Tenzi za Rohoni – 131

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

PIGA SANA VITA VYEMA

1.Piga sana vita vyema
Kwa ushujaa daima,
Yesu ndiye nguvu zako,
Yesu ndiye kweli yako.

2.Kaza mwendo, ushindane
Angaza macho, umwone
Yesu ndiye njia yako,
Naye ndiye tuzo lako.

3.Tupa kizito, simama,
Tazama mbele, si nyuma;
Ni yeye uzima wako,
Naye ni kipendo chako.

4.Tangamka, uamini
Akushika mikononi
Hageuki, akupenda,
Kuwa naye una pia.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi