Tenzi za Rohoni – 121

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

LIKO LANGO MOJA WAZI

1.Liko lango moja wazi,
Ni lango la mbinguni;
Na wote waingiao
Watapata nafasi.

Lango ndiye Yesu Bwana
Wote waingie kwake,
Lango! Lango
La Mbinguni ni wazi.

2.Yesu ndiye lango hili,
Hata sasa ni wazi,
Kwa wakubwa na wadogo,
Tajiri na maskini.

3.Hili ni lango la raha,
Ni lango la rehema;
Kila mtu apitaye
Hana majonzi tena.

4.Tukipita lango hili
Tutatua mizigo,
Tuliochukua kwanza,
Tutavikwa uzima.

5.Hima ndugu tuingie
Lango halijafungwa,
Likifungwa mara moja
Halitafunguliwa.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi