SOMA HII ITAKUSAIDIA

Kuna mambo ambayo huwa yanatokea kwenye maisha yetu na tunabaki kujiuliza yanasababishwa na nini, na mengine yamegeuka kuwa sehemu ya maisha yetu.

Nimefatilia na nikagundua watu wengi wanaishi maisha magumu na ya umaskini kwa sababu wanaamini maisha ni magumu , cha ajabu na cha kushangaza ni kwamba mtu anapambana kutoka kwenye hali ngumu ya maisha huku bado anaamini moyoni mwake pia anakiri kwa kinywa chake ya kwamba maisha ni magumu, jambo ambalo siyo sawa.

Kanuni ya ki-Mungu inasema hivi  “Kwa maana kwa moyo mtu HUAMINI HATA KUPATA haki, na kwa kinywa HUKIRI HATA KUPATA wokovu.”.  (Warumi 10 : 10 )

Inawezekana ulikuwa unajua ama hujui, ila fahamu hivi;  chochote unachokiamini ndani ya moyo wako hugeuka kuwa sehemu ya maisha yako vile vile chochote unachokili kwa kinywa chako hugeuka kuwa sehemu ya maisha yako.

Kwa mfano kipindi hiki utasikia asilimia kubwa ya watu wanakiri kwa vinywa vyao ya kwamba hakuna hela na wengine wanaamini kabisa ndani ya mioyo yao ya kwamba hakuna hela na hali hii ya watu kutokuwa na hela imegeuka kuwa sehemu ya maisha yao kwa sababu watu wanaamini na kukiri kwa vinywa vyao ya kwamba hela hamna kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata hicho anachoamini na kwa kinywa hukiri hata kupata hicho anachokiri.

Mfano mwingine ni kwa namna  watu wengi wanavyolalamika kuhusu ugumu wa mwezi wa kwanza , Utasikia watu wanakiri kwa vinywa vyao wakisema mwezi wa kwanza ni mgumu, jambo ambalo siyo sahihi. Mwezi wa kwanza unakuwa mgumu kwa asilimia kubwa ya watu kwa sababu watu wanaamini hivyo na kukiri hivyo, kwa hiyo ugumu wa mwezi wa kwanza umegeuka kuwa sehemu ya maisha yao kutokana na kuamini kwao pamoja na kukiri kwao.

USHAURI WANGU KWAKO

Amini na kukiri kile unachokitaka kenye maisha yako, usiamini na kukiri kile usichokitaka.

Tazama hapa kwenye hii mistari ya kitabu cha mwanzo, Mungu aliona vitu vitatu kwenye nchi

1.Ukiwa  2. Utupu  3. Giza  , lakini Mungu hakutamka vile alivyoona bali alitamka kile alichotaka ambacho ni nuru.

Mwanzo 1:1-3  “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.  Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.”

Nimeguswa nikushirikishe haya kwa uchache.

Mungu akubariki sana.

 

Mwalimu D. R. Kabyemela

0714 606 500 / 0757 263 226

Ufalme wa Mungu Kwanza

www.kinet.org

U M K

 

One thought on “SOMA HII ITAKUSAIDIA

  1. Pingback: sourcing in china

Comments are closed.