Tenzi za Rohoni – 129

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

KARIBU NA WEWE

1.Karibu na wewe,
Mungu wangu
Karibu zaidi,
Bwana wangu
Siku zote niwe
Karibu na wewe,
Karibu zaidi
Mungu wangu.

2.Mimi nasafiri
Duniani,
Pa kupumzika
Sipaoni,
Nilalapo niwe
Karibu na wewe,
Karibu zaidi
Mungu wangu.

3.Na kwa nguvu zangu
Nikusifu;
Mwamba, uwe maji
Ya wokovu;
Mashakani niwe
Karibu na wewe;
Karibu zaidi
Mungu wangu.

4.Na nyumbani mwa juu,
Baba yangu,
Zikikoma hapa
Siku zangu,
Kwa furaha niwe
Pamoja na wewe,
Karibu kabisa
Mungu wangu.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi