Tenzi za Rohoni – 136

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

MSIFUNI, YESU NDIYE MKOMBOZI

1.Msifuni ,Yesu ndiye mkombozi;
Imbeni ya pendo zake kuu,
Sujuduni,malaika mlioko,
Jina lake liwe na sifa kuu.
Kama vile mchunga uchungavyo
Vivyo sisi kutwa atachunga.
Msifuni mlio wakw watoto
Msifuni aliye mchunga.

2.Msifuni,Yesu ndiye mkombozi;
Akateswa tupate ongoka;
Ndiye Mwamba,Dhamana ya kuokoka;
Sujuduni kwake muangikwa,
Yesu aliyeudhiwa na hamu
Kwa pendo za baba yake Mungu.
Aliyefyolewa na kusulubiwa.
Msifuni ndilo letu fungu.

3.Msifuni,Yesu ndiye Mkombozi;
Shindukeni,enyi malango juu;
Bwana Yesu tangu milele Mwokozi,
Mvikeni taji, ni yake tu.
Atakuja kuitawala nchi,
Yesu,Mwombezi wetu wa Mungu.
Msifuni, ni mfalme wa salama;
Ndiye kweli mwana wake Mungu.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi