inafungua lango la muda ndio maana hapo biblia inasema kuwa mwanzo wa mwaka kwenu.

Mungu alipita usiku na wakijua kabisa ile damu ilishikilia ule muda na aliwaambia usiku wa manane na ina maana ile damu ililinda muda. Na damu inaweza fanya kitu cha Mungu na Mungu atapita muda huo kuhukumu miungu na kuzuia kisasi cha shetani.(Kutoka 12:2, 29)

Kwa hiyo unaweza tumia damu ya Yesu kuzuia ndoto ambazo zinaweza kukuharibu  na nilitumia damu ya Yesu kuzuia ile ndoto ambayo yule dada aliyekuwa anazini usiku maana nilijua naweza block hiyo ndoto kwa damu ya Yesu kwa kuzuia muda anaoota.

Biblia inasema Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu, katika zile nyumba watakazomla.

KUTOKA. 12:7

Sasa kama walichukua damu na kuitia katika  miimo ya malango na katika agano jipya maandiko yanasema  “Kwa imani akaifanya Pasaka, na kule kunyunyiza damu, ili yule mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao.Waebrania 11:28”

Sasa kama unaweza kunyunyiza damu kama maandiko yalivyosema  inakuwa inafanya kazi ya kuzia kama ilivyofanya kazi.

Glory to God Glory to God.

5.Wanaoitumia damu wasivunje mashart waliyopewa kwenye kuitumia hiyo damu

Nanyi twaeni tawi la hisopu, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu ye yote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi. KUTOKA. 12:22

Si suala tu la imani  bali ni pamoja na masharti. Ndio maana ukivunja mashart hupewi adhabu ila ukivunja sheria ndio utapata adhabu ila ukikosea masharti utapata hasara ya kile ulichotakiwa kupata.  Ndio maana biblia inasema walitakiwa wakae ndani na waweke damu.

Sasa wasingefuata yale masharti inakuwa hasara kwao ndio maana  hata wewe unatakiwa kufuata kama neno la Bwana lilivyoeleza. Ndio maana hata Rahabu aliambiwa nae afunge kamba kama ishara ya agano.

Mungu akija kwako ataangalia damu na iliyoweka kwenye nyumba yako au ofisi yako na ukiweka hiyo damu ya Yesu Ujue haitanyamaza.

Hata wachawi wakiona damu ya Yesu ujue hawataingiaa kwako. Hakikisha unaenda kwenye  biblia yako ili kujenga imani yako

Kazi ya damu ya Pasaka kama walivyoelekezwa

 1. Damu ilishughulika na wazaliwa wa kwanza ili wasiangamizwe

Maana ile damu ilikuwa ni ishara kuwa akiona damu atamlinda mzaliwa wa kwanza maana wao ni lango la kupitisha vitu

Kuna wazaliwa wa kwanza kicheo na haki. Na wao ndio wanatakiwa wawe na baraka double kwa ajili ya wengine  hakikisha wazaliwa wa kwanza wanalindwa na damu watapona na wengine kwa sababu wao wako salama.

 1. Pia unaweza paka damu ya Yesu hata nje, nilikuwa mkoa mmoja na semina niliachilia damu kwenye hema nikaona watu watakimbia na kutoka nje, nikasema na hata huko nje moto nako uliwaka watu walikimbia hata kule nje.

Weka kwenye matendo imani yako juu ya damu ya Yesu chukua mstari mmoja mmoja weka kwenye matendo.

??Baada ya hapo wimbo wa damu ya Yesu??

Shukran kwa Mungu kwa kuweka mambo haya. Jina la Bwana libarikiwe sana sana.

==Glory to God Glory to God ==

 

SEMINA YA NENO LA MUNGU NA MWL MWAKASEGE.

UWANJA WA TANGAMANO TANGA 9 JUNE 2017

SOMO MBINU ZA KUOMBEA NDOTO ILI USIKWAME KIMAISHA.

*SIKU YA TANO*

 

Bwana Yesu asifiwe leo ni siku ya Tano na mpaka sasa tumejifunza mbinu moja tu.

1.Kutumia damu ya Yesu katika kuombea ndoto.

Angalia somo la ndoto yapo kama kumi hivi yaliyobaki ntaweka baada ya muda si mrefu. Sasa nipo naandaa kitabu na usiseme hadi nisubiri kitabu wakati kuna  sehemu unaweza pata kwa sehemu. Na kitabu kikiwa tayari ntawatangazia na utakipata ila sasa endelea kufuatilia hili somo. Nenda kwenye banda letu la Kanda pale nunua CD au DVD na sikiliza na kusikiliza. Maana haya masomo yana siri nyingi sana unahitaji kujua.

Mimi Mungu alianza kunifundisha habari za ndoto tokea mwaka 1984 lakini mpaka leo nazidi kufuatilia na kujifunza na bado sijajua vyote. Hivyo endelea kujifunza na kufuatilia kwa ukaribu.

Jana tuliangalia namna ya kuimarisha imani yako katika damu ya Yesu.

Tumepitia vipengele 6 Jana na leo tutaangalia kipengele cha 7 ili tufanye zoez la tulichojifunza.

Nilianza kwa kukuambia ile ndoto ya dada aliyefuatwa na yule baba na alitaka kumuoa na alipomkataa yule baba akawa anamjia katika ndoto na kuzini nae. Na alikuwa anaomba kwa kujifunika kwa damu ya Yesu lakini bado alikuwa anazini kwenye ndoto. Na aliponishirikisha na kumuombea kwa kutumia damu ya Yesu  ile ndoto aliyokuwa anaota ilikatika mara moja na akawa haoti tena.

Sasa aliniuliza tofauti ya kuomba kwake na kuomba kwangu kwa kutumia damu ya Yesu ilikuwa  kwenye nini.

Na jana tuliona kuwa wengine katika ndoto nilizokuambia walitumia damu ya Yesu  walivuka, na wengine walitumia Jina la Yesu badala ya damu ya Yesu na walikwama.

Sasa leo nataka ujue tofauti yake ni nini.

7 Damu ya Yesu inashughulikia kwa mafanikio zaidi mambo yaliyo kwenye ndoto kwa kutumia mwongozo wa neno la Mungu.

Kuna watu wameota juu ya nyoka katika ndoto zao. Na tuone biblia inasemaje na damu ya Yesu inatumikaje kufanya kazi katika kuombea hizi ndoto kwa kufuata neno la Mungu.

Sasa 17 Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. Warumi 10 :17 na 1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

Waebrania 11 :1

Maana yake unasoma mstari na unaangalia ni mambo gani yanayotarajiwa katika ule mstari na ndani ya moyo wako unaingia uhakika na biblia inasema kwa imani twafahamu na ukipata imani ujue na ufahamu utakuja na utaona vitu katika ulimwengu wa roho  vile unataka kuona. Na ujue ukiona hivyo Ameeen  ndio vitakupa uvumilivu wa kusubiri.

Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.UFUNUO. 12:7-11

Hawakumshinda tu kwa damu bali kwa damu na neno maana neno linakupa uhakika. Jana tuliona kuwa kama damu huitumii na Mungu nae hataitumia kukusaidia. Na kumbuka hili jambo, hakikisha damu inatumika.

Kwa wana wa Israel wasingefuata maelezo ya neno la Mungu kama walivyoelekezwa katika kutumia damu katika miimo ya  malango na kizingiti cha juu maana Mungu angeangalia na asione damu basi uwe na uhakika wazaliwa wao wa kwanza nao wangekufa.

Si suala la kutumia tu damu tumia kwa imani ili iachilie nguvu za Mungu katika kukusaidia. Nenda kwenye maandiko  vizuri.

Yohana 1:1-3, 14 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.YOHANA. 1:1-3, 14

Kwa hiyo Mungu alifanyika neno na neno likawa mwili na tukamfahamu  kwa jina lake kama Yesu. Na Yesu alikuwa ni neno linalotembea.

Sasa  Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwa-mwitu huwakamata na kuwatawanya. Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake. Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi; kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo.YOHANA. 10:10-15

Sasa unaona Yesu anasema anautoa uhai na jana tuliangalia kuwa damu imewekwa kwenye madhabahu ili ifanye upatanisho  kwa niaba yetu kwa sababu uhai uko ndani ya damu.

Na Yesu alipokuwa anatoa uhai wake alimaanisha kuitoa damu kwa kipindi chake Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.LUKA. 22:20

Na aliposema hivyo alimaanisha kuwa hiyo damu inatolewa kwa kipindi hiki  cha agano jipya.

Angalia pia mstari huu  _Palikuwa na Wayunani kadha wa kadha miongoni mwa watu waliokwea kwenda kuabudu kwenye sikukuu. Basi hao walimwendea Filipo, mtu wa Bethsaida ya Galilaya, wakamwomba, wakisema, Bwana, sisi tunataka kumwona Yesu. Filipo akaenda, akamwambia Andrea; kisha Andrea na Filipo wakamwambia Yesu. Naye Yesu akawajibu, akasema, Saa imefika atukuzwe Mwana wa Adamu. Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.YOHANA. 12:20-24

Yesu alipowaambia “Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi” alikuwa anamaanisha kuwa nikisha kufa na kufufuka mtanijua Mimi ni nani.

Nakufundisha hivi ili ujue kutumia jina la Yesu kimamlaka kwa nafasi yake.

Yesu alipewa jina la Yesu mara tatu na kwa sababu tatu kwa njia tatu

1.alipewa wakati anazaliwa  ili awe mwokozi wa ulimwengu.

_Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.MATHAYO. 1:21

2.Alipewa alipokufa msalabani.

tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.WAFILIPI. 2:8-11

Alipewa alipotii kupita msalabani.

 1. Alirithi jina alipofufuka

3 Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu; 4 amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao. Waebrania 1 :4

Alifanyika mrithi alipofufuka.

Sasa.

1.Jina la kwanza (Kwa jina la kwanza linatupa kuokolewa kwa jina la Yesu watu wanaokolewa).

2.La msalabani ( Linakupa mamlaka  kila goti litapigwa)

3.La tatu ( linakupa kutembea katika urithi)

Kwa hiyo nakupa sababu hizi ili uweze kuelewa kuwa jina la Yesu ni jina la kiagano. Mahali damu ya Yesu  haijafanya kazi haliwezi kukusaidia.

Mfano:.

1.Umeota umeumwa na Nyoka maana yake nini?

8 Mwenye kuchimba shimo atatumbukia ndani yake; Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma. Mhubiri 10 :8

Wakasafiri kutoka mlima wa Hori kwa njia ya Bahari ya Shamu; ili kuizunguka nchi ya Edomu, watu wakafa moyo kwa sababu ya ile njia. Watu wakamnung’unikia Mungu, na Musa, Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu. BWANA akatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa. Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung’unikia Mungu, na wewe; utuombee kwa BWANA, atuondolee nyoka hawa. Basi Musa akawaombea watu. Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi. Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi. HESABU. 21:4-9.

Maana yake ukifanya kitu kinachoondoa ulinzi wa Mungu ndani yake nyoka atakuuma.

Nyoka akikuuma kuna vitu viwili ndani yake.

1.Ni adhabu toka kwa Mungu

2.Shetani  kaona mahali kuna mlango na kaja kukuuma.

Sasa ukiona unaumwa na nyoka usikimbilie tu kuomba bali nenda kwenye

Ezekiel  22:30-31 Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu. Kwa sababu hiyo nimemwaga ghadhabu yangu juu yao; nimewateketeza kwa moto wa hasira yangu; nami nimeileta njia yao wenyewe juu ya vichwa vyao, asema Bwana MUNGU.

Biblia inasema boma likivunjika kunakuwa na mpenyo, kwa hiyo si suala la kukemea pepo au kukemea nyoka ni suala la kuomba toba kwanza ya kujenga boma

Kuna mtu aliota kaenda kwao na nyoka alisimama kwenye uwanja wa nyumbani kwao na alimng’ata kidole chake cha mguu. Na alikuwa ameokoka na alikemea lakini aling’atwa kidole na alipoamka aliona kidole kinatoa damu.

Hivi ni vitu halisi unahitaji kujua kuwa kama damu ya Yesu haijatumika ujue hata ukikemea jina Yesu halitakusaidia.  Na damu ilitakiwa imsaidie kushughulika na dhambi zake na uovu wa wazazi wake maana yalikuwepo maagano.

Kwa hiyo alipokemea nyoka ilimuuma na sio kuwa jina Yesu halina nguvu hapana ni kwa sababu damu ingemsaidia katika toba kushugulika na lile agano ndipo angetumia jina la Yesu sasa lingemsaidia.

Hata wana wa Israel Mungu alipowaambia kuwa watumie damu ya mwana kondoo ilikuwa ni kwa ajili ya toba ya uovu wa wazazi wao ambao ndio kilikuwa chanzo kikuu cha wao kwenda Misri na kuingia utumwani.

Ukiumwa na Nyoka sumu na laana vinaingia ndani yako.

BWANA akatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa.

HESABU. 21:6

Sumu ya nyoka iliwaua kimwili na walikufa kabisa

_Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.

MWA. 3:4-5.

Mungu alisema nyoka atakupiga kisigino na alimaanisha hatua zao zitakwama. Na shetani akikuuma kisigino kuna kitu anawinda.

Pia akikuuma mkono anawinda uchumi wako. Ee Bwana, ubariki mali zake, Utakabali kazi ya mikono yake; Uwapige viuno vyao waondokao juu yake, Na wenye kumchukia, wasiinuke tena.Kumbukumbu la Torati 33:11

BWANA ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako.KUM. 28:8

Shetani anakuwa anawinda Baraka zako.

Akikuuma tumboni chini ya kitovu chako anawinda ndoa yako, na uzazi wako na siku zako za mwezi zinaharibika na anaharibu kupata kwako mimba.

Mwingine aliota kaumwa na nyoka kwenye kidole cha Pete ya ndoa na hamna mtu aliyemsaidia kujua hapo maana nae hakujua cha kufanya  na ndoa yake iliharibika. Maana nyoka aliweka sumu ya kuua ndoa yake.

Jana nilikuambia   kuwa unaweza kuelekeza damu  kwenye eneo. Na unaweza ukaelekeza eneo alilokuuma.

Tafuta kwenye maandiko damu ya Yesu inatumikaje. Mfano damu inafuta dhambi uwe na uhakika hata sumu inafuta na kuondoa basi na wewe fanya hivyo ondoa hiyo sumu kwa damu ya Yesu.

Kuna mtu aliniambia kaota ndoto imeingia kwenye duka lake na biashara yake iliharibika.

Na mwingine aliota nyoka kaingia ndani kwake, ndoa yake iliharibika. Na mwingine aliota nyoka kaingia mguuni kwake na kapotelea huko huko.

Nyoka kuingia mahali maana yake nini

Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.

MWA. 3:24

Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.

2 KOR. 11:3

Nilikuwambia lengo la somo hili kuimarisha uhusiano wako na Mungu.  Kuwa Nyoka aliingia katika bustani lengo lake ni kuharibu fikra zao.

Ile bustani ilikuwa na mipaka na Mungu aliwafukuza watoke katika bustani ya Eden. Shetani alikuwa anataka kuharibu mazingira ya kiroho na kufikiri kwao na hali ya uchumi iliharibika.

Kila mtu ana Eden ya kwake yaani mazingira ya kiroho ambayo Mungu kamkusudia mtu huyo akae ili afikiri Ki-Mungu.  Kama kufanikiwa afanikiwe Ki-Mungu sasa shetani akija anaharibu hayo mazingira ya kiroho na utajua kuwa fikra zako zinaharibika na usipokuwa mwangalifu unaona kabisa unafukuzwa nje ya hayo mazingira.

Sasa kama umeota ndoto Nyoka  kalala kitandani kwako ujue anakuja kuvuruga fikra zenu. Wewe na mke wako kama hakuumi  kalala tu angalia vizuri hapo.

Saa nyingine unaona katika ndoto nyoka kakaa kanisani anataka kuvuruga hali ya kiroho ya hilo eneo kanisa. Mfano yuko madhabahuni anawinda kufikiri kwa mchungaji kama ni kwa wakristo ujue anataka kuvuruga fikra za wakristo.

Kama hujajua namna maandiko yanavyosema na kuelewa vizuri hizi ishara utafanya kwa kubahatisha na utakosea kulenga matumizi ya damu ya Yesu kwako.

Ukiona nyoka anakuja jikoni ujue ugomvi unakuja na msichana wa kazi.  Kama unafanya kazi na kwa mtu ujue kuwa ugomvi na mwenye nyumba.

Kuna mwingine aliota ndoto nyoka kaingia mguuni kwake na kapotelea huko hakujua cha kufanya na alinisikia nikifundisha kwa njia ya mtandao na tulipoanza maombi nae alishika mguu wake huko huko alikokuwa na mguu wake ukaanza kutetemeka . Na alipata shida kwa sababu hakujua cha kufanya mapema wakati nyoka kaingia.

Kama huyo nyoka aliingia huko ndani na kabana huko alibana na kufikiri kwake  na neno linasema vita yetu ni ya kiroho  na shetani akitaka kukuwamisha anakwamisha fikra zako maana biblia inasema aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo.

Sasa shetani yeye anachowinda ni kubana fikra zako ili ukose mawazo mazuri ya kwenda mbele. Ndio maana tunaona Adam na Hawa shetani alisababisha Mungu awafukuze na uchumi wao uliharibika.(Mungu aliwaambia mtakula kwa jasho)

Ukiota ndoto nyoka anakukimbiza ina maana shetani anataka kukukosesha utulivu wako wa kufuatilia ndoto (vision) ambayo Mungu kakupa

Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume. Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.UFUNUO. 12:13-14

Unapoota nyoka kasimama mbele yako unaona hila za shetani kuua ndoto zako.

Ukiona nyoka mkubwa ina maana vita yako ni kubwa Pia ya ndoto zako ni kubwa sana.

Musa vita yake ya kwanza ilikuwa ni nyoka kutoka kwa  wachawi ili kuua ndoto yake.

na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.EBR. 12:24.

Lazima ujifunze kuachilia damu iseme.

Ukiota nyoka anatoka mdomoni mwa mtu. Na anatoa vitu kwenye mdomo wake maana yake nini

Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule.

UFU. 12:15

Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.

UFU. 12:16

Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

UFU. 12:9

Ukiona nyoka anatoa vitu na anataka kukushambulia wewe au anatoka mahali.

Mungu anakuonesha kuwa maneno yenye sumu, hila ,mashtaka , laana.

Ee BWANA, uniokoe na mtu mbaya, Unihifadhi na mtu wa jeuri.  Waliowaza mabaya mioyoni mwao, Kila siku huondokesha vita.   Wamenoa ndimi zao kama nyoka, Sumu ya fira i chini ya midomo yao.  Ee BWANA, unilinde na mikono ya mtu asiye haki; Unihifadhi na mtu wa jeuri; Waliowaza kuzipotosha hatua zangu.ZAB. 140:1-4

Kwenye mdomo wa nyoka inatoka na sumu na kuleta udanganyifu na akatishe namna ya kukwamisha mana nyingine anashtaki na kukuletea mashtaka kwa kila kitu kwa hiyo lazima umshinde kwa damu  Yesu na neno

Pia tunaona ardhi ilimsaidia Mwanamke na ikafungua kinywa chake na kumeza mto na inameza kila kitu na inapotea.

Ardhi ina nguvu sana katika kukusaidia na kuna kitu cha kukusaidia.

Ukiota ndoto kakuviringa kwenye  mguu au mkono au chochote maana yake nini

Paulo alipokuwa amekusanya mzigo wa kuni, na kuuweka motoni, nyoka akatoka kwa ajili ya ule moto akamzonga-zonga mkononi. Wenyeji walipomwona yule nyoka akilewa-lewa mkononi, wakaambiana, Hakosi mtu huyu ni mwuaji; ambaye ijapokuwa ameokoka katika bahari haki haimwachi kuishi. Lakini yeye akamtukusia motoni asipate madhara. Wao wakadhani ya kuwa atavimba au kuanguka chini kwa kufa ghafula; na wakiisha kumwangalia sana, na kuona kwamba halimpati dhara lo lote, wakageuka, wakasema kwamba yeye ni mungu. MDO 28:3-6

1.Shetani alitaka kuziba kuamini kwao na shetani anataka kupoteza imani na wewe.

2.Waache kufanya kitu unachotaka kufanya. Paulo alipekwa pale kwa ajili ya injili.  Maana wito wake ulikuwa ni kwa ajili watu wa mataifa.

Na Paulo hadi alimposhinda yule shetani ndipo aliposikilizwa.

3.Kuua kuwepo kwako na anaua thamani yako inapotea.

Ukimkuta nyoka kalala kwenye kitu au mti mkubwa au fimbo

Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.

UFU. 13:2

Maana yake unashindana na uongozi unaotumia nguvu za giza. Na unapoona kuna mapambano nyumbani angalia kitu Mungu anakuonesha. Inategemea Mungu anakuonesha kwa picha ipi.

Kwa hiyo mshinde kwa damu ya Yesu ikusaidie kuongea mbele ya nyoka.

Ukiota umempiga nyoka na umemuua maana yake umeshinda

nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.MWA. 3:15

Kama hajafa basi ujue umemjeruhi na jeraha lake litapona.

Yesu alisema iweni na busara kama nyoka ” Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.Mathayo 10:16″

Ukiota ndoto unaona nyoka anagombana na kondoo maana yake Mungu anakuambia kuwa hiyo vita inahitaji busara.

Ni neema sana.. na twende kumshukuru Mungu kwa kutufundisha juu ya damu ya Yesu.  Maana hatuwezi lipa thamani ya damu ya Yesu.  Ila sadaka yako inaachilia imani yako kwa Mungu.

Ungana nasi kutoa sadaka hii kushukuru Mungu kwa neema hii angalia link pale juu  chukua namba za simu.

Jina la Bwana libarikiwe sana sana. Tuonane tena kesho

==Glory to God Glory to God==

 

SEMINA YA NENO LA MUNGU NA MWL C. MWAKASEGE.

UWANJA WA TANGAMANO TANGA 10 JUNE 2017

SOMO MBINU ZA KUOMBEA NDOTO ILI USIKWAME KIMAISHA.

SIKU YA SITA

 

Bwana Yesu asifiwe, leo ni siku yetu ya sita hapa Tanga mjini. Na katika maeneo mengine huwa naruhusu watu kuandika ndoto na kukusanya na kuziombea na ningeweza tumia muda mwingi kuombea ila kazi yangu kubwa sana ni kufundisha ndio maana hapa nataka ujifunze  ili hata siku nyingine na wewe ujue  cha kufanya.

Kukuombea tu haitoshi kama sitakufundisha namna ya kufanya wewe mwenyewe ili kuombea ndoto zako unazokuwa unaota.

Jifunze kutega sikio kwa haya ambayo Mungu anakufundisha maana kuna siku moja yatakusaidia.

Mpaka  sasa tumejifunza mbinu moja.

1.Kutumia damu ya Yesu. Na tafuta CD na sikiliza na kusikiliza juu yat masomo yaliyopita yatakusaidia.

*MBINU YA PILI:

OMBEA NDOTO KWA KUTUMIA MWONGOZO WA KIASHIRIA KILICHOAMBATANA NA NDOTO HUSIKA*

Ikawa, mwisho wa miaka miwili mizima, Farao akaota ndoto; na tazama, amesimama kando ya mto. Na tazama, ng’ombe saba wazuri, wanono, walipanda kutoka mtoni, wakajilisha manyasini. Na tazama, ng’ombe saba wengine wakapanda nyuma yao kutoka mtoni, wabaya, wamekonda, wakasimama karibu na wale ng’ombe wenginet ukingoni mwa mto. Kisha hao ng’ombe wabaya waliokonda wakawala wale ng’ombe saba wazuri, wanono. Basit Farao akaamka. Akalala, akaota ndoto mara ya pili. Tazama, masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa, mema. Na tazama, masuke saba membamba, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao. Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka, kumbe! Ni ndoto tu.   Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo.MWANZO. 41:1-8

Farao aliota ndoto hii na ilikuja mara mbili kwa namna tofauti ila ilikuwa ni moja. Sasa katika kuota ndoto  huwa inatokea sana mtu unaota ndoto na ukishtuka unaona  ni afadhali kwani  ilikuwa ni ndoto tu maana ingekuwa halisi unaona ingekupa wakati mgumu sana.

Sasa ukiona namna hiyo jua kuwa hiyo sio ndoto tu ni halisi katika ulimwengu wa Roho. Na tunaona katika mstari wa nane kiashiria hicho.

8 Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo.

Mwanzo 41 :8

Weka Pause kidogo hapo Twende kwenye Ayubu

14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; Ayubu 33 :14-15

Mungu anatumia ndoto kama njia mojawapo ya kuzungumza na mtu. Pata nafasi nenda kwenye Biblia na kuna ndoto zisizo pungua 20 na nimesoma karibu zote na mambo mbali mbali.

Mungu anazungumza na mtu kwa njia ya ndoto kumuonyesha mambo yaliyoko kwenye ulimwengu wa roho  ambayo yanakuja au anaweza zungumza na watu kwa njia ya ndoto kusema mambo yaliyotokea yanayowahusu.

Ndoto inakuonesha

?Wakati ujao

?Wakati uliopo

?Wakati uliopita.

Ndio maana ni muhimu sana kujua mambo haya.

Sasa tuangalie mambo muhimu leo katika ishara au viashiria katika  ndoto.

1.Neno kiashiria maana yake ni ishara inayofuatana na ndoto inayokuhimiza na kukuarifu kuwa usiipuzie hiyo ndoto.

Neno kiashiria  linatokana na neno ishara (kwa lugha ya kiswahili tunaweza ita kiashiria ni kivumishi adjective)

MFANO:

_8 Basi itakuwa, wasipokusadiki, wala kuisikiliza sauti ya ishara ya kwanza, wataisikiliza sauti ya ishara ya pili.

Kutoka 4 :8_

Ishara ina sauti, sasa inapoambatana na Sauti ina maanisha nini?

17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; Marko 16 :17

Ishara inakuonesha mahali pa kutazama, mfano ukiona mgonjwa anapona kwa maombi mtazame Yesu, ukiona muujiza mtazame Yesu ndio inavyotakiwa kwa mujibu wa Marko 16:17. Si suala la kumtazama anaeomba bali mtazame Yesu.

Na ndio maana Mungu aliwaambia wana wa Israel kuwa Damu hii mnayopaka itakuwa ni ishara kwenu maana yake ni kama kibao kinachokuongoza kwenda mahali fulani. Mfano  angalia huko barabarani  utaona kinakuonesha Segera km 299. Ina maana hauko Segera ila kinataka ujue kuwa baada ya km hizo utakuwa segera sasa huwezi ita hapo kwenye kibao ni segera.

Sasa kuna watu wanapoona muujiza wanashusha na mizigo yao badala ya kuwa wamtazame Yesu wao wanautazama muujiza. Hii sio sawa muujiza ni ishara ya kukuonesha Kuna Yesu.

Mungu alipowaambia wana wa Israel kuwa wapake damu katika miimo ya malango  ili atakapo pita kuua wazaliwa wa kwanza wa Misri, Lengo lake alikuwa anataka kuwaonesha kuwa wamtazame mzaliwa wa kwanza kama lango.

1 Wakamjia Mafarisayo na Masadukayo, wakamjaribu, wakamwomba awaonyeshe ishara itokayo mbinguni. 2 Akajibu, akawaambia, [Kukiwa jioni, mwasema, Kutakuwa na kianga; kwa maana mbingu ni nyekundu.3 Na asubuhi, mwasema, Leo kutakuwa na dhoruba; kwa maana mbingu ni nyekundu, tena kumetanda. Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa mbingu; lakini, je!t Ishara za zamani hizi hamwezi kuzitambua?] Mathayo 16 :3

Ishara inakupa kujua majira husika kujua kuwa hii ndoto ni ya lini na itatokea lini. Ishara inapokuwa kibao inakupa kutazama ndani ya ndoto kuna kitu gani.

Ishara inapokuwa sauti  inakupa kusema tegat sikio maana kuna kitu cha kufuatilia usipende tu kutafuta tafsiri ya ndoto bali chukua na ujumbe ulioko ndani yake.

Kasome biblia yako Nebukadreza alipoota ndoto  ya mti kukatwa alifurahia tu kupata tasfiri alipuuzia ujumbe alioambiwa kuwa.Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha.Danieli 4:27.

Lakini ule ushauri aliupuuzia. Na alipewa tafsiri na ujumbe lakini yeye alifurahia tasfiri na akaacha ujumbe (hadi atakapotambua kuwa mbingu ndizo zinazotawala) na akaishia kukaa kwenye “adhabu kwa nyakati saba”.

20 Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.] Marko 16 :20

Saa nyingine ishara inakuja kulithibitisha neno ukisoma biblia yako vizuri hao wanafunzi walipokuwa wanahubiri, Mungu alikuwa analithibitisha lile neno ili wale waliokuwa wanasikiliza wamtazame Mungu.

Maana yake wale wanaosikiliza neno  linalohubiriwa wamtazame Yesu maana kama  walidharau neno linalohubiriwa wanamdharau Yesu ndio maana alisema Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma.Mathayo 10:40

Ndio maana kama nakuja kufundisha neno la Mungu si suala tu la kuchukua notes au somo ninalojisikia bali lazima niombe Mungu anipe somo la siku hiyo kwa ajili ya watu wake.

4 Kizazi kibaya na cha zinaa chataka ishara; wala hakitapewa ishara, isipokuwa ishara ya Yona. Akawaacha, akaenda zake. Mathayo 16 :4

Ishara hii inakuonesha uhusikaji wa kizazi, kuna baadhi ya ndoto utaota ishara  zinazo husisha kizazi kimoja na kingine.Ishara itakusaidia kujua.

2 Viashiria vinavyo kuja na ndoto vipo vya aina mbali mbali

8 Hata asubuhi roho yake ikafadhaika;

Mwanzo 41 :8a

Kiashiria kimojawapo  kinachokuja na ndoto ni roho kufadhaika na unaweza pata mfadhaiko

?Wakati ukiwa ndotoni.

?Au baada ya kuamka

?Baada ya kukumbuka hiyo ndoto (kila ukikumbuka hiyo ndoto)

Ukiona hivyo jua kuwa unahitaji kufuatilia.

Na hapa kwa Farao tunaona aliota ndoto usiku lakini alifadhaika asubuhi

_5 Wakaota ndoto wote wawili, kila mtu ndoto yake usiku mmoja, kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri waliofungwa gerezani.6 Yusufu akawajia asubuhi, akawaona wamefadhaika.

Mwanzo 40 :5-6_

Ile kufadhaika ilikuwa ni ishara  kuwa wanahitaji kufuatilia hizo ndoto  yaani wasipuuzie.

_7 Akawauliza hao maakida wa Farao, waliokuwa pamoja naye katika kifungo, nyumbani mwa bwana wake, akisema, Mbona nyuso zenu zimekunjamana leo?

8 Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Kufasiri si kazi ya Mungu? Tafadhalini mniambie. Mwanzo 40 :7-8_

Kiashiria kingine ni kuwa na kiu ya kutaka tafsiri ya ndoto. Ngoja nizungumze hivi. Kujua kuendesha gari, hakukupi  uhalali wa kupewa leseni hadi ujue ishara za barabarani. Hata ukienda kwa traffic wanacheki kwanza ujuzi wa ishara mbali mbali na ukifeli hapo hawana hata haja ya kuendelea kucheki namna unavyoendesha gari. Na watasema kasome upya.

Sasa watu wengi kama wanaandika ndoto hawaweki ishara za kuwakumbusha kwenye ndoto  wanaandika kijumla jumla tu, na ndio maana vitu vingi sana  unakosa kwa sababu ishara ndio zinakusaidia hata kujua namna ya kuomba na namna ya kushughulika na hiyo ndoto.

Kwa hiyo kama unasikia msukumo wa kutafuta tasfiri ya ndoto ujue hiyo ni ishara ya kuwa unahitaji kufuatilia.

Ishara nyingine ni kuota ndoto moja mara mbili

32 Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi. Mwanzo 41 :32

Ukiota ndoto mbili lakini ina maana moja, ni kuwa Mungu anakukuwekea msisitizo

Pia inawezekana ndoto ya kwanza hukusikia

14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Ayubu 33 :14

Maana yake kama hujasikia Mungu anairudisha tena hiyo ndoto, ni sawa na mtu anaota ndoto za shule  mara nyingi. Kila akiomba Mungu nisaidie hapa anarudishwa shule na bahati mbaya sana hajui shule maana yake nini na mtihani maana yake nini?

Kuna mtu mmoja aliniandika akasema Mwl naota niko shule kila nikikaribia kufanya mtihani…

1.Ndoto ya kwanza akawa kipofu

2.Katika mtihani mwingine akaona wenzake wanamaliza ila yeye hajaanza bado ( Yote ni kwenye ndoto hiyo hiyo.).

Sasa kama hajajua mtihani maana yake nini hatoki hapo au tu Roho Mtakatifu amsaidie kutoka hapo kwa kuomba kwa kunena kwa lugha.

1 Hata katika mwaka wa pili wa kumiliki kwake Nebukadreza, Nebukadreza aliota ndoto; na roho yake ikafadhaika, usingizi wake ukamwacha. Danieli 2 :1

Hii ni ishara, ilimpa shida sana huyu mfalme maana alikosa usingizi. Na kama mtu mwingine  akiota hiyo ndoto aliye mwepesi kuandika huwa anaandika, na kuomba  maana kuna wengine hawafanyi hivyo.

3 Mfalme akawaambia, Nimeota ndoto, na roho yangu imefadhaika hata niijue tafsiri yake.4 Ndipo hao Wakaldayo wakamwambia mfalme, kwa lugha ya Kiaramu, Ee Mfalme, uishi milele; tuambie sisi watumishi wako ile ndoto, nasi tutakuonyesha tafsiri yake.

Danieli 2 :4

Ile umeota ndoto na umesahau na bado unataka kujua tafsiri yake. Maana kama umesahau si rahisi sana kufuatilia.

13 Katika mawazo yaliyotoka katika maono ya usiku, Hapo usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu.14 Hofu iliniangukia na kutetema, Ayubu 4 :13-14a

Hofu ni ishara na kile kilichotokea Mwilini mwako. Kwa mfano unaota unakemea na ukifingua mdomo unakuta unakemea na ameota unalia na ukiamka unakuta kuna machozi machoni kwako, unaota umeumwa na nyoka au mdudu ukiamka unaona alama.

14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; 16 Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,17 Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi; Ayubu 33 :14-17.

Ukiota Ndoto ambayo inapingana na kitu ulichowaza au kufikiria angalia vizuri  uwe mwangalifu sana na uamuzi unaotaka kufanya.

Kwa mfano. Habari zay Yusufu na Mariam.

18 Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 19 Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. 20 Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 24 Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe; Mathayo 1 :18-20,24

Umeona hiyo habari, Yusufu aliota ndoto iliyokuwa inapingana na kusudio lake, kama ni hatari Mungu atakuambia jambo unalopingana nalo na atakavyokusudia kuvuka hapo .

1 Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danielii aliona ndoto, na maono ya kichwa chake, kitandani mwake; basi akaiandika ndoto, akatoa habari ya jumla ya mambo hayo. Danieli 7 :1

Ukiota ndoto na ukapata msukumo wa kuiandika maana yake ni kiashiria kuwa unahitaji kuifuatilia.

Andika ndoto ambazo zinakuja na viashiria. Kama upo kama mimi nakaa karibu  na kalamu na karatasi naandika saa hiyo hiyo.

Jizoeze kuandika na usiandike kijumla andika na ishara ulizoona.

Mfano ulijisikiaje ulipoota hiyo ndoto.

JAMBO LA TATU: OMBEA HIYO NDOTO HUKU UKITUMIA KIASHIRIA KAMA MWONGOZO WA KUJUA KAMA UMEIOMBEA IPASAVYO.

Leo nataka ulitazame hapa kama mtu wa jikoni ili ujue namna ya kumuomba hapa.

Ndoto ya Nebukadreza  ilikuja na viashiria kama vinne hivi maana unaweza sahau ndoto ila kiashiria huwezi sahau.

1 Hata katika mwaka wa pili wa kumiliki kwake Nebukadreza, Nebukadreza aliota ndoto; na roho yake ikafadhaika, usingizi wake ukamwacha.

Danieli 2 :1

?1.Roho yake kufadhaika hicho ni kiashiria no 1

?2.Usingizi kumwacha

Mfalme akawaambia, Nimeota ndoto, na roho yangu imefadhaika hata niijue tafsiri yake. Danieli 2 :3

?3. Hamu ya Kutaka kujua tasfiri

Ndoto ambazo zilikuja na ishara ghafla moyoni mwako zinakuwa zinarudi.

12 Basi kwa hiyo mfalme akaghadhibika sana, akaona hasira nyingi, akatoa amri kuwaangamiza wenye hekima wote wa Babeli. Danieli 2 :12

?4.Kama inakuletea hasira na kughadhabika (nacho ni kiashiria)

Ishara ya kwanza hadi 3 haikusukuma kitu ila ya nne ilisukuma kupata ndoto na tafsiri yake.

Yusufu alipoota ndoto ya kwanza alikuwa kijana mdogo na aliposema wale wenzie walimchukia .

Na Aliposema mara ya pili  waliishia kumuuza.

Sasa hii ndoto ilikuwa na kiashiria cha hasira. Biblia inasema kuna hasira na ghadhabu .

Unapoona ndoto inakuja na ishara nyingi ina maana Mungu anakusisitizia  kuwa fuatilia hiyo ndoto kwa haraka. Na kuna kitu zaidi ya kimoja unachohitaji kukitilia mkazo.

Daniel alikuwa ni mmoja wa wenye hekima na amiri jeshi alimweleza Daniel juu ya hasira ya mfalme (hasira za mfalme) ili kufuatilia.

Kiashiria kilichomsukuma Daniel kuombea ndoto ni hasira aliyokuwa nayo mfalme.

Sasa usikimbilie  kuomba tafsiri ya ndoto kwa watu  bali nenda kwa Mungu maana kazi ya kufasiri ndoto ni ya Mungu.

Lakini sijajua kwanini Nebukadreza alienda kwa wachawi maana tunaona Daniel aliposikia juu ya habari za ndoto ya mfalme alienda moja kwa moja kwa Mungu.  Ni ndoto chache sana katika biblia utaziona kwa style hii.

Kazi moja wapo ya  ishara ni kukusukuma kwenda kumtafuta Mungu. Na sisemi ni vibaya kwenda kwa mtu maana anaweza kukupa tafsiri potofu  na mwingine hata kama hajui atasema anajua au atakupa tasfiri inayofanana na ya Mungu ila  akaua imani yako.

Ndio maana Mungu hawezi kukuruhusu moja kwa moja uende kwa watu kienyeji kienyeji.

VIASHIRIA.

1.Roho yake kufadhaika

2.Usingizi kukatika

3.Kutaka kujua tafsiri

4.Hadi aliposikia hasira ndipo Daniel alienda kuomba.

HATUA ZA KUOMBA KWA KUFUATA KIARISHIRIA

1.Kila wakati angalia ni kiashiria gani kinachokusukuma kuomba  ndicho utakitumia kupima kama umemamiliza kuombea ndoto au bado.

2.16 Basi Danielii akaingia, akamwomba mfalme ampe muda, kisha yeye atamwonyesha mfalme tafsiri ile. Danieli 2 :16

Tenga muda wa kuiombea hiyo ndoto. Daniel  aliomba Muda wa kuombea ndoto ya mfalme. Na wewe ukishaona kiashiria/ishara tenga muda wa kuombea hiyo ndoto.

 1. 17 Ndipo Danielii akaenda nyumbani kwake, akawapasha habari kina Hanania, na Mishaeli, na Azaria wenzake; 18 ili waombe rehema kwa Mungu wa mbinguni kwa habari ya siri hiyo, ili kwamba Danielii na wenzake wasiangamizwe pamoja na wenye hekima wa Babeli. Danieli 2 :17-18

Daniel aliwatafuta wenzake ili wamsaidie kuomba juu ya ndoto ile maana na wao uwe na uhakika walipata kiashiria  kama alichopata Daniel.

MFANO;Yesu alipokuwa bustani ya Eden (Mathayo 26:36-41 na Luka 22:43-45). Soma vyote ili uone. Yesu alienda katika bustani na wanafunzi wake 3 na alisema roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa. Na akaanza kuomba na alipoona hawaombi aliwafuata na kuwaambia haloo mbona hamkukesha pamoja na mimi akarudi kuomba tena.

Wanafunzi wake walillala na walilala kwa sababu ya roho ya huzuni kama ile ile aliyokuwa nayo Yesu .

Kama unaomba hakikisha hadi kiashiria kigeuke maana kama ni huzuni igeuke hadi kuwa Furaha. Yesu aliomba na Mungu akamtumia malaika wakaja kumtia nguvu na akaomba hadi alivuka. Maana alikuwa na jambo zito sana  maana alikuwa anapambana na mawazo yaliyomo ndani yake .

Na Yesu alibananwa namna hiyo kuwa anatakiwa kuomba usifikiri hakuwa na kazi zingine kama ni wagonjwa walikuwepo wa kuombewa na kazi zingine zilikuwa zinamsubiri ila kwa umuhimu wa maamuzi aliyotakiwa kufanya ilistopisha kila kitu na aliomba hadi akavuka.

Na Mungu alipotaka kuwainua akina Petro ilikuwa lazima na wao wawekewe kishiria kile kile cha huzuni.

_36 Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake. 37 Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba.38 Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake.Luka 2 :36- 38.

Huyu alikuwa nabii wa maombi maana mtu anayemuombea nabii nae anakuwa na mindset ya nabii.

Ukipewa mzigo wa kumuombea Mwl na wewe unakuwa unawaza kama mwalimu na unakuwa na neno kama ninalopewa kufundisha siku hiyo na wewe unashangaa mbona hii mistari na mimi ndiyo niliyopewa? Maana ule upako ninao kuwa nao Mungu anakuwekea na wewe ili uombe ipasavyo. Sasa hiyo sio gurantee kuwa na wewe umepewa kuwa Mwl hapana kazi yako ni kumuombea Mwl.

Ndio maana kiashiria kikija kwako lazima uombe hadi kile kiashiria kiondoke. Maana yale tenga muda omba hadi uvuke.

Mzigo wa akina Daniel aliondoka hadi alipopewa tafsiri ya ndoto na Mungu maana kama kishiria kisingeondoka kama asingepata tasfiri.

Daniel alipopata ujumbe alirudi kumshukuru. Kama Mungu  kakusaidia kupata tasfiri tenga muda wa kmushukuru. Rudi kushukuru ili na siku nyingine Mungu akusaidie.

Mfano: Nilikuwa nafundisha  Dar es Salaam  na niliwapa ushuhuda wa kwangu , baba Yangu alipokufa nilisikia mzigo wa kubeba maana mimi nyumbani kwetu ni mkubwa. Na kila mara niko safari na kule kwetu Arusha na Tukuyu ni km 1400. Sasa huwezi kwenda mara moja tu. Basi Mungu aliniambia kuwa muda wa baba kuishi umeisha nikamuomba Mungu azuie kidogo ili asubiri subiri. Sasa siku moja baba aliwaambia wadogo zangu kuwa siku zangu za kuishi zimefika mwisho ila kaka yenu (yaani mimi) hataki niondoke. Alisema hata nikiondoka kaka yenu yupo atawasaidia .Basi  nikamuachia aende tu (niliacha kuomba maombi kwa Mungu ili amuongezee muda wa kuishi) na kuna kiashiria kilikuwa kinanisumbua na nikaanza  kuomba  je nilikosea nilipomuachia aende.

Sasa nikaota Ndoto niko hotelini ghafla nikamuona mhubiri wa marekani anakula pale nikasema na mhudumu wa pale hotelini naomba niletee pale ili nikae nae na nilipokaribia kufika basi akainuka na kugeuza sura yake nikaona kumbe ni baba yangu ila alivyokaa nilijua ni mhubiri.

Akanitazama na akatoa kisu cha chakula na uma akanipa na akaondoka hakusema chochote. Basi nikasikia sauti ikisema “nitakushibisha kwa wingi wa siku (Zaburi 91). Mungu alikuwa ananiambia kuwa baba yako alimaliza siku zake za kuishi.

Nikaenda kuzungumza na mama kumuuliza je baba aliaga alisema Baba alisema anataka afe kabla ya mama.

Na alimuonesha mama kuwa mchungaji akifa anavikwa hivi.(baba yangu alikuwa mchungaji)

Basi kuna mtu alinisikia na kuniambia Mwakasege huo ushuhuda wako unafanana na wa kwangu nimeota  kama hiyo ndoto yako , sasa  baba yangu yupo kwa maana hiyo (kama ndoto yako) ina maana baba yangu anakaribia kufa.

Na aliponiambia hivyo na yeye akaanza kupata mzigo wa kuliombea maana alikuja elewa maana yake nini ile ndoto baada ya kusikia ushuhuda ndio alikuja kujua cha kufanya .

Farao alipo ota ndoto angeweza puuzia lakini ingekuwa hasara sana

Fikiri Yusufu ( Mume wa Mariam) angepuuzia ndoto aliyo ambiwa kuwa Herode anataka kumuua mtoto unafikiri ingekuaje?

Na mama Jusi nao wangepuuzia ndoto waliyoambiwa na malaika kuwa wasirudi njia  ile (Kwa Herode) na wakapuuzia ina maana Yesu angeuawa akiwa bado mdogo.

Herode alikuwa anajitahidi afanye kama ndoto na mke wake  alivyoota alivyosema kateswa usiku kwenye ndoto .(Alitaka Yesu asihukumiwe maana hakuwa na hatia)

Kuna mtu mmoja aliniambia kuwa aliota ndoto pocha yake imeibiwa na kuamka asubuh alipoenda kazini cheo chake alishushwa saa mbili asubuh. Alikuwa na allowance ya usiku tu lakini hajua cha kufanya. Mungu alikuwa anamuambia kuwa si halali wewe kushushwa cheo (kuibiwa pochi maana yake pesa zake kuibiwa) na Mungu alikuwa anajaribu kuksemesha kuwa omba sasa. Na alikuwa na allowance ya usiku tu na hakufanya hivyo na asubuh ndipo cheo chake kilishushwa.

Jua mbinu za kuombea ndoto na nilikuambia kuwa kama hujui vizuri omba kwa kunena kwa lugha ili Roho Mtakatifu akusaidie. Mungu anatupenda sana sisi wanadamu hapendi tuvamiwe na vitu bila sisi kujua kwa hiyo ndio maana anatuambia kwa njia ya ndoto. Na utaratibu wote upo kwenye biblia.

Maombi.

Jina la Bwana libarikiwe sana.

==Glory to God Glory to God==

 

SEMINA YA NENO LA MUNGU NA MWL MWAKASEGE.

UWANJA WA TANGAMANO TANGA 11 JUNE 2017

SOMO MBINU ZA KUOMBEA NDOTO ILI USIKWAME KIMAISHA.

SIKU YA SABA NA YA MWISHO

 

NAMBA ZA HUDUMA  http://www.mwakasege.org0/kuchangia.htm

TUENDELE MBELE

Jana tulianza kuangalia Mbinu ya pili na kukumbusha tu kidogo mbinu hizi.

Kutumia Damu ya Yesu

Kuombea ndoto kwa kutumia kiashiria kilicho ambatana na ndoto.

Jana  nilikuonesha vitu vitatu katika hii mbinu  ya pili

A). Maana ya kiashiria kama kilivyotumika katika somo hili. (Ishara zinazoambatana na ndoto ili kumsaidia yule anayeota ndoto asije akapuuzia)

B).  Jinsi viashiria vinavyojitokeza tofauti tofauti. (Nilikuambia kuwa ndoto moja inaweza ikawa na kiashiria zaidi ya kimoja.

C). Ombea hiyo ndoto huku ukitumia kiashiria kama mwongozo wa kujua kama umeiombea ipasavyo.

Leo tuangalie kipengele cha nne nacho ni hiki

 1.  Tumia kiashiria kuombea ndoto kwa msukumo wa muda uliomo ndani ya ndoto

Tutapitia mfano wa ndoto iliyopo katika Daniel 4:1-37 soma sura yote ila hapa tutaangalia kwa sehemu.

Hii ndoto ina muda wa aina mbili.

 1. Muda wa Kwanza ni ule muda wa nyakati 7 za adhabu ikiwa Nebukadreza hatafuata Ushauri wa maelekezo aliyopewa.

Danieli 4:16 “moyo wake ubadilike, usiwe moyo wa binadamu, na apewe moyo wa mnyama; nyakati saba zikapite juu yake’.

Danieli 4:23-25 “Tena, kwa kuwa mfalme alimwona mlinzi, naye ni mtakatifu, akishuka kutoka mbinguni, akisema, Ukateni mti huu, mkauangamize; ila kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya kondeni; kikatiwe maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na wanyama wa kondeni, hata nyakati saba zipite juu yake; 24 tafsiri yake ni hii, Ee mfalme, nayo ni amri yake Aliye juu, iliyomjia bwana wangu, mfalme; 25 ya kuwa utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni, nawe utalazimishwa kula majani kama ng’ombe, nawe utatiwa maji kwa umande wa mbinguni, na nyakati saba zitapita juu yako; hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa yeye amtakaye, awaye yote”.

Huu ni muda wa kwanza unaona katika ndoto uko peupe na ulikuwa unahusika na nyakati saba za adhabu. Na hakulazimika kupita katika adhabu ikiwa angefuata ujumbe (Ushauri) aliopewa. Hii ni shida sana hata kwa watu wengi wanapenda  kupata tafsiri na kuacha ujumbe.

Ndoto inaweza ikaja kwa ishara  yaani mafumbo sasa wengi wanataka kujua maana tu na wana acha ujumbe

Ukisoma biblia yako utaona kuna baadhi ya ndoto katika biblia zina ujumbe na hatujaambiwa ndoto yenyewe ilikuaje na tafsiri yake ila tumepewa ujumbe wake.

Mfano unaona alionywa kwa njia ya ndoto. Ila hatuoni ndoto ilikuaje biblia haisemi ndio maana usiishie tu kupata tafsiri tafuta na ujumbe wa hiyo ndoto.

Sasa katika ndoto kuna muda na watu wengi hawajui namna ya kujua muda uliomo ndani ya ndoto ukija kimafumbo au hata kama kuna muda ujue ujumbe  na kuufanyia kazi.

 1. Muda wa pili – uliokuwa unahusika kuona kama Nebukadreza yuko tayari kutengeneza mambo yake ili kufuata Ushauri.

Hii ndoto haijaweka wazi. Ngoja tuangalie mistari ya biblia

Danieli 4:26-33 “Na kwa kuwa waliamuru kukiacha kisiki cha shina lake; ufalme wako utakuwa imara kwako, baada ya wewe kujua ya kuwa mbingu ndizo zinazotawala. 27 Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha. 28 Hayo yote yakampata mfalme Nebukadreza. 29 Baada ya miezi kumi na miwili, alikuwa akitembea ndani ya jumba la kifalme katika Babeli. 30 Mfalme akanena, akasema, Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe kao langu la kifalme, kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu?

31 Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee mfalme Nebukadreza, maneno haya unaambiwa wewe; Ufalme huu umeondoka kwako. 32 Nawe utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni; utalishwa majani kama ng’ombe, na nyakati saba zitapita juu yako, hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yote. 33 Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadreza; alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng’ombe, na mwili5 wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege”.

Angalia vizuri biblia inasema baada ya miez 12 ya kuota ndoto ndipo mambo yale yalitokea.  Lakini hiki kilikuwa kipindi muhimu sana kwake kwa sababu kama angetumia vizuri ange epukana na adhabu ya miaka 7 ( kama angetubu).

Nebukadreza alipewa kiashiria  ndani yake kilichokuwa kinambana na kumkumbusha  kuwa ndoto yake inahitaji kufuatiliwa kwani haijaisha bado na inahitaji kufuatiliwa  lakini alipuuzia na akapata kukaa kwenye adhabu kwa nyakati saba.

Namshukuru Mungu kwa sababu ya Nebukadreza  kwa kuliweka  wazi jambo hili. Na kama unasoma biblia yako utaona Daniel hakuandika yeye hii “press release” maana inaonesha kuwa kuna mahali alicopy.

Angalia vizuri biblia inasema – “Daniel 4:1-4

Mfalme Nebukadreza, kwa watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wanaokaa katika dunia yote; Amani iongezeke kwenu.

Mimi nimeona vema kutangaza habari za ishara na maajabu, aliyonitendea Mungu aliye juu.

Ishara zake ni kubwa kama nini! Na maajabu yake yana uweza kama nini! Ufalme wake ni ufalme wa milele; na mamlaka yake ni ya kizazi hata kizazi.

Mimi, Nebukadreza, nalikuwa nikistarehe katika nyumba yangu, nikisitawi katika nyumba yangu ya enzi”.

Ukisoma sura yote ya nne unaona hii ni press release (Taarifa kwa vyombo vya habari vya wakati ule) ya Nebukadreza. Na Daniel ina maana kuna mahali aliitoa  na Kuweka kwenye kitabu hiki. Na Roho Mtakatifu anataka na sisi tujifunze mambo yaliyomo ndani ya hii ndoto maana ina mambo mengi mazuri ya kujifunza.

Pia hata baada kupelekwa msituni bado alikuwa na nafasi ya kutengeneza hebu tuangalie tena mistari michache.

Daniel 4:14-15 “Akapaza sauti yake, akasema, Ukateni mti huu, yafyekeni matawi yake, yapukusieni mbali majani yake, na kuyatawanya matunda yake, wanyama na waondoke hapo chini yake, na ndege katika matawi yake. 15 Walakini kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya kondeni; kikapate maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na wanyama katika majani ya nchi;

Hapa tunaona Nebukadreza alikuwa kichaa na katika ulimwengu wa Roho alikuwa amefungwa.

Mungu alisema kisiki kibaki imara maana yake ile nafasi yake ibaki isichukuliwe na mtu “hata atakapojua kuwambingu ndizo zinazotawala”.

Kama wewe ni mwanasheria unaona kabisa adhabu ni iko wazi kabisa yaani alitakiwa tu *atambue na kumpa Mungu heshima yake katika maisha yake na ile adhabu ingeweza  fupishwa.

Mathayo 24:22 “Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo”.

Wateule maana yake ni watu walioteuliwa kusimamia kusudi maalum na ina maana siku zinaweza punguzwa hata kama wengine wanapata mateso ila kama wewe ni mteule hizo siku zinaweza fupishwa.

Sasa wakati Mungu ananipitisha kwenye hiyo mistari nilitaka kujua uteule wa Nebukadreza upo kwenye nini.

Mungu alimpa Nebukadreza kazi ya afisa magereza ili kusimamia kazi ya kuwafunga wana wa Israel kwa miaka 70.

Kazi ya Nebukadreza alikuwa amepewa kazi ya kuwafunga (hii ilitokana na wana wa Israel kuabudu miungu mingine) na alipewa na kazi ya kuchukua vyombo vya Hekalu la Sulemani vya sadaka. Na alipewa avitunze ili siku Mungu akivihitaji avichukue. Sasa mtoto wake alipovitumia Mungu alimtandika siku hiyo hiyo.

Uwe mwangalifu sana kutofautisha katika ya utumishi na wokovu. Maana hauendi mbinguni kwa ajili ya utumishi bali kwa kuwa na uhusiano mzuri na Yesu. Maana wako watu kama Nebukadreza  Mungu anawatumia na kuwatandika tena. Kamwangalie Farao wa Kipindi cha akina Musa .Mungu alimwambia Farao kuwa nalikusimamisha kwa kusudi hili ili nguvu zangu zionekane kwako lakini alikuwa anaabudu miungu mingine.

Mungu  aliwahi kutumia punda kuongea na akiongea kwa ajili ya kumwambia mtumishi wake lakini sasa sio ticket ya Punda  kwenda mbinguni.

Wengine bado hawajadaka ‘’Yesu alipokuwa anaenda Yerusalem alipanda Punda na alitandikiwa na vitambaa na nguo lakini tunona Yesu alienda nae hadi mlango wa Hekalu na akamuacha pale mlangoni hakuingia nae hekaluni’’.

Kuna mtu Mungu anazungumza nae hapa. Usifikiri kumtumikia Mungu ni ticket ya kwenda mbinguni. Tengeneza roho yako na Yesu. Kasome biblia yako siku Yesu akija kuna wengine atawaambia tokeni kwangu maana sikuwajua kamwe. Na watasema mbona tulitoa pepo kwa jina lako. Lakini hapa nataka uone walitumika lakini mbinguni hawaendi.

Ninachotaka uone ni kuwa kuna muda umepewa wa kuwa utakapotambua ya kwamba Mungu ndiye anatawala uweze kutoka kwenye adhabu.

Katika wakati huu wa agano jipya ina maana ukiomba toba ili Mungut akusamehe na akutoe  kwenye adhabu uwe na uhakika atafanya hivyo.

Ngoja niseme hivi  “saa zinaonesha muda kwa kutumia mishale, sasa mishale ni kiashiria kuwa kuna muda kwa hiyo hutatatazama mishale tu bali utaangalia na muda.

Kwa hiyo katika ishara lazima kuangalia na kipengele cha muda kilichopo. Jana tuliona katika habari ya Daneil 2. Tuliona kiashiria kile cha nne (cha hasira ya mfalme) kilipofika kwa Daniel ndicho kilichomsukuma Daniel kuomba Ili kupata tafsiri ile ya ndoto ya mfalme. Baada ya kuomba Daniel na wenzake walipata ndoto na tafsiri yake.

Nebukadreza hakujua kuwa muda aliopewa wa kutengeneza kile alichotakiwa kukifanya ili asiingie kwenye adhabu. Katika agano jipya biblia inasema  “Warumi 8:14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu”

Kwa hiyo Roho anapokuja ndani yako anakuzaa mara ya pili na pia anaweka uongozi wa Mungu katika kuongoza hatua zako kila siku. Katika agano jipya  biblia inasema hawatasema mjue Mungu kila mtu atanijua. Pia mahali pengine panasema “na uzima wa milele ndio kumjua Mungu wa kweli na wa pekee (Yohana 17:3)”  kwa hiyo Roho Mtakatifu anapokupa uzima wa milele ina maana atakuongoza toka ndani yako kujua hatua kwa hatua.(ndani yako tengeneza ushirika na Roho Mtakatifu na atakuongoza kufuata na neno maana neno ni taa miguu petu)

Ndio maana mafunuo ambayo hayapo sawa na neno ni rahisi sana kukupoteza, maombi ambayo yatasimama bila kukueleza mpaka wa neno la Mungu utajikuta unapitiliza hadi kuingia shimoni. Shetani hana shida na unavyoomba ila shida yake ni kusoma neno. (Biblia)

Shetani hana shida ukiomba maana ukiomba bila kuwa na neno itafika muda utaacha kuomba, kwa sababu huna mafuta ndani yako.kama una neno  ndani yako na ukaomba maombi yako yanakuwa na nguvu Yesu alisema_Yohana 15 :7 Lakini 7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa._

Sasa kuomba kunajua automatic ndio maana ukiwa  kama huna neno ndani yako ni sawa na gari ikawa na mafuta ikakosa taa uwe na uhakika haiwezi kutembea usiku. Watu ambao wa maombi na hawana neno huwa wanapaki wakifika kwenye giza. Yaani ukiwa kwenye shida kama huna neno unajikuta umepaki na umeacha kuomba. Kwa sababu huna neno

Kuna ndoto zingine zikija kwako hazitakupa nafasi (muda) ya kwenda kwa mwingine ili akusaidie kuomba.  Ndio maana nakusisitiza kuwa na neno ambalo litakusaidia moja kwa moja kuomba wewe mwenyewe.

Jambo la pili: zijue dalili zinazokujulisha kuwa uiombee ndoto kwa msukumo wa muda uliomo ndani ya ndoto

Nebukadreza hajukujua dalili  na muda wa miezi 12 aliyokuwa nayo ya kutengeneza  maana wamgemueleza kuwa ana huo muda angejua namna ya kutafuta msaada.

Dalili za kuangalia.

1.Msisitizo utakao upata au mshangao unaoupata moyoni mwako unapofanana kimahesabu na vitu ulivyoota.

Mwanzo 40:8-22 Pia angalia na Mwanzo 41.

Mwanzo 41:25 -31 .25 Yusufu akamwambia Farao, Ndoto ya Farao ni moja; Mungu amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu. 26 Wale ng’ombe saba wema ni miaka saba; na yale masuke saba mema ni miaka saba. Ndoto ni moja.27 Na wale ng’ombe saba, dhaifu, wabaya, waliopanda baada yao, ni miaka saba; na yale masuke saba matupu yaliyokaushwa na upepo wa mashariki, yatakuwa miaka saba ya njaa. 28 Ndivyo nilivyomwambia Farao, ya kwamba Mungu amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu. 29 Tazama, miaka saba ya shibe inakuja, katika nchi yote ya Misri. 30 Kisha kutakuja miaka saba ya njaa baada yake; na shibe ile yote itasahauliwa katika nchi ya Misri, na njaa itaiharibu nchi.31 Wala shibe ile haitajulikana katika nchi kwa sababu ya njaa inayokuja baadaye, maana itakuwa nzito sana.

Na unaona hii ndoto ilikuwa na ujumbe wa miaka 14, ya shibe na ya njaa na haikushia tu hapo tunaona maana ilisema  Mwanzo 41 :32 32 Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi.

Mungu akikuambia kwa namna hiyo ina maana kuna ujumbe wa kuandaa maana Yusufu alimpa na ujumbe wa kufanya(maelezo au mkakati). Endelea pale mbele utaona

Mwanzo 41:33-38  33 Basi, Farao na ajitafutie mtu wa akili na hekima amweke juu ya nchi ya Misri. 34 Farao na afanye hivi, tena akaweke wasimamizi juu ya nchi, na kutwaa sehemu ya tano katika nchi ya Misri, katika miaka hii saba ya kushiba. 35 Na wakusanye chakula chote cha miaka hii myema ijayo, wakaweke akiba ya nafaka mkononi mwa Farao wakakilinde kuwa chakula katika miji. 36 Na hicho chakula kitakuwa akiba ya nchi kwa ajili ya miaka hiyo saba ya njaa, itakayokuwa katika nchi ya Misri, nchi isiharibike kwa njaa. 37 Neno hilo likawa jema machoni pa Farao, na machoni pa watumwa wake wote. 38 Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake?

Na ujumbe huu ulisaidia karibu  dunia nzima iliyokuwepo wakati ule. Hadi mzee Yakobo akaja na familia yake kwenda Misri ili kuhifadhi maisha yake kutokana na njaa iliyokuwepo.

Na ukiona namna hiyo kama kuna namba jua kuna maana yake., ‘’Enzi za kwetu zile msichana akivaa kwa ajili ya Harusi kulikuwa  hamna mahali unaona mgozi yake. Miguuni alikuwa anavaa stokens nyeupe, mkononi anavaa gloves nyeupe, usoni anafunikwa na vitambaa 3 na kichwani anavaa taji.  Kitambaa cha tatu atafuniliwa mbele ya Bwana Arusi. Akiingia kansan anakuwa kafunikwa na vitambaa hivyo 3. Akifika kansan wakati wa kufunga ndoa  anafunuliwa ndipo unaona na taji. Na ukitazama unaweza fikiri kuwa ni kitu cha kawaida ila Mungu anataka kuonyesha kuwa kanisa ni bibi harusi. Siku tutakapofunuliwa tukiwa mbele yake ndipo tutaonekana. Sasa katika ulimwengu wa Roho  tumevikwa mavazi meupe maana yake tumetakaswa lakini pia unalindwa na utukufu wa Mungu. Shetani akikitafuta kukuona hawezi kwa sababu unefunikwa na utukufu wa Mungu

Sasa ile namba 3 (kufunikwa vitambaa vitatu) ni namba ya Yesu. Sijajua siku hizi wanavaaje. Ngoja nisisende huko.

Ukiota ndoto ndani yako ya aina hiyo ina maana ni ishara  inayokuonesha kuwa kuna jambo la kufuatilia kwa kuangalia hizo namba /alama .

Kamwamgalie Musa alipokuwa anachuga ng’ombe za baba yake na aliona moto aliona kichaka kinawaka moto. Na ule moto uliendelea kuwaka na aliposema Ngoja nigeuke na alipogeuka akasikia sauti kutoka katika kichaka, Mungu alimwambia vua viatu vyako.

Mungu anapogundua kuwa humsikilizi  ananyamaza  ila ishara itaendelea kuwepo. Anachotaka ni hadi ugeuke yaani utie attention yako ili kumsikiliza. Na ukiamua kufuatilia ghafla ule ujumbe utakuja na ule mzigo/muda uliomo katika ule ujumbe utakuja kwako.

Biblia inasema Mathayo 11:28-30  28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; 30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.

Ile ishara ikija kwako itakubebesha mzigo wa kuomba kwa ajili ya kujiandaa na ile miaka 7. Yule mwemyeshaji na waokaji walikuwa na allowance ya siku 3  waliaombiwa na hawakushughulikia. Mmoja alinyongwa na mwingile alirudishwa kazini.  Sasa Ngoja tuje kwa wakati wa sasa ambao tuna Roho wa Mungu.

Roho Mtakatifu akikupa allowance ya siku tatu ina maana anataka uwe na maandiko uweze kujua ili  ushughulike (uombe) mana yule mwokaji alikatwa kichwa. Adhabu ile haikuondoka. Lakini usije jifariji kuwa  kwa kuwa umepuuzia hiyo ndoto hakitatokea ulichoota uwe na uhakika allowance ya muda ikiisha kitakuja kama ulivyoota.(Siku ya kwanza nilikuambia sio lazima ulicho ota kitokee (unaweza omba au fuata ulichoambiwa/shauriwa katika ujumbe ili kisitokee kwa damu ya Yesu) isipokuwa kwa ni jambo la uhakika Mungu analotaka kulithibitisha kama kwa ndoto ya Farao).

Mungu anasema na watu kwa njia ya ndoto haijalishi ni Mkristo  au sio Mkristo Mungu anazungumza kwa njia ya ndoto ila tafsiri yake lazima ipo kwenye biblia.

2 Unaposikia msukumo wa kuisema hiyo ndoto kwa  mhusika hata kama unasikia kusita moyoni mwako

Ukisoma habari za Yusufu katika ile Mwanzo 35: 5-6 unaona aliota ndoto na alipoota ile ndoto akapata msukumo wa kuwasimulia ndugu zake na wakakasirikia na aliwaambia tena. Lakini hakujua kuwa ile kusikia msukumo wa kusema ni kiashiria.

Mungu akikuletea msukumo wa kusema au kusita kukisema  ina maana ulifuatilie hili jambo au uliombee kwanza kabla hujalisema maana inategemea Mungu uliyemuambia atalipokea namna gani.

Ndugu zake Yusufu walielewa ile tafsiri ya ndoto ndio maana walikasirika maana ndoto ilihusu maisha yao ya baadae.

Katika biblia kuna mifano mbali mbali, Pilato alipokuwa anataka kutoa hukumu ya Yesu aliashirisha hadi kesho yake asubuh. Mke wake usiku alipata mateso kwenye ndoto na mke wake akamwambia Pilato  mume wake awe makini na Yesu maana kateswa kwenye ndoto usiku.

Sasa haina maana Mungu alikuwa anataka Yesu asipite msalabani bali alikuwa anataka Pilato asiingie kwenye laana ya kumhukumu Yesu na ndio maana alidaka na kilimlalia na alijaribu hata kuwaambia kuwa  nimfungulie Yesu au Baraba.. na alinawa na mikono na  akasema sina hatia juu ya mtu huyu. Alichokuwa anawainda ni ile ndoto ya mke wake.

Ninachotaka uone ni kuwa yule mama alikuwa na allowance ya masaa machache tu ya kuifuatilia ile ndoto, hakuwa na muda wa kusema ntaomba nitafute kikundi cha maombi ili tuombe kansan.

Mtu mmoja alinisikia nikifundisha baada ya kupata hasara iliyotokea baada ya kuota ndoto usiku kuwa kuna mtu kaiba pochi yake ndogo iliyokuwa ndani ya pochi kubwa. Na sijajua kama aliombea, maana aliniandikia sasa kesho yake asubuh saa mbili  akashushwa cheo. Na Mungu alikuwa anamwambia kuwa kipato chako kinapunguzwa kuna mtu anakuibia sio halali na ikatokea alipoingia ofisini saa mbili asubuh.

Ukiota Ndoto ndio maana ni muhimu sana kuomba na ndio maana Mungu anakunyang’anya usingizi ili uombe maana iko mbele yako.

Kama hujui namna ya kuomba omba kwa kunena kwa lugha na omba hadi usike wepesi  kama ndoto imekuletea huzuni omba hadi uone Furaha kama ilikuletea sononeko omba hadi hiyo hali iondoke.

Kama ulikuwa umekosa amani omba hadi amani irudi kama ni raha imeondoka omba hadi  irudi na usiachie njian. Sa nyingine unaomba na unapata tafsiri robo au nusu omba hadi upate tafsiri yote maana ile ishara haitaondoka kwako hadi upate ile tafsiri yote.

Ndio maana jana nilikuambia ndoto inayokuja na viashiria viwili vitatu maana yake kuna kuna vitu zaidi ya kimoja unavyohitaji kutia maana nani ndani ya hiyo ndoto.

 1. Upako wa kuomba unapokuja na ndoto

Zinakujulisha  kuwa hilo jambo karibu litatokea ndio maana unapewa na mtaji wa nguvu za kuomba ili uombe hadi uvuke. Ndio maana mtu anaomba kwenye ndoto na unaamka na unakuta unaomba na Mungu anakupa mtaji huo kuwa kama kuna hatari katika ulimwengu wa roho upangue kwa maombi kwa hiyo omba hadi hiyo hali umevuka.

4.Kiashairia kujitokeza kwa nguvu mwanzoni

Angalia habari za Bwana Yesu katika ile _

Mathayo 26:36-38  36 Kisha Yesu akaenda pamoja nao mpaka bustani iitwayo Gethsemane, akawaambia wanafunzi wake, Ketini hapa, hata niende kule nikaombe. 37 Akamchukua Petro na wale wana wawili wa Zebedayo, akaanza kuhuzunika na kusononeka. 38 Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamojay nami._

Sasa huzuni inaweza ikaanza kidogo kidogo ila sasa ikija kubwa kiasi hicho ina maana ina kitu kikubwa sana. Sasa Yesu aliposema nina huzuni nyingi kiasi cha kufa  ina maana hiyo huzuni imesimamisha kila kitu.

Utaona baada ya Yesu kuomba na alipovuka ndipo tunaona muda mfupi Yuda akatokea na kumsaliti. Alikuwa na muda mchache sana chini ya masaa 12  na alitakiwa aombe hadi avuke.

Mungu kwa kuwa anakupenda s anakuletea kiashiria kizito kama hicho ili ufuatilie  na upate kuvuka.

Ila sasa unakuta wengi wanapopata kiashiria kama hicho wanaandika barau kazini kuwa jamani sijisikii vizuri au wakiona hivyo wanasema Ngoja niende hospitali kupima  na unapima na daktari anasema hauna shida lakini ndani unaona unakandamizwa na tunaona Yesu akianguka chini kwa kifudi fudi. Mwingine hata kama ni mfanya biashara  anasema leo sijisikii vizuri na sijui kuna nini nimecheki watoto wote wako salama  na kila kitu kiko salama ila sujui leo ngoja leo sitoki.

Na unabaki nyumbani unalala na huombi na unakuta hata kuangalia TV huwezi au hata kusoma simu napo huwezi. Maana hicho kiashiria kinataka uombe. Sasa tunaona na akina Petro nao walilala na biblia inasema walilala kwa huzuni. Na hawakuletewa huzuni ila walale bali waombe.

Mungu anakuletea hicho kiashiria ili uombe na lazima ujifunze njia mbali mbali za kuomba.

5.Kiashiria kinaanza kidogo kidogo na kuongezeka kadri ndoto unavyosimulia hiyo ndoto.

Daniel 2:5-13

Nebukadreza aliota ndoto na akasahau, akawaita wale watu wake na akawaambia na ishara kabisa

?Moyo wangu ulifadhaika

?Usingizi ukiniacha

?Na anatafuta tafsiri yake.

?Na cha nne alipata hasira.

Na tunaona walianza kubishana nae kidogo kidogo somo hiyo habari, ghafla hasira ikaenda juu na akamuita amiri wake mkuu na akasema ua hawa watu na wote wenye hekima.

Kiashiria cha hasira  ndicho kilimsukuma Daniel kuomba na akaenda kwa mfalme na kumwambia nipe muda ili niombe. Kiashiria kikija namna hivyo hatua ya kwanza ni anza kuomba.

Omba hadi utue huo mzigo. Na ikifika mzigo wa namna hiyo inabid uombe. Sasa huwezi kuomba kwa mfululilizo kutokana na majukumu tuliyonayo.

Kama ni mfanya kazi muda ule wa chai nenda hata chooni kwa dk chache omba. Na lunch time nayo omba tena kwa sababu ya haraka la hilo jambo. Usisingizie kuwa huna mahali pa kuomba.

Jaribu kumsemesha kuku ambaye ana yai na anataka kutaga, mwambie hamna mahali pa kutagia ujue tu atapanda hata kwenye kabati na kuvunja vyombo ili tu apate mahali pa kutagia  yai.

Sasa wewe una yai la maombi unatakiwa utage wewe unasema sina mahali pa kutagia, basi ujue hujabanwa na yai linalotaka kutoka.

Mwisho wa semina.. na sadaka kwa Mungu.

Hakikisha unapa CD za masomo haya. Kama uko mkoani angalia link pale juu.

Kama hujaokoka hakikisha unaokoka ili masomo haya yawe msaada kwako. Angalia link pale juu.

Na kufikia hapo ndio mwisho wa mfululizo wa semina hii ya Tanga June 2017. Sifa na utukufu kwa Bwana Yesu.  shukrani kwa Mwl Mwakasege,  Kamati ya  Tanga na Huduma ya Mana na wahusika wote kwa kufanikisha semina hii kufanyika. Mungu awabariki sana

Napenda pia kumshukuru Mungu kwa timu nzima tulioshirikia kuandika masomo haya kwa njia mbali mbali.Mungu awabariki sana.

By:

Felix…

==Glory to God Glory to God ==