Tenzi za Rohoni – 116

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

BWANA U SEHEMU YANGU

1.Bwana u sehemu yangu,
Rafiki yangu wewe;
Katika safari yangu
Tatembea na wewe;
Pamoja na wewe,
Pamoja na wewe,
Katika safari yangu
Tatembea na wewe.

2.Mali hapa sikutaka,
Ili niheshimiwe,
Na yanikute mashaka
Sawa sawa na wewe,
Pamoja na wewe,
Pamoja na wewe,
Heri nikute mashaka
Sawasawa na wewe.

3.Niongoze safarini,
Mbele unichukue
Mlangoni kwa Mbinguni
Niingie na wewe.
Pamoja na wewe,
Pamoja na wewe,
Mlangoni kwa mbinguni,
Niingie na wewe.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi