Tenzi za Rohoni – 117

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

TUFANI INAPOVUMA

1.Tufani inapovuma
Sana moyoni mwangu,
Huona pa kujificha
Mkononi mwa Mungu.

Hunificha, hunificha
Adui hatanipata,
Hunificha, hunificha,
Mkononi mwake.

2.Pengine kuna taabu
Yanisongeza kwake;
Naijua si hasira,
Ni ya mapenzi yake.

3.Adui wakiniudhi
Nami nikisumbuka,
Mungu atavigeuza
Vyote viwe baraka.

5.Niishipo duniani
Ni tufani daima,
Anilindapo rohoni
Nitakaa salama.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

2 thoughts on “Tenzi za Rohoni – 117

  1. Pingback: fotbollströjor

Comments are closed.