Tenzi za Rohoni – 112

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

NILIKUPA WEWE MAISHA YANGU

1.Nilikupa wewe
Damu ya moyoni,
Ili wokolewe,
Winuke ufuni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini?

2.Nilikupa miaka
Yangu duniani
Upate inuka,
Kuishi Mbinguni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini:

3.Niliacha nuru
Za Baba, Mbinguni,
Kwingia taabu
Za ulimwenguni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini?

4.Niliteswa sana,
Mateso kifoni,
Usije yaona
Hayo ya motoni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini?

5.Nimekuletea
Huku duniani
Upendo na afya
Zatoka Mbinguni:
Nimekunyimani?
Umenipa nini?

6.Nipe siku zako,
Udumu mwangani;
Na taabu yako,
Wingie rahani
Nafsi, pendo, mali,
Twae Imanweli.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi