Tenzi za Rohoni – 126

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

NI MJI MZURI

1.Ni mji mzuri,
Mbali sana;
Watu wanawiri
Kama jua;
Waimba kwa tamu,
Tuna wema hakimu:
Sifa na idumu,
Kwake Bwana.

2.Ni mji mzuri
Twende sote!
Una na fahari
Msikawe!
Raha tutaona,
Dhambi hapana tena;
Hatutaachana
Siku zote.

3.Ni mji mzuri;
Macho yote
Huko wanawiri
Kama pete;
Baba tutamwona,
Tukifanywa tu wana;
Tumo kupendana
Naye sote.

4.Ni mji mzuri;
Tusipotee
Na tuwe hodari,
Tuupate!
Tufunze, tutume
Kwa taji na ufalme:
Sifa na zivume
Siku zote.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi