Tenzi za Rohoni – 105

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

KUWATAFUTA

1.Kuwatafuta wasioweza,
Kuomba wamrejee Yesu,
Kuwaambia maneno yake,
“Njooni kwangu, nawapenda”.

Nitakwenda, (kwenda), niwatafute
Waongofu (wa Bwana) wageuke,
Waingie (wote) katika zizi
La Mkombozi (wetu) Yesu kristo.

2.Kuwatafuta wasioweza,
Waonyeshwe Mwokozi wetu,
Kuwaongoza, wapate wote
Uzima wa milele.

3.Kazi hiyo nataka kufanya,
Leo nimesikia mwito
Kuwainua waangukao,
Waletwe kwake Yesu njia.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi