Tenzi za Rohoni – 135

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

MAPENZI YA MILELE

1.Mapenzi ya milele
Ndiyo yanipendezayo;
Yalinipenda mbele,
Sina fahamu nayo;
Sasa amani yake
Tele rohoni mwangu,
Ni mimi kwa kuwa wake,
Na yeye kuwa wangu,
Ni mimi kuwa wake,
Na yeye kuwa wangu

2.Mbingu zinang’ara juu,
Na nchi nayo vivyo;
Macho ya dunia tu
Hayajaona hivyo;
Nyuni huimba sana,
Maua yana rangi,
Ni kumjua Bwana
Na pendo zake nyingi,
Ni kumjua Bwana
Na pendo zake nyingi,

3.Mambo mengi maovu
Nayo yenye kutisha,
Sasa hayana nguvu,
Si yenye kututisha;
Ni mkononi mwake,
Nalindwa salamani
Ninajua ni wake,
Ni wake mapenzini.
Ninajua ni wake,
Ni wake mapenzini.

4.Wake hata milele,
Si kutengana tena;
Hunipa raha tele
Moyoni mwangu, Bwana;
Hiyo nchi na Mbingu
Zitatoweka zile,
Ni wake, Yeye wangu,
Milele na milele.
Ni wake, Yeye wangu,
Milele na milele.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi