Tenzi za Rohoni – 2

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

TWAMSIFU MUNGU

1.Twamsifu Mungu kwa Mwana wa Pendo,
Aliyetufia na kupaa juu.

Aleluya! Usifiwe; Aleluya! Amin.
Aleluya! Usifiwe, utubariki.

2. Twamsifu Mungu kwa Roho Mtukufu,
Ametufunulia Mwokozi wetu.

3. Twamsifu Mwana, aliyetufia,
Aliyetwaa dhambi akazifuta.

4. Twamsifu Mungu wa neema yote,
Ametukomboa akatuongoza.

5. Tuamshe tena, tujazena pendo,
Na moyoni uwashe moto wa Roho.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi