Muda

16997836_276071752826968_1855426015871815309_nTumekuwa tukilichukulia kawaida sana suala na kutokuwa watu wa kufuata muda katika kila mambo mengi, tukihesabia hayana madhara sanaaa, na mbali zaidi tumejisifu kuwa uswahili ni asili yetu.
Hatari Sana.

Bila kujua suala la kuzingatia kufanya jambo katika muda wake mahali pake lina athar kubwa sana katika ulimwengu wa roho.

Muda ni Lango katika Ulimwengu wa roho hvyo linaweza kuruhusu baraka ama laana.

-Watu wanaoenda na muda/wanaukomboa wakati maandiko yanawaita wenye Hekima_
-Na kwann waukomboe wakati, kwa sababu hizi ni zama za uovu.
Dhambi nying zinazofanyika zinatokana na matumizi mabaya ya Muda.
-Na katika kuukomboa wakat pia ujue nini yaliyo mapenzi ya Mungu ili kuyatimiliza hayo.

Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;

MKIUKOMBOA WAKATI kwa maana zamani hizi ni za uovu.

Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.

EFE. 5:15‭-‬17 SUV

Tusome namna Daudi alifanya matumizi mabaya ya muda na yakamletea madhara.

Hata ikawa, MWANZO WA MWAKA MPYA, WAKATI WATOKAPO WAFALME KWENDA VITANI, Daudi akampeleka Yoabu, na watumishi wake pamoja naye, na Israeli wote; wakawaangamiza wana wa Amoni, wakauhusuru Raba.
LAKINI DAUDI MWENYEWE AKAKAA YERUSALEM.
Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho.

2 SAM. 11:1‭-‬2 SUV

Kilichofuata Daudi alizini na yule mwanamke Betsheba mke wa Uria mwanajeshi wake.
Na baada ya kufanya hvyo Daudi aliagiza Uria auwawe vitani ili kufuta aibu.

Turudi sasa, Kwa wakati Daud alipanda juu ya dari la nyumba hata kumuona mwanamke na kumtamani na kuzini naye alitakiwa kuwa vitani, wakati ule ulikuwa wa vitani kama maandiko yanavyoonyesha ni wakati wafalme uenda vitani Lakini Daudi alitumia muda huo kwa jambo lisilo la muda huo.
MADHARA.
aliingia kwenye dhambi ya uzinzi na kuua.

Shetan anafaham kuwa anamuda mchache sana wa kuwepo dunian hvyo anatumia ipasavyo muda wake na ndo maana kuna huu msemo 24/7 yipo kazini
na ss bila kujua tunatumia muda visivyo na hatimaye tunampa ibilisi nafasi ya kutimiza malengo yake.

wala msimpe Ibilisi nafasi.
Waefeso 4:27

Daudi alikutwa na mengi katika ufalme wake kutokana na dhambi iliyosababishwa na matumizi mabaya ya muda.

MUDA

@ Madam Doreen MaClean