Tenzi za Rohoni – 128

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

MMOJA APITA WOTE

1.Mmoja apita wote,
Atupenda;
Zaidi ya ndugu wote,
Atupenda;
Rafiki wa duniani,
Wote hatuwaamini;
Yesu kwa kila zamani,
Atupenda.

2.Kumjua ni uzima,
Atupenda;
Jinsi ajaavyo wema
Atupenda;
Yeye ametununua
Kwa damu aliyomwaga,
Dhambini kutuokoa,
Atupenda.

3.Sasa tunaye rafiki,
Atupenda;
Hupenda kutubariki;
Atupenda;
Twapenda kumsikia,
Atwita kukaribia,
Nasi tutamwamania,
Atupenda.

4.Husamehe Dhambi zetu,
Atupenda;
Hushinda adui zetu,
Atupenda;
Anatwonea huruma,
Hatupati ila mema,
Anatwongoza salama,
Atupenda.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi