SHERIA YA KUTUMIA MALAIKA

Waefeso 6: 12 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”

Kwenye maisha yetu ya Ufalme tumefahamu sana kuhusu Jeshi la malaka wabaya na nguvu zao za giza lakini tumesahau kujifunza na kulitumia jeshi letu la Malaika watakatifu.

Tulijifunza kwenye Biblia kazi ya jeshi hili la Malaika watakatifu nahizi ni Baadhi ya sheria zao.

Mathayo 26: 53 “Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?”
Luka2: 13 “Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema,”

Mwanzo 32: 1 “1 Yakobo akashika njia yake na malaika wa Mungu wakakutana naye.Naye Yakobo alipowaona, alisema, Hili ni jeshi la Mungu. Akapaita mahali pale, Mahanaimu. Basi, Yakobo akapeleka wajumbe mbele yake kwenda kwa Esau nduguye mpaka nchi ya Seiri katika nyika ya Edomu.”

Zaburi 148: 2 “Msifuni, enyi malaika wake wote; Msifuni, majeshi yake yote.”

Waebrania 12: 22 “Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,”

Tumejifunza kwamba unapookoka unaingia kwenye Ufalme wa Mungu na huko unakutana na majeshi ya Ufalme ambao ni Malaika watakatifu. Tumejifunza kwamba malaika ni polisi wa Ufalme na pia ni wanajeshi wa Ufalme lakini kama hujui kuwatumia unakuwa hufanyi kitu ndani ya Ufalme. Tumeona pia kuna mambo mengine ambayo sisi tunafanya kama wana wa Ufalme, kuna mambo mengine ambayo malaika wanayafanya na kuna mambo mengine Neno la Mungu linayafanya na sio sisi. Kwa mfano:-

Luka 10:19 “Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.”

Maana yake ni sisi tunaokanyaga si Mungu, Unaweza kumkuta mtu anamwomba Mungu ashuke aje akibariki chakula chake na ashuke amlinde usiku kucha kitu ambacho hakiwezekani kwa Mungu kutoka kwenye kiti chake cha Enzi kwenda nyumbani kwa mtu kumlinda. hivyo ndivyo tulivyokuwa tukiamini lakini sasa tumeshafahamu maarifa kwamba siri ya Nguvu zetu Kuwa ndani ya Ufalme wa Mungu kuishika katiba yake ambayo ndiyo inatupa maelekezo ya namna ya kutenda hapa duniani.

Ufunuo 12: 12 “Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.”

Wakamshinda kwa damu ya mwanakondoo ina maana ndani ya Ufalme kuna silaha inayoitwa Damu ya mwanakondoo ambayo tunaweza kuitumia kushinda kila tatizo ‘unapokuwa kwenye maombi unakuwa unaitumia damu ya Mwanakondoo kushinda’, kwenye Maandiko imeandikwa neno la Mungu ni nyundo ivunjayo mawe vipandevipande, ni Upanga uuwao kuwili. Ukishafahamu sheria hii ndipo sasa unaamua kuitumia kupenya sehemu yeyote.
Pia tumejifunza kwamba tunayo silaha ya Malaika ambao ni watumishi wetu na tunao uwezo wa kuwaagiza kwenda mahali popote kutenda kazi.

SHERIA YA MALAIKA ANAYEWEZA KUFUNGUA MILANGO

Matendo ya mitume 5: 19 “lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema,”

Huyu malaika ameenda mpaka gerezani akawatoa watu wa Mungu gerezani. Tunajifunza wakati wa kwenye maombi unaweza kumtuma malaika huyu aende akafungue milango ya biashara iliyofunga, ndoa illiyofunga, kazi, milango ya kupata kiwanja, milango ya kupata visa, milango ya promotion iliyofunga na akaenda kufungua milango uliokwama kwa damu ya Yesu. Watu wa duniani kwenye Ufalme wao huenda kwa waganga wa kienyeji lakini sisi Mungu wa Ufalme wetu anazo nguvu nyingi kuliko mungu wao na tunaweza kutenda mambo makubwa kuliko wao.

Unapowatumia malaika fahamu kwamba wana lugha zao ambazo ni Biblia(katiba) ambayo ni Neno la Mungu na kunena kwa lugha(lugha ya Ufalme), unapomtuma malaika uwe unataja sheria inayomhusu kwenye Biblia na uombe.

Mfano Unatakiwa useme:-
“Baba Mungu katika jina la Yesu imeandikwa kwenye sheria ya Matendo ya mitume 5:19 sheria ya kumtuma malaika mwenye uwezo wa kufungua milango yeye aliyeifungua milango ya gereza la akina Paulo aende akafungue mlango ya magonjwa ulionishikilia, biashara yangu iliyofunga, milango ya safari iliyofunga ifunguke kwa jina la Yesu Amina.” Unaomba na kutaja maeneo uliyofungwa na Fahamu kuwa malaika huyu atatenda sawasawa na maneno yako.

SHERIA YA MALAIKA WA KUTOROSHA GEREZANI

Matendo ya Mitume 12: 8 “Malaika akamwambia, Jifunge, kavae viatu vyako. Akafanya hivyo. Kisha akamwambia, Jivike nguo yako, ukanifuate.”

Mtu wa Mungu Petro alikuwa amefungwa ili kesho yake aende akauwawe pamoja na mwenzake yakobo ambaye aliuwawa usiku uleule. Hiki ni kitengo maalum cha uokoaji ambacho hutumika pale wakati wa dharula ili unapokuwa kwenye hatari na hujui jinsi ya kuokoka unaweza kumwagiza malaika huyu akaja akakuokoa.

Waebrania 13: 2 “Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.”

Sheria hii inaungana na sheria ya malaika anayeweza kujigeuza kuwa mtu. Malaika anaweza kujigeuza akawa mtu akaja akaongea na wewe kama binadamu lakini unatakiwa ujifunze kuongea vizuri na watu sababu wengine wanaweza wakawa ni malaika wamekuja kukusaidia hapo ulipo. Mfano mzuri ni malaika waliokwenda kuteketeza miji ya Sodoma na Gomora walipitia kwa Ibrahimu wakala chakula kama wanadamu lakini walikuwa malaika na baadae kwenda kuiteketeza miji ile. Pia Joshua alipokuwa anaingia mji wa Ai akakutana na malaika ambaye alikuwa kama mtu amevaa mavazi ya kivita ambaye hakuwa na sehemu aliyotokea.

Wakati mwingine malaika anaweza akakutokea na usijue kama ni malaika, Yakobo alitokewa na malaika ambaye alimlazimisha ambariki lakini yeye hakuwa malaika wa kutoa baraka. Malaika Gabrieli alizuiliwa kumpelekea Danieli taarifa sababu yeye hakuwa malaika wa vita mpaka Malaika Mikaeli alipoenda kumtoa sababu yeye ni malaika wa vita.

Ufunuo12:7 “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na Ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.”

Shetani ameshindwa mbinguni ameshindwa duniani ameshindwa kuzimu sababu Yesu alipokuwa msalabani alimfuata mpaka kuzimu akamponda kichwa.

Tunapojifunza kuhusu Ufalme wa Mungu shetani hapendi hata kidogo sababu watu wakijua watauishi na kustawi duniani. Yesu kwenye Biblia alifundisha sana kuhusu habari njema ya Ufalme.

Mathayo 24:

Hilo Neno injili ya Ufalme ni injili ambayo itahubiriwa mpaka tawala za kidunia zigeuke kuwa tawala za mwanakondoo. Watu watakuwa wakitenda mambo kwa uaminifu si kwa kuogopa kuonewa hapana bali ni kwasababu watakuwa wanaishi kwa kufuata mila ya Ufalme. Furaha ya Ufalme wa Mungu haitamaanisha umepata nini bali imetoka kwa Mungu na ipo ndani ya Ufalme wake.

SHERIA YA MALAIKA YA KUMPELEKEA MTU UGONJWA/KIFO

Matendo ya mitume 12: 21 “Basi siku moja iliyoazimiwa, Herode akajivika mavazi ya kifalme, akaketi katika kiti cha enzi, akatoa hotuba mbele yao. Watu wakapiga kelele, wakisema, Ni sauti ya Mungu, si sauti ya mwanadamu. Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango, akatokwa na roho. Neno la Bwana likazidi na kuenea.”

Kwenye ulimwengu wa kale hakukua na neno bakteria au vairasi ndio maana ukisoma neno change kwenye Biblia ya kiingereza limeandikwa kama minyoo(Worms). Mfalme herode alikuwa anasifiwa na watu sana kwasababu ya kuhutubia kwake wakamfananisha na sauti ya Mungu jambo ambali lilimfanya Mungu amtume malaika wa kuleta magonjwa ndipo akafariki. Kila ugonjwa una kiumbe nyuma yake. Mashetani huwa wana uwezo wa kugeuka na kuvaa miili ya backteria wa magonjwa.

MAMBO YA MWANAUME
Kuolewa ni kitu cha kwanza, sio upendo hata ukitafuta kwenye biblia huwezi kuon. Kwenye biblia imeandikwa kwamba enyi waume wapendeni wake zenu maana yake ukishaoa ndipo upendo unafuata, Lengo la mwanaume kuoa kwenye biblia ni kuwa ndani ya uwepo wa Mungu, cha pili ni kuwa na kazi sio kitu cha kufanya, kazi ilikuja kabla ya laana sababu Mungu alipomuumba Adamu alimpa kazi ya kulima na kuitunza bustani ya Edeni. Ukiona mwanaume anaamka asubuhi anapiga mswaki na kuulizia chai iko wapi na baadaye anaangalia TV na kuulizia chakula cha mchana mpaka jioni huyo sio mwanaume wa ukweli. Lengo la mwanaume ni kufanya kazi hata kama hauna kazi ondoka uende ukazunguke ili upate kitu urudi jioni.

Kama wewe ni dada kabla hujaolewa na huyo kaka muulize kama ana kazi?, muulize atakutunza?, mwanaume anatakiwa ajue kutunza familia, kutunza watoto, kutunza mke, na likitokea tatizo mwanaume ndiye anayetakiwa kutunza. Baada ya Mungu kumpa Adam maelekezo ya kuilima bustani ya Edeni na kuitunza Mungu alimpa mwanaume Maono”matunda ya mtu wa katikati usile ila ya miti mingine waweza kula. Mwanaume anatakiwa awe na maono, baadaye Mungu akaona si vema mtu huyu akae peke yake. Maana yake Mwanaume unatakiwa uwe na kazi, ujue kutunza, uwe na maono ya maisha yako, na ukishakuwa na hayo yote ndipo uoe. Mungu alimpa Adam mtu wa kufanana naye wakiwa ndani ya bustani ya Eden yaani wakiwa kwenye uwepo wa Mungu. Kama wewe unajiuliza utajuaje huyu ni mke/mume wangu? Jibu ni kwamba mkutane kanisani kwenye uwepo wa Mungu.

Mafanikio yanatabirika. Ukimwona mtu hanywi pombe, sio mzinzi, sio mwasherati, havuti sigara, anamtumikia Mungu unaweza kumtabiria kwamba mtu huyu atafanikiwa na ataishi miaka mingi. Ukiona mtu ni mlevi, mwasherati, anavuta sigara, mzinzi, mwizi anafanya kila aina ya dhambi basi utajua tu kwamba ni lazima mtu wa namna hiyo maisha yake hayatakuwa na Amani wala furaha na ataishi kwenye miaka ya 50 mpaka 60 atafariki .

SHERIA YA MALAIKA ANAYELAZIMISHA FALME ZA DUNIA ZIWE ZA MWANAKONDOO

Ni malaika anayelazimisha Ufalme wa Mfalme Yesu usambae duniani, ni malaika anayelazimisha mila ya Ufalme wa mbinguni isambae Duniani.

Ufunuo 10: 5 “Na yule malaika niliyemwona, akisimama juu ya bahari na juu ya nchi, akainua mkono wake wa kuume kuelekea mbinguni, akaapa kwa yeye aliye hai hata milele na milele, yeye aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na nchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na wakati baada ya haya; isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu; hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowahubiri watumishi wake hao manabii.”

Huyu malaika wa Saba akishatokea itakuwa hakuna wakati tena
Ufunuo 11: 15 “Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa Ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.”

Malaika hawa kuanzia wa kwanza mpaka wa Saba ni malaika wanaotimiza ratiba ya Mungu, malaika huyu wa saba ni malaika ambaye anaachia nguvu zisizo za kawaida kwa maana kutakuwa na Utawala wa Ufalme wa Mungu na nguvu itaachiwa kwa namna isiyokuwa ya kawaida.
MALAIKA WA KUWAFUNGA RAIA WA KUZIMU
Ufunuo 20: 1 “Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu”

Kama tulivyoona malaika watakatifu wanatoka mbinguni na uvaa miili na kuja hapa duniani vivyohivyo na kuzimu kuna malaika ambao wanakuja duniani wakivaa miili ya Binadamu ili wawe na mahusiano ya kimwili na mtu wapate kuharibu Maisha yao.
Mashetani wanaweza kuwa binadamu ili aharibu Maisha ya mtukama vilekwa kuchukua nyota yake kwa ajili ya matumizi ya kujenga Ufalme wao. Kuna watu wanang’ang’ana kuwa na mahusihano ya kimwili lengo lao sio kuoana bali lengo ni kuchukua nyota yake mtu.

Lengo jingine la shetani kuvaa mwili wa mwanadamu ni kutumia kuzaa uzao wa kishetani duniani. Mwanamke anapokuwa anahusiana na mtu anakuwa hazai kwasababu mayai yake yamechukuliwa pale alipokutana na jini mtu kimwili, hata wakati mwingine mwanawake anaweza akaambiwa ana ‘hormonal imbalance’. “Unaweza Ukaombewa ukatokwa na tatizo hili kwa jina la Yesu”.

Tumeweza kuwatambua malaika wenye miili ya kibinadamu ambao sio watu kuliko kuwaelewa malaika wa nuruni ambao sio watu na sasa malaika hawa tunajua kuwatumia na leo tunamtumia malaika huyu mwenye mnyororo aende akawafunge kwa jina la Yesu, tumia malaika wa Moto ateketeze kila Ugonjwa na mashetani yaliyokusumbua na kukuzunguka Maisha yako kwa damu ya Yesu Amen.

“SHERIA YA KUTUMIA MALAIKA”

ASKOFU MKUU  Dr  JOSEPHAT GWAJIMA
JUMAPILI YA TAREHE 15/05/2016