Tenzi za Rohoni – 100

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

TUMRUDIE BWANA

1.Mbona washangaa njiani?
Mbona warejea nyuma?
Warudi tena gizani
Alimokutoa Bwana?

2.Ni ya bure yote haya,
Uliyofunzwa ya Mungu?
Ni bure amekufia
Bwana Yesu kwa uchungu?

3.Wamtia kristo aibu
Na maneno yake pia?
Siku yaja ya hesabu,
Utamjibuje Bwana?

4.Upandapo tena hayo,
Halafu utayavuna.
Rudi kwa Bwana upesi,
Mwombe akupokee tena.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi