Tenzi za Rohoni – 1

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

MWOKOZI UMEOKOA

1. Mwokozi umeokoa,
Nimekuwa wako wewe.
Damu imenisafisha;
Sifa kwa mwana Kondoo.

Utukufu, Aleluya!
Sifa kwa Mwana Kondoo!
Damu imenisafisha,
Utukufu kwa Yesu!

2. Nilijitahidi sana
Ila sikupata raha;
Bali kwa kumtegemea
Nilipata Baraka.

3. Daima namwegemea
Damu ikifanya kazi,
Nikioga kwa chemichemi
Itokayo Mwokozi.

4. Sasa nimewekwa wakfu;
Nitaishi kwako wewe:
Fahari nashuhudia
Ya wokovu wa bure.

5. Nasimama kwake Yesu,
Ameponya roho yangu;
Ameniondoa dhambi,
Anifanye mzima.

6.Nilikuwa kifungoni,
Niliteswa na dhambi,
Nilifungwa minyororo
Yesu akanifungua.

7. Sifa, ameninunua!
Sifa, nguvu za wokovu!
Sifa, Bwana huhifadhi!
Sifa zake milele.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi