Tenzi za Rohoni – 120

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

ENYI WANADAMU

1.Enyi wanadamu mbona
Sana mwatanga-tanga,
Kama kondoo wanyonge,
Wasio na mchunga?
Yuko mchunga mmoja
Mwenye mapenzi mema;
Haya kutaneni kwake,
Atawachunga vyema.

2.Mungu tunamwona kuwa
Mwenye uwezo wote;
Na nguvu zake zapita
Mawazo yetu yote:
Ni Baba,mapenzi yake
Ni makubwa hakika;
Hatuwezi kuyajua,
Na hayana mpaka.

3.Rehema za Mungu nazo
Zina upana sana;
Kama huo wa bahari,
Mwisho wake hapana;
Haki yake ina mema,
Kwa hayo twashukuru,
Kwetu uko msamaha,
Furaha na uhuru.

4.Mapenzi yake mapana,
Sisi hatuna cheo
Cha kutosha, nao moyo
Una wema upeo;
Ukombozi mwingi mno
Katika damu yake;
Sote twapata furaha,
Kwa maumivu yake.

5.Yesu mkaribieni
Njoni msife myoyo;
Njoni kwake kwa imani,
Mema yake ni hayo;
Heri tuwe kama wana
Tushike neno lake,
Daima atujaza
Tele furaha yake.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi