Tenzi za Rohoni – 110

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

MAPYA NI MAPENZI HAYO

1.Mapya ni mapenzi hayo,
Asubuhi tunayo,
Saa za giza hulindwa
Kwa uzima kuamshwa.

2.Kila siku, Mapya pia
Rehema, wema, na afya,
Wokofu, na msamaha,
Mawazo mema, furaha.

3.Tukijitahidi leo
Na mwendo utupasao,
Mungu atatueleza
Yatakayompendeza.

4.Mambo yetu ya dunia
Mungu atayang’aria,
Matata atageuza
Yawe kwetu ya Baraka.

5.Yaliyo madogo, haya
Mungu tukimfanyia,
Yatosha: tutafaidi
Huvuta kwake zaidi.

6.Ewe Bwana, siku zote,
Tusaidie kwa yote:
Mwendo wetu wote vivyo,
Uwe kama tuombavyo.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi