Tenzi za Rohoni – 102

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

KAZI YANGU IKIISHA

1.Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka;
Na kuvaa kutokuharibika,
Nitamjua Mwokozi nifikapo ng’amboni;
Atakuwa wa kwanza kunilaki.

Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.

2.Furaha nitapata nikiona makao
Bwana aliyotuandalia;
Nitamsifu mwokozi kwa rehema na pendo
Vilivyonipa pahali Mbinguni.

3.Nao waliokufa katika Bwana Yesu,
Nitawaona tena huko juu;
Lakini nifikapo kwake huko Mbinguni,
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.

4.Milangoni mwa mji Bwana atanipitisha,
Pasipo machozi wala huzuni.
Nitauimba wimbo wa milele; lakini
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi