Tenzi za Rohoni – 134

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

JUU YAKE LANGU SHAKA

1.Juu yake langu shaka,
Yesu namuwekea,
Nami sitafedheheka
Nikimtegemea.

Natumai, natumai,
Nnatumai kwake tu;
Natumai, natumai,
Natumai kwake tu.

2.Juu yake, dhambi zangu;
Aniosha kwa damu;
Nionekane kwa Mungu,
Nisiye na laumu.

3.Juu yake yangu hofu;
Kwake nimetulia;
Sipotei kwa upofu
Njia aning’azia.

4.Juu yake raha yangu;
Humuangalia tu;
Mwenye kila ulimwengu,
Aniruzuku na huu.
5.Juu yake, moyo wangu;
Hali yangu na mali;
Mimi wake, Yeye wangu,
Twapasana kamili.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi