Tenzi za Rohoni – 106

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

MUNGU AWE NANYI DAIMA

1.Mungu awe nanyi daima,
Hata twonane ya pili,
Awachunge kwa fadhili,
Mungu awe nanyi daima.

Hata twonane huko juu,
Hata twonane kwake kwema;
Hata twonane huko juu,
Mungu awe nanyi daima.

2.Mungu awe nanyi daima;
Ziwafunike mbawaze,
Awalishe, awakuze;
Mungu awe nanyi daima.

3.Mungu awe nanyi daima;
Kila wakati wa shani
Awalinde hifadhini;
Mungu awe nanyi daima.

4.Mungu awe nanyi daima;
Awabarikie sana,
Awapasulie kina;
Mungu awe nanyi daima.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi