Tenzi za Rohoni – 113

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

NI MFALME WA MAPENZI

1.Ni Mfalme wa mapenzi
Ndiye anichungaye,
Sipungukiwi, hawezi.
Kunipoteza yeye.

2.Kando ya mji mazima
Yeye huniongoza
Katika malisho mema
Daima hunilaza.

3.Mara nyingi hupotea
Kwa ukaidi wangu,
Naye huniandamia,
Hunirudisha kwangu.

4.Uvulini mwa mauti,
Siachi hatari kamwe,
Wewe Bwana huniachi,
Mwokozi wangu wewe.

5.Waniandikia meza
Neema kwako tele.
Kwa wewe, yote naweza.
Na msalaba mbele.

6.Kamwe hautapungua
Uule wema wako;
Mwisho, atanichukua,
Juu, niimbe kwako.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi