Tenzi za Rohoni – 16

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

KUMTEGEMEA MWOKOZI

1.Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa;
Kukubali neno lake
Nina raha moyoni.

Yesu,Yesu namwamini,
Nimemwona thabiti;
Yesu,Yesu,yu thamani,
Ahadi zake kweli.

2.Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa,
Kuamini damu yake
Nimeoshwa kamili.

3.Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa,
Kwake daima napata
Uzima na amani.

4.Nafurahi kwa sababu
Nimekutegemea;
Yesu,Mpendwa na Rafiki
Uwe nami dawamu.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi