Tenzi za Rohoni – 15

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

CHA KUTUMAINI SINA

1.Chakutumaini sina
Ila damu yake Bwana,
Sina wema wa kutosha
Dhambi zangu kuziosha;

Kwake Yesu nasimma,
Ndiye mwamba: ni salama
Ndiye mwamba: ni salama.

2. Njia yangu iwe ndefu
Yeye hunipa wokovu;
Mawimbi yakinipiga
Nguvu zake ndiyo nanga.

3. damu yake na sadaka
Nategemea daima,
Yote chini yakiisha
Mwokozi atanitosha.

4. Nikiitwa hukumuni,
Rohoni nina amani
Nikivikwa haki yake
Sina hofu mbele zake.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi