Tenzi za Rohoni – 119

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

SI DAMU YA NYAMA

1.Si damu ya nyama
Iliyomwagika
Iwezayo kuondoa
Dhambi za wakosa.

2.Yeye Bwana Yesu
Sadaka ya Mungu,
Mwenye damu ya thamani,
Ni mwokozi kweli.

3.Kwa imani yangu,
Namshika yeye,
Naziweka dhambi zangu
Juu ya kichwa chake.

4.Mzigo wa dhambi
Sichukui tena,
Ameuchukua yeye,
Juu ya msalaba.

5.Bwana Yesu ndiye,
Mwokozi wa kweli
Tumsifu siku zote,
Twapata uhuru.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi