Tenzi za Rohoni – 115

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

KILIMA KANDO YA MJI

1.Kilima kando ya mji
Alikufa Bwana;
Kuokoa wakosaji
Akateswa sana.

2.Kabisa hayasemeki,
Mateso dhaifu
Alikufa mwenye Haki
Tupate wokovu.

3.Alimwaga damu yake
Ili tuwe wema,
Tufae kukaa kwake
Mbinguni daima.

4.Hatuna mwenye imani
Aliye na haki,
Wa kutosha yetu deni,
Rafiki Yesu tu.

5.Alijua peke yake
Kufungu Mbingu
Ufunguo damu yake
Kondoo wa Mungu.

6.Aliyetupenda hivyo
Nasi tumpende,
Tukamtumai vivyo
Na kazi tutende.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi