Tenzi za Rohoni – 26

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi

YESU UNIPENDAYE

1.Yesu unipendaye
Kwako nakimbilia,
Ni wewe utoshaye,
Mwovu akinijia;
Yafiche ubavuni,
Mwako maisha yangu;
Nifiikishe mbinguni
Wokoe moyo wangu.

2.Ngome nyingine sina;
Nategemea kwako.
Usinitupe Bwana ,
Nipe neema yako,
Ninakuamania
Mwenye kuniwezesha;
Shari wanikingia,
Vitani wanitosha.

3.Nakutaka Mpaji
Vyote napata kwako;
Niwapo muhitaji,
Utanijazi vyako;
Nao waangukao
Wanyonge wape nguvu;
Poza wauguao,
Uongoze vipofu.

4.Bwana umeniosha
Moyo kwa damu yako;
Neema ya kutosha
Yapatikana kwako;
Kwako Bwana naona
Kisima cha uzima;
Mwangu moyoni Bwana,
Bubujika daima.

Bonyeza hapa kurudi kwenye Orodha kuu ya Tenzi