Tenzi za Rohoni – 122

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

BWANA YESU

1.Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Mbona unaumia? Unateseka sana,
Kwa ajili ya kuomba,
Waomba na jasho jingi likageuka damu.

Kumbe! Ni dhambi zangu zinazokuumiza.
Bwana wangu, Mungu wangu,
Mimi leo, naja kwako
Ili niziungame.

2.Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Mbona unaumia, na mizigo mizito?
Umejitwalia wewe, msalaba mabegani
Kwa ajili ya watu.

3.Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Mbona unatukanwa, wawambwa kama mwizi,
Bila kosa ukalia, Baba yangu, wasamehe,
Chukua roho yangu.

4.Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Muda ulipofika, nchi ikawa giza,
Mbinguni pakatulia,
Angani pakawa kimya,
Watu wakaogopa.

5.Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Jinsi ulivyoumwa, ukamwomba Baba,
Leo umeshinda kifo, sasa wapaa Mbinguni,
Naimba, Haleluya.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi