Tenzi za Rohoni – 101

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

TWONANE MILELE

1.Nyimbo na tuziimbe tena
Za alivyotupenda mbele;
Kwa damu ya thamani sana!
Mbinguni twonane milele.

Twonane milele,
Twonane bandarini kule;
Twonane milele,
Twonane bandarini kule.

2.Hupozwa kila aoshwaye,
Kwa damu ya Kondoo yule;
Ataishi afurahiye
Vya Yesu mbinguni milele.

3.Hata sasa hufurahia
Tamu yake mapenzi yale,
Je, kwake tukifikilia,
Kutofarakana milele?

4.Twende mbele kwa jina lake,
Hata aje mwokozi yule,
Atatukaribisha kwake,
Tutawale naye milele.

5.Sauti zetu tuinue
Kumsifu Mwokozi yule,
Ili watu wote wajue
Wokovu u kwake milele.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi