Tenzi za Rohoni – 103

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

KAA NAMI

1.Kaa nami, ni usiku tena;
Usiniache gizani, Bwana;
Msaada wako haukomi;
Nili peke yangu, kaa nami.

2.Siku zetu hazikawi kwisha,
Sioni la kunifurahisha;
Hakuna ambacho hakikomi,
Usiye na mwisho kaa nami.

3.Nina haja nawe kila saa;
Sina mwingine wa kunifaa;
Mimi nitaongozwa na nani
Ila wewe? Bwana, kaa name.

4.Sichi neno uwapo karibu;
Nipatalo lote, si taabu;
Kifo na kaburi haviumi;
Nitashinda kwako, kaa nami.

5.Nilalapo nikuone wewe,
Gizani mote nimulikiwe;
Nuru za mbinguni hazikomi,
Siku zangu zote kaa nami.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi