Tenzi za Rohoni – 104

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

TWASOMA NI NJEMA SANA

1.Twasoma, ni njema sana
Mbinguni, kwa Bwana;
Twasoma, dhambi hapana,
Mbinguni kwa Bwana;
Malaika wema wako,
Vinanda vizuri viko,
Na majumba tele yako,
Mbinguni kwa Bwana.

2.Siku zote ni mchana,
Ni nchi ya raha;
Wala machozi hapana,
Ni nchi ya raha;
Walioko wanuona
Uso wa Mwokozi, tena
Jua jingine hapana,
Ni nchi ya raha.

3.Nyama na vitu viovu
Havimo kabisa;
Kifo nacho, na ubovu,
Havimo kabisa.
Ni watakatifu wote,
Wameoshwa dhambi zote;
Wasiosafiwa wote
Hawamo kabisa.

4.Tuna dhambi, pia sote,
Mwokozi akafa;
Kwake tutaoshwa zote,
Mwokozi akafa;
Kwake twapata wokovu,
Tutawona utukufu;
Mbinguni tutamsifu;
Mwokozi akafa.

5.Baba, mama, ndugu zetu,
Twendeni kwa Bwana;
Huku chini sio kwetu,
Twendeni kwa Bwana;
Tusishikwe na dunia,
Na dhambi kutulemea;
Tutupe vya chini pia,
Twendeni kwa Bwana.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi