Tenzi za Rohoni – 18

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

AKIFA YESU NIKAFA NAYE

1.Akifa Yesu nikafa naye
Uzima upya huishi naye;
Humtazama mpaka nje:
Nyakati zote ni wake yeye.

Nyakati zote nimo pendoni,
Nyakati zote ni uzimani,
Humtazama hata atokee,
Nyakati zote mimi ni wake.

2. Vita sipigi visivyo haki,
Na Bwana wangu hapiganiki;
Beramu yake haitwaliki,
Napo po pote hila sitaki.

3. Sina mashaka, akawa mbali;
Mizigo yote aihimili;
Ananituliza Imanweli,
Nyakati zote mimi husali.

4. Sina huzuni na mimi sidhii;
Simwagi chozi, wala siguni;
Sikuti afa, ila kitini
Daima hunifikiri mimi.

5. Kila unyonge huusikia;
Kila ugonjwa kwake hupoa;
Yesu ni mwenye kuniokoa
Nyakati zote hunijalia.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi