Tenzi za Rohoni – 123

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

NIMEKETI MIMI NILI KIPOFU

1.Nimeketi mimi nili kipofu
Gizani nangojea macho;
Ewe Bwana Yesu mwenye wokovu,
Ondoa dhambi zangu nzito.

Huruma hakuna aonaye,
Gizani nagojea macho,
Sasa nitakase nikusihiye,
Yesu, na dhambi zangu nzito.

2.Tangu siku nyingi nimepofuka
Natamani uso nikwone;
Ewe Bwana Yesu, mwenye baraka
Sema neno, basi, nipone.

3.Nimeketi mimi nili na giza,
Nami ya kutumai sina;
Ili nasikia kunong’oneza,
“Kwake Yesu kuna kupona.”

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi