Tenzi za Rohoni – 108

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

TWENENDA SAYUNI

1.Mpendao Bwana
Ije raha yenu!
Imbeni nyimbo za raha
Wa ibada yenu.

Twenenda Sayuni,
Mji mzuri Sayuni;
Twenenda juu Sayuni
Ni maskani ya Mungu.

2.Wasiimbe wao
wasioamini,
Watoto wa Mungu ndio
waimbao chini.

3.Twaona rohoni
Baraka za Mungu,
Tusijafika Mbinguni
Kwenye utukufu.

4.Tutakapo mwona
Masumbuko basi,
Huwa maji ya uzima,
Anasa halisi.

5.Tupaaze sauti,
Na fute machozi,
Twenenda kwa Imanweli
Naye ni Mwokozi.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi