Tenzi za Rohoni – 132

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

SAUTI SIKILIZENI

1.Sauti sikilizeni
Za waimbao juu,
“Aleluya, Aleluya,
Aleluya, mkuu!”
Wako makundi-makundi
Kama nyota wang’ara,
Kwa makuti ya mitende,
Na meupe wamevaa.

2.Wazazi na manabii
Wafanyaji wa njia;
Mashahidi, waandishi,
Nao wafalme pia!
Mabikira kina-mama,
Wajane wa kusali,
Waimba wakikutana
“Msifunu Imanweli”.

3.Watu toka huzunini
Wameosha na nguo,
Ni kwa damu yake Yesu;
Maonjo, mbali nao!
Walitekwa, walikatwa
Hata kwa misumeno,
Kwao kifo na shetani
Walishindiwa mno.

4.Mungu mumo mwake Mungu,
Nuru mumu mwa nuru,
Kwa kufungamana mwako
Tutaishi mahuru;
Tujalize, Imanweli,
Kujaa kwako wewe
Mungu Baba, Mungu Mwana,
Mungu Roho, tunawe.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi