Tenzi za Rohoni – 23

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

NI SALAMA ROHONI MWANGU

1.Nionapo amani kama shwari,
Ama nionapo shida;
Kwa mambo yote umenijulisha,
Ni salama rohoni mwangu.

Salama rohoni,
Ni salama rohoni mwangu.

2.Ingawa shetani atanitesa,
Nitajipa moyo kwani
Kristo ameona unyonge wangu,
Amekufa kwa roho yangu.

3.Dhambi zangu zote, wala si nusu,
Zimewekwa msalabani;
Wala sichukui laana yake,
Ni salama rohoni mwangu.

4.Ee Bwana himiza siku ya kuja,
Panda itakapolia;
Utakaposhuka sitaogopa
Ni salama rohoni mwangu.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi